BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Rais wa Urusi Vladimir Putin amemzawadia mwenzake wa Zimbabwe helikopta ya Rais, kwa mujibu wa wizara ya habari ya Zimbabwe.
Zawadi hiyo itatolewa hivi karibuni, taarifa hiyo iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii imesema.
Rais Emmerson Mnangagwa anahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Urusi na Afrika huko St Petersburg pamoja na viongozi wengine wa Afrika.
Urusi pia iliahidi kutoa Ngano bure kwa Zimbabwe na nchi nyingine tano za Afrika.
Zimbabwe ina uhusiano wa muda mrefu na Urusi kuanzia vita vya ukombozi dhidi ya utawala wa wazungu wachache.
Ni miongoni mwa nchi za Kiafrika ambazo zimeshikilia msimamo wa kutoegemea upande wowote katika vita vya Ukraine, zikikataa kulaani Urusi kwa uvamizi huo.