Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT

Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT

ila we mzee naamini kabisa utaanza kuchomwa hapa hapa duniani yaani utaanza kuteseka hapa hapa duniani halafu kuzimu ni muendelezo tu
Hivi hizo hela mnazoiba hamuwaonei huruma watanzania?
Mamilioni ya watoto wa kitanzania wanasoma shule chakavu hapa nchini, huduma za afya ni ghali sana kwa mwananchi wa kawaida, mfumuko wa bei ni mkubwa sana kwa maisha ya Sasa, miradi lukuki inasuasua na kama inatekelezwa basi sio kwa wakati kwa sababu ya ufisadi, WIZI, uhujumu na ubadhirifu uliopitiliza uovu, lakini nyie mnaona sawa tu mateso ya watanzania kunufaisha matumbo yenu

MUNGU ninayemuamini ni mkuu sana hakika hataacha haya yapite katika JINA LA YESU KRISTU ALIYE HAI

kila kilichofichwa kitafunuliwa na hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe
Dr. Mwigulu Nchemba
 
PUUZENI TAARIFA YA NIPASHE, HAKUNA UCHOTAJI FEDHA BOT, HUU NI MWENDELEZO WA KUZUA TAHARUKI KWA MAKUSUDI, BOT INASIMAMIA KWA UMAKINI SANA SHERIA ZA NCHI NA MIIKO YA BENKI KUU ZOTE DUNIANI.

Nimesoma taarifa hiyo ambayo inatokana na uchambuzi wa NGO iitwayo WAJIBU inayoongozwa na Mzee Ludovic Uttoh, CAG Mstaafu. Kwa ujumla maelezo ya taarifa hiyo yanaeleweka na hayana utata wowote, hivyo sijui kwa nini mwandishi wa Nipashe ameeleza kuwa KUNA UTATA BoT.

Taarifa imeelezea suala ambalo ni la kawaida na huwa linafanyika kila mwaka kutokana na Sheria ya BoT inayoruhusu kutoa advances or Short Term Loans kwa Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo yanakuwa hayajapata mapato. Kwa mujibu wa kifungu cha 34 hadi 37 cha BoT Act, Serikali inaruhusiwa kukopa hadi 18% ya makusanyo halisi ya ndani ya mwaka uliopita. HILI LIMEKUWA LIKIFANYIKA HIVYO TANGU BOT IANZISHWE, BOT NI BENKI YA SERIKALI, SERIKALI UCHUKUA ADVANCE KWA MUJIBU WA SHERIA BADALA YA KUKOPA KWA RIBA KUBWA KUTOKA BENKI ZA KIBIASHARA.

Hivyo, kwa mwaka 2022/23, Serikali ilikuwa inaweza kukopa BoT kiasi kinachofikia TZS. 4.5 trillion. Hivyo, taarifa ya kuwepo kwa mkopo wa TZS. 1.7 trilioni ni suala ambalo liko ndani ya wigo unaokubalika kisheria. Kiasi hicho kilipofika mwisho wa Mwaka kilijumuishwa kwenye Treasury Bonds za Mwaka husika ambazo zinaendelea kulipia riba kama sehemu ya mikopo ya ndani.

Utaratibu huo ni wa kawaida na ufanyika kwa Benki Kuu za nchi nyingi duniani, pindi Serikali inapohitaji Fedha za kugharamia Bajeti wakati bado inaendelea kujipanga na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali. Ndio maana hata IMF waliridhika kuwa BoT na Serikali wamezingatia Sheria na taratibu za kimataifa kama inavyotakiwa. Kutokana na uzingatiwaji wa Sheria hizo, Bodi ya IMF waliridhia kutoa USD. 300 milioni kwa mwaka 2023/24 na Benki ya Dunia waliridhia kutoa USD. 750 milioni kwa mwaka 2023/24 kwa kuwa tathmini ya Pili ya program ya IMF iliyofanyika Desemba 2023 iliangalia masuala mbalimbali yakiwemo ya mapato, matumizi, madeni, uzingatiwaji wa Sheria ya BoT, ukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, urari wa biashara, thamani ya shilingi na usimamizi wa masoko ya fedha nchini.

Kutokana na maelezo haya, nadhani mwandishi wa gazeti la Nipashe hakupaswa kusema kuwa kuna utata BOT tena bila hata kuulizia au kuomba ufafanuzi kutoka BoT. Inawezekana aliandika kwa nia ovu ya kuupotosha umma, kuidhalilisha BoT na kusababisha taharuki kwa jamii. Aidha, inawezekana mwandishi ameandika kwa kutojua Sheria suala ambalo angeuliza angepewa ufafanuzi unaotakiwa.

Kutokana na maelezo hayo, BoT itaandaa taarifa kwa umma na kukanusha na kutoa elimu kuwa hakuna utata wowote uliopo kutokana na taarifa hizo bali ni suala la kawaida ambalo Serikali inaruhusiwa kukopa kwa kuzingatia ukomo wa 18% ya mapato halisi ya mwaka uliopita, kama ilivyo kwa Sheria za nchi nyingine duniani. Hata ukomo huu upo kwenye viwango karibiana kati ya Nchi zote za EAC.

View attachment 3047891
Siku moja inakuja, nyie endeleeni kuchuma na kufaidi na watoto wenu
 
Jamanii jamanii waja mna nongwa mnataka mpaka ndugu waziri ajute kuja Jf kuanzisha Uzi.
Mkuu Nuzu, Nuzulati , kiukweli baadhi ya wana jf sio wastaarabu kabisa, badala ya appreciation ya uwepo wake, wanataka kumkera, hata mimi nina hoja zangu kumhusu, kila nikimuuliza, humuoni tena!, baada ya kulijua hilo, simuulizi tena!, I just appreciate uwepo wake.
Tujifunze kuwa appreciative!.
P
 
Sambamba na taarifa za uzushi na za uwongo ila ukweli serikali imekuwa na matumizi mabaya na yasiyo na tija kiasi cha kupelekea kutolewa taarifa hizo, kama mnashindwa kujisahihisha basi tumieni kwa faragha tusione wala kusikia!
Mh waziri roho zinatuuma mno ila tunakosa cha kufanya ,ingawa wakati si wa milele.
Raisi Samia ndio Muasisi wa matumizi ya anasa Serikalini
 
Mkuu Nuzu, Nuzulati , kiukweli baadhi ya wana jf sio wastaarabu kabisa, badala ya appreciation ya uwepo wake, wanataka kumkera, hata mimi nina hoja zangu kumhusu, kila nikimuuliza, humuoni tena!, baada ya kulijua hilo, simuulizi tena!, I just appreciate uwepo wake.
Tujifunze kuwa appreciative!.
P
Yaani yeye kukanusha ufisadi wake tuna appreciate nini hapa
 
Ndio kama umekuja kututhibitishia tena hizi tuhuma nazo zinakaukweli fulani.

Unachanganya sana maelezo, umeeleweka mpaka hapo kwenye serikali inaweza kukopa short term loan, kufidia temporaryy budget short fall; kwa mujibu wa sheria.

Unapotuvuruga ni kusema short term loan (imegeuka kuwa ‘treasury bond), ambalo ni deni la muda mrefu mnalolipia riba. Na mkopo wenyewe mshaujumuisha kwenye deni la taifa.

Maana yake huo mkopo uliotakiwa kuwa wa (wa short term) kawaida muda wake ni maximum ya miezi 12 deni liwe limelipwa. Lengo likiwa kufidia temporary ‘budget shortfall’ mkipata makusanyo mrudishe hilo deni.

Mwaka umepita bado deni alijalipwa BoT mpaka leo. Sanasana mmeamishia kwenda kwenye long term debt; si ndio uchotaji wenyewe huo wa akiba kutoka BoT.
 
1721563531797.png
 
Muheshimiwa Dr. Mwigulu Nchemba, tatizo lako kubwa ni kwamba, huwa unaanzisha mada humu JF, na watu wakikushushia nondo kukuonyesha umetudanganya kiasi gani, huwa hurudi kujibu hoja. Unaingia mitini na kuanzisha uzi mwingine wenye uelekeo ule ule. Mwisho wa siku wenye akili tunajua tu UNATUINGIZA CHAKA..!!

Na kwa hili, NIPASHE wakiamua kwenda deep na kurudi na maushahidi, mtaishia kulifungia kama mlivyofanya kwa gazeti la motomoto bada ya kuripoti kuwa mmeuza Ngorongoro. Mlikana na mmiliki wa gazeti la motomoto bwana Stanley Katabalo, akauwawa.
Lilikuwa Gazeti la Mfanyakazi ambalo Stan Katabalo alikuwa ni mwandishi wake.Aliuliwa kwa Kufuatilia sakata la Loliondo Gate (OBC) ambayo leo wanamiliki Nchi ndani ya Tanganyika yetu.
 
Mkuu Nuzu, Nuzulati , kiukweli baadhi ya wana jf sio wastaarabu kabisa, badala ya appreciation ya uwepo wake, wanataka kumkera, hata mimi nina hoja zangu kumhusu, kila nikimuuliza, humuoni tena!, baada ya kulijua hilo, simuulizi tena!, I just appreciate uwepo wake.
Tujifunze kuwa appreciative!.
P
Pascal, kama kweli wamekopa kutoka BOT, una uhakika gani kuwa zimekopwa na kulekezwa kwenye matumizi yaliyokusudiwa?

Taarifa ya Nipashe ni vizuri pia tukaipata badala ya kusikia habari ya upande mmoja tu.
 
Yaani tunshukuru mtu kutimiza wajibu wake!
Hakika safari ni ndefu mno!
Tumshukuru kwa uwepo wake jf, Waziri kuingia jf na kujibu hoja sii miongoni mwa wajibu wake!, Waziri hawajibiki jf, hivyo uwepo wake humu ni ametuheshimu sana, turudishe heshima, Mawaziri zaidi waingie, juzi nimemuona Gerson Msigwa , hii ni heshima kubwa kwa jf, lets be appreciative.
P
 
Back
Top Bottom