Punguza misaada, watu hawana kumbukumbu

Punguza misaada, watu hawana kumbukumbu

minded tips

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2018
Posts
479
Reaction score
859
Habari za majukumu wana mizengo bila shaka muwazima wa afya naomba kwenda kwenye mada moja kwa moja

PUNGUZA MISAADA WATU HAWANA KUMBUKUMBU
[emoji117]Watu wanapost sana huo msemo hapo bila kujua wanakosea san ipo hivi unapomsaidia mtu tarajia malipo kutoka kwa Mungu na sio kwa binadamu yeyote yule ila kizazi cha leo baadhi yao wanataka akikusaidia na wewe umsaidie yani ni mwendo wa biashara[emoji849] tena nieleweke hivi Mungu hajakataza kulipiza wema kwa mtu aliyekufanyia wema ila isiwe deni maana kuna watu mpaka leo wanaogopa kuweka mapito yao wazi kwa kuogopa kusimangwa baada ya kutatuliwa matatizo yao

UNAPOKUA NA NAFASI YA KUWASAIDIA WATU KWA KADLI UWEZAVYO KIROHO SAFI WASAIDIE BILA KUANGALIA UTAFAIDIKA NA NINI WASAIDIE NA USISUBIRI SHUKRANI

IMG_20210714_104132_149.jpg
 
Sahihi kabisa mkuu,

Pia ukisha msaidia mtu basi sio uanze kumfuata fuata tena kisa tu ulimsaidia, ukisha msaidia endelea tu na mishe zako, ukianza kumfuata fuata ndio zile unaanza kumsema, mara sijui siku hizi hanisalimi, mara hanitafuti, kumsaidia mtu haimaanishi kua huyo mtu ageuke na kua mtumwa kwako kisa tu ulimsaidia.

Tenda wema nenda zako, usingoje shukurani.
 
Sahihi kabisa mkuu,

Pia ukisha msaidia mtu basi sio uanze kumfuata fuata tena kisa tu ulimsaidia,ukisha msaidia endelea tu na mishe zako,ukianza kumfuata fuata ndio zile unaanza kumsema,mara sijui siku hizi hanisalimii,mara hanitafuti,kumsaidia mtu haimaanishi kua huyo mtu ageuke na kua mtumwa kwako kisa tu ulimsaidia,

Tenda wema nenda zako,usingoje shukurani.
Hiki ndio kinachonichoshaga mimi kabisaaaaaaaaa
 
Mkuu huo ndio ukweli, usifanye matatizo ya wenzako yawe ya kwako, kila mtu ashinde mechi zake !
 
Mkuu huo ndio ukweli, usifanye matatizo ya wenzako yawe ya kwako, kila mtu ashinde mechi zake !
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]kah
 
Na hii ipo hadi kwa wazazi wa kiafrika, utasikia mara nilikusomesha, nilikunyonyesha, nilikubeba.....sasa unajiuliza hivi ukizaa mtoto unategemea huyo mtoto ajibebe, ajinyonyeshe, ukizingatia pia na wenyewe wamezaliwa na wakafanyiwa hayo.
 
Tatizo hili aiseee
 
Mkuu huo ndio ukweli, usifanye matatizo ya wenzako yawe ya kwako, kila mtu ashinde mechi zake !
Nilikuwaga hivyo kabisa, au tuseme ndivyo nilivyoumbwa nilikuwa mtu akiniambia shida yake karoho kanaruka mno mpaka nitoe msaada enzi tuhela tunanitembelea.

Bwana we sio kila siku ni jumamosi ilipofika jpili tule tuhela tukapotea Potea ndivyo nilivyowajua walimwengu kila unayemgusa kuwa una shida anakujibu sina.

Mungu si mjomba naiona jmosi yangu inanukia tena nimekuwa mchumi kuliko, aje mtu na shida yake roho moja inasema mpe, roho ya pili inasema mnyime naambatana na ya pili.

Nilichojifunza wema usizidi uwezo mtu akilia shida ya laki mpe 20 yeye ndiye atakuwa wa kwanza kukucheka mambo yakienda kombo.
 
Sahihi kabisa mkuu,

Pia ukisha msaidia mtu basi sio uanze kumfuata fuata tena kisa tu ulimsaidia,ukisha msaidia endelea tu na mishe zako,ukianza kumfuata fuata ndio zile unaanza kumsema,mara sijui siku hizi hanisalimii,mara hanitafuti,kumsaidia mtu haimaanishi kua huyo mtu ageuke na kua mtumwa kwako kisa tu ulimsaidia,

Tenda wema nenda zako,usingoje shukurani.
ni changamoto sana sema haya mambo ndivyo yalivyo yani shida sana.
 
Saidia watu ambao unaona kabisa hawa wako kwenye uhitaji na si kujipendekeza hovyo kwa Mungu aliyempatia mwanaume adhabu ya kula kwa jasho
 
Back
Top Bottom