Quarter ya kwanza ya mwaka imeendaje?

Quarter ya kwanza ya mwaka imeendaje?

Slow but sure, Mungu aibariki na kuyatia mwanga malengo yetu yakafanikiwe
 
March inaenda kwa speed...je zile resolution tulizojiwekea zinaendaje? Wale wa gym mmeanza? Wale wa diet...beer na nyama choma tumepumzisha? Na zile financial goals vipi? Biashara tumeanzisha au bado team mshahara tu?
At least niweza kuwa ndani ya malengo kwa 90%
 
Huu mwaka unaenda Kasi Sana hasa hii march Leo tulikuwa tunajiuliza hili maana still tuna January effect Hali bado haijakaa Sawa na mtaani mzunguko wa pesa hakuna....all in all huu mwaka nimeweka lengo moja Tu nijitahidi nimalize MBA yangu nothing more
 
Sasa mipango ikifeli si unajaribu na imani pia? Hivi kama mipango ya miaka kibao ipo haitimii unapanga mipya ya nini?
Unabadili njia na unajithamini kwanini ulifeli kutimiza malengo, sometimes kupanga malengo ni Kuji stress bora ufuate maisha yanavyokupeleka...Ila kupanga malengo ni Bora zaidi
 
Huwa yanatimia au unapanga kwasababu unapenda kupanga? Mbona maisha ni yale yale?
Kuna malengo ya muda mfupi na muda mrefu haya ya muda mfupi kama kuongeza Mtoto,kuboresha nyumbani kidogo yanatimia, malengo ya muda mrefu ni kizungumkuti kutimiza unaishia kupeleka mbele
 
Kuna malengo ya muda mfupi na muda mrefu haya ya muda mfupi kama kuongeza Mtoto,kuboresha nyumbani kidogo yanatimia, malengo ya muda mrefu ni kizungumkuti kutimiza unaishia kupeleka mbele
Mazuri mengi uliyonayo hata hikuyapanga, ulijikuta tu umetoboa hivyo bahati ina sehemu yake katika maisha, akili, vipawa, karama bila bahati atahaso sana
 
Alhamdulillah Mungu anamsaidia uhakika wa Milo mitatu upo hayo mengine tuone mwaka ujao😀
 
Back
Top Bottom