Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Acha kuamini hawa watu.Asante sana kwa ufafanuzi huu, this is good!, well done!.
Ukamsahau Daud Balali Makusudi au?Sawa
Rip Prof Malima
Rip Steven Kibona
Rip Dr Mgimwa
Kumbe mambo ya Fedha ni Magumu sana
Mtamchafulia skafu yake kwa kutokwa jasho jingi.Maana ninyi hamna dogo.Maswali utadhani mnaua nyati au mnamkamata mbojo.Ungekuwa ukishakanusha hapa Kisha unakuwepo tukiuliza maswali ingesaidia sana. Ila unaandika weeee Kisha unapotea sasa sijui ni dharau zako tu au nini sijui. Unahisi kwa kuwa una doctorate ya uchumi basi ukishasema kitu ni sharti tuelewe na tunyamaze fullstop!
Mbona ni kama taarifa inatolewa kwa hamaki, au kuna jambo limefichwa na serikaliPUUZENI TAARIFA YA NIPASHE, HAKUNA UCHOTAJI FEDHA BOT, HUU NI MWENDELEZO WA KUZUA TAHARUKI KWA MAKUSUDI, BOT INASIMAMIA KWA UMAKINI SANA SHERIA ZA NCHI NA MIIKO YA BENKI KUU ZOTE DUNIANI.
Sawa mkuu,PUUZENI TAARIFA YA NIPASHE, HAKUNA UCHOTAJI FEDHA BOT, HUU NI MWENDELEZO WA KUZUA TAHARUKI KWA MAKUSUDI, BOT INASIMAMIA KWA UMAKINI SANA SHERIA ZA NCHI NA MIIKO YA BENKI KUU ZOTE DUNIANI.
Nimesoma taarifa hiyo ambayo inatokana na uchambuzi wa NGO iitwayo WAJIBU inayoongozwa na Mzee Ludovic Uttoh, CAG Mstaafu. Kwa ujumla maelezo ya taarifa hiyo yanaeleweka na hayana utata wowote, hivyo sijui kwa nini mwandishi wa Nipashe ameeleza kuwa KUNA UTATA BoT.
Taarifa imeelezea suala ambalo ni la kawaida na huwa linafanyika kila mwaka kutokana na Sheria ya BoT inayoruhusu kutoa advances or Short Term Loans kwa Serikali ili kukidhi mahitaji ya matumizi ambayo yanakuwa hayajapata mapato. Kwa mujibu wa kifungu cha 34 hadi 37 cha BoT Act, Serikali inaruhusiwa kukopa hadi 18% ya makusanyo halisi ya ndani ya mwaka uliopita. HILI LIMEKUWA LIKIFANYIKA HIVYO TANGU BOT IANZISHWE, BOT NI BENKI YA SERIKALI, SERIKALI UCHUKUA ADVANCE KWA MUJIBU WA SHERIA BADALA YA KUKOPA KWA RIBA KUBWA KUTOKA BENKI ZA KIBIASHARA.
Hivyo, kwa mwaka 2022/23, Serikali ilikuwa inaweza kukopa BoT kiasi kinachofikia TZS. 4.5 trillion. Hivyo, taarifa ya kuwepo kwa mkopo wa TZS. 1.7 trilioni ni suala ambalo liko ndani ya wigo unaokubalika kisheria. Kiasi hicho kilipofika mwisho wa Mwaka kilijumuishwa kwenye Treasury Bonds za Mwaka husika ambazo zinaendelea kulipia riba kama sehemu ya mikopo ya ndani.
Utaratibu huo ni wa kawaida na ufanyika kwa Benki Kuu za nchi nyingi duniani, pindi Serikali inapohitaji Fedha za kugharamia Bajeti wakati bado inaendelea kujipanga na kukusanya mapato kutoka katika vyanzo mbalimbali. Ndio maana hata IMF waliridhika kuwa BoT na Serikali wamezingatia Sheria na taratibu za kimataifa kama inavyotakiwa. Kutokana na uzingatiwaji wa Sheria hizo, Bodi ya IMF waliridhia kutoa USD. 300 milioni kwa mwaka 2023/24 na Benki ya Dunia waliridhia kutoa USD. 750 milioni kwa mwaka 2023/24 kwa kuwa tathmini ya Pili ya program ya IMF iliyofanyika Desemba 2023 iliangalia masuala mbalimbali yakiwemo ya mapato, matumizi, madeni, uzingatiwaji wa Sheria ya BoT, ukuaji wa uchumi, mfumuko wa bei, urari wa biashara, thamani ya shilingi na usimamizi wa masoko ya fedha nchini.
Kutokana na maelezo haya, nadhani mwandishi wa gazeti la Nipashe hakupaswa kusema kuwa kuna utata BOT tena bila hata kuulizia au kuomba ufafanuzi kutoka BoT. Inawezekana aliandika kwa nia ovu ya kuupotosha umma, kuidhalilisha BoT na kusababisha taharuki kwa jamii. Aidha, inawezekana mwandishi ameandika kwa kutojua Sheria suala ambalo angeuliza angepewa ufafanuzi unaotakiwa.
Kutokana na maelezo hayo, BoT itaandaa taarifa kwa umma na kukanusha na kutoa elimu kuwa hakuna utata wowote uliopo kutokana na taarifa hizo bali ni suala la kawaida ambalo Serikali inaruhusiwa kukopa kwa kuzingatia ukomo wa 18% ya mapato halisi ya mwaka uliopita, kama ilivyo kwa Sheria za nchi nyingine duniani. Hata ukomo huu upo kwenye viwango karibiana kati ya Nchi zote za EAC.
View attachment 3047891
Naonewa mimi...naonewa mimi...naonewa sana!😂🙏Hii ndo ID yako nyingine ww mwendawazimu