Punguza kujihurumia ili uvuke bonde ulilopo

mushijcob

Senior Member
Joined
May 20, 2015
Posts
104
Reaction score
69
#USIISHIE_NJIANI

Habari Rafiki Yangu, Leo ni siku nyingine mpya kabisa ambayo unatakiwa uende ukaitumie vyema ili kufikia mafanikio kwenye kile ulichoamua kukifanyia kazi.
Usikubali kuipoteza siku yako kwa kufanya mambo ya kawaida.

USIJIHURUMIE SANA.
Ili upate matokeo makubwa zaidi wakati mwingine inabidi ufanye kitu cha ziada. Yaani uende mbele zaidi ya vile ulivyozoeaga kufanya.

Kama huwa unasoma vitabu ongeza speed zaidi. Kama ni kuamka ongeza muda wa kuamka yaani amka mapema zaidi.

Wakati mwingine kama ulikua unalala mapema ili upate matokeo makubwa inabidi upunguze muda wa kulala kidogo kwa muda unaopigania matokeo makubwa.

Ndio hivyo rafiki ukitaka zaidi toa zaidi.
Ongeza juhudi zaidi.
Ongeza maarifa zaidi.
Ongeza idadi ya wateja zaidi.

Hakuna matokeo yatakayokuja yenyewe bila ya wewe kuweka juhudi zaidi.

Endelea kusonga mbele na usiishie njiani.
Unaweza kubadili mpango lakini usibadili lengo.
Unaweza kuongeza kuona mbali zaidi lakini usibadili maono na ndoto yako.

Punguza kujihurumia ili uvuke bonde ulilopo.


[HASHTAG]#JacobMushi[/HASHTAG]
www.mushijacob.com

Sent from my TECNO-C8 using JamiiForums mobile app
 


""Unaweza kubadili mpango lakini usibadili lengo.""

Ufafanuzi tafadhali
 
Safi sn!! Nimeipenda hii watu km nyie mbaweza hata kutengeneza vitabu au kuandaa kipindi cha kuelimisha jamii
 
Kama ulikua unatumia elfu 30 kwa siku ongeza ifike laki moja...acha kujihurumia wewe
 
Noted
 
vitu nilivyofanya bila kkujihurumia ndio hadi sasa vinadumu.
Hata yesu anasema mtu akikwambia nenda maili moja nenda nae maili mbili.
Maana yake jiongeze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…