Putin kaishiwa? Ripoti zinasema Russia yatumia wanajeshi wa North Korea kupigana vita ya Ukraine!

Tunachojua Donbus yote unaenda,krunsk Ukraine kashatoka Sasa hizi report za loliondo Kwa Babu endeleeni nazoo
 
Hivi Ukraine mnaichukulia poa sana eenh.? Ile nchi sio under dog hata kidogo kwa kifupi ilikua vizuri sana kijeshi kabla haijaelemewa
Ukraine sio ya kuifananisha na Russia.
Fuatilia historia baina ya hayo mataifa mawili wamepigana mara ngapi kesha urudi hapa.
Au fuatili Crimea ilivyoporwa ndio utajua Urusi ina nguvu kiasi gani.
 
Kwani Urusi kwa nini asitumie Nyuklia kuwabomoa hao NATO na majeshi ya US wanao sumbua hadi leo!!? Majeshi ya Ukraine yameshaisha kitambo tu, hao wanaosumbua ni NATO na US ARMY, hao ni Nyuklia tu Mr Putin.
 
Urusi huwa hakubali hizi taarifa, hata alipoambiwa anatumia mercenaries alikataa. Ila kwa India tu tuliona namna Serikali ya India iliingilia kati na kufanikiwa kuwarudisha raia wake waliokua wanapigana upande wa Urusi.
 
Urusi huwa hakubali hizi taarifa, hata alipoambiwa anatumia mercenaries alikataa. Ila kwa India tu tuliona namna Serikali ya India iliingilia kati na kufanikiwa kuwarudisha raia wake waliokua wanapigana upande wa Urusi.
Jeshi lipo tofauti na nyinyi jinsi mnavyodhani.

Kuna kipindi Jwtz ilipeleka vijana wake kwenye mission moja vijana wetu waliuawa na sababu hawakuweza kutumia kiusahihi na kwa wakati silaha zao eneo la vita.

Jeshi mkishafanya mazoezi ni lazima mpelekwe kwenye mission yoyote ili lipimwe mazoezi waliyofanya silaha wanaouwezo wa kutumia hizo mbinu kwenye vita halisi? Ndicho kinachofanyika.

Russia jeshi lake ni kubwa na linajitosheleza. Kinachotokea washirika wake wanapeleka baadhi ya vikosi ili wapate uzoefu wa vita na mfano mwengine ni China.

China haijawahi kupigana urban warfare. Vita vya Ukraine ni urban warfare. Kinachofanyika China anapeleka baadhi ya vikosi vyake ili vipate uzoefu na uzoefu huo unapelekwa kwenye training kwa jeshi la China ili kuongeza mbinu kwa jeshi na mfano ikitokea wakaivamia Taiwan ili wafanye sweeping watapigana kwenye majengo na wanajeshi wa Taiwan.

Hao South korea kijeshi bado hawawawezi North Korea. Kuna mwaka meli ya kijeshi ya NK ilipoteza uelekeo na kuingia South Korea na waligoma kujisalimisha na meli yao ikatua nanga.

South Korea ilitumia nguvu kubwa kupambana na wanajeshi 50 wa NK zaidi ya wiki wanapambana nao. Mwishoni wanajeshi wa NK walijiua baada ya wengine kuuliwa kwenye mapambano kwa kuhofia kukamatwa wakiwa hai.
 
Huko huko Ukraine wamekufa wanajeshi kibao wa NATO
 
Halafu huyu ndie apigane na USA NATO? Mwenzie Israel anapigana na Nchi karibu 4 kwa wakati mmoja
Na wale wanajeshi wa Marekani zaidi ya 1k walienda kufanya nini huko Israel!?
 
Halafu huyu ndie apigane na USA NATO? Mwenzie Israel anapigana na Nchi karibu 4 kwa wakati mmoja
Acha utoto. Hata Israel inasaidiwa na USA, France, UK kwenye kuzuia mabomu ya Iran na hata kushambulia Houthi, Iran Proxies huko Syria na Iraq n.k
 
Asubuhi ya leo nimeona taarifa kupitia Azam tv kuwa US alitaka kuwawekea vikwazo Israel kuhusu vyakula vya misaada.
Kumbe misaada ya kibinadamu ilikuwa inatolewa kwa ajili ya Gaza Israel anazuia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…