Quarantine workout's kwenye kona

Quarantine workout's kwenye kona

george kessy

Member
Joined
Jun 24, 2017
Posts
56
Reaction score
75
Habari wakuu

Miaka hii ya karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa la vijana mapopompo ,wavivu, na wenye kutokujua au kutokutaka kujua kesho yao.bado sijatazamia sababu zao ,yani kuwa namna hii na hii sio target yangu.

Karne hii ya 21 dunia imejawa na fursa kibao ,kila kona kila sekta ukituliza kichwa tu unatusua.hili halina ubishi.teknolojia imetanuka vyakutosha ,uchumi umeleta fursa kibao,kilimo na ufugaji pia

Sie kama vijana inatupasa kuacha upompompo na kufikilia juu ya kesho yetu.kesho yetu itakapokuwa bora;

Familia zetu zitakula na kulala vizuri

Account zetu zitasoma pay pay pay

Afya zetu zitakuwa imara

Tutakuwa na amani na ndugu zetu na marafiki pia

Hakuna mwamba yeyote humu ndani asiotaka maisha namna hii.

Hebu jiulize mifuko iko dolo alfu unakafamilia cha mtoto mmoja,huna any source of income ,ajira ulioitegemea boss amenunua machine kuokoa mshahara wake aliokuwa anakulipa wewe (machine imekureplace kazini) na huna anything kusema kitakusukuma kutoka katika msala huo.

Yes anything can happen hii ni karne ya 21 bhana.

Ykianza kujiona rockstar na mipamba ya bei mbaya,simu ya bei mbaya na huna any source of income zaidi ya kulia lia tu mahome kwenu ndo utoboe ujue unasafari ndefu sana,siku zitafika washikaji watakugeuza mboga ,utaanza kusema umelogwa,labda umenenewa mabaya lakini haikuwa evo nyuma.

Mindset zetu zisibaki kule insta kuangalia wowo,miduku,misambwanda yakina dada na vitu vingine ambavyo havina faida kwetu,hakuna mduku au msambwanda wa insta utakuja kukuletea ugali ,kukulipia kodi,kuwatibu wazazi wako ,zaidi ya kukupa ndoto za usiku alfu imetoka eyo(furaha ya muda mfupi).

Quarantine workout's ipo kwenye kona ni moja ya issue ambayo inanifanya niwashike wana tudiscuss issue mbalimbali katika nyanja muhimu kwetu kwa sisi vijana.

Tutaezaje piga profit katika teknolojia ya sasa?

Tutaezaje piga profit katika kilimo na ufugaji wa kisasa?

Tutaezaje piga profit katika uchumi kwa ujumla?

Wakati huu wa quarantine ambapo issue nyingi zimedolola ndo wakati sahii wakuweza tazama vitu kiundani zaidi ili pale kipyenga cha COVD19 kuisha kitakapopulizwa tujue tunarukia fursa gani,tujue tunaboreshaje maisha yetu,tujue tunajengaje ushirikiano wetu hata kwa watu wa 3 tu .

Jioni njema more information zitakuja post inayofwatia!

Note: Take it or leave it


jojijo
 
Back
Top Bottom