Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini, Kim Yong-hyun, amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba wanajeshi sita wa Korea Kaskazini waliuawa katika shambulizi la makombora nchini Ukraine karibu na Donetsk mnamo tarehe 3 Oktoba.
Hii inakuja wakati ambapo mahusiano kati ya Pyongyang na Moscow yanazidi kuimarika. Korea Kaskazini imekanusha tuhuma za kusambaza silaha kwa vikosi vya Urusi vinavyopigana katika uvamizi wa Ukraine.
Kim alisema, "Tunaamini kuwa kuna uwezekano wa kuwa na majeruhi miongoni mwa maafisa na wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Ukraine, kutokana na sababu mbalimbali," na kuongeza kuwa Seoul inatarajia Pyongyang itatuma zaidi ya wanajeshi kusaidia juhudi za vita za Urusi.
Souce: Aljazeera