Nov 08, 2023 03:33 UTC
Muhammad Bagheri Qalibaf, Spika wa Bunge la Iran alisema hayo jana katika mazungumzo yake ya simu na mwenzake wa Algeria, Ibrahim Boughali, ambapo wamejadiliana kuhusu matukio yanayoendelea Gaza.
Qalibaf amebainisha kuwa, nchi za Kiislamu zinapasa kuchukua hatua za dharura za kukomesha jinai za kutisha zinazoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wasio na hatia wa Gaza.
Amesema wahanga wakuu wa mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo lililozingirwa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni watoto wadogo na wanawake.
Spika wa Bunge la Iran ameashiria nafasi ya makundi ya muqawama katika kukabiliana na chokochoko za Wazayuni na kueleza kwa: Nguvu ya harakati ya muqawama imeulazimisha utawala huo kutoa majibu ya woga.
Amesema utawala wa Kizayuni umegeuka na kuwa chombo cha mauaji kisichodhibitiwa na kilichopindukia kwa kufanya uhalifu kupitia kupuuza na kukiuka sheria zote za kimataifa.