Qatar ni taifa la kuigwa kwa kusimamia maadili na misingi ya nchi yao. Kwanini tusiwaige?

Qatar ni taifa la kuigwa kwa kusimamia maadili na misingi ya nchi yao. Kwanini tusiwaige?

engijape

Senior Member
Joined
Nov 8, 2014
Posts
178
Reaction score
97
Pamoja na mgao wa umeme, nafuatilia kombe la dunia, na moja kati ya vitu nilivyofurahishwa navyo, ni namna hawa wenyeji Quatar walivyosimama kidete kutetea utamaduni na mila za nchi yake.

Hili ni jambo zuri na huenda katika vitu vilivyosababisha nchi hiyo kuwa juu sana kimaendeleo ni misingi yake yenyewe isio shabiana na misingi ya kuletewa na mataifa mengine. kwa hili tuna la kujifunza ambalo ni namna nchi inaweza kuwa na misimamo yake binafsi bila kushurutishwa na taifa lingine.

Nawasilisha
 
Kama hao wakubwa wangejua kuwa mambo yatakuwa hivyo, sidhani kama wangewapa nafasi hiyo!
Wamewaponza na wengine wenye itikadi kama za hao Qatar!
 
Kwa nchi maskini na tegemezi kama Tanzania, hilo sahau.
 
Wana hela hawategemei vyoo vya shule vijengwe kwa msaada wa watu wa marekani.
 
Back
Top Bottom