Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT

Kwanza hongera kwa kazi Mheshimiwa waziri wa fedha. Angalau leo nimekuona huku. Naomba niende nje ya hii mada ya upigaji huko BOT! Hoja yangu ipo kwenye swala la mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Vigezo vilivyowekwa ni vya kibaguzi na vinatuumiza sisi wazazi wenye watoto wanaosoma vyuo binafsi.

Unakuwa na mtoto anasoma kozi ya kipaumbele kwenye mkopo lakini ananyimwa eti tu kwamba amesoma private tangu primary. Hivi mnajua jinsi wazazi tunavyojibana kusomesha watoto huko private?

Hiki Kigezo ni cha kibaguzi. Kama serikali inasema hela haitoshi kwanini isitoe mkopo kwa wanafunzi wote angalau upande wa pesa ya kujikimu tu ili wazazi wote tubaki tunakimbizana na ada? Au itoe mkopo wa asilimia 50 kwa wanafunzi wote bila kujali vigezo?

Liangalieni hilo Mheshimiwa! Cha kushangaza nyie viongozi watoto wenu wanapata hiyo mikopo pamoja na kwamba wamesoma shule za International. Mmeweka vigezo ili kuwadhibiti watoto wa wakulima wakati wa kwenu wananufaika!
 
Sielewi kitu kabisaa hiyo mikopo ya Matrilioni inaenda wapi? Mbona hali inazidi kuwa mbaya tu? Inasikitisha sana Morogoro Road usiku hakuna hata taa barabarani?
Angalieni na mahitaji muhimu ya Watanzania mbona kumekuwa na mifumuko ya bei hata kwa yale mahitaji ya muhimu? Vocha, sukari na vyakula vyote?
Duniani hapa sisi sote tunapita tu, zingatieni na vipaumbele kwa Wananchi wa kawaida.
 
Kaka Paskali,
Huyu muheshimiwa, angekuwa anarudi kujibu hoja. Kutuwekea tu mambo yake halafu watu wakimshushia nondo za kuonyesha ametuingiza chaka kiasi bila yeye kurudi na kujibu hoja za watu ni kuonyesha anadanganya sana.
Mkuu Ngali, Ngalikihinja , inaonekana huyu ni mtoto wa mama, hachelewi kususa na kuingia mitini, hivyo twende nae taratibu, kitendo cha kujitokeza in personal kuja kukanusha timely, kinastahili pongezi na ku boost jf profile, tumshukuru kwa hili, ametuheshimisha, nasi tumuheshimu, tusimchokoe sana tukampoteza tena, watoto wa mama huwa hawachelewi kususa na kuzira!.
P
 
Alafu anko na wewe unapenda sana kufata upepo. Deep inside you know all this is horse shit but hujaamua tu kua investigative journalist ili ukimpamba huyu jamaa uwe na ushahidi sio maneno ya sherehe kama hayo hapo juu.
I thought u would have set an example for younger journalists rather than just pampering someone
 
Wao husema "jibu la mjinga ni kukaa kimya" ukiona hivyo basi ni maswali ya wajinga, wao wenye akili hawawezi kujibu.
 
Akisusa watakula wengine Sina uhakika kama anaweza susa
 
Simply because amekuja inpersonal hapa JF, and so the minister is talking the truth?!!?? 😳😳
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…