SEHEMU YA 2
jina la mwisho likawa la Mukasha.Job
alihisi kutetemeka kwa ndani alipoliona
jina Mukasha.
“Your days are numbered
Mukasha” akawaza na kupiga namba za
rais.Haukupita muda simu ikapokelewa
“Hallow Austin” akasema Rais
Ernest
“Mheshimiwa rais samahani mimi
si Austin” akasema Job
“Wewe ni nani? Austin yuko wapi?
“Naitwa Job mheshimiwa rais.Ni
rafiki wa Austin.Nimekupigia
kukujulisha kuwa Austin amepata
matatizo usiku huu .Amepigwa risasi
kwa hiyo hali yake si nzuri.Naomba
msaada wako .Tunahitaji kumkimbiza
hospitali anahitaji kufanyiwa upasuaji
wa haraka”
“Oh my God !! ..akasema Rais
Ernest.Taarifa ile ilimstua sana
“Mzee !! ..akaita Job
“Samahani kijana,taarifa hii
imenistua sana.Nani amefanya tukio
hilo? Akauliza Ernest
“Mheshimiwa rais,tutaongea
mambo hayo yote baadae lakini kwa
sasa naomba utusaidie lile
linalowezekana kuokoa maisha ya
Austin hali yake si nzuri hata
kidogo.Tunataka kumkimbiza hospitali
lakini hatujui ni hospitali ipi
tutampeleka .Tunaomba msaada wako “
“Mpelekeni Kobwe
hospital.Ninawasiliana na madakatari
wa pale kuwajulisha jambo hilo.Mimi
mwenyeee ninaelekea huko sasa hivi”
akasema rais
“Ahsante mzee” akajibu Job na
kukata simu
“Mfunge huyu mwanamke
tutashughulika naye baadae,kwanza
tumuhudumie Austin” akasema Job na
Amarachi akamfunga Maria kwa waya
miguu na mikono kisha wakamtoa
Austin na kumuingiza garini.
“Job niache mimi nimkimbize
hospitali huyu majeruhi wewe baki
ushughulikie mambo ya hapa.Hatuwezi
wote kwenda huko na kuacha hapa
peke yake.Nitakujulisha kila
kinachoendelea huko ila kuwa makini
sana na Yule mwanamke nimemuona ni
hatari sana.Mtibu jeraha lake asije
akapoteza damu nyingi tukampoteza”
akasema Amarachi na kuwasha gari
akaondoka kwa kasi kubwa
Baada ya Amarachi kuondoka Job
akarejea sebuleni akamtazama Maria
kwa hasira akaichukua bastora ile
aliyoitumia Maria akaelekea juu
“Huyu mwanamake amewezaje
kumpiga risasi Austin? Anaonekana si
mtu wa kawaida huyu.Austin
amewezaje kukaa naye kwa muda huu
wote bila kutambua kuwa anaishi na
mtu hatari?Namfahamu Austin ni mtu
mwepesi mno kumtambua mtu yeyote
kama ni hatari lakini kwa huyu
mwanamke ameshindwa kumtambua ni
mtu wa namna gani,inanishangaza
sana.Huyu mwanamke aombe Mungu
wake Austin asipone kwani kwa namna
ninavyomfahamu Austin akipona sijui
atamfanya nini” akawaza Job
akilifungua kabati lenye dawa na vitu
mbali mbali vya matibabu akachukua
vitu anavyovihitaji na kushuka chini
akamuendea Dr Marcelo na kumuwekea
kitu Fulani puani .Dr Marcelo akapiga
chafya mfululizo na kuzinduka.Job
akamfuata Maria pale chini akamshika
kiganja chake cha mkono kilichopigwa
risasi akakichunguza,risasi ilikuwa
imepita na kutokea upande wa
pili.Akamimina dawa Fulani ya maji
pale penye jeraha na Maria akapiga
ukelele mkubwa.Dawa ile ilimsaidia
kuzuia damu kuendelea
kumwagika.Akalifunga jeraha na
kumuinua akampandisha ghorofani
akampeleka katika chumba maalum cha
mahojiano.Ndani ya kila chumba
kulikuwa na viti vitatu ,meza moja na
mashine kadhaa.Akamketisha katika kiti
kikubwa akamfunga mikono na
kuifunga katika pingu zilizounganishwa
na kile kiti akafanya hivyo pia kwa
miguu.Akamtazama Maria kwa hasira
“Omba kwa Miungu yote
unayoifahamu Austin asipone kwani
endapo akipona nakuhakikishia
atakufanya kitu kibaya mno ambacho
hukuwahi kukifikiria.You don’t know
him.Anapochokozwa hakuna wa