Python Vs PHP Ipi inanifaa ? (All beginner's questions) Episode 1

Python Vs PHP Ipi inanifaa ? (All beginner's questions) Episode 1

Asee kwenye point ya community naomba nikupinge kidogo

Ukifanya tafiti nyepesi ktk dev community kuanzia youtube, quora, insta,twitter utagundua kuwa kwa sasa python ina watu wengi(i.e wanaojifunza na wanaofundisha)

Sababu mara nyingi kwanini python inapendwa kuliko php au lugha nyingine utakutana na swala la urahisi wa syntax yake,binafsi sijasoma python ila nimefanya php college coz ndo kama lugha vyuo vingi wanafundisha ila ukisikiliza developers wengi wa kwenye mtandao wanarecommend python wakida ni beginner friendly mpaka imefika hatua kwa sababu ya wepesi wa syntax yake imekuwa lugha inayofata baada ya HTML(i.e not programming language) kwa wepesi kulingana na maoni ya wengi

kuhitimisha nakubaliana na wewe kuwa issue sio language ipi nyepesi au ugumu ila kikubwa ni product gani unataka kutoa then hiyo ndo inaweza kupa ni tool gan utembee nayo. Ila ukweli ni kuwa PHP ni king katika web I guess hata JF backend PHP imehusika
Ndio mkuu upo sawa kabisa, Nakwakukazia JF aijasukwa from Scratch imetumia xenforo (Community Forum Platform) na app yake wametumia Taptalk. All in All xenforo ni php pure from scratch na database ni mysql.
 
Mada kama hizi husababisha watu walumbane utadhani vita vya kidini, mimi PHP ndio kula yangu kwa zaidi ya miaka kumi sasa, nimefanya miradi kwenye lugha nyingi, zingine hata sikumbuki syntax yake, ile tu mteja alisisitiza ufanywe kwenye hiyo lugha, ila mwisho wa siku huwa naangukia kwenye PHP.

Kwa miradi ya humu Afrika yaani Kibongo Bongo sijawahi kuona sababu za kuihama PHP, labda pale nikumbane na issue ambayo haiwezekani kabisa kwa PHP. Sasa utakuta mtu amekusanya analysis za kule uzunguni ambapo aina yao ya miradi iko level nyingine ya juu halafu ndio atatumia kuponda PHP humu.

Kijana yeyote ambaye unataka kupiga mzigo kwenye miradi ya Kiafrika, usipumbazwe hadi uepuke kuijua PHP, ifanye iwe base yako halafu hizi zingine hakikisha unazijua na kila moja umuhimu wake.....lakini nakuhakikishia hautakaa uepuke PHP. Kimsingi jifunze concepts za software engineering kiundani, namna gani unaweza kutumia mfumo kama Domain Driven Development (DDD) mpaka utengeneze system yako iliyotulia na kuwa portable baina ya frameworks.
 
mathsjery anapendaga sana kuiponda PHP na kuipa promo Python.

Namshaanga kweli...

Wakati PHP ndio inatuweka mjini wadau.
Ulisikia wapi?
Sasa AI na ML tufanye kwa PHP?, Labda tumeweuka mimi PHP ndo mother language na naitumia kila siku na hata sasa naandika php hapa.

PYTHON naitumia kwa data science na pia Nina mradi WA watu hapa

Hayo mashindano niweke hapa nikumbuke vizuri?
 
Mi mwenyewe programming ya kwanza kujifunza ni PHP Kisha nikapiga java

Leo hii (10/8/2021) mtu akiniuliza kati ya PHP na Python, nkamwambia ajifunze tu python sabab php market yake ni ndogo these days, hata ukiingia sokoni unakuta wanatakiwa developers Wengi Sana wa python kuliko php (kwa research niliyofanya Kati ya developer 10 wakitafutwa, 2 wa php basi washatafutwa 8 wa Python)
 
Mi mwenyewe programming ya kwanza kujifunza ni PHP Kisha nikapiga java

Leo hii (10/8/2021) mtu akiniuliza kati ya PHP na Python, nkamwambia ajifunze tu python sabab php market yake ni ndogo these days, hata ukiingia sokoni unakuta wanatakiwa developers Wengi Sana wa python kuliko php (kwa research niliyofanya Kati ya developer 10 wakitafutwa, 2 wa php basi washatafutwa 8 wa Python)
Acha uongo we jamaa...
PHP market yake ni ndogo?
 
Sijui kwann hizi mada huwa zinakuwa fupi, yaani sio siri kwa ma developer vitu kama hivi ndio tunatakiwa tuvione sana kwenye hili jukwaa
 
Mi mwenyewe programming ya kwanza kujifunza ni PHP Kisha nikapiga java

Leo hii (10/8/2021) mtu akiniuliza kati ya PHP na Python, nkamwambia ajifunze tu python sabab php market yake ni ndogo these days, hata ukiingia sokoni unakuta wanatakiwa developers Wengi Sana wa python kuliko php (kwa research niliyofanya Kati ya developer 10 wakitafutwa, 2 wa php basi washatafutwa 8 wa Python)
We keyboard worries kwann wasema php market yake ni finyu sana hapa TZ????
 
Me nadhani si suala lakulinganisha programming language ndio mana kila leo watu huvumbua language mpya ili kutafuta ubora zaidi lakini php na python zote zina utofauti kutokana na kazi husika na muda mwengine mtu anaweza asione thaman ya kitu husika kwakua tu hakipendi kitu hicho ila kwa uhalisia zaid kitu muhimu ni customer requirements maana unaweza kuivaa kwenye python au php halafu mteja anataka ufanye kazi yake kwa .Net
 
Kama target yako ni Tanzania pekee basi market ipo kwa PHP ila Kama target ni kuwa international, jifunze tu python, kama wewe ni programmer Anza kutafuta kazi za programming za nje (remote works) alafu uje tena
Market ipi hio unayoizungumzia?
Ya Data science au?
 
Unaweza ku quantify hii statement na namba? Wangapi wako kwenye PHP na Wangapi Python?


Hakuna namna ya kujua Python inapendwa kuliko PHP. Ni vigumu sana kwa sababu hakuna collected statistics.


Hapa kuna misconception.
Syntax ya Py sio nyepesi hata. Kuandika if statement kwenye Python na PHP
Code:
if($x == 2)
   {
echo 'it Works';
}

Code:
if $x == 2:
echo 'it Works';

Hapo PHP itafanya kazi ila Python hola! Python iko so strict na ni unnatural kwa watu wengi ambao wana background ya C-Like languages. Hii inaifanya isiwe beginner friendly since dominant languages ni C-Like.

Ila Python inapendwa mashuleni kwa strict syntax yake ambayo inaifanya iwe nzuri kufundishia discipline kwa wanafunzi na beginners. Once ukiitumia Python, kuandika code vizuri inakuwa sehemu ya maisha yako. Pili ukiisha ielewa vyema unaweza kuandika code fupi. Plus ina modules za kutosha!


Yeah, that is the bottom line. Right tool for the right Job. When two languages does the same thing, the key is preference!

Hakuna python syntax yenye dollar sign kwenye variable declaration
 
Hello Tech members

Moja kati ya maswali yanayojirudia rudia sana kwenye ulimwengu wa Teknolojia ni "Nijifunze kipi Kati ya Language Y na Language X
Au kati ya Framework Y na Framework X?"

Kwa beginner, hii ni dilemma ambayo hana hakika njia ipi ni salama au sahihi kwake

Kwenye Web programming,hata wakati naanza kujifunza hili swali lilikua linanitesa sana
Kati ya Python na PHP ipi nijifunze, au ipi inafaa kutumika kwenye Web Programming

Ku make story short.........Kwa mda sasa Natumia PHP kama backend language kwa Project yoyote ya Client wangu
So kama bado wewe ni beginner na unataka kuwa Web au App developer, ila huna hakika ni Language ipi utumie kati ya hizo

Huu ni ushauri wangu
Ukiwa katika Dilemma yoyote ya namna hii kwenye Programming, kumbuka kwanza kitu kimoja

Programming Language is just a tool
Program yoyote iliyoandikwa kwenye Language fulani,inaweza kuandikwa kwenye Language nyingine (Ignore Runtime, Memory usage au Urahisi wa kuiandika)
So hakuna kitu Special kwenye Python ambacho hakipo kwenye PHP

So Program yoyote ile unayoweza kuifikiria, au Algorithm yoyote iliyowahi kuandikwa inaweza kuandikwa kwenye Language yoyote ile
Hii concept kwenye Computer Science, tunaita Turing Completeness

Tuje kwenye Swali la msingi, Kwanini Nimechagua PHP badala ya Python

  1. Market Share
    80% ya websites zote duniani zimeandikwa kwa kutumia PHP
    All major web servers zina support PHP
    Hii maana yake nini? ni kwamba kuna chance kubwa ya kumpata Client anayetafuta PHP Developer kuliko Client anayetafuta Python Developer

    Wordpress, ambayo ni popular Content Management System imeandikwa kwa kutumia PHP
    So kwa urahisi wa kupata Client au Ajira, PHP kwangu ni winner

  2. Community
    Hapa sina haja ya kuandika sana,PHP ina Community kubwa kuliko Python
    Hii maana yake ni nini? ni rahisi sana kupata Solution ya codes za PHP kuliko Python pale unapo kwama

  3. Framework
    Python ni rahisi, ina elegant syntax zinazopendeza kuliko PHP lakini nilipojifunza Django ambayo ni popular Web Framework
    Kwa Python Developer I have to admit, sikuipenda
    Haina Developer Experience nzuri niki compare na Laravel
    To be honest, zijaona mpaka sasa Framework yenye Pattern na Structure inayoeleweka kama Laravel

  4. Speed
    PHP imepitia Modifications nyingi mpaka kufikia sasa (PHP 8)
    Na hizo modifications zime boost sana Speed ya PHP
    Kitu ambacho ni nadra sana kwa Python developer ku kwambia ni kwamba, speed ya PHP ( kwanzia version 7)
    Ni mara tatu ya Python
    Means Project yoyote iliyoandikwa kwa PHP ina run mara tatu haraka ya Project yoyote ya Python
    Just chukua Algorithm yoyote, mfano Bubble sort (ambayo ni very slow) then implement kwenye language zote uone tofauti kwenye
    Performance
    View attachment 1881269

Mwisho tambua kuwa PHP na Javascript ni languages mbovu in terms of Design ila cha muhimu sio hicho
Python ni nzuri in terms of Syntax na design ila cha muhimu sio hiki pia

Unaweza kuandika Codes mbaya kwenye Python vile vile unaweza andika Codes nzuri kwenye PHP,issue ni Mindset

Kwa ushauri kuhusu Tech,au Web development
Contact : 0748333586
View attachment 1881276

Credit kwa kaka Stefano Mtangoo
Hivi ni baadhi ya vitu unique kuhusu Python ambavyo sikua navijua before sijajua kwa PHP


Hivi ni baadhi ya vitu Python inavyo ila PHP haina
1. PHP haiwezi kuwa embeded kwenye C++ na pia kui plug Python kwenye C++ haiwezekani. Unaweza kuandika C extension ya PHP na kui register kwenye ini but ni process tedious kuliko kutumia Python. Python ilitengenezwa ikiwa na extensibility upfront!

2. PHP haiwezi kutumika kwenye data analysis. Sio kwa sababu hiwezi kufanywa ikawa, ila from design PoV haikuwa designed kwa ajili hiyo. Hakuna libraries na tools za kufanya extensive data analysis kama Python na Py tayari ni de-facto kwenye data science.

3. PHP Haiwezi kutengeneza purely Desktop app. Unaweza kufinyanga PHP ikatoa desktop app kama wxPHP au PHPGTK lakini Python inafanya hili kwa urahisi. Hii ni kutokana na architect za Interpreters ambapo ni rahisi ku ship Py interpreter kuliko PHP interpreter, Plus PHP itahitaji container server.

Haya ni baadhi ambayo PHP haiwezi kufanya. Of course Py ina yake ambayo haiwezi kufanya au ni ngumu kufanya ilhali kwa PHP ni
breeze!

Kuhusu Speed ya PHP Vs Python
Na C++ v/s python au C++ v/s php?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom