The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Hiyo habari iko kimkakati sana 😂Mheshimiwa ni akili ndogo tu kujua hizi heading za magazeti ni kwa ajili ya kuuza gazeti. Usisahau nipashe inahitajika ilipe mishahara, nssf, umeme, transport and other factory overhead costs.
Waandishi wetu hawa akina millard ayo na habari zao za kuset positive, brand awareness and expansion huwa hawako serious wala hawana data. Wao wanaandika tuu
Huyu mtu hapaswi kupewa maneno malaini anapaswa kuoigwa nyundo kwa hatua tuliyo fika kwa sasa iko iviii…. Ubaya ubwelaAsante sana kwa ufafanuzi huu, this is good!, well done!.
Niliwahi kushauri, dawa ya uongo ni ukweli, uongo ukisemwa bila kukanushwa hugeuka ukweli.
Nimependa jinsi ulivyojitokeza in person kujibu na kukanusha, nashauri ijengee uwezo ile idara yako ya gvt communications pale wizarani, uongo ukitolewa Nipashe, ukanushwe Nipashe huku jf iwe ni cc only.
Kiukweli I was very right about you tangu enzi zile Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa! ila yale maswali yangu, hujawahigi kuyajibu, kila nikikuuliza unayakwepa na unapotea jumla!, naomba nisiyarudie usije ukapotea tena, uwepo wako humu una thamani kubwa kwa maslahi ya taifa kuliko hoja personal unazokwepa kuzijibu.
Nimefarijika sana kukuona.
P
Tueleze pesa za kununua na kuendesha timu za mpira wa miguu za ligi kuu unazipata kwa mshahara gani?PUUZENI TAARIFA YA NIPASHE, HAKUNA UCHOTAJI FEDHA BOT, HUU NI MWENDELEZO WA KUZUA TAHARUKI KWA MAKUSUDI, BOT INASIMAMIA KWA UMAKINI SANA SHERIA ZA NCHI NA MIIKO YA BENKI KUU ZOTE DUNIANI.
Nimesoma taarifa hiyo ambayo inatokana na uchambuzi wa NGO iitwayo WAJIBU inayoongozwa na Mzee Ludovic Uttoh, CAG Mstaafu. Kwa ujumla maelezo ya taarifa hiyo yanaeleweka na hayana utata wowote, hivyo sijui kwa nini mwandishi wa Nipashe ameeleza kuwa KUNA UTATA BoT.
Taarifa imeelezea suala ambalo ni la kawaida na huwa linafanyika kila mwaka kutokana na Sheria ya BoT inayoruhusu kutoa advances or Short Term Loans kwa Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo yanakuwa hayajapata mapato. Kwa mujibu wa kifungu cha 34 hadi 37 cha BoT Act, Serikali inaruhusiwa kukopa hadi 18% ya makusanyo halisi ya ndani ya mwaka uliopita. HILI LIMEKUWA LIKIFANYIKA HIVYO TANGU BOT IANZISHWE, BOT NI BENKI YA SERIKALI, SERIKALI UCHUKUA ADVANCE KWA MUJIBU WA SHERIA BADALA YA KUKOPA KWA RIBA KUBWA KUTOKA BENKI ZA KIBIASHARA.
Hivyo, kwa mwaka 2022/23, Serikali ilikuwa inaweza kukopa BoT kiasi kinachofikia TZS. 4.5 trillion. Hivyo, taarifa ya kuwepo kwa mkopo wa TZS. 1.7 trilioni ni suala ambalo liko ndani ya wigo unaokubalika kisheria. Kiasi hicho kilipofika mwisho wa Mwaka kilijumuishwa kwenye Treasury Bonds za Mwaka husika ambazo zinaendelea kulipia riba kama sehemu ya mikopo ya ndani.
Utaratibu huo ni wa kawaida na ufanyika kwa Benki Kuu za nchi nyingi duniani, pindi Serikali inapohitaji Fedha za kugharamia Bajeti wakati bado inaendelea kujipanga na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali. Ndio maana hata IMF waliridhika kuwa BoT na Serikali wamezingatia Sheria na taratibu za kimataifa kama inavyotakiwa. Kutokana na uzingatiwaji wa Sheria hizo, Bodi ya IMF waliridhia kutoa USD. 300 milioni kwa mwaka 2023/24 na Benki ya Dunia waliridhia kutoa USD. 750 milioni kwa mwaka 2023/24 kwa kuwa tathmini ya Pili ya program ya IMF iliyofanyika Desemba 2023 iliangalia masuala mbalimbali yakiwemo ya mapato, matumizi, madeni, uzingatiwaji wa Sheria ya BoT, ukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, urari wa biashara, thamani ya shilingi na usimamizi wa masoko ya fedha nchini.
Kutokana na maelezo haya, nadhani mwandishi wa gazeti la Nipashe hakupaswa kusema kuwa kuna utata BOT tena bila hata kuulizia au kuomba ufafanuzi kutoka BoT. Inawezekana aliandika kwa nia ovu ya kuupotosha umma, kuidhalilisha BoT na kusababisha taharuki kwa jamii. Aidha, inawezekana mwandishi ameandika kwa kutojua Sheria suala ambalo angeuliza angepewa ufafanuzi unaotakiwa.
Kutokana na maelezo hayo, BoT itaandaa taarifa kwa umma na kukanusha na kutoa elimu kuwa hakuna utata wowote uliopo kutokana na taarifa hizo bali ni suala la kawaida ambalo Serikali inaruhusiwa kukopa kwa kuzingatia ukomo wa 18% ya mapato halisi ya mwaka uliopita, kama ilivyo kwa Sheria za nchi nyingine duniani. Hata ukomo huu upo kwenye viwango karibiana kati ya Nchi zote za EAC.
View attachment 3047891
Naunga mkono hojaModerator ingekuwa busara sana taarifa hii ingeambatana na hiyo taarifa inayokanushwa ya gazeti la NIPASHE pamoja na taarifa hiyo ya taasisi ya WAJIBU inayoongozwa na Ludovic Uttoh (CAG) wa zamani
Yeye anasema mnadanganya kwanini kumbi za harusi zinajaa na barabarani kuna namba E kibao.Ondoa tozo kwenye miamala na upunguze kodi iwe rafiki hapo ndio wananchi watapunguza taharuki,hali huku mtaani ni mbaya mno biashara ndogo zinakufa na watanzania wa kumudu milo 3 kwa siku wanazidi kupungua
Naibu wake atamjibiaTunaomba ujibu maswali kwenye huu uzi wako
Uvivu wako wa kusoma usiufafanishe na waziri weweSiamini unawaza sawa sawa kama wengine wanavyowaza
Kuweka post kwenye mitandao unayotumia ni ku-copy na ku-paste th
Ila comments unasoma moja moja, ww hiyo kazi ungeiweza? Usome waliocomment insta wote na uwajibu, usome Twitter na uwajibu na huku jf napo uwajibu
Uvivu wako wa kusoma utakufanya uwe chawa wa Viongozi na kumtetea kwani amekuambia ameshindwa kujibu au wewe ni katibu wake binafsiUmeandika pumba bila kujua hii amepost kote ambako ana account
Nilikusaidia kutumia akili kuwa hawezi kujibu sababu anatumia mitandao mingiUvivu wako wa kusoma usiufafanishe na waziri wewe
Uvivu wako wa kusoma utakufanya uwe chawa wa Viongozi na kumtetea kwani amekuambia ameshindwa kujibu au wewe ni katibu wake binafsi
MSawa
Rip Prof Malima
Rip Steven Kibona
Rip Dr Mgimwa
Kumbe mambo ya Fedha ni Magumu sana
Mkuu mbona hukuwataja nguli wegine kama Mr. Amir Jamal na Mr D. C. Msuya?Sawa
Rip Prof Malima
Rip Steven Kibona
Rip Dr Mgimwa
Kumbe mambo ya Fedha ni Magumu sana