Pwagu na Pwaguzi.

Pwagu na Pwaguzi.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
1.Kwenye mwanzo wa tufani,si mvua huchonyota
Akili huwa ni fani,na dhamira kutusuta
Nalo dimba la zamani,huonekana kashata
Pwagu hupata pwaguzi,mchama ago hanyele.

2. Bubu yule hukumbukwa,jinsi tulivyomsuta
Kwa jinsi tunavyo nyukwa,gumba zetu zina juta
Kilobaki ni paukwa,nyumbu wagonga ukuta

Pwagu hupata pwaguzi,mchama ago hanyele.

3.Tatizo hanalo pwagu,pwaguzi kupewa nyota
Ndaro zinakua sugu,hadi nahisi twaota
Zao lilohama Pugu,wanga walishalichota
Pwagu hupata pwaguzi,mchama ago hanyele.

4.Mbali umeshazima,tunawasikia bata
Kumla tena mzima,utakua umedata
Huko umekata pema,na pabaya panakwita
Pwagu hupata pwaguzi,mchama ago hanyele.

5.Funga domo usiseme,ukakosa pakupita
Kisha upachikwe ndeme,uzione sita sita
Milihoi awatume,wakulima wa Morita
Pwagu hupata pwaguzi,mchama ago hanyele.

6.Mbwa wasio bweka,watakuja kumn'gata
Tebwere talaanika,sa njia ina matuta
Kiti hakito kalika,utapasuka ukuta
Pwagu hupata pwaguzi,mchama ago hanyele.

SHAIRI-PWAGU NA PWAGUZI.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom