Pwani: Mkazi wa Kibaha aomba kazi ya Kunyonga Watu

Pwani: Mkazi wa Kibaha aomba kazi ya Kunyonga Watu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1694870042832.png

Washiriki wa Mkutano wa haki jinai Kibaha, mkoani Pwani, wamejikuta wanabaki hoi baada ya mmoja wa wakazi mkoani humo, Ramadhani Mauridi, kueleza kuwa anatamani siku moja angeajiriwa na Serikali ili akafanye kazi ya kunyonga watu waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo.

Amesema kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na taarifa zinazoelezwa na vyombo mbalimbali kuwa ni zaidi ya miaka 10 sasa adhabu hiyo imekuwa haitekelezwi, huku matukio ya mauaji yakiendelea kushamiri nchini hivyo ni vema Serikali ifikie hatua ya kuliangalia hilo ikiwemo hata kuajri watu wenye roho ngumu kama yeye ili waifanye kazi hiyo.

"Haiwezekani mtu anaua kwa makusudi halafu anaenda kukaa gerezani miaka na miaka bila kunyongwa hilo haliwezekani, kama mtu amekutwa na hatia ya kuua naye anyongwe lakini siyo unasikia wengine wanaanza kusema haki za binadamu kwani yeye alipokuwa anaua alikuwa hajui kuwa kuna haki za binadamu? Amehoji mkazi huyo katika mkutano huo uliofanyika Septemba 15, 2023 mjini Kibaha.

Kwa upande wake Hawa John amesema kuwa wakati wajumbe wa haki jinai wakiendelea kufikisha mrejesho kwa jamii juu ya kasoro walizobaini kwenye maswala ya kisheria, suala la baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi kutowalinda watu wanaotoa taarifa za wahalifu linapaswa kuangaliwa ili kulinda usalama wao.

"Kuna baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wanapelekewa taarifa juu ya waharifu, lakini haohao askari wanawaambia waharifu kuwa asingekuwa fulani kutuambia, sisi tusingejua; sasa hilo ni hatari, ni vema sheria iwabane askari wenye tabia hiyo," amesema.

Mjumbe wa tume hiyo, Profesa Edward Hosea, amesema kuwa katika ufuatiliajj wao wamebaini kuwa sheria nyingi zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kulinda haki za wananchi.

"Hata utitiri wa majeshi unapaswa kuangaliwa na kuundiwa sheria upya kwani uwepo wake umekuwa ukileta hofu kwa jamii mfano kuna Jeshi la Zimamoto na Uokoaj na kazi yao kubwa ni kuzima moto, hawa wanapaswa kuwa taasisi tu na siyo kuwa kwenye mfumo wa jeshi," amesema.

Ameongeza kuwa hata majeshi yanayotumika kulinda misitu yasiwe kwenye mfumo wa kutumia silaha kwani hali hiyo inawatia hofu raia.

Mjumbe mwingine wa tume hiyo, Dk Laurean Ndumbaro, amesema kuwa kutosainiwa kwa adhabu ya kifo kwa watu wanaohukumiwa kutumikia adhabu hiyo kwa muda mrefu, kumesababisha uwepo wa mlundikano wa wafungwa wengi magerezani hivyo mapendekezo yao ni kuona utekelezaji huo unaangaliwa upya.

MWANANCHI
 
Hiyo nafasi iko wazi muda mrefu watu hatuna kazi kitaa , na mimi naomba hiyo nafasi ya kunyonga hasa mkinipangia kazi kanda ya ziwa ntajituma sana kazini
 
Kama hana kazi za kufanya mwambieni alete CV yake tumpe kazi.
Issue za kunyonga hazitamfikisha popote.
 
Ameongeza kuwa hata majeshi yanayotumika kulinda misitu yasiwe kwenye mfumo wa kutumia silaha kwani hali hiyo inawatia hofu raia.

Aliyetoa hii hoja ya kijinga nae ni Msomi?

Wanalinda misitu na silaha dhidi ya raia au majangili wenye silaha nzito kuzidi hata nguvu ya walinzi.
Mtoa hoja aje upya.
 
Hiyo tume si ilishamaliza kaz yake, Sasa hiz kampeni za kaz gani tena.
 
Amesema kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na taarifa zinazoelezwa na vyombo mbalimbali kuwa ni zaidi ya miaka 10 sasa adhabu hiyo imekuwa haitekelezwi, huku matukio ya mauaji yakiendelea kushamiri nchini hivyo ni vema Serikali ifikie hatua ya kuliangalia hilo ikiwemo hata kuajri watu wenye roho ngumu kama yeye ili waifanye kazi hiyo.
Matukio ya mauwaji yameshamiri huku adhabu ya kunyonga wanajidai hawawezi

Huyu Muuliza swali sijui kama hiyo Task Force imemwelewa.

Kama nimeelewa vizuri yuko sahihi.
 
Ni bora wenye hatia 100 kubaki hai, kuliko asiye na hatia mmoja kunyongwa
Cha ajabu under ccm regime mnyonge ananyongwa mafisadi wanabaki.
Ndio maana mwanachi wemye hasira kali kaomba hiyo kazi apewe.

Wanaonyonga na kuua watu wanaachwa wanakula maisha harafu mtanzania hohe hahe akikamatwa na Nyama ya Swala akitafuta kitoweo anafungwa Miaka 20
 
Arudishe Kadi ya Uanachama wa CCM tu hasira zote zitaisha.
Au, ainyonge Kadi hiyo na kuitupa ofisi ya CCM, manake atakuwa ameonyesha roho inayotakiwa kuwaondoa hawa mafisadi. Kuwa na roho Ngumu tu!
 
Back
Top Bottom