TANZIA Pumzika kwa amani Mzee Gregory Shigella

Status
Not open for further replies.
Kwanini kila kitu tuige nchi zilizoendelea. Malkia Elizabeth alizikwa mazishi private na hayakuwa live?

Kila watu na taratibu zao, Waarabu mtu akifia Thailand na watoto wake wako Afghanistan wanaweza wasiambiwe mwili ukazikwa na wakisia baadae wataridhika kabisa. Baadhi ya Wanigeria wanaweza kaa na mwili zaidi ya mwezi.

Kisa kitu hukipendi na kipya haimaanishi ni ulimbukeni. Hakuna madhara kwa jamii sasa yanini kutaka kisifanyike. Mbona hata wengine wanaweza sema kuiga nchi zilizoendelea ndio ulimbukeni wenyewe
 
Raha ya milele umpe Eeh Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie APUMZIKE KWA AMANI [emoji120]
 
Sijajua kama alikuwa ni mtu maarufu kitaifa au la!, ila kilichonivutia ni kwamba mzee alikuwa anakubalika katika jamii ingawa hakuwa na utajiri.

Watu wengi tunaamini ili ukubalike katika jamii ni lazima uwe na pesa.

Sasa nauliza, ni mbinu gani za kutumia ili sisi ambao hatuna hela angalau tuwe tunaheshimika katika familia, ukoo na jamii hata kushirikishwa mawazo tu linapotokea suala mfano msiba, harusi!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
R.I.P 🙏🏽
 
Nimesema ustaarabu. Kwangu mimi ni ujinga kuonyesha live kwa dunia mazishi ya mpendwa wako. Kama wewe unataka basi kodi hata TV zote za ulimwengu u-live stream.
 
Hapo inabidi uwe na akili kubwa.

Uwe na kile Wafaransa wanachokiita "savoir faire".

Yani uwezo wa kujua nini cha kusema, nini cha kuacha kusema, nini cha kufanya, nini cha kuacha kufanya, kwa wakati gani, kwa namna gani, kwa mipaka gani, nini ukubali, nini ukatae, ujue uhuru wako unaishia wapi, uhuru wa mwenzako unaanzia wapi, jamii inataka vipi, wewe unataka nini, unawezaje ku navigate matakwa ya jamii na yako bila kuleta mgogoro, unawezaje kuwa mtu wa msaada kwa jamii bila ya kuwa mtu mwenye pesa nyingi.

Si kazi ndogo, na ukiona mtu kaweza hiyo, ujue mara nyingi katumia akili sana.
 
Poleni kwa msiba mkuu

Maisha yake yakawe kioo chenu cha kujitazama na kujikagua
 
Pole kwa wafiwa, ila huu ushamba na ulimbukeni wa ''live streaming'' ya mazishi ni ujinga uliopitiliza. Mazishi ni kitu cha private hakitakiwi kuonyeshwa kwenye internet. Huu ulimbukeni unaivamia jamii yetu kwa kasi kabisa.
Hapa umesema ni ushamba na ulimbukeni kufanya live streaming ya mazishi na ujinga kupitiliza.
Nimesema ustaarabu. Kwangu mimi ni ujinga kuonyesha live kwa dunia mazishi ya mpendwa wako. Kama wewe unataka basi kodi hata TV zote za ulimwengu u-live stream.
Hapa unasema kwako wewe, sasa sijui aliyekufa ni wewe au mzee Gregory Shigella.

Ingekuwa ni msiba wako, mzazi, mkeo au mwanao sheria zako zingekuwa applicable.
Msiba haukuhusu kabisa hivyo kuita maamuzi ya watu ushamba, ulimbukeni na ujinga kupitiliza ndio ulimbukeni wenyewe huo. Watu wamefanya live streaming ya mazishi ya mpendwa wao wewe unawapangia masharti eti "ustaarabu"
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…