QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Hizi hadithi za JF itabidi mtu unazisoma baada ya kuambiwa imeisha. La sivyo utapata mateso tu ya kuziwaza.
 
Mi nlijua itakuwa imefika mwisho......Lege njo =o basi jamaa angu
 
Baada ya kimya kirefuuu cha haja.

Wale ambao huwa mnaenda jikoni na kuanza kumpelekea habari za huku jf mpishi mpaka anaharibu pishi na kuchelewesha acheni.

Kama mnamfuata huko na kusoma someni huko huko ya huku myaache huku huku.
 
Baada ya kimya kirefuuu cha haja.

Wale ambao huwa mnaenda jikoni na kuanza kumpelekea habari za huku jf mpishi mpaka anaharibu pishi na kuchelewesha acheni.

Kama mnamfuata huko na kusoma someni huko huko ya huku myaache huku huku.
Mkuu naamini leo hutatuangusha
 
LEGE ni MTU asiyeaminika kwasasa. Ni mbaya sana kupoteza uaminifu.
Mkuu umaninifu hauwezi kupotea zaidi ya wadau hapa kuleta wingi.wa kujua na kuharibu mambo.kuna wadau humu viherehere sana ndio wanaharibu mambo.ila jf haiwezi poteza sifa zake burudani itashuka hapa mwanzo mwisho kwa kuwa hata wao na wengi humu story hizi wamepata kuzifaham humu humu.jukwaani
 
Sawa sawa mkubwa, karibu ulete vitu sasa.
 
[emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36] [emoji36]
 
LEGE hivi sasa ni saa saba usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki... Tarehe 3 ya mwezi wa 6 mwaka 2017, chondechonde fanya kusuuza roho za watu..
 
QUEEN MONICA SEASON 4


SEHEMU YA 1



ILIPOISHIA SEASON ILIYOPITA
“Marcelo nimebanwa sana
tafadhali.Usiniache nikajisaidia hapa
.Mimi si mhalifu na sistahili kufanyiwa
hivi.Nimesema nitawaeleza kila kitu
kwa hiyo basi naomba unifungua
Marcelo nikajisaidie.Una bastora hapo
,itume endapo nitafanya jambo lolote la
kipuuzi.Ninakwenda kujisaidia na
nikimaliza utanifunga kamba zenu.”
Akasema Maria.Marcelo akamtazama
kwa wasi wasi mwingi
“Amebanwa sana na halitakuwa
jambo jema kumuacha akajisaidia
hapa.Ngoja nimfungue akajisaidie”
akawaza Marcelo na kwenda
kumfungua Maria waya aliofungwa
mikononi.
“Thank you Marcelo for this.You
are real a gentleman.Show me the
toilet” akasema Maria na Mara tu
Marcelo alipogeuka bila kutarajia
akajikuta amepigwa pigo zito kichwani
lililompeleka chini na kumpoteza
fahamu. Haraka haraka akaichukua
bastora iliyokuwa juu ya meza.
“Its my turn now.He wants to
know who I am and now the time has
come to know who I real am” akasema
Maria kwa sauti ndogo na kwa
tahadhari akaenda kuchungulia
dirishani
“Sioni mtu yeyote nje.What is this
place? I need to get out of this place now
before these monsters comes down”
akasema Maria kwa kunong’ona na kwa
haraka akaenda mlangoni akakinyonga
kitasa kwa lengo la kuufungua mlango
“Stop right there !! ikasema sauti
kali ya Austin aliyekuwa amesimama
katika ngazi akitokea ghorofani.
“Slowly put your gun down and
push it to me !!!.akasema Austin kwa
sauti kali
Taratibu Maria akaushusha chini
mkono uliokuwa na bastora kwa lengo
la kuiweka chini kama alivyoamriwa
lakini kabla bastora ile haijagusa chini
kukatokea kitendo ambacho Austin
hakuwa amekitarajia.Kwa wepesi wa
aina yake Maria akageuka na
kuvurumisha risasi upande aliokuwa
amesimama Austin ambaye alianguka
huku akivuja damu.Bastora yake ikifuka
moshi Maria akamuendea Austin
aliyekuwa amelala akivuja
damu,machozi yakamtoka
“I’m sorry my love.Sikutegemea
kama siku moja tungefika hapa.Ni
afadhali nikuue kuliko kukupa nafasi ya
kunifahamu mimi ni nani.I love you
Austin and God will forgive me for what
I’m going to do” akasema Maria kwa
sauti ndogo na kuelekeza bastora katika
kichwa cha Austin na ukasikika mlio wa
risasi.
ENDELEA......................
aria alianguka chini
baada ya mlio ule wa
risasi kusikika.Kiganja
chake cha mkono wa kulia kilichokuwa
kimeshika bastora kilikuwa kinavuja
damu .Katika mlango wa kuingilia
sebuleni alisimama mwanamke mmoja
mweusi wastani na mwenye nywele
ndefu aliyevalia mavazi meusi akiwa na
bastora mkononi iliyokuwa ikifuka
moshi.Mwanamke Yule akatembea
M
kumuendea Maria aliyekuwa amelala
chini akigugumia kwa maumivu .
“Don’t move!!! Akamuamuru Maria
huku akimuelekezea bastora
“Don’t shoot!! Please don’t shoot
me! Akaomba Maria
Mlio ule wa risasi ulimstua sana
Job aliyekuwa chumbani, akashuka
chini kwa haraka akiwa katika
tahadhari kubwa
“Amarachi!! Akasema Job
akishangaa sana kwa hali aliyoikuta
pale sebuleni
“Nini kimetokea hapa? Akauliza
Job huku akimfuata Austin na kumgeuza
“She shot him” akajibu Amarachi
“Maria ?!! akauliza Job kwa
mshangao huku akimkazia macho Maria
aliyekuwa amelala chini akivuja damu
katika kiganja chake cha mkono wa
kulia.Job akataka kuinuka kumfuata
Maria Amarachi akamzuia
“Achana naye Job.Tuwasaidie
kwanza hawa waliojeruhiwa kwa risasi
kwani wanazidi kupoteza damu nyingi”
akasema Amarachi.Job akamchunguza
Austin na kugundua alikuwa amepigwa
risasi nne.Moja katika bega la
kushoto,nyingine kifuani na mbili
pajani.Akahisi kichwa kuchanganyikiwa
“Amepigwa risasi nne” akasema
Job
“Job tusipoteze muda.Huyu mtu
anazidi kupoteza damu.We need to save
him.Nilipokuwa msituni nilifundishwa
namna ya kutibu majeraha ya risasi
.Nipe sanduku la huduma ya kwanza ili
tuzuie kwanza damu isiendelee kutoka
halafu tutafute namna ya kufanya”
akasema Amarachi akiwa bado
amemuelekezea Maria bastora
“Hata mimi nafahamu pia namna
ya kutibu majeraha kama haya ya risasi
lakini kwa hapa hatuwezi kufanya
chochote.Austin anahitaji upasuaji wa
haraka sana kuondoa risasi mwilini na
hasa hii iliyopo kifuani.Lazima
tumkimbize hospitali haraka” akasema
Job
“Tutampeleka hospitali ipi? Kokote
tutakakompeleka watahitaji kupata
kibali cha polisi na kama ujuavyo polisi
lazima watake maelezo ya kina ya
kilichotokea.Uko tayari kuwaeleza
ukweli? Akauliza Amarachi.Job akafikiri
haraka haraka na kupata wazo
“I need to call president” akasema
Job akamsachi Austin akachukua simu
yake akaifungua mahala kwa kuhifadhia
majina na namba za simu .Kulikuwa na
majina manne tu.Jina la kwanza lilikuwa
la Ernest,kisha Monica halafu Linah na
 
SEHEMU YA 2



jina la mwisho likawa la Mukasha.Job
alihisi kutetemeka kwa ndani alipoliona
jina Mukasha.
“Your days are numbered
Mukasha” akawaza na kupiga namba za
rais.Haukupita muda simu ikapokelewa
“Hallow Austin” akasema Rais
Ernest
“Mheshimiwa rais samahani mimi
si Austin” akasema Job
“Wewe ni nani? Austin yuko wapi?
“Naitwa Job mheshimiwa rais.Ni
rafiki wa Austin.Nimekupigia
kukujulisha kuwa Austin amepata
matatizo usiku huu .Amepigwa risasi
kwa hiyo hali yake si nzuri.Naomba
msaada wako .Tunahitaji kumkimbiza
hospitali anahitaji kufanyiwa upasuaji
wa haraka”
“Oh my God !! ..akasema Rais
Ernest.Taarifa ile ilimstua sana
“Mzee !! ..akaita Job
“Samahani kijana,taarifa hii
imenistua sana.Nani amefanya tukio
hilo? Akauliza Ernest
“Mheshimiwa rais,tutaongea
mambo hayo yote baadae lakini kwa
sasa naomba utusaidie lile
linalowezekana kuokoa maisha ya
Austin hali yake si nzuri hata
kidogo.Tunataka kumkimbiza hospitali
lakini hatujui ni hospitali ipi
tutampeleka .Tunaomba msaada wako “
“Mpelekeni Kobwe
hospital.Ninawasiliana na madakatari
wa pale kuwajulisha jambo hilo.Mimi
mwenyeee ninaelekea huko sasa hivi”
akasema rais
“Ahsante mzee” akajibu Job na
kukata simu
“Mfunge huyu mwanamke
tutashughulika naye baadae,kwanza
tumuhudumie Austin” akasema Job na
Amarachi akamfunga Maria kwa waya
miguu na mikono kisha wakamtoa
Austin na kumuingiza garini.
“Job niache mimi nimkimbize
hospitali huyu majeruhi wewe baki
ushughulikie mambo ya hapa.Hatuwezi
wote kwenda huko na kuacha hapa
peke yake.Nitakujulisha kila
kinachoendelea huko ila kuwa makini
sana na Yule mwanamke nimemuona ni
hatari sana.Mtibu jeraha lake asije
akapoteza damu nyingi tukampoteza”
akasema Amarachi na kuwasha gari
akaondoka kwa kasi kubwa
Baada ya Amarachi kuondoka Job
akarejea sebuleni akamtazama Maria
kwa hasira akaichukua bastora ile
aliyoitumia Maria akaelekea juu
“Huyu mwanamake amewezaje
kumpiga risasi Austin? Anaonekana si
mtu wa kawaida huyu.Austin
amewezaje kukaa naye kwa muda huu
wote bila kutambua kuwa anaishi na
mtu hatari?Namfahamu Austin ni mtu
mwepesi mno kumtambua mtu yeyote
kama ni hatari lakini kwa huyu
mwanamke ameshindwa kumtambua ni
mtu wa namna gani,inanishangaza
sana.Huyu mwanamke aombe Mungu
wake Austin asipone kwani kwa namna
ninavyomfahamu Austin akipona sijui
atamfanya nini” akawaza Job
akilifungua kabati lenye dawa na vitu
mbali mbali vya matibabu akachukua
vitu anavyovihitaji na kushuka chini
akamuendea Dr Marcelo na kumuwekea
kitu Fulani puani .Dr Marcelo akapiga
chafya mfululizo na kuzinduka.Job
akamfuata Maria pale chini akamshika
kiganja chake cha mkono kilichopigwa
risasi akakichunguza,risasi ilikuwa
imepita na kutokea upande wa
pili.Akamimina dawa Fulani ya maji
pale penye jeraha na Maria akapiga
ukelele mkubwa.Dawa ile ilimsaidia
kuzuia damu kuendelea
kumwagika.Akalifunga jeraha na
kumuinua akampandisha ghorofani
akampeleka katika chumba maalum cha
mahojiano.Ndani ya kila chumba
kulikuwa na viti vitatu ,meza moja na
mashine kadhaa.Akamketisha katika kiti
kikubwa akamfunga mikono na
kuifunga katika pingu zilizounganishwa
na kile kiti akafanya hivyo pia kwa
miguu.Akamtazama Maria kwa hasira
“Omba kwa Miungu yote
unayoifahamu Austin asipone kwani
endapo akipona nakuhakikishia
atakufanya kitu kibaya mno ambacho
hukuwahi kukifikiria.You don’t know
him.Anapochokozwa hakuna wa
 
SEHEMU YA 3


kumtuliza.Si yeye tu.Jiandae pia
kukutana na mimi.I’m a monster!!
akasema Job kwa hasira na kutoka mle
chumbani akashuka chini akamkuta
Marcelo ameketi sofani
“Nini kilitokea? Hizi damu hapa
sebuleni zimetoka wapi? Akauliza
Marcelo.Job akamtazama kwa hasira na
kumuuliza
“Tulikuacha hapa wewe na Yule
mwanamke nini kilitokea?
“Alibanwa na haja ndogo
akaniomba nimfungue akajisaidie
nikafanya hivyo lakini mara tu
nilipomfungua nilipigwa na kitu kizito
nikapoteza fahamu.Austin yuko wapi?
Hizi damu zimetoka wapi? Akauliza
Marcelo kwa wasi wasi
“Natamani nikurukie na kuuchafua
uso wako kwa makonde mazito .Jambo
ulilolifanya bila kutafakari hivi sasa
linataka kuchukua uhai wa Austin !!!
“Kwani nini kimetokea? Austin
yuko wapi? Akauliza Marcelo
“Hukupaswa kuwa dhaifu kiasi
hicho na kumwamini yule
mwanamke.Alikulaghai na wewe wewe
ukahadaika.Unadhani Austin alikuwa
mjinga kumfunga vile wakati ni mpenzi
wake? Tayari alikwisha gundua
kitu.Mwanamke Yule uliyemfungua
amempiga risasi nne Austin na hivi
tuongeavyo amekimbizwa hospitali.He’s
fighting for his life.Hiyo damu
unayoiona hapo chini ni damu ya Austin
iliyomwagika kwa sababu ya ujinga
ulioufanya.Muombe Mungu wako
Austin apone kwani ikitokea vinginevyo
mimi na wewe tutakuwa na maongezi”
akasema Job.Marcelo akainamisha
kichwa.Maneno yale ya Job yalimchoma
sana
“I’m so fool.Kwa nini nikawa
mjinga kiasi kile na kushindwa
kung’amua kwamba Yule mwanamke ni
hatari? I’m so weak.Ujinga wangu
umesababisha Austin aingie katika
hatari kubwa na ninamuomba Mungu
apone” akawaza huku akilengwa na
machozi
“Ee Mungu msaidie Austin
apone.Sifahamu nini hatima ya maisha
yangu endapo Austin atapoteza
maisha.Ni yeye ninayemtegemea
anivushe katika wakati huu mgumu
nilionao” akawaza
“I won’t forgive myself if Austin
will die. !! akawaza Marcelo .Job
akachukua chombo na kuifuta damu
pale sebuleni.Marcelo akaendelea
kujiinamia akiwaza na kumuomba
Mungu amponye Austin.
*********************
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…