Python Vs PHP Ipi inanifaa ? (All beginner's questions) Episode 1

Ndio mkuu upo sawa kabisa, Nakwakukazia JF aijasukwa from Scratch imetumia xenforo (Community Forum Platform) na app yake wametumia Taptalk. All in All xenforo ni php pure from scratch na database ni mysql.
 
Mada kama hizi husababisha watu walumbane utadhani vita vya kidini, mimi PHP ndio kula yangu kwa zaidi ya miaka kumi sasa, nimefanya miradi kwenye lugha nyingi, zingine hata sikumbuki syntax yake, ile tu mteja alisisitiza ufanywe kwenye hiyo lugha, ila mwisho wa siku huwa naangukia kwenye PHP.

Kwa miradi ya humu Afrika yaani Kibongo Bongo sijawahi kuona sababu za kuihama PHP, labda pale nikumbane na issue ambayo haiwezekani kabisa kwa PHP. Sasa utakuta mtu amekusanya analysis za kule uzunguni ambapo aina yao ya miradi iko level nyingine ya juu halafu ndio atatumia kuponda PHP humu.

Kijana yeyote ambaye unataka kupiga mzigo kwenye miradi ya Kiafrika, usipumbazwe hadi uepuke kuijua PHP, ifanye iwe base yako halafu hizi zingine hakikisha unazijua na kila moja umuhimu wake.....lakini nakuhakikishia hautakaa uepuke PHP. Kimsingi jifunze concepts za software engineering kiundani, namna gani unaweza kutumia mfumo kama Domain Driven Development (DDD) mpaka utengeneze system yako iliyotulia na kuwa portable baina ya frameworks.
 
mathsjery anapendaga sana kuiponda PHP na kuipa promo Python.

Namshaanga kweli...

Wakati PHP ndio inatuweka mjini wadau.
Ulisikia wapi?
Sasa AI na ML tufanye kwa PHP?, Labda tumeweuka mimi PHP ndo mother language na naitumia kila siku na hata sasa naandika php hapa.

PYTHON naitumia kwa data science na pia Nina mradi WA watu hapa

Hayo mashindano niweke hapa nikumbuke vizuri?
 
Mi mwenyewe programming ya kwanza kujifunza ni PHP Kisha nikapiga java

Leo hii (10/8/2021) mtu akiniuliza kati ya PHP na Python, nkamwambia ajifunze tu python sabab php market yake ni ndogo these days, hata ukiingia sokoni unakuta wanatakiwa developers Wengi Sana wa python kuliko php (kwa research niliyofanya Kati ya developer 10 wakitafutwa, 2 wa php basi washatafutwa 8 wa Python)
 
Acha uongo we jamaa...
PHP market yake ni ndogo?
 
Sijui kwann hizi mada huwa zinakuwa fupi, yaani sio siri kwa ma developer vitu kama hivi ndio tunatakiwa tuvione sana kwenye hili jukwaa
 
We keyboard worries kwann wasema php market yake ni finyu sana hapa TZ????
 
Me nadhani si suala lakulinganisha programming language ndio mana kila leo watu huvumbua language mpya ili kutafuta ubora zaidi lakini php na python zote zina utofauti kutokana na kazi husika na muda mwengine mtu anaweza asione thaman ya kitu husika kwakua tu hakipendi kitu hicho ila kwa uhalisia zaid kitu muhimu ni customer requirements maana unaweza kuivaa kwenye python au php halafu mteja anataka ufanye kazi yake kwa .Net
 
Kama target yako ni Tanzania pekee basi market ipo kwa PHP ila Kama target ni kuwa international, jifunze tu python, kama wewe ni programmer Anza kutafuta kazi za programming za nje (remote works) alafu uje tena
Market ipi hio unayoizungumzia?
Ya Data science au?
 

Hakuna python syntax yenye dollar sign kwenye variable declaration
 
Na C++ v/s python au C++ v/s php?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…