Jerry Farms
JF-Expert Member
- Jul 18, 2022
- 344
- 350
Je, wewe n mmoja wapo ya wale wanunuao sabuni kwa kufata manukato pasi na kujali viambata viitengenezayo sabuni husika?
Hili ni moja wapo ya zoea baya la walaji wa bidhaa mbali mbali nnchini. Moja wapo ya walaji hawa ni watumiaji wa sabuni za kuogea.
Matumizi ya Sabuni zenye viambata vya dawa yamekua ni zoea la wengi wetu. Na hii imechagizwa na zoea la kutumia sabuni pasi na kufata ushauri wa wataalamu wa ngozi. Mtu hapa atasema, " nitoke kwangu nikaulize juu ya sabuni kwa daktari! Muda natoa wapi", hii n hoja dhaifu sana. Kama huna muda ndg mlaji basi chukua hata muda wa kusoma nini kilichounda sabuni yako.
Punguza matumizi makubwa ya sabuni zote zenye viambata vya dawa. Jitahidi usome kipeperushi cha sabuni yako. Heko kwa watengenezaji wa sabuni za Rungu/Family medicated soap hawa angalau wameweka angalizo katika sabuni zao, japo maandishi ya angalizo yameandikwa kwa kijimuandiko kidooogo usipokua makini hutaona katazo.
Kasha la sabuni ya Family M Soap
*Nenda kwa Mangi/Poti omba sabuni hii....ichunguze kwa umakini takuna na maneno haya:
*Sabuni hii ina TCC
*Unashauriwa Usitumie mara kwa mara.
Madhara ya matumizi makubwa ya sabuni dawa kwa Ngozi.
-Uharibifu wa ustahimilivu wa "asili" wa ngozi kuulinda mwili dhidi ya bakteria.
-Ukavu wa ngozi, kupasuka kwa ngozi, muwasho na vijipele.
-Usugu wa dawa ( dawa za matibabu ya ngozi kushidwa kufanya kazi kwa wale wenye matatizo ya ngozi). Vilevile matumizi ya mara kwa mara ya sabuni dawa huwafanya bakteria wa magonjwa ya ngozi kujenga mfumo wa usugu hivyo kutokuzuilika kwa dawa tumiwa iliyoko katika sabuni.
-Matatizo ya homoni
Kiambata cha "triclosan" kimeonesha matokeo hasi kwa watumiaji wa sabuni zenye kiambata hiki. Miongoni mwa madhara hayo ni: matatizo ya afya ya uzazi, matatizo ya tezi na wakati mwingini kuchagiza kwa ukuaji wa vimelea vya baadhi ya aina ya kansa.
Kama hakuna haja ya matumizi ya sabuni dawa, ndugu tumia sabuni ya kawaida tu kuogea( kama ni mpenzi wa manukato tafuta ya manukato wale wasio na hizo tumia hata ya kufuria. Kwa nini utumie sabuni dawa alhali huna ugonjwa wa ngozi!
Mtanzania, jenga tabia ya kusoma vifungashio au makasha ya bidhaa ujue ABC za bidhaa husika kabla ya kuitumia. Jukumu la utunzaji wa afya linaanza na wewe mlaji.