Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mwanzoni Putin alionekana ni tishio zaidi kwa usalama wa nchi za Magharibi na Marekani, ila sasa anaonekana ni tishio pia kwa ustawi wa maisha ya watu katika mataifa haya(kiuchumi na kijamii) kupitia swala la gesi na hili halitomuacha salama.
Hili swala la gesi linaongeza sababu za mataifa haya kumuona Putin ni tishio kwa ustwai wa watu wao na pia kwa ustawi wa kiuchumi katika mataifa haya, hivyo lazima watafute namna ya kumshughulikia na ikibidi kumuondoa madarakani.
Unapoona Marekani kajiingiza mahal kijeshia au vinginevyo, basi ujue hapo kuna masilahi ya kiuchumi au sababu za kiusalama na hizi ndio sababu za Marekani kujiingiza katika mataifa ya Kiarabu na ikibidi hata kupigana vita waweke watawala ambao watakuwa vibaraka wao.
Kwa msingi huo, Putin kwa sasa lazima aondolewe kwa kutengenezewa fitina za kisiasa nchi mwake au kugombanishwa na wananchi wake kwa uchumi wa nchi yake kuvurugwa kupitia vikwazo, n.k.
Akiendelea kuwa kiburi huku akiendelea kutishia usalama na ustawi wa watu katika nchi hizi, basi atatafutiwa sababu kama zile za Saddam Hussein kuhalalisha uvamizi wa NATO na Marekani kumuondoa madarakani kwa gharama yoyote.
Kwa sasa mataifa haya yanaweza kuwa na mipango ya siri kumkabili Putin katika vita ya nyuklia ili kupunguza au kuondoa kabisa uwezekano wa Russia kutumia nyuklia au hata akizitumia, madhara yasiwe makubwa (wanawwza kumuwahi na kumvuruga kabisa au vinginevyo).
Wacha tusubiri.