antimatter
JF-Expert Member
- Feb 26, 2017
- 47,274
- 126,778
Hiyo falsafa kwa Afrika ya watu weusi haina tija kabisa, huzalisha madikteta, wauaji, mafisadi, uporaji, wizi, hatimaye umaskini uliotopea..Kataa demokrasia ,kikubwa mpate kiongozi mmoja ,mzalendo akae madarakani, hakuna mambo ya uchaguzi wala vyama vya siasa ,hapo lazima mfanikiwe.
Mijadala ya siasa ni utapeli haina faida.
Mifano ni hawa hapa-:
1. Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa za Banga, Zaire.
2. Jean-Bédel Bokassa, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR),
3. Hastings Kamuzu Banda, Malawi
4. Robert Gabriel Mugabe, Zimbabwe
5. Francisco Macias Nguema, Equatorial Guinea.
6. Idd Amin Dada, Uganda
..nk
Wote hao walijigeuza miungu, yaani watawala wa milele, na hakuna cha maana walichoacha baada ya kufurushwa kwa nguvu au mauti, zaidi ya umaskini wa kutupwa, madeni yasiyolipika, maumivu na shida tele kwa wananchi wao..