Pwani kujitenga na Kenya

yahoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Posts
3,526
Reaction score
1,409
Eneo la Pwani nchini Kenya limetangaza mpango mkakati Wa kujitenga kutoka Kenya...madai yao ni kwamba wamepuuzwa na sana na serikali zote zilizotawala Kenya..so wanajipanga kwaajili ya kutekeleza mpango wao na watakuwa tayari kwa changamoto zote watakazokutana nazo pindi watakapoliamsha dude...source KTN news
 
Hahaa huku kenya hakuna FFU Eeeh yan mtu unaamka unajitangazia uburu wa eneo
 
Mzimu wa Catalonia umebisha hodi kwa jirani
 
Waje Tizee
 
Hiyo ndio faida ya mifumo ya majimbo.

Wasipokua makini kila jimbo litatanga kujitenga.

Wajitenge wajiunge na upande wetu tufanye kazi.
 
Niliona kwenye press yao wakisema kwamba wanatambua watakutana na mabonde, milima, jasho na damu lakini hatimaye watafanikiwa....ukizingatia eneo la Pwani wengi wao ni waislam, naanza kuogopa
 
Ifahamike vizuri kuwa ni Joho na Kingi wanaotaka kujitenga na Kenya wala sio wakaazi wa Pwani.
 
Ifahamike vizuri kuwa ni Joho na Kingi wanaotaka kujitenga na Kenya wala sio wakaazi wa Pwani.
Kichwa yako imejaa chang'aa na ukabila, kwa hiyo kila mtu mwenye mawazo tofauti na kabila lako basi unaona sio sawa, kwani Mombasa kudai kujitenga imeanza na Joho au King?, umesahau Mombasa Republican council (MRC) walivyokuwa wakilalamika wakauliwa karibu wote?, acha kuficha kichwa chako ndani ya kwapa, huo ndiyo ukweli, Kenya is a country with about 40 Nations, soon others will follow, stay tuned
 
Niliona kwenye press yao wakisema kwamba wanatambua watakutana na mabonde, milima, jasho na damu lakini hatimaye watafanikiwa....ukizingatia eneo la Pwani wengi wao ni waislam, naanza kuogopa
acha udini kengenge ww
 
Ifahamike vizuri kuwa ni Joho na Kingi wanaotaka kujitenga na Kenya wala sio wakaazi wa Pwani.
Movement ya mombasa Republican imeanza lini? Ile wanayosema pwani sio Kenya!
 
Hakuna secession itakayotokea hapa Kenya. Mtangoja sana Mkono uanguke kama vile fisi hungoja Mkono wa binadamu uanguke aule.
 
Yote hiyo nikupressure odinga apate hata kipisi cha mkate... Hahahaha.. Tatizo hawana numbers za kufanya hayo. Yatasalia maoni tu hayo
 
Hiyo ndio faida ya mifumo ya majimbo.

Wasipokua makini kila jimbo litatanga kujitenga.

Wajitenge wajiunge na upande wetu tufanye kazi.
na ndio maana huku tz CCM haitaki kusikia kabisa huo ujinga,hofu ni kuwa wakikubali hiko kitu pemba tunaisahau kaskazini napo tunaweza pata shida kuicontrol maana ina upinzani mkubwa na upinzani lazima watumie advantage ya majimbo kufanya wanayotaka ikiwepo na kujitenga.

ubaya wa kenya ni kuwa majimbo mengi yamegawanyika si tuu kisiasa bali kikabila zaidi,kwahiyo wakipanga kujitenga ni kabila zima linajitenga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…