LGE2024 Pwani: Watoto wa kidato cha kwanza wajiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, Wakuta wameandikiwa wana umri wa miaka 30 na kuendelea

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ccm wana vituko sana.
Sijui kwanini hawaiamini.
Kama ni kweli kuna huu ujinga kwanini wana taka uchaguzi? Si wakae hadi watakapo choka kuliko kutumia rasilimali zetu hovyo na kutupotezea muda kwa matokeo waliyo nayo mikononi?
 
Ujinga mwingi sana halafu wanatufanya sisi wananchi kama hatujielewi, Mungu huachia mabaya yatokee halafu atayaondoa yote. CCM wamekuwa wa hovyo sana sijui kwa faida ya nani na sijui wanapata nini?
 
Ccm ina matatizo sana. Kwahiyo tulioenda kujiandikisha kihalali wote ni wehu tu sasa.
 
Kama katiba mpya haijabadilika sitokuja kupiga kura ja familia yangu yote nimepiga marufuku...kunyanyua mguu kwenda kupiga kura na nina mpango wa kulazimisha ukoo mzima usipige kura...maana hakuna kitu itabadilisha.
 
Pwani si ndiyo top five ya uandikishaji? Kumbe waliandika na vitoto?
 
CHADEMA yatoa elimu ya namna ya kuwawekea pingamizi wapiga kura walioandikishwa kinyume cha sheria :


View: https://m.youtube.com/watch?v=bd6Cn59DG14
8. Sifa za Mpiga Kura
Mkazi yeyote atapiga kura endapo atakuwa na sifa zifuatazo:-
1. Awe ni raia wa Tanzania.
2. Ana umri wa miaka kumi na nane (18) au zaidi.
3. Awe ni mkazi wa eneo la Kitongoji, Kijiji au Mtaa husika.
4. Hana ugonjwa wa akili uliothibitishwa na Daktari anayetambulika
na Serikali au Bodi ya Utabibu.
5. Awe amejiandikisha kupiga kura katika eneo husika.


Kupoteza Sifa za Kupiga Kura
1. Mtu hatakuwa na haki ya kupiga kura kama hana mojawapo ya
sifa tano (5) zilizotajwa hapo awali.
2. Kama atakuwa amejiandikisha kupiga kura katika kituo zaidi ya
kimoja.

7. Mkazi ambaye amejiandikisha ana haki ya kukagua orodha ya
wapiga kura katika muda wa siku saba (7) tangu tarehe ya
orodha hiyo kubandikwa sehemu ya matangazo kwa lengo la
kuweka pingamizi kuhusu usahihi wa orodha hiyo au kuomba
orodha hiyo irekebishwe kwa kuongeza jina lake, kubadilisha
taarifa zilizo katika orodha hiyo au kufuta jina lililoorodheshwa
kwa vile aliyeorodheshwa amefariki.
 
7. Mkazi ambaye amejiandikisha ana haki ya kukagua orodha ya
wapiga kura katika muda wa siku saba (7) tangu tarehe ya
orodha hiyo kubandikwa sehemu ya matangazo kwa lengo la
kuweka pingamizi kuhusu usahihi wa orodha hiyo au kuomba
orodha hiyo irekebishwe kwa kuongeza jina lake, kubadilisha
taarifa zilizo katika orodha hiyo au kufuta jina lililoorodheshwa
kwa vile aliyeorodheshwa amefariki.
 
Kama ni kweli nawaonea huruma sana wanaofanya hivyo. Kwa mungu sio mbali. Ukifumba jicho utajuta kwanini umewafanyia hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…