PostGE2025 Pumzika kwa amani Kelvin Lameck, mwandishi wa Baraka FM - Mbeya aliyeuawa akiwa kazini

PostGE2025 Pumzika kwa amani Kelvin Lameck, mwandishi wa Baraka FM - Mbeya aliyeuawa akiwa kazini

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
312
Reaction score
1,433
Huyu anaitwa Kelvin Lameck alikuwa mwandishi wa radio inaitwa Baraka FM.

Ameuawa akiwa kazini kufuatilia maandamano wakati wa Uchaguzi.

Kifo chake kimeacha simanzi kubwa miongoni mwa familia, marafiki, na wasikilizaji wake waliompenda kutokana na ucheshi na bidii yake kazini.

Kelvin alikuwa miongoni mwa watangazaji nguli katika tasnia ya utangazaji mkoani Mbeya, akijulikana kwa sauti yake yenye mvuto na utendaji uliogusa mioyo ya wengi.

Wengi wameendelea kutuma salamu za rambirambi na kuombea pumziko la amani kwa roho ya marehemu Kelvin Lameck.
1762239597779.png
 
Tunaambiwa hawa walikuwa wakenya, yaan hawatak kukiri kosa wakiulizwa kama walileta askari kutoka Uganda wanakana, wakiulizwa kuhusiana na waliouawa wanasema hao walikuwa raia wa nchi nyingine. Hawajielewi hata
 
Ni maumivu juu ya maumivu kwakweli.

Halafu bado lile shetani linajinasibu eti "kazi na utu"

Apunzike kwa amani mtumishi
 
Kwa binadamu mwenye utu na aibu kidogo asingeweza hata kujiapisha haraka haraka hivi.

Unajiapisha katika kati ya majonzi mazito na huku watu bado wana wasi wasi hata chakula ndani hawana...!! Hiyo ni Hitler hakuwa na roho ngumu kiasi hiki.
 
View attachment 3496885

Huyu anaitwa Kelvin Lameck alikuwa mwandishi wa radio inaitwa Baraka FM.

Ameuawa akiwa kazini kufuatilia maandamano wakati wa Uchaguzi.

Kifo chake kimeacha simanzi kubwa miongoni mwa familia, marafiki, na wasikilizaji wake waliompenda kutokana na ucheshi na bidii yake kazini.

Kelvin alikuwa miongoni mwa watangazaji nguli katika tasnia ya utangazaji mkoani Mbeya, akijulikana kwa sauti yake yenye mvuto na utendaji uliogusa mioyo ya wengi.

Wengi wameendelea kutuma salamu za rambirambi na kuombea pumziko la amani kwa roho ya marehemu Kelvin Lameck.
Atakuwa ametoka nchi gani kwa mujibu wa rais wenu?
 
Kevin lameck Alikuwa anajiita msemaji wa watu wasiokuwa na mahali pa kusemea
 
Back
Top Bottom