Punguzo bei ya mafuta halijagusa wananchi

Punguzo bei ya mafuta halijagusa wananchi

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Dar es Salaam. Wakati bei za mafuta zikizidi kushuka nchini kwa miezi miwili mfululizo, hali ya bidhaa na nauli bado zimesalia kuwa juu, huku wahusika wakisema bado kuna haja ya kushusha zaidi bei za mafuta ili kupoza makali hayo.

Mjadala huo umeibuka ikiwa ni siku mbili tangu Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) itangaze bei mpya za mafuta za Oktoba ambapo kwa Dar es Salaam lita moja ya petroli itauzwa kwa Sh2,886 ikipungua kutoka Sh2,969 mwezi uliopita, huku bei ya dizeli ikishuka hadi Sh3,083 kutoka Sh3,125 na bei ya mafuta ya taa ikishuka kwa Sh60 hadi kufikia 3,275 mwezi huu.

“Bado tunategemea mafuta yaendelee kushuka angalau kufikia Sh2,200, Sh2,000 au Sh1,900 ndiyo tuzungumzie masuala ya bei za nauli,” alisema Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Joseph Priscus.

Priscus alisema kuwa bei ya nauli itaendelea kama ilivyo kwasababu bei ya mafuta iliyoshuka ni ndogo sana.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa), Elias Lukumay aliyesema kwa upande wao bado bei mpya za mafuta hazina faida chanya na wanaamini bado bei zinaweza zikashuka zaidi ili kuleta matokeo chanya.

Naye Mtaalamu na mtafiti wa masuala ya Uchumi, Profesa Abel Kinyondo alisema kushuka kwa mafuta kunaweza kusiwe na tija kwa mtumiaji wa mwisho kama hakutakuwa na udhibiti wa mamlaka husika kwa watoa huduma.

“Utafiti unaonyesha kuwa mara nyingi mafuta yakishuka bei, nafuu hiyo inaishia kuwanufaisha wafanyabiashara na haiwafikii watumiaji wa mwisho ambao ni wananchi, hivyo ndio maana nchi inakuwa na kitengo cha kudhibiti hali hiyo ambayo kwa Tanzania tunayo Tume ya Ushindani (FCC),” alisema.

Profesa Kinyondo alisema kuwa kuna ushabihiano mkubwa wa kushuka kwa bei ya mafuta na bei za bidhaa, hasa kupitia mfumuko wa bei.

“Tafiti zinaonyesha kuwa bei ya mafuta ikishuka na pia mfumuko wa bei unashuka kwenye nchi husika. Pia inaeleza iwapo mafuta yakishuka kwa asilima 40, mfumuko wa bei utashuka kwa asilimia 10,” alisema.

“Bei ya mafuta ikishuka haimaanishi bei za bidhaa nazo zitashuka kwa kipindi hicho, lazima kuwe na kuchelewa kidogo (delay response) kutokana na kuwepo kwa mzigo mwingi wa bidhaa zilizonunuliwa kipindi kilichopita (kabla ya mafuta kushuka bei),” aliongeza.

Kwa upande wake Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar, Profesa Haji Semboja alisema kuwa kushuka kwa bei ya mafuta siyo sababu pekee itakayofanya kushuka kwa bei ya bidhaa katika nchi zinazoagiza mafuta, ikiwemo Tanzania.

“Kushuka kwa bei za bidhaa sokoni, haitegemei tu kushuka kwa bei ya mafuta, ila kuna sababu mbalimbali zinaathiri, hasa kwa nchi kama Tanzania ambayo mafuta tunayotumia tunayaagiza kutoka nje ya nchi.

“Sababu nyingine tunayoitegemea ni hali ya kilimo chetu ambacho kinategemea zaidi mvua kuliko umwagiliaji,” alisema.

“Hata hivyo hakukuwa na sababu halisi za kwenye uzalishaji zilizosababisha kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia, maana hata vita inayosemwa ya Ukraine na Russia haikuathiri uzalishaji wa mafuta, bali wazalishaji wakubwa walichukulia hicho kama kisingizio,” aliongeza Profesa Semboja.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Mkoa wa Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabrouk ameeleza kushuka kwa bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwao bado hakuna unafuu wowote.

Alisema hataki kuishutumu Serikali kuhusu hilo kwa kuwa haina mchango wowote katika hilo kwa kuwa suala la mafuta lina wenyewe. “Sisi tuvumilie tu mpaka watakapoamua kushusha bei ya mafuta kwa kiwango kikubwa basi na sisi tutaweza kupata unafuu wa maisha kwa kushusha bei za nauli,” alisema Mabrouk.

Kwa upande wake dereva wa pikipiki, Joramu Munuo ameeleza kwamba kushuka kwa bei ya mafuta inawasaidia sana kwa kuwa wanawapata abiria wengi na wanaweza kuyafikia mahesabu wanayotakiwa kupeleka kwa wamiliki wa pikipiki hizo.

Credit: Mwananchi
 
Bei ikishuka huko nje, wanasubiria

Ishuke kidogo, wakati watumiaji wanasubiria ishuke inapanda tena

[emoji1] huu usanii tu

Ova
 
Bei ikishuka huko nje....wanasubiria
Ishuke kidogo.....wakati watumiaji wanasubiria ishuke.....inapanda tena

[emoji1] huu usanii tu

Ova
 
Kama halijagusa Wananchi basi Wananchi wasogelee punguzo waliguse.
 
Back
Top Bottom