ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Kuna jambo huwa linanishangaza sana kuhusu hili jina la QNET.
kila mwaka tunasikia vijana kutapeliwa kwa kuahidiwa nafasi za kazi lakini mwisho wa siku wanaishia kutoa fedha na kuachwa bila kile walichoahidiwa.Ila nashindwa kuelewa nchi kivipi inashindwa kukomeza hilo mara moja na milele kwa sababu utapeli wao ni wa wazi kbs na ni very simple
mapaka unashindwa kuelewa QNET ni kampuni inayojihusisha moja kwa moja na matukio haya, au kuna watu wanaotumia jina lake kufanya utapeli?
Na kama ni matapeli wanaotumia jina la kampuni hiyo, kwa nini wanaendelea kutumia jina hilohilo ambalo limekuwa likihusishwa na malalamiko mengi? Kwa nini wasibuni jina jingine?
Je, tatizo ni sheria, utekelezaji wa sheria, ukosefu wa elimu kwa vijana au kuna jambo jingine ambalo hatulijui?
WanaJamiiForums, mwenye uelewa wa QNET atusaidie. Hii kampuni inafanya biashara gani hasa, na kwa nini jina lake linaendelea kuhusishwa na tuhuma za utapeli wa ajira?