Q Chillah anahitaji msaada gani?

Q Chillah anahitaji msaada gani?

Q-Chillah bado ana nafasi kubwa kimuziki. Inabidi asome soko linataka nini kwasasa na aendane nalo.
Pia ashirikishe vijana wanaotamba kwasasa kama Asley, Baraka Da Prince, Dogo Janja n.k.
Ila asiwashirikishe Vijana wa WCB. Hao wameishatengwa na Media hawatomfikisha popote.
wametengwa na media but hawajatengwa na jamii
 
Akamuombe msamaha QS mhonda, sitasahau yale maneno q chief aliyokuwa anamtupia QS kwenye kipindi cha friday night EATV.

QS alimdhamini na kumfadhili pesa nyingi mpaka jamaa kurudi tena na kwenda kutoa video south na Adam Juma ila QChief alijiona mjanja na dharau zile alizoonesha siku ile sijui kama jamaa anaweza kufanikiwa kwenye muziki.


Aende kulima kwao Muheza
 
Namsikiliza Msanii Q Chillah Muda Huu, Sielewi hata Anataka Nini? Huruma Ya Watu Ama? Kuacha Muziki mbona ni Mambo ya Kawaida Sana! Wengi Wameacha, Aache Kulia Lia
Kinacho mgharimu ni mkataba alio usitisha na yule Engenieur aliye anza naye kazi kwa kumdhamini ilikuwa ni kosa kubwa sana, Q Chillah alisikiliza ushauri mbaya wa watu eti ameshakua ajitegemee na kudai engenieur ana mnyonya familia nayo ikaingilia kati kuwa alisaini mkataba mbovu. sasa asilalamike akubaliane na matokeo ya ushauri mbaya maana alivunja mkataba ina mgharimu sasa.
 
Namsikiliza Msanii Q Chillah Muda Huu, Sielewi hata Anataka Nini? Huruma Ya Watu Ama? Kuacha Muziki mbona ni Mambo ya Kawaida Sana! Wengi Wameacha, Aache Kulia Lia


Wasanii wa bongo fleva wanachosha sana. Serikali inabidi iwakamate na kuwaweka jela tu.
 
Sawa tu,watu wanakula vumbi mitaani mixer jua kali na bado mambo magumu..yeye anakuja kulialia kuhusu kusaidiwa
Duu hii hatari sana wamrejee mungu wawoo ndiyo lililobaki....na siyo kuomba msaada Mwenye msaada nimungu pekee yakee...
Ujue hawa jamaa baadhi yao wakiwaga kwenye mafanikio wanakuwa na dharau hata ndugu wanatengananao ndo maana wengi wao wakikosa soko wanatamani wangezaliwa wanawake ili waolewe!
 
Huyu si ndiyo alimtungia wimbo baba yake mzazi kuwa anamfuatafuata baada ya kuona yeye AMEKUWA TAJIRI!!?
Nimekumbuka Mkuu:
"Si ulinizaa wewe ukanikataa (baba) Sasa iweje unaona mi nafaa.
Si ulinizaa wewe ukanikataa(baba) Sasa iweje unaona mi nafaa
...."
 
Chillah alisikiliza ushauri mbaya wa watu eti ameshakua ajitegemee na kudai engenieur ana mnyonya familia nayo ikaingilia kati kuwa alisaini mkataba mbovu
Na hapa ndio wasanii wengi wanaumia. Wanasahau kuwa Anaekudhamini/Meneja nae hua anaingia gharama za kukutangaza pamoja na gharama zingine kama malazi, usafiri -wakienda kufanya maonyesho. Wanasahau kuwa huko kukua pia ni juhudi za mdhamini/meneja!!
 
Mbona kuna wasanii walikaa miaka mingi na bila kufanya vizuri..yeye ajipange tu sahizi...

Akae akijua sahizi mziki mzuri tuna sikiliza gheto mziki wa drama ndo huo tuna uwita hit song... achague afanye mziki upi

Sent from my SM-G530H using JamiiForums mobile app
 
Q-Chillah bado ana nafasi kubwa kimuziki. Inabidi asome soko linataka nini kwasasa na aendane nalo.
Pia ashirikishe vijana wanaotamba kwasasa kama Asley, Baraka Da Prince, Dogo Janja n.k.
Ila asiwashirikishe Vijana wa WCB. Hao wameishatengwa na Media hawatomfikisha popote.

Yaan ww ndo mbovu wa kifikiri inaonekana upo ktk mateam team hasiojielewa leta point ya kueleweka ktk mada au ndo team kibamia nini
 
Back
Top Bottom