Hivi ni kweli kuwa punyeto iliyokithiri hupelekea tatizo la kukauka na kusinyaa kwa ngozi?
- Tunachokijua
- Punyeto ni tendo analofanya mtu, likihusisha kujisisimua sehemu zake za siri ili afikie utimilifu wa kihisia (Orgasm).
Takwimu
Tofauti na jinsi ambavyo watu wengi hudhani, tendo hili halijali jinsia ya mtu. Wanaume na wanawake wote hupiga punyeto.
Katika utafiti mmoja uliofanyika nchini Marekani ukihusisha vijana wa kike na kiume wenye umri kati ya miaka 14-17, 73.8% ya wavulana wote waliofanyiwa utafiti walikiri kupiga punyeto mara kadhaa, huku 48.1% ya wasichana wote waliofanyiwa utafiti wakikiri pia kufanya tendo hili.
Kwa watu wazima wenye umri kati ya miaka 57-64, 63% ya wanaume hupiga punyeto, huku wanawake wakiwa ni 32%.
Punyeto na kukauka kwa ngozi
JamiiForums imefuatilia jambo hili kwa kurejea machapisho mbalimbali pamoja na tafiti za afya. Tumebaini mambo yafuatayo;
- Punyeto haisababishi kukauka au kusinyaa kwa ngozi
- Madhara makubwa ya tendo hili ni kuleta uraibu, utegemezi, kuvimba na kuchubuka kwa sehemu za siri, kutokuridhika kirahisi, uchovu mkubwa pamoja na kudhoofisha mahusiano ya watu wa jinsia tofauti.
- Nadharia za ubaya wa jambo hili kwa kiwango kikubwa huwa na asili ya dini
Ni tendo zuri kwa watu waliotengwa na jamii, pia ni njia ya kujikinga na ujauzito usio tarajiwa pamoja na magonjwa ya zinaa.