Putin hana budi kuchochea vita ili anusurike

Putin hana budi kuchochea vita ili anusurike

Uhamasishaji wa kijeshi Urusi na kura za haraka za maoni katika maeneo yanayokaliwa mashariki mwa Ukraine ni ishara za udhaifu.

Putin amekosea; gharama wanalipa maelfu ya Warusi kwa maisha yao.

Rais Putin hawezi kurudi tena nyuma: Na ikiwa atashindwa katika vita vyake vya uvamizi dhidi ya Ukraine, itamgharimu madaraka yake, na yumkini zaidi ya hayo. Hali iatkuwa hivyo kwa wawakilishi wa bunge la Duma, ambao hatma yao hivi imeunganishwa na ile ya mkuu huyo wa Kremlin.

Wote wako katika hali ya taharuki kufuatia mafanikio ya karibuni ya vikosi vya jeshi la Ukraine katika kurejsha maeneo ya nchi yao yaliokaliwa.

Hali inaitishia Moscow kushindwa kijeshi, jambo ambalo hakuna alielitarajia mjini Moscow. Kutokana na hofu hiyo, Putin ameamuru kuwekwa tayari wanajeshi laki tatu wa akiba kwa ajili ya kwenda uwanja wa vita.
Jukumu la wanajeshi hao litakuwa kuzuwia kasi ya vikosi vya Ukraine kusonga mbele zaidi.

Putin Amedhoofika na alietengwa.
Uturuki, India na hata China ziliweka wazi kwamba zinapinga vita vya Putin, zinaunga mkono uhuru wa mipaka ya Ukraine. Na zilikuwa sababu za msingi:

Vita hivyo ni mzigo kwa uchumi wa dunia na vivyo hivyo kwa mamlaka ya wanasiasa hao, ambao Putin alitumai kupata uungwaji wao mkono kwa ajili ya vita vyake.

Mabadiliko ya mwelekeo katika Kremlin
Kwa mtazamo wa Kremlin, mambo hayangeweza kuendela hivi. Hivyo mjini Moscow, Putin anaharakisha kubadili mwelekeo na hivyo ukusanyaji huo wa wanajeshi kwa sehemu ni kukiri juu ya udhaifu wa kijeshi mashariki mwa Ukraine.

Kwa matangazo ya kuitisha kura ndani ya siku chache katika maeneo yaliotekwa kuhusu kujiunga na shirikisho la Urusi, ni wazi kwamba wa Ukraine hawataki kujiunga na Urusi. Kwa sababu kura inayofanyika mbele ya mtutu wa bunduki, kura ya maoni katika magofu, hakuna yeyote duniani anaweza kuichukulia kwa uzito.

Putin anataka kupata mali zilizoporwa. Maeneo yaliotekwa yatakuwa sehemu ya shirikisho la Urusi. Kisha Putin anaweza kutoa wito wa kutetea taifa kwa kutumia nguvu za kijeshi. Kile kinachoitwa operesheni maalumu ya kijeshi, ambayo ina mipaka ya muda na nafasi na ambayo haikuhusika kwa vyovyote na maisha ya kila siku ya Warusi walio wengi, inageuka kihistoria utetezi wa ardhi ya Urusi kwa njia zote, ikiwemo silaha za nyuklia.

Mtu haitaji kuwa nabii mkuu kutabiri mwisho unaokaribia wa neno operesheni maalumu. Propaganda ya Kremlin italizika neno hilo. Badala yake, kutakuwa uongo zaidi na zaidi wa kipumbavu na kuchanganya, uzushi, vitisho ambavyo vituo vya televisheni vinavyodhibitiwa na serikali vitatumia kuwarubuni Warusi.

Hata sasa inadaiwa kuwa Urusi haifanyi vita dhidi ya Ukraine, lakini inanjitetea nchini Ukraine dhidi ya Marekani na Uingereza. Hilo wanaliamini wanaotaka kuamini.

Uchochezi mpya wa Putin utachuliwa kwa uzito na viongozi wa dunia wanaokutana hivi sasa katika hadhira kuu ya Umoja wa Mataifa mjini new York. Lakini sera yao kuelekea Moscow haitabadilika pakubwa. Kiev itaendelea kupokea silaha, jeshi lake litadelea kupambana. Na wanajeshi 300,000 wa akiba wa Urusi? Hawajawahi kuwa vitani, hawana zana za kutosha. Ni watu wenye familia, wanaume wanaotenganishwa na maisha ya kila siku dhidi ya matakwa yao.

Source: DW
Dw siwaamini sana,mtu ambaye anataka kuunganisha maeneo yaliyotekwa kuwa aridhi ya urus kwa kupiga kura ya maoni unasema ameshindwa vita,hata wakati anaichukua marioupaul tuliambiwa hawez anapigwa sna wakawa wanapost vifaa vilivyoharibiwa kanakwamba anapigika sana,lakin mwisho wa siku mkweli amejulikana
 
Una akili za kitoto sana, zile za ubabe na ubazazi wa enzi za shule ya msingi. Geopolitics sio rahisi kama hilo povu unalotoa hapa.
Andikeni hata nyuzi 600 per day, andikeni nyuzi ndefu zenye kuwafurahisha ila ukweli Ukraine amepoteza tena majimbo mengine kama ilivyo cremea. Kama kweli Ukraine na west ni wababe basi wayarudishe hayo majimbo, au waingie urusi kuchukua maeneo kama urusi anavyofanya. Hapa JF tutadanganyana mpaka mwisho.
 
Mkomunisti usizidiwe na mahaba kwa CCP, huo ndio UkweRiii, umezagaa kwenye vyombo vyote huru vya habari duniani.
Kuhusu Turkey, China na India Dw imeandika kichekesho[emoji38] na huo uchambuzi wote umeonekana wa hovyo.
Screenshot_20220922-114135_Twitter.jpg
20220922_114330.jpg
 
Usisijie habari ya vita,acha kabisa ukienda front ndo utajua vita ni nini.mpaka sasa unaweza ukakuta UKRAINE kapoteza mara 10 ya wanajeshi wa URUSI.maana mizinga tu aliyoitupa URUSI ndani ya ardhi ya UKRAINE ni za maelfu ya tani.

Hii vita unaona kama kuna ushindani ni kwa sababu ni vita kati ya URUSI VS (MAREKANI+NATO+UKRAINE).

UKRAINE imepoteza zaidi unavyojua wewe ila ndo iyo wakubwa wameamua kutuingiza kwenye mgogoro mwingine mkubwa.Hii vita ishakuwa ya pande mbili na pasipo kukaa mezani basi tutafika tu kwenye nuclear maana hakutakuwa na namna.URUSI awezi kukubali kushindwa na MAREKANI NA NATO
Wanajeshi wa Ukraine walikabiliana na majeshi ya Urusi tena wale wenye mafunzo kamili na uzoefu wa vita wakiwa na vifaa tele vya kijeshi tena wakiwa wameingia Kiev na wakawashinda tena kwa kishindo halaf ndo eti sasa wawaogope hao wa reserve ambao wengi wao sio full trained na hawana uzoef wa kutosha yaan jeshi la ukraine liogope jeshi la akiba? na mpaka urusi inatumia reserve ni kumaanisha urusi ana hali tete kwenye uwanja wa vita.
 
Usisijie habari ya vita,acha kabisa ukienda front ndo utajua vita ni nini.mpaka sasa unaweza ukakuta UKRAINE kapoteza mara 10 ya wanajeshi wa URUSI.maana mizinga tu aliyoitupa URUSI ndani ya ardhi ya UKRAINE ni za maelfu ya tani.

Hii vita unaona kama kuna ushindani ni kwa sababu ni vita kati ya URUSI VS (MAREKANI+NATO+UKRAINE).

UKRAINE imepoteza zaidi unavyojua wewe ila ndo iyo wakubwa wameamua kutuingiza kwenye mgogoro mwingine mkubwa.Hii vita ishakuwa ya pande mbili na pasipo kukaa mezani basi tutafika tu kwenye nuclear maana hakutakuwa na namna.URUSI awezi kukubali kushindwa na MAREKANI NA NATO
Na marekani na NATO pia hawawezi kukubalia na wenyewe
 
Haha wenye.mafunzo kamili sio wafungwa tena?? Mbona jamaa zenu wanalia mrusi kutumia wafungwa na majeshi ya kukodi
.....taarifa zenu wenyewe mnajipiga OG
Hapa kazungumzia wale paratroopers waliofyekwa kule Kyiv
 
Labda mori za kimasai.....jimbo lipi limerudi zaidi ya hivyo vijiji mrusi alivyoona hana haja ya kupigania sana,,,rudisheni hicho kipande kinachomegwa
Muda bado sana.., kwani urusi aliteka hizo sehemu kwa siku Moja,
 
Mkomunisti usizidiwe na mahaba kwa CCP, huo ndio UkweRiii, umezagaa kwenye vyombo vyote huru vya habari duniani.View attachment 2364482View attachment 2364483
Naomba unioneshe hotuba Xi Jinping akimwambia Putin aache kupigana Ukraine?

Note: China toka awali february ili pendekeza njia ya diplomacy [ mazungumzo ] kumaliza huu mgogoro ila sio hicho inacho fanya west kupeleka silaha Ukraine,hii toka mwanzo kabisa wa OP na msimamo wa China hauja badilika mpaka sasa umebaki kuwa huhu.
 
Dw siwaamini sana,mtu ambaye anataka kuunganisha maeneo yaliyotekwa kuwa aridhi ya urus kwa kupiga kura ya maoni unasema ameshindwa vita,hata wakati anaichukua marioupaul tuliambiwa hawez anapigwa sna wakawa wanapost vifaa vilivyoharibiwa kanakwamba anapigika sana,lakin mwisho wa siku mkweli amejulikana
Kura ya maoni na woga tu wa fashisti Putin baada ya kuona kichapo kinazidi kuwa kikali
Lakini Hilo halitayarudisha nyuma majeshi ya Ukraine..,ndio maana wao wanazidi ku-advance
 
Sawa yote hayo yalishaonekana kuwa ipo siku vita vya nuclear vitatokea wala haiwezi kuepukika.

Medvedev kasema kuwa silaha yoyote ile hata kama ni nuclear itatumika kwenye kulinda ardhi ya WARUSI ndani na UKRAINE.

Kama UKRAINE akiamua kukaza basi Nuclear aina budi kutumika kwenye hii vita
Na marekani na NATO pia hawawezi kukubalia na wenyewe
 
Hapa kazungumzia wale paratroopers waliofyekwa kule Kyiv
Wale mliosema mmeua wanajeshi elf 50 na kwamba hadi mwezi wa3 hapo mrusi atakua kaishiwa wanajeshi na vifaa na pia vikwazo vitamvuruga sana??
 
Una akili za kitoto sana, zile za ubabe na ubazazi wa enzi za shule ya msingi. Geopolitics sio rahisi kama hilo povu unalotoa hapa.
Kuweka picha ya Einstein kwenye avatar unadhani ndio akili? Wewe uliyesoma PHD una nini cha kunizidi? Kunya anye kuku akinya bata kaharisha.
 
Back
Top Bottom