Uchaguzi 2020 Pwani: Mtu 1 mbaroni kwa madai ya kumteka mgombea Udiwani CHADEMA

Uchaguzi 2020 Pwani: Mtu 1 mbaroni kwa madai ya kumteka mgombea Udiwani CHADEMA

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mtu mmoja (jina linahifadhiwa) anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za kuhusika kumteka nyara mgombea udiwani kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Kerege Wilaya ya Bagamoyo, Martine Sultan.

kamanda.jpg


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 22, mwaka huu, katka Kitongoji cha Manofu, Kerege ambapo watu wanne wanaodaiwa kuwa wanaume, walimteka mgombea huyo.

Wankyo alisema baada ya jeshi hilo kupata taarifa, walifuatilia na kumkamata mmoja wa watuhumiwa hao akiwa katika Kijiji cha Janga, Mlandizi wilayani Kibaha.

Alisema mtuhumiwa huyo pamoja na mgombea udiwani, walikutwa katika eneo hilo wakitumia gari aina ya Toyota RAV4 (namba zimehifadhiwa).

Kwa mujibu wa Kamanda Wankyo, chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na kwamba watu wengine watatu bado hawajajulikana walipo.

Kamanda Nyigesa alisema upelelezi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwakamata watuhumuwa wengine watatu. aliomba mwananchi yeyote mwenye taarifa kuhusiana na tukio hilo, atoe ushirikiano kwa njia yoyote na vyombo vya dola.

Katika tukio lingine, Jeshi la Polisi linamshikilia Gale Salabo (32) mkazi wa Mafumbi wilayani Kisarawe kwa tuhuma za kumuua babu yake, Haima Nasri.

Kamanda Nyigesa alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 11:00 jioni katika eneo la Mafumbi. Alisema taarifa za awali zinadai kuwa mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kumtuhumu marehemu kuiba ‘sola panel’ yake.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Kituo Cha Afya Chole na mtuhumiwa anashikiliwa kwa mahojiano na upelelezi ukikamilika, atafikishwa mahakamani.


Ippmedia
 
Back
Top Bottom