QNET Yakanusha Kuhusishwa na Udahili wa Kilaghai wa Vijana 125 Singida

QNET Yakanusha Kuhusishwa na Udahili wa Kilaghai wa Vijana 125 Singida

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kampuni ya kimataifa ya QNET inayojihusisha na biashara ya mauzo ya moja kwa moja, imekanusha kuhusika na shughuli za udahili wa kilaghai zinazodaiwa kuwahusisha vijana 125 kutoka mikoa 11 nchini Tanzania, zilizoripotiwa kufanyika mkoani Singida.

Kwa mujibu wa taarifa ya kampuni hiyo, vijana hao wanadaiwa kushawishiwa kutoa fedha kwa ahadi za ajira na mafanikio ya haraka ya kifedha, huku baadhi yao wakiripotiwa kuishi katika mazingira yasiyofaa. QNET imesema uchunguzi wake wa ndani umebaini kuwa watu waliotambuliwa kuhusishwa na shughuli hizo si wasambazaji huru waliosajiliwa na kampuni hiyo.

Meneja Mkuu wa QNET Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini, Jared Thwaits amesema kampuni hiyo imesikitishwa na madai hayo, akisisitiza kuwa imekuwa ikiendesha biashara ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 28 na haivumilii vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili na taratibu zake za biashara.

Thwaits amesema QNET haiuzi nafasi za ajira, haitoi ahadi za mapato ya uhakika wala kuruhusu watu kukusanya fedha kwa kutumia ahadi za ajira au utajiri wa haraka. Ameongeza kuwa kampuni hiyo iko tayari kushirikiana na mamlaka za Tanzania katika uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini ukweli na kuwawajibisha waliohusika.

QNET imeeleza kuwa mfumo wake wa biashara unategemea mauzo ya bidhaa za afya, ustawi na mtindo wa maisha kupitia Wasambazaji Huru, badala ya kuuza nafasi za ajira au kuandikisha watu kwa ahadi za mapato ya uhakika. Kampuni hiyo imeonya kuwa matumizi mabaya ya jina lake yanaweza kusababisha wananchi kupata hasara za kifedha.

Soma Pia: Vijana 125 watelekezwa Singida baada ya kuahidiwa kazi za Q NET licha ya kutozwa kiasi cha fedha

Aidha, kampuni hiyo imewahimiza wananchi kuthibitisha uhalali wa fursa zinazotolewa na watu wanaojitambulisha kuwa wawakilishi wake kabla ya kufanya malipo au kuingia katika makubaliano ya kibiashara. Kupitia mpango wake wa QNET Against Scams, kampuni hiyo imesema inaendelea kuhamasisha umma kuhusu udahili wa kilaghai na matumizi yasiyoidhinishwa ya jina lake.
 
Back
Top Bottom