PUTS 2-3......Ni Tsh. Ngapi wakuu........???

Kisaka80

Senior Member
Joined
Feb 4, 2012
Posts
151
Reaction score
94
Wakuu wana JF,


Naomba mnisaidie coz nataka kufanya maamuzi magumu lakini kinachotatiza ni hii PUTS 2-3 kuwa ni Tsh. ngapi. Kuna kazi ya Assistant lecture imetangazwa UDOM, mie sifa ninazo na ninataka kuomba hiyo job but kwa sasa nina job nyingine tena GVTS ambayo basic ni 954,000/= sasa nataka wataalamu mnishauri je kwa hiyo rate ya PUTS 2-3 ni sh.ngapi, na je hali ya maisha ya Dodoma kwa hiyo PUTS 2-3 inaweza mtu kukutoa kimasomaso na kusonga mbele?

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa mtakao weza nipa mwangajuu ya hili li-kitendawili langu.


Asante,kazi njema ndugu zangu.
 
Ngoja waje na mchanganuo wa hizi PUTS tupate faida wengi.
 
Kimbilia UDOM ndugu yangu hapo unachelewa kama una sifa ni vema utakwenda kuanza na PUTS 2 ambayo inaanzia sh. 1,549,000/= hii ilikuwa kabla ya nyongeza ya Kikwete ya mwezi July mwaka huu. Kwa hiyo inaweza kuwa imeongezeka kidogo, sina data kamili baada ya nyongeza.
 
@ Achengula,

ASANTE SANA MKUU KWA DATA ZAKO.

Pia Asante kwa ushauri mzuri.
 
Milllion moja na laki saba flani wakikukata makato yote unabakiwa kama na milion na laki mbili fln hivi.But nakushauri usiache kazi kwanza maana kuwa na sifa haitoshi wengi wana sifa sasa je utapata maana unaweza kukuta mpo mia tano wanatakiwa watu watano maana wasomi sasa ni wengi na usishangae wengine watatoka kwenye vyuo vingine kuja omba hapo ytayari wao watakuwa na advantage maaana wana uzoefu but nakushauri kama una sifa omba nafasi zaidi ya moja .Nakutakia mafanikio mema na mtangulize mungu katika hilo.Thenkyuuu
 
MKOBA2011


NAKUSHUKURU SANA KIONGOZI,

Nimepokea ushauri wako vema na nitajitahidi kuzingatia yote uliyoshauri mkuu.
 
Last edited by a moderator:
kalambe million hizo achana na laki tisa. (angalizo ni kwamba kwa vile utakuwa assistant lecturer kama ulikuwa unakula allowances nje ya mshahara wa laki tisa huko serikalini, Udom hicho kitu sahau utangoja mshahara from month end to another hakuna marupurupu mpaka utakapopata Phd ndo ukiwa mjanja utaanza kupata hela za research na consultancy. Labda uanze kupiga misele ya kufundisha vyuo vingine
 
sure, tazama mshahara wa sasa na benefits nyingine za kando kisha pima per month..unaweza kuta mbali na laki9 kuna viposho vinavyopatikanaga vikafika mpka mil1.5,
wkt ukifwata ya mil1.2 iyo ikawa haina rupurupu matokea tena kamshahara kanabana...all the best kaka, pima benefits kwanza nje ya mshahara..allowances zote, meals, transport, housing etc
 
Achana na hizo m+. Huku njaa tupu, wanafunzi 500+, usije ukajuta kwa nini uliacha hizo laki 9. Hakuna marupurupu, dili za kufundisha vyuo vingine tabu kupata tayari zina wenyewe, maisha dom yapo juu, nyama kg 5000, samaki wabich kg 6000. Sokoni ukiingia na laki unarudi na kapu lipo nusu. Nyumba kodi ipo juu. Kwa kifupi kama uan kazi usiache ukaja udom, utajuta bora tukwambie mapema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…