Mrengwa wa kulia
JF-Expert Member
- Mar 21, 2022
- 1,091
- 3,695
Uhamasishaji wa kijeshi Urusi na kura za haraka za maoni katika maeneo yanayokaliwa mashariki mwa Ukraine ni ishara za udhaifu.
Putin amekosea; gharama wanalipa maelfu ya Warusi kwa maisha yao.
Rais Putin hawezi kurudi tena nyuma: Na ikiwa atashindwa katika vita vyake vya uvamizi dhidi ya Ukraine, itamgharimu madaraka yake, na yumkini zaidi ya hayo. Hali iatkuwa hivyo kwa wawakilishi wa bunge la Duma, ambao hatma yao hivi imeunganishwa na ile ya mkuu huyo wa Kremlin.
Wote wako katika hali ya taharuki kufuatia mafanikio ya karibuni ya vikosi vya jeshi la Ukraine katika kurejsha maeneo ya nchi yao yaliokaliwa.
Hali inaitishia Moscow kushindwa kijeshi, jambo ambalo hakuna alielitarajia mjini Moscow. Kutokana na hofu hiyo, Putin ameamuru kuwekwa tayari wanajeshi laki tatu wa akiba kwa ajili ya kwenda uwanja wa vita.
Jukumu la wanajeshi hao litakuwa kuzuwia kasi ya vikosi vya Ukraine kusonga mbele zaidi.
Putin Amedhoofika na alietengwa.
Uturuki, India na hata China ziliweka wazi kwamba zinapinga vita vya Putin, zinaunga mkono uhuru wa mipaka ya Ukraine. Na zilikuwa sababu za msingi:
Vita hivyo ni mzigo kwa uchumi wa dunia na vivyo hivyo kwa mamlaka ya wanasiasa hao, ambao Putin alitumai kupata uungwaji wao mkono kwa ajili ya vita vyake.
Mabadiliko ya mwelekeo katika Kremlin
Kwa mtazamo wa Kremlin, mambo hayangeweza kuendela hivi. Hivyo mjini Moscow, Putin anaharakisha kubadili mwelekeo na hivyo ukusanyaji huo wa wanajeshi kwa sehemu ni kukiri juu ya udhaifu wa kijeshi mashariki mwa Ukraine.
Kwa matangazo ya kuitisha kura ndani ya siku chache katika maeneo yaliotekwa kuhusu kujiunga na shirikisho la Urusi, ni wazi kwamba wa Ukraine hawataki kujiunga na Urusi. Kwa sababu kura inayofanyika mbele ya mtutu wa bunduki, kura ya maoni katika magofu, hakuna yeyote duniani anaweza kuichukulia kwa uzito.
Putin anataka kupata mali zilizoporwa. Maeneo yaliotekwa yatakuwa sehemu ya shirikisho la Urusi. Kisha Putin anaweza kutoa wito wa kutetea taifa kwa kutumia nguvu za kijeshi. Kile kinachoitwa operesheni maalumu ya kijeshi, ambayo ina mipaka ya muda na nafasi na ambayo haikuhusika kwa vyovyote na maisha ya kila siku ya Warusi walio wengi, inageuka kihistoria utetezi wa ardhi ya Urusi kwa njia zote, ikiwemo silaha za nyuklia.
Mtu haitaji kuwa nabii mkuu kutabiri mwisho unaokaribia wa neno operesheni maalumu. Propaganda ya Kremlin italizika neno hilo. Badala yake, kutakuwa uongo zaidi na zaidi wa kipumbavu na kuchanganya, uzushi, vitisho ambavyo vituo vya televisheni vinavyodhibitiwa na serikali vitatumia kuwarubuni Warusi.
Hata sasa inadaiwa kuwa Urusi haifanyi vita dhidi ya Ukraine, lakini inanjitetea nchini Ukraine dhidi ya Marekani na Uingereza. Hilo wanaliamini wanaotaka kuamini.
Uchochezi mpya wa Putin utachuliwa kwa uzito na viongozi wa dunia wanaokutana hivi sasa katika hadhira kuu ya Umoja wa Mataifa mjini new York. Lakini sera yao kuelekea Moscow haitabadilika pakubwa. Kiev itaendelea kupokea silaha, jeshi lake litadelea kupambana. Na wanajeshi 300,000 wa akiba wa Urusi? Hawajawahi kuwa vitani, hawana zana za kutosha. Ni watu wenye familia, wanaume wanaotenganishwa na maisha ya kila siku dhidi ya matakwa yao.
Source: DW