Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Nimesikitika sana ,kuumia sana,kuhuzunika sana na kusononeshwa sana na taarifa za uongo,uzushi, uchonganishi na ufitini zilizoletwa humu jukwaani na mwana jukwaa zinazosema ya kuwa Mimi nimeteuliwa au kupewa nafasi ndani ya CCM.
Niseme ya kuwa taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wa aina yoyote ile hata chembe.nilijaribu kutoa ripoti kuwa mada na andiko lile lilikuwa la uongo na kuomba mada ile ifutwe lakini kwa bahati mbaya bila kujuwa sababu zake andiko halikufutwa.
Najuwa lengo la andiko lile lilikuwa ni kutaka kujenga taswira na kupandikiza mawazo na hisia Mbaya kwa wana jukwaa kuonekana kuwa naandika hapa jukwaani kwa kuwa nalipwa au nipo hapa jukwaani kwa kazi maalumu inayotokana na malipo,jambo ambalo siyo la kweli na halina ukweli wa aina yoyote ile.
Niseme tu ya kuwa mimi silipwi na mtu wala chama kuwepo hapa jukwaani .sipo katika malipo ya aina yoyote ile na wala sijawahi kulipwa kufanya kazi ya kuandika hapa jukwaani. Nafanya nifanyayo kwa hiyari yangu,kwa uzalendo wangu kwa Taifa langu,upendo na mapenzi makubwa kwa chama changu cha CCM, imani yangu kubwa na isiyopimika katika mzani wa aina yoyote ile kwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan pamoja na serikali yake.
Naandika kwa gharama zangu za muda,akili na pesa zangu mwenyewe.nanunua vocha kwa pesa zangu mwenyewe zinazotokana na jasho langu Mwenyewe. Kazi nayo fanya ni kazi ya kujitolea bure kabisa. Pamoja na matusi yote makubwa kwa madogo nayo tukanwa ,kejeli,kudhalilishwa na kutweza utu wangu bado naendelea kufanya kazi hii kwa kujitolea na kwa hiyari yangu Pasipo kuhitaji malipo zaidi ya kuusema ukweli tu.
Siwezi nikakaa kimya nikiona RAIS wangu anatukanwa au chama changu cha CCM kinashambuliwa au serikali yangu inachafuliwa au Taifa langu lina chafuliwa. Nipo tayari kutetea na hata ikibidi kusimama mwenyewe katika uwanja wa vita ya hoja bila matusi wala lugha ya udhalilishaji kwa wapinzani wangu.
Ndio Maana pamoja na kutukanwa matusi yote ,huwezi ukaniona nikimtukana mtu.
mimi najikita katika hoja na siyo matusi.ningekuwa najibu matusi basi ningekuwa nilishafungiwa humu jukwaani na kuwapa ushindi maadui zangu wanaotamani nipotee hata leo hii. Jambo ambalo limeshindikana kwa sababu nimeweza kuruka viunzi na mitego yao yote. Nimeishinda hofu na uoga na nimeishinda mitego ya maadui zangu. Nipo imara na tayari muda wote kuendelea na mapambano . Sirudi nyuma Zaidi ya kusonga mbele.
Wana CCM tusimame imara kuisemea na kuitetea serikali yetu na chama chetu.tutembee vifua mbele kwa sababu Rais wetu amefanya kazi kubwa sana zinazotupa nguvu ya kutembea vifua mbele na kueleza makubwa yaliyofanywa na serikali yetu na chama chetu.hakuna kukaa kinyonge wala kuogopa. Njooni uwanjani kishujaa ,ushindi upo upande wetu na watanzania wapo upande wetu.
Sisi ndio tumaini la watanzania,sisi ndio nuru ya Taifa hili,sisi ndio nyota ya matumaini.Tusimame pamoja kuwaunganisha watanzania na kuwaonyesha njia.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.