Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT

Puuzeni taarifa ya Nipashe, hakuna uchotaji fedha BoT

Ni mimi sijaelewa
 

Attachments

  • Screenshot_20240721-152439_Chrome.jpg
    Screenshot_20240721-152439_Chrome.jpg
    255.7 KB · Views: 3
Nyinyi pakueni hela zote mzimalize, uzeni kila kitu, hamna haja hata ya kukanusha kitu. Watanzania wamewaachieni nchi muifanye vile mnapenda.
Wao hawahusiki na hii nchi, hii nchi ni yenu viongozi wote na familia zenu. Mali yenu fanyeni mnavyotaka iwe.
 
Ungekuwa ukishakanusha hapa Kisha unakuwepo tukiuliza maswali ingesaidia sana. Ila unaandika weeee Kisha unapotea sasa sijui ni dharau zako tu au nini sijui. Unahisi kwa kuwa una doctorate ya uchumi basi ukishasema kitu ni sharti tuelewe na tunyamaze fullstop!
Anakazi nyingi za kufanya jamanii bado na mitandao mingine huko anatakiwa akakanushe😀
 
Ukiunganisha Tanzanialink
Tumshukuru kwa uwepo wake jf, Waziri kuingia jf na kujibu hoja sii miongoni mwa wajibu wake!, Waziri hawajibiki jf, hivyo uwepo wake humu ni ametuheshimu sana, turudishe heshima, Mawaziri zaidi waingie, juzi nimemuona Gerson Msigwa , hii ni heshima kubwa kwa jf, lets be appreciative.
P
hatuhitaji kuwa appreciative. Hii ni forum kama nyingine tu. Iwe facebook, x, instargram. Wao kuwepo ni kuonesha hii forum ni muhimu ila sio wao ndio muhimu.
 
ila we mzee naamini kabisa utaanza kuchomwa hapa hapa duniani yaani utaanza kuteseka hapa hapa duniani halafu kuzimu ni muendelezo tu.

Hivi hizo hela mnazoiba hamuwaonei huruma watanzania?

Mamilioni ya watoto wa kitanzania wanasoma shule chakavu hapa nchini, huduma za afya ni ghali sana kwa mwananchi wa kawaida, mfumuko wa bei ni mkubwa sana kwa maisha ya Sasa, miradi lukuki inasuasua na kama inatekelezwa basi sio kwa wakati kwa sababu ya ufisadi, WIZI, uhujumu na ubadhirifu uliopitiliza uovu, lakini nyie mnaona sawa tu mateso ya watanzania kunufaisha matumbo

MUNGU ninayemuani ni mkuu sana hakika hataacha haya yapite katika JINA LA YESU KRISTU ALIYE HAI

kila kilichofichwa kitafunuliwa na hakuna jiwe litakalosalia juu ya jiwe
😀😀😀 ujue anasoma na kucheka haya maombi ya mwamposa😀😀
 
Hivi ina maana viongozi hata ule ubinadamu kidogo tu kwa wananchi hawana ? Huku tunachambwa kwamba kura zetu si kitu ukienda kule sijui mbuga ichimbwe madini hujakaa sawa miradi mingi inasua sua na kusimama sababu ya upigaji ,viongozi ni lazima mjue hawa hawa wananchi mnaowaona mazombie ipo siku watawashangaza ,

Najua mkikaa huko mnasema hakuna wa kutugusa nchi hii lakini angalie siku inakuja ,inauma sana kuna watu wanakufa nchi hii kwa kukosa paracetamol tu nyie hamuyaoni hayo mnatuona manyani
 
Hata Robot au AI huwa ni interactive yaani ukiuliza unajibiwa..., ndio maana nilisema sababu hatuna Jukwaa la Propaganda uzi za huyu jamaa zingepelekwa Jukwaa la matangazo sababu anachofanya ni kuleta propaganda na kujisafisha na kupoteza muda wetu kama walipa Kodi... Ni mwendo tu wa kutwambia tupuuze wakati logic inaniambia kama mwizi ni mwizi kweli ni vigumu kukubali kwamba ni mwizi (Hususan mwizi huyo kama tunampa nafasi ya kujibu tuhuma kwa kumuuliza maswali anakata kona)
 
1. Wizi wa ununuzi wa RADAR (BAE system co.) Madalali walipata £ 12,000,000

2. Wizi wa Amatus Liyumba katika Ujenzi wa B.O.T twin towers .. Shilingi Billioni 400

3. Wizi wa akaunti ya EPA Shilingi 133 billioni.

4. Wizi katika Mradi wa kusafisha dhahabu wa Mwananchi Gold .. Dola Milioni 6

5. Wizi wa Buhemba Goldmine (Meremeta) Shilingi Billioni 155

6. Upotevu wa Shilingi Trilioni 1.5

7. Tegeta Escrow Account Shilingi Billioni 306

8. Wizi wa kuprinti pesa BOT, Shilingi Billioni 104

9. Wizi wa Alex Stewart (Audit firm) Shilingi 221 Billioni.

10. Richmond scandal Shilingi Billioni 172

11. Loliondo Gate by Stan Katabalo

12. DP World, Mradi wa kuendeleza Bandari.

13. Viongozi hawana woga kwa sababu hawanyongwi.
😀😀😀 Atanyongwa na nani sasa wakati wanashirikiana na wanyongaji.
 
Asante sana kwa ufafanuzi huu, this is good!, well done!.

Niliwahi kushauri, dawa ya uongo ni ukweli, uongo ukisemwa bila kukanushwa hugeuka ukweli.

Nimependa jinsi ulivyojitokeza in person kujibu na kukanusha, nashauri ijengee uwezo ile idara yako ya gvt communications pale wizarani, uongo ukitolewa Nipashe, ukanushwe Nipashe huku jf iwe ni cc only.
Kiukweli I was very right about you tangu enzi zile Mwigulu Lameck Nchemba, Is The Most Genuine So Far!-Can Make The Best President!-Nimeguswa! ila yale maswali yangu, hujawahigi kuyajibu, kila nikikuuliza unayakwepa na unapotea jumla!, naomba nisiyarudie usije ukapotea tena, uwepo wako humu una thamani kubwa kwa maslahi ya taifa kuliko hoja personal unazokwepa kuzijibu.
Nimefarijika sana kukuona.
P
Umesoma upande mmoja umekuja na comment, kwa nini usisome na upande wa pili ujiridhishe? Then think critically!!
 
Back
Top Bottom