Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT

Mm ni mmoja wa wanaoweka uzito wa huku kuitwa home of thinkers, neno great mm nilishalitoa.
Ww ni mtupu kichwani, hapa tu niseme tuanze kujadili treasury bonds and treasury bills utakimbia
Kwani tujadili huko na wakati kuna hoja mezani imetolewa na NIPASHE? anzisha uzi wako wa treasury bonds and treasury bills tutakuja huko tumalizane na Mwigulu kwanza hizi ni kodi zetu
 
Utawezaje kuunga mkono jambo ikiwa hulielewi vizuri?
But comment yangu ililenga kukujibu uliposema huku sio fb, as if upo timamu sana wakati ww ni mweupe kichwani
 
Wewe kama damu imekurukia siyo mbaya tetetea ujangili wa mali za umma, sisi tunataka uchunguzi huru, kama hakuna upotevu mnaogopa nini uchunguzi huru? si ndiyo utawasafisha?
 
PUUZENI TAARIFA YA NIPASHE, HAKUNA UCHOTAJI FEDHA BOT, HUU NI MWENDELEZO WA KUZUA TAHARUKI KWA MAKUSUDI, BOT INASIMAMIA KWA UMAKINI SANA SHERIA ZA NCHI NA MIIKO YA BENKI KUU ZOTE DUNIANI.

Nimesoma taarifa hiyo ambayo inatokana na uchambuzi wa NGO iitwayo WAJIBU inayoongozwa na Mzee Ludovic Uttoh, CAG Mstaafu. Kwa ujumla maelezo ya taarifa hiyo yanaeleweka na hayana utata wowote, hivyo sijui kwa nini mwandishi wa Nipashe ameeleza kuwa KUNA UTATA BoT.

Taarifa imeelezea suala ambalo ni la kawaida na huwa linafanyika kila mwaka kutokana na Sheria ya BoT inayoruhusu kutoa advances or Short Term Loans kwa Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo yanakuwa hayajapata mapato. Kwa mujibu wa kifungu cha 34 hadi 37 cha BoT Act, Serikali inaruhusiwa kukopa hadi 18% ya makusanyo halisi ya ndani ya mwaka uliopita. HILI LIMEKUWA LIKIFANYIKA HIVYO TANGU BOT IANZISHWE, BOT NI BENKI YA SERIKALI, SERIKALI UCHUKUA ADVANCE KWA MUJIBU WA SHERIA BADALA YA KUKOPA KWA RIBA KUBWA KUTOKA BENKI ZA KIBIASHARA.

Hivyo, kwa mwaka 2022/23, Serikali ilikuwa inaweza kukopa BoT kiasi kinachofikia TZS. 4.5 trillion. Hivyo, taarifa ya kuwepo kwa mkopo wa TZS. 1.7 trilioni ni suala ambalo liko ndani ya wigo unaokubalika kisheria. Kiasi hicho kilipofika mwisho wa Mwaka kilijumuishwa kwenye Treasury Bonds za Mwaka husika ambazo zinaendelea kulipia riba kama sehemu ya mikopo ya ndani.

Utaratibu huo ni wa kawaida na ufanyika kwa Benki Kuu za nchi nyingi duniani, pindi Serikali inapohitaji Fedha za kugharamia Bajeti wakati bado inaendelea kujipanga na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali. Ndio maana hata IMF waliridhika kuwa BoT na Serikali wamezingatia Sheria na taratibu za kimataifa kama inavyotakiwa. Kutokana na uzingatiwaji wa Sheria hizo, Bodi ya IMF waliridhia kutoa USD. 300 milioni kwa mwaka 2023/24 na Benki ya Dunia waliridhia kutoa USD. 750 milioni kwa mwaka 2023/24 kwa kuwa tathmini ya Pili ya program ya IMF iliyofanyika Desemba 2023 iliangalia masuala mbalimbali yakiwemo ya mapato, matumizi, madeni, uzingatiwaji wa Sheria ya BoT, ukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, urari wa biashara, thamani ya shilingi na usimamizi wa masoko ya fedha nchini.

Kutokana na maelezo haya, nadhani mwandishi wa gazeti la Nipashe hakupaswa kusema kuwa kuna utata BOT tena bila hata kuulizia au kuomba ufafanuzi kutoka BoT. Inawezekana aliandika kwa nia ovu ya kuupotosha umma, kuidhalilisha BoT na kusababisha taharuki kwa jamii. Aidha, inawezekana mwandishi ameandika kwa kutojua Sheria suala ambalo angeuliza angepewa ufafanuzi unaotakiwa.

Kutokana na maelezo hayo, BoT itaandaa taarifa kwa umma na kukanusha na kutoa elimu kuwa hakuna utata wowote uliopo kutokana na taarifa hizo bali ni suala la kawaida ambalo Serikali inaruhusiwa kukopa kwa kuzingatia ukomo wa 18% ya mapato halisi ya mwaka uliopita, kama ilivyo kwa Sheria za nchi nyingine duniani. Hata ukomo huu upo kwenye viwango karibiana kati ya Nchi zote za EAC.

View attachment 3047891
Mh @Dk. Mwigulu Nchemba unaonaje Nipashe wakakanusha taarifa hii wenyewe? Manake wametupasha na tumepashika kisawasawa itabidi sasa watupooze manake tumepashika sana tunakaribia kuungua
 
Watanzania hatujawahi kuwa serious na Wala uwezekano wa kuwa serious hivi karibuni siuoni, nyie kuleni tu na vile kamba zimekatika........!
 
PUUZENI TAARIFA YA NIPASHE, HAKUNA UCHOTAJI FEDHA BOT, HUU NI MWENDELEZO WA KUZUA TAHARUKI KWA MAKUSUDI, BOT INASIMAMIA KWA UMAKINI SANA SHERIA ZA NCHI NA MIIKO YA BENKI KUU ZOTE DUNIANI.

Nimesoma taarifa hiyo ambayo inatokana na uchambuzi wa NGO iitwayo WAJIBU inayoongozwa na Mzee Ludovic Uttoh, CAG Mstaafu. Kwa ujumla maelezo ya taarifa hiyo yanaeleweka na hayana utata wowote, hivyo sijui kwa nini mwandishi wa Nipashe ameeleza kuwa KUNA UTATA BoT.

Taarifa imeelezea suala ambalo ni la kawaida na huwa linafanyika kila mwaka kutokana na Sheria ya BoT inayoruhusu kutoa advances or Short Term Loans kwa Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo yanakuwa hayajapata mapato. Kwa mujibu wa kifungu cha 34 hadi 37 cha BoT Act, Serikali inaruhusiwa kukopa hadi 18% ya makusanyo halisi ya ndani ya mwaka uliopita. HILI LIMEKUWA LIKIFANYIKA HIVYO TANGU BOT IANZISHWE, BOT NI BENKI YA SERIKALI, SERIKALI UCHUKUA ADVANCE KWA MUJIBU WA SHERIA BADALA YA KUKOPA KWA RIBA KUBWA KUTOKA BENKI ZA KIBIASHARA.

Hivyo, kwa mwaka 2022/23, Serikali ilikuwa inaweza kukopa BoT kiasi kinachofikia TZS. 4.5 trillion. Hivyo, taarifa ya kuwepo kwa mkopo wa TZS. 1.7 trilioni ni suala ambalo liko ndani ya wigo unaokubalika kisheria. Kiasi hicho kilipofika mwisho wa Mwaka kilijumuishwa kwenye Treasury Bonds za Mwaka husika ambazo zinaendelea kulipia riba kama sehemu ya mikopo ya ndani.

Utaratibu huo ni wa kawaida na ufanyika kwa Benki Kuu za nchi nyingi duniani, pindi Serikali inapohitaji Fedha za kugharamia Bajeti wakati bado inaendelea kujipanga na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali. Ndio maana hata IMF waliridhika kuwa BoT na Serikali wamezingatia Sheria na taratibu za kimataifa kama inavyotakiwa. Kutokana na uzingatiwaji wa Sheria hizo, Bodi ya IMF waliridhia kutoa USD. 300 milioni kwa mwaka 2023/24 na Benki ya Dunia waliridhia kutoa USD. 750 milioni kwa mwaka 2023/24 kwa kuwa tathmini ya Pili ya program ya IMF iliyofanyika Desemba 2023 iliangalia masuala mbalimbali yakiwemo ya mapato, matumizi, madeni, uzingatiwaji wa Sheria ya BoT, ukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, urari wa biashara, thamani ya shilingi na usimamizi wa masoko ya fedha nchini.

Kutokana na maelezo haya, nadhani mwandishi wa gazeti la Nipashe hakupaswa kusema kuwa kuna utata BOT tena bila hata kuulizia au kuomba ufafanuzi kutoka BoT. Inawezekana aliandika kwa nia ovu ya kuupotosha umma, kuidhalilisha BoT na kusababisha taharuki kwa jamii. Aidha, inawezekana mwandishi ameandika kwa kutojua Sheria suala ambalo angeuliza angepewa ufafanuzi unaotakiwa.

Kutokana na maelezo hayo, BoT itaandaa taarifa kwa umma na kukanusha na kutoa elimu kuwa hakuna utata wowote uliopo kutokana na taarifa hizo bali ni suala la kawaida ambalo Serikali inaruhusiwa kukopa kwa kuzingatia ukomo wa 18% ya mapato halisi ya mwaka uliopita, kama ilivyo kwa Sheria za nchi nyingine duniani. Hata ukomo huu upo kwenye viwango karibiana kati ya Nchi zote za EAC.

View attachment 3047891
Baada ya kuifilisi mifuko ya hifadhi ya jamii, sasa wamehamia BOT! Nchi ngumu sana hii.
 
Mkuu Ngali, Ngalikihinja , inaonekana huyu ni mtoto wa mama, hachelewi kususa na kuingia mitini, hivyo twende nae taratibu, kitendo cha kujitokeza in personal kuja kukanusha timely, kinastahili pongezi na ku boost jf profile, tumshukuru kwa hili, ametuheshimisha, nasi tumuheshimu, tusimchokoe sana tukampoteza tena, watoto wa mama huwa hawachelewi kususa na kuzira!.
P
hili nalo neno
 
Maelezo yako hayaendani na ulicho ambatanisha apo chini......

Unajua kuwa alama za mtu mnafiki ni tatu......!!

.....Mojawapo ni pale anapoaminiwa hufanya khiyana,
 
naona kuna gap hapo kati ya kuchotwa kutoka kwenye makusanyo na kuchotwa katika ukopaji.

mmekopa pesa,tunaomba transations,lakini ikisemekana easy kwa kujibu kuwa mmekopa na inaonekana kuwa hakuna taarifa ya kukopa hapo ni utata.
 
Back
Top Bottom