QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 19


Nilimtolea Marcelo maneno
makali ,nilikuwa na hasira sana wakati
ule .Muda mrefu sijafanya kazi natakiwa
kujizuia sana kutokuwa na hasira za
kupitiliza kwani ninaweza kujikuta
nikifanya maamuzi yasiyofaa.” Akawaza
Job
Alielekea moja kwa moja katika
supermarket akafanya manunuzi ya vitu
mbali mbali ambavyo wangevihitaji pale
nyumbani kisha akaliacha gari lake pale
supermarket na kukodisha taksi
akamtaka dereva ampeleke Savannah
hotel ambako Boaz na mwanae Maria
walikuwa wamefikia
**********************
Monica aliwasili hospitali
alikolazwa Austin.Hakupata usumbufu
wowote,akaelekezwa kilipo chumba
alimolazwa Austin akaelekea huko
haraka bila kuwajali watu waliokuwa
wakimtazama .Alisalimiana na walinzi
wakamruhusu aingie ndani.Austin
alikuwa usingizini.Maria akamsogelea
na kuuweka mkono katika paji la uso
akaita kwa sauti ndogo
“Austin ...”
Taratibu Austin akafumbua macho
na kukutana na sura ya Monica ambaye
macho yake yalijaa machozi
“Oh ! Monica Ahsante umekuja
kuniona” akasema Austin
“ Pole sana Austin.Vipi maendeleo
yako?
“Nashukuru naendelea vyema.Hali
yangu si mbaya” akasema Austin na
machozi yakaongezeka machoni kwa
Monica
“Nyamaza kulia
Monica.Ninaendelea vizuri.”
“ I’m deeply hurt Austin.Who did
this to you and why? Akauliza Monica
huku akilia
“Please don’t cry Monica,Njoo hapa
karibu “ akasema Austin .Monica
akaketi kitandani
“Jana nilikuwa na baadhi ya rafiki
zangu tukinywa pombe katika baa
Fulani kumbe kuna majambazi
walikuwa wanatufuatilia.Baadae wakati
tunaondoka tukavamiwa na mimi katika
harakati za kupambana nao nikapigwa
risasi nne nikakimbizwa hapa hospitali
.Nawashukuru madaktari walinifanyia
upasuaji na kuokoa maisha yangu”
Austin akadanganya
“Pole sana Austin.Najua lengo lako
lilikuwa jema la kuwasaidia wenzako
,lakini tafadhali usicheze na watu wenye
silaha ,wangeweza kukuua .Tafadhali
usicheze na masha yako.Ukiondoka
wewe utaacha majozi makubwa kwa
ndugu,mkeo na watoto kama unao na
hata kwa sisi marafiki zako.Nilistuka
sana nilipopewa taarifa hizi kwani siku
si nyingi mmoja wa rafiki zangu naye
alipigwa risasi na akanusurika kifo”
akasema Monica na kuangusha machozi
“Anaendeleaje huo rafiki yako?
Alipigwa risasi na nani?
“Anaendelea vizuri.Mpaka sasa
bado haijafahamika nani alimpiga risasi
“ akasema Monica
Waliendelea na maongezi mengine
wakiongelea mambo mbali mbali.Austin
alifarijika sana kwa ujio ule wa Monica
.Wakati wakiendelea na maongezi mara
akaingia Amarachi
“ Hi.You must be Monica.I’m
Amarachi.Ni rafiki wa Austin na ndiye
uliyeongea naye simuni.karibu sana”
akasema Amarachi kwa uchangamfu
mkubwa na kumfanya Monica ambaye
sekunde kadhaa zilizopita alikuwa
akitoa machozi atabasamu
“ oh ! kumbe ni wewe.Ahsante
sana kwa kunipa taarifa za tukio
hili.Nimefurahi kukufahamu.Unasema
unaitwa nani? Akauliza Monica
“ Naitwa Amarachi”
“Oh ! Amarachi.Nigerians names.”
Akasema Monica
“ Ndiyo.Asili yangu ni Nigeria
lakini kwa sasa ni mtanzania.”
“ Nafurahi kukufahamu
Amarachi.Austin ni rafiki yangu na
ndiyo maana nimefika mara moja baada
ya kupata zile taarifa toka kwako”
“Amarachi” akaita Austin na
Amarachi akamsogelea karibu
“Huyu anaitwa Monica Benedict ni
rafiki yangu.Huyu ndiye aliyetengazwa
 
SEHEMU YA 20


hivi karibuni kuwa ni mrembo namba
moja wa Afrika”
Uso wa Amarachi ukachanua kwa
tabasamu
“Wow ! kumbe ni wewe Monica !!
Siamini kama nimekutana na malkia wa
Afrika.Oh!Monica come give me a hug”
akasema kwa furaha Amarachi na
Monica akainuka akakumbatiana na
Amarachi
“Nimefurahi sana kukutana nawe
Monica.You are so beautifull.I love you
hair so much” akasema Amarachi huku
akizishika nywele za Monica ambaye
alikuwa anatabasamu
“Hizi nywele zako ni nzuri mno.Ni
halisi? Akauliza Amarachi na kuukata
unywele mmoja akautazama
“Ni nywele halisi kabisa.Sipendi
kutumia nywele bandia”
“Ni nywele nzuri mno.Monica
unajua sana kujitunza.Waliokuchagua
kuwa mrembo kuliko wote Afrika
hawakukosea” akasema Amarachi
Waliendelea na maonegzi mengine
hadi alipokuja daktari Amarachi na
Monica ikawalazimu kutoka nje.
“Austin nimefurahi sana hali yako
inaendelea vyema.Nitakuja tena baadae
mchana kukutazama.Amarachi
atanijulisha kama kutakuwa na tatizo
lolote” akasema Monica akamuaga
Austin akatoka nje akiongozana na
Amarachi ambaye alimsindikiza hadi
katika maegesho akaondoka .Daktari
alipotoka ,Amarachi akaingia huku
akitasamu na kumuonyesha Austin ule
unywele wa Monica
“Ahsante sana Amarachi.Ulifanya
vizuri sana kuupata unywele huo ambao
nautafuta mno” akasema Austin
“Usijali Austin.Mimi na Job tupe
kazi yoyote na tutaifanya kwa wakati
huu ambao bado uko kitandani
ukipumzika”
“ Job aliponieleza kuhusu wewe
nilipata ugumu kidogo kukubaliana
naye.I don’t trust people easily.Baada ya
kunihakikishia kuwa anakuamiani
ndipo nilipokubaliana naye lakini
nilihitaji kuona nawe ana kwa ana
.Nimefanikiwa kukuona na
nimethibitisha kuwa unao uwezo
mkubwa sana zaidi ya alivyonieleza Job”
akasema Austin
“Nashukuru Austin kwa
kunikubali.Nadhani Job alikueleza
historia yangu hadi nilipofika hapa.It’s
an awfull story.Nimepitia mambo mengi
magumu na ya kukatisha tamaa lakini
nashukuru niliyavumilia yote hadi leo
hii nimefika hapa nilipofika
.Namshukuru mno Job ambaye ndiye
aliyenisaidia nikaja Tanzania na
ninaishi mpaka leo kwa amani.Hakuna
anayeweza kudhani mimi ni raia wa
Nigeria kwa namna Job
alivyonipika.Amefanya kazi kubwa ya
kunibadilisha hadi nikawa hivi
.Amarachi wa sasa si Yule wa za zamani
.Nilimchukia kila mtu na kumuona
adui,sikuona thamani ya utu
.Kilichokuwa moyoni mwangu ni kitu
kimoja tu kisasi.kwa mambo
niliyofanyiwa nilitamani niwe muuaji
mkubwa .nilitamani siku moja
kuingizwa katika vitabu vya historia
kwa kuua watu wengi lakini haya yote
yalitoweka akilini mwangu baada ya
kukutana na Job.Ni mtu mwenye
sehemu kubwa sana katika maisha
yangu na ndiyo maana unapomtaja
Amarachi huachi kumtaja pia Job kwani
kila ninapopiga hatua moja yeye huwa
nyuma yangu” akasema Amarachi kwa
hisia kali.Ukimya mfupi ukapita Austin
akasema
“ Tutaongea mengi baada ya
kutoka hapa hospitali leo.Nimekwisha
ongea na madaktari na kuwaomba
waniruhusu leo niondoke.Sitaki
kuendelea kukaa hapa
hospitali.Natakwia kuongoza
mapambano hata kama niko kitandani”
akasema Austin na kumuelekeza
Amarachi auweke ule unywele katika
pakiti ndogo ya nailoni.
“ Kazi ya rais imekamilika .Tayari
ninao unywele wa Monica.Kinachofuata
sasa ni kwenda kufanya kipimo cha
vinasaba kuhakiki kama kweli Monica ni
mtoto wa rais.Baada ya zoezi hilo
kukamilika kitakachofuata sasa ni
mapambano makali na Alberto’s.”
akawaza Austin
******
 
SEHEMU YA 21

b aliwasili savannah hotel
akashuka katika taksi akaingia ndani
akiwa na begi dogo.Akaomba kupatiwa
chumba kwa muda wa siku
mbili.Akapatiwa chumba ghorofa ya
nne.Wakati akipelekwa katika chumba
alichopewa alikuwa akichunguza namna
hoteli ile ilivyokaa.Hakukuwa na
kamera za ulinzi ndani bali kulikuwa na
kamera kadhaa nje.Job akatabasamu
baada ya kuingia katika chumba
alichokodi
“Sitakiwi kupoteza muda
hapa.Natakiwa haraka sana nifanye kazi
iliyonileta.Nitaanzia katika chumba cha
Maria ambacho kwa mujibu wa
mpangilio wa vyumba vya hoteli hii
kitakuwa ghorofa ya pili.”
Akalifungua begi lake dogo akatoa
kadi za kufungulia milango ya vyumba
vya Maria na Boaz akaiweka vyema
bastora yake akatoka na kuanza
kushuka chini taratibu huku akionekana
kucheza na simu yake.Alifanya vile ili
mtu yeyote asiwe na wasiwasi
naye.Alipotembea alikuwa akisoma
namba za vyumba hadi alipokifikia
chumba cha Maria.Akatazama huku na
huko lakini hakukuwa na mtu yeyote na
haraka haraka akaipitisha kadi ile
katika mlango ukafunguka akaingia
ndani.Jicho lake likatua kitandani
kulikokuwa na kompyuta ya Maria
akaichukua na kuipakia katika begi lake
.Mezani kulikuwa na pochi ndogo
akaifungua na kutazama ndani
kulikuwa na pesa na kadi tatu za
benki,akaipakia pochi ile katika begi
“Hivi vinaweza nisaidia kupata
chochote kutuwezesha kumfahamu
Maria ni nani.Kuna sanduku kubwa
humu lakini sina muda wa
kupekua.Sitaki nikutwe humu ndani.”
Akawaza Job na kutoka katika kile
chumba akatembea taratibu na kwa
tahadhari kuelekea katika chumba cha
Boaz.Hatua kama nne kabla ya kukifikia
chumba cha Boaz,mlango wa chumba
cha jirani ukafunguliwa na wahudumu
wakatoka wakiwa na torori lililojaa
mashuka ,wakafungua mlango wa
chumba cha Boaz kwa ajli ya kufanya
usafi.
“Nimechelewa wanafanya
usafi.Sina muda wa kusubiri zaidi.Hivi
nilivyopata vinanitosha sana na endapo
kutakuwa na ulazima wa kurudi katika
chumba cha Boaz nitafanya hivyo.Ngoja
niondoke” akawaza Job na bila kupoteza
muda akaondoka zake .Karibu na ile
hoteli kulikuwa na kituo cha taksi
akakodi moja na kuelekea supermket
alikoacha gari lake
 
SEHEMU YA 22






IKULU DAR ES SALAAM
Tayari wageni wote walioalikwa
kushuhudia kiapo cha mkuu mpya wa
majeshi walikwisha wasili katika
ukumbi mdogo wa ikulu na mtu pekee
aliyekuwa akisubiriwa ni rais wa
jamhuru ya muungano wa Tanzania
Ernest Mkasa.Bendi ya jeshi iliendelea
kutumbuiza wageni kwa muziki wakati
rais akisubiriwa.Maongezi yalikuwa ni
ya chini chini
“Ndugu wageni waalikwa
tunaombwa tusimame sasa rais wa
jamhuri ya mungano wa Tanzania
anaingia ukumbini” Sauti ya
mkurugenzi wa habari ikuli ikasikika na
watu wote mle ukumbini wakasimama
.Rais akiwa ameongozana na walinzi
wake akaelekea moja kwa moja katika
kuti alichoandaliwa na bila kupoteza
mda zoezi la kiapo likaanza.Jenereani
lameck Msuba akala kiapo na rasmi
akawa ndiye mkuu mpya wa majeshi
Zoezi la kiapo
lilipokamilika,likafuata zoezi la picha
ambapo rais alipiga picha na watu
mbalimbali waliohudhuria hafla
ile.Ratiba ya siku hii ilikuwa fupi sana
hivyo zoezi la picha lilipokamilika rais
akawa na maongezi ya faragha na mkuu
mpya wa majeshi
“Hongera sana jenerali Msuba”
akaanzisha maongezi rais Ernest akiwa
na Jenerali lameck katika chumba cha
mazungumzo ya faragha
“ Ahsante sana mheshimiwa rais”
akajibu Lameck kwa ukakamavu
“ Sitaki kuchukua muda mrefu
nataka Lameck nataka nikuache
ukaanze kuyatumikia majukumu yako
mapya hivyo nitajielekeza moja kwa
moja katika mambo yale ya
msingi.Kwanza kabisa nataka
nikujulishe kwamba kuna mtu mmoja
ambaye ndiye aliyekupendekeza kwa
nafasi hii ya mkuu wa majeshi na mimi
nikaridhika na kukuteua mara
moja.Anaitwa Austin January.
Mshangao mkubwa ukaonekana
katika sura ya Lameck
“ Austin January ??akauliza
“ndiyo” akajibu rais
“Haya ni maajabu.Yuko hai?
“Ndiyo yuko hai”
Zikapita sekunde kadhaa za
ukimya halafu Lameck akasema
“Nilikutana na Austin wakati
nikiwa masomoni katika chuo cha
kijeshi nchini Marekani.Yeye alikuwa
katika mafunzo ya operesheni maalum
za kupambana na magaidi.Toka hapo
tukawa marafiki wakubwa.Baadae
nilisikia kwamba alipotea nchini
Somalia katika mapambano na
wanamgambo wa Alshabaab
alipoongoza kikosi maalum
kuwakomboa watanzania waliotekwa
na kikundi hicho.Nimestuka kusikia
yuko hai”
“ Yuko hai na yuko hapa hapa Dar
es salaam.Yuko hapa kwa kazi maalum
niliyompa lakini kwa sasa makazi yake
ni nje ya nchi” rais akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“ Jenerali lameck ,kuna mambo
mazito yanayoendelea hapa nchini kwa
sasa na hii ndiyo sababu kwa siku kama
mbili zilizopta mmesikia kuna mambo
makubwa yametokea.Nimeivunja
serikali yangu na ninataka kuisuka
upya.Niko katika operesheni kubwa ya
kuisafisha nchi hii na Austin ndiye mtu
ninaye shirikiana naye.” Rais Ernest
akamueleza Lameck kwa kirefu kuhusu
Alberto’s na namna walivyomtumia
kukita mizizi yao hapa Tanzania.Lameck
alibaki na mshangao mkubwa alikosa
neno la kusema
“Nashindwa niseme nini
mheshimiwa rais ila pole sana kwa
hayo yote uliyoyapitia lakini hongera
vile vile kwa maamuzi uliyoyachukua na
unayoendelea kuyachukua .Wewe ni
rais wa mfano Afrika na dunia.Hili
ulilolifanya na unayoendelea kuyafanya
 
SEHEMU YA 23



ni mambo makubwa sana na binafsi
ninakuunga mkono katika mapambano
haya.Hatuwezi kukubali kuchezewa
kiasi hiki na hawa watu.Mimi ni mmoja
wa watu ambao hawako tayari kuona
nchi hii nzuri ikibadilika na kuingia
katika laana.Kwa hiyo mheshimiwa rais
mimi kuanzia sasa ni mshirika wako
katika mapambano haya makubwa.Kazi
ya jeshi ni kuilinda nchi dhidi ya
wavamizi ambao si lazima wawe ni wale
wanovamia mipaka yetu ya kijiografia
bali hata hawa Alberto’s ni wavamizi
pia.Wanataka kuharibu misingi mizuri
tuliyojengewa na wazee wetu
waliomwaga damu zao kulipigania taifa
hili.Wanataka kusimika tamaduni zao
na kuondoa za kwetu .Binafsi kama
mzalendo wa taifa hili siko tayari kuona
nchi yetu ikikwanguliwa rangi yake
nzuri ya asili kwa sababu tu ya watu au
kikundi cha watu wachache kwa
manufaa yao kwa hiyo narudia tena
kukuhakikishia kwamba niko pamoja
nawe katika vita hii,ninakuunga mkono
na niko tayari kutoa ushirikiano
mkubwa sana wa jeshi kila pale
utakapohitajika” akasema Lameck huku
uso wake ukionyesha hasira
“Jenerali Lameck sasa ninaamini
maneno ya Austin kwamba wewe ni
mzalendo wa kweli wa nchi nchi
hii.Nimefurahishwa sana na maneno
yako na ninaamini kwa pamoja
tutashinda mapambano haya .Kuna
mambo mawili ambayo nayahitaji toka
kwako kama sehemu ya kuniunga
mkono katika mapambano haya”
akanyamaza kidogo halafu akaendelea
“Kwanza ninahitaji kikosi cha
makomando toka jeshi la wananchi kwa
ajili ya kunilinda.Nahitaji makomando
kumi na mbili leo hii.Sina imani tena na
walinzi wanaonilinda.Kama watu
nisiowafahamu waliweza kuingia hadi
chumbani kwangu na kunitolea vitisho
ni wazi kuwa sina ulinzi na hii ni picha
halisi kuwa muda wowote Alberto’s
wanaweza wakaniua.Nahitaji ulinzi
imara na wenye uhakika” akasema
Ernest
“Kwa hilo umepata mheshimiwa
rais.Muda mfupi tu baada ya kutoka
hapa nitaelekeza kikosi hicho kifike
hapa haraka.”akasema Lameck
“ Ahsante sana .Hilo lilikuwa la
kwanza.Jambo la pili ni kama
nilivyokueleza kuwa mimi na Austin
tayari tumekwisha yaanza mapambano
na hawa jamaa,na kadiri tunavyozidi
kusonga mbele ndivyo mambo mbali
mbali yanavyozdi kujitokeza kiasi cha
kuifanya operesheni hii kwenda
taratibu.Tayari nimekwisha wapunguza
nguvu kwa hiyo sitaki kuwapa nafasi ya
kujipanga upya.Natakiwa kuitumia
nafasi hii kuwamaliza kabisa katika uso
wa Tanzania kwa hiyo nimebuni
mpango wa siri ambao nitakushirikisha
wewe pekee,Sitaki Austin afahamu
kuhusu hiki ninachofikiria kukifanya”
“ Umepanga kufanya nini
mheshimiwa rais kuwamaliza hawa
Alberto’s” akauliza Lameck
“ Ninataka kuomba kufanya
mazungumzo nao na nitawataka
wakusanyike viongozi wao wote pamoja
na wafuasi wengine.Nitawaambia
kwamba nataka kufanya makubaliano
nao ili niwape uhuru wa kufanya
shughuli zao.Nina uhakika mkubwa
watakubali.Muda mfupi kabla ya mimi
kuhudhuria katika kikao hicho nataka
hoteli hiyo ilipuliwe na asitoke hata mtu
mmoja”
Ernest akanyamaza akamtazama
Lameck
“Mheshimiwa rais naomba
usinielewe vibaya lakini awali
ulinieleza kuwa hata mkeo naye ni
mfuasi wa imani au mtandao huu wa
Alberto’s tena ni mtu mwenye nafasi ya
juu.Si yeye tu bali hata makamu wa rais
na sehemu kubwa ya wabunge.Endapo
mpango huu utatekelezwa ni wazi
hakuna atakayetoka hai ndani ya hiyo
hoteli akiwemo pia mkeo .Swali langu ni
je una uhakika na hiki unachotaka
kukifanya mheshimiwa rais? Akauliza
Lameck
“ My wife is a devil.Si mwanamke
wa kuonewa huruma hata kidogo.Yeye
ni chanzo cha Alberto’s kuotesha mizizi
yao hapa Tanzania.Alitumiwa
 
SEHEMU YA 24


kunishawishi niwe rais ili Alberto’s
waweze kunitumia kwa manufaa
yao.Kwa hiyo hana thamani tena
kwangu wala kwa nchi” akasema
Ernest.Ukapita ukimya mfupi Lameck
akasema
“Huu utakuwa ni msiba mkubwa
sana ambao haujawahi kutokea kwa
taifa”
“ Ni kweli utakuwa ni msiba
mkubwa kwa sababu si hao tu
ninaotaka kuwafuta katika uso wa
Tanzania.”akasema Ernest
“ Kuna wengine tena zaidi ya hao?
Akauliza Lameck
“Ndiyo.Nataka dakika ambayo
hoteli walimo Alberto’s hapa dar es
salaam italipuliwa,mjini Dodoma pia
ukumbi wa bunge ulipuliwe”
Jenerali lameck akasimama na
kumtazama rais Ernest kwa mshangao
mkubwa
“ Mr President is this a joke?
“ No ! its not a joke.Ni kweli kabisa
nataka ukumbi wa bunge ulipuliwe tena
kwa bomu zito na asitoke hata mbunge
mmoja.”
“Mr President ..!! Lameck akataka
kusema kitu lakini rais akamzuia
“ Awali ulinieleza kwamba uko na
mimi na unaniunga mkono katika
mapambano haya.Kama kweli ulikuwa
unamaanisha maneno yako na una nia
ya dhati ya kutaka kuisafisha nchi hii
basi utakubaliana na hiki ninachotaka
kukifanya.”
“ Mheshimiwa rais niko pamoja
nawe katika mapambano haya lakini si
kwa kumwaga damu nyingi kiasi
hicho.Hakuna namna nyingine ya
kufanya kuwamaliza Alberto’s zaidi ya
hii unayotaka kuitumia?
“Nasikitika hakuna jeneral
Lameck.Kama unadhani una mawazo
mazuri zaidi nayakaribisha” akasema
rais na Lameck akabaki kimya
“Huna mawazo mbadala kwa hiyo
tunaendelea na mpango wangu.Sikiliza
Lameck watu hawa wamewekeza nguvu
kubwa bungeni.Kuna mambo mengi
ambayo wanataka kuyabadili zikiwemo
sheria mbali mbali za nchi hii na yote
hayo yatafanyikia bungeni .Kwa hiyo
bunge ni sehemu nyingine
waliyowekeza nguvu kubwa. Ninafikiria
kumteua waziri mkuu mpya lakini
lazima aidhinishwe na bunge na endapo
si mtu ambaye anakubalika na Alberto
basi hawezi kupitishwa kwani Alberto’s
wana idadi kubwa ya wabunge wafuasi
wao.Kitu kingine kibaya ni kwamba
wabunge wanaweza kupiga kura ya
kutokuwa na imani na rais na
wakaniondoa madarakani kisha
akawekwa mtu wao na kufifisha juhudi
zote za kuisafisha nchi.Siko tayari kwa
hilo kwa hiyo lazima niwawahi kabla
hawajaniwahi na kuniondoa.Nguvu ya
kupambana nao bado ninayo kwa hiyo
lazima niitumie.Hata kama
tukiwaondoa viongozi wao
tukawaaacha wabunge bado Albertio’s
watakuwa na nguvu kwa hiyo tukiamua
kuwaondoa basi tuondoe wote kabisa ili
wasipate tena nguvu ya kujipenyeza na
kuotesha mizizi yao hapa
Tanzania.Hawa ni watu wabaya mno
,tusiwafanyie mzaha hata
kidogo.Maamuzi tutakayoyafanya leo ni
kwa ajili ya watoto wetu,wajukuu na
vitukuu wetu.Bila kufanya maamuzi
magumu leo vizazi vyetu vitapotea
kwani lengo la Alberto’s ni kuwapoteza
wanadamu wengi kwa kufanya mambo
yale yasiyompendeza mwenyezi
Mungu.Ni heri tukapotea sisi kuliko
watoto wetu.kwa hiyo Lameck niunge
mkono tafadhali katika hili
ninalotakakulifanya” akasema rais
“Mheshimiwa rais nauona msingi
wa hoja yako na nina kubaliana nawe
kabisa lakini haya yatakuwa ni mauaji
makubwa ambayo hayajawahi kutokea
katika historia ya taifa hili.Kingine ni
kwamba utaendesha vipi serikali bila
bunge? Utatoa wapi fedha? Jambo la
tatu ni vipi endapo utafanyika
uchunguzi na ikabainika kwamba wewe
ndiye muhusika mkuu wa mauaji hayo?
Akauliza lameck
“ Kuhusu fedha za kuendesha
serikali hakuna tatizo kwani tayari
bajeti imekwisha pitishwa na bunge
 
SEHEMU YA 25

kwa hiyo fedha zipo.Tume ya uchaguzi
itatangaza uchaguzi mwingine wa
wabunge na hapo hakutakuwa na
Alberto’s tena.Watapatikana wabunge
wapya na nitaunda serikali ya watu
waaadilifu.Tutachafuka kwa damu za
watu tuliopoteza lakini nchi itakuwa
safi.Utakuwa ni msiba mkubwa si hapa
Tanzania pekee bali hata afrika na dunia
kwa ujumla lakini ni afadhali tukalia na
kuomboleza kwa mwezi au
mwaka mmoja kuliko watoto wetu
wakaenda kuangamia milele kwa
matendo yasiyofaa.Kuhusu kufanyika
uchunguzi ni kwamba hakutakuwa na
uchunguzi wowote utakaofanyika na
hakuna yeyote atakayejua kwamba sisi
tunahusika.Nitafanya makubaliano na
kikundi cha Alshabaab ambao
watajitangaza kuhusika na shambulio
hilo mara tu litakapotokea.”
“ Alshabaab?!! Hiki ni kikundi cha
kigaidi.Unataka kushirikiana na magaidi
hawa katika mpango huu? Akauliza
lameck
“Watakachokifanya hawa
Alshabaab ni kuutangazia ulimwengu
kuwa wao ndio wahusika wakuu wa
shambulio hilo lakini kila kitu
tutakitekeleza sisi.” Akasema rais
.Kukawa kimya
“Say something general Lameck”
akasema rais.Lameck akamtazama kwa
makini halafu akasema
“ Mheshimiwa rais wewe ni amiri
jeshi mkuu wa majeshi yote na sisi sote
tuko chini yako.Sisi ni watekelezaji tu
wa maagizo yako.Neno lako ni amri
kwangu kwa hiyo siwezi kupinga
chochote utakachoniagiza
nikifanye.Kwa kuwa tayari umekwisha
amua hivyo sisi tutatekeleza kwa hiyo
mheshimiwa rais maagizo yako
yatatekelezwa”
“ Good” akasema rais halafu
kukawa kimya tena.Baada ya muda
Ernest akasema
“ general Lameck I know you are
not comfortable with this but I have no
other way.This is difficult to me also but
I have no other way.Lazima niisafishe
nchi.Kutatokea mtikisiko mkubwa lakini
nakuahdi nitakulinda”
“ Thank you mr president” akajibu
Lameck
“ Kubwa unalopaswa kulizingatia
Lameck ni usiri.Hili ni jambo la siri
kubwa kati yangu nawe kwa hiyo
hapaswi mtu mwingine afahamu zaidi
ya wale makamanda utakaoona
wanafaa kushirikishwa katika jambo
hili.Onyo ni kwamba sintakuwa na
huruma kwa yeyote atakayevujisha juu
ya jambo hili”
“ Nitalizingatia hilo mheshimiwa
rais.” Akasema Lameck.
“ Good.Kikao cha bunge kinaanza
kesho kutwa kwa hiyo inatakiwa
mipango yote iwe imekamilika hadi
kufikia kesho jioni.Nataka kesho jioni
mimi na wewe tuonane ili tuweze
kupeana mikakati ya mwisho”
“Sawa mheshimiwa rais ,kwa
upande wangu hakutakuwa na
tatizo.Kuna ndege mbili za kivita
ambazo huruka juu ya anga la dar es
salaam kuimarisha ulinzi kila
siku.Ndege hizi huruka juu sana kiasi
kwamba si rahisi kuonekana.Kwa
kawaida ndege hizi huwa zimebeba
makombora mazito na huwa tayari
kushambulia muda wowote amri
ikitolewa.Ukiacha hapa dar es salaam
ndege hizi pia huruka mjini Dodoma
ambako ambako nako kuna ikulu ya
rais.Kwa hiyo mheshimiwa rais
tutazitumia ndege hizi na utakapotoa
amri yako tu sisi tunayasambaratisha
majengo hayo mawili Dar es salaam na
Dodoma.”
“ Nafurahi kusikia hivyo.Endelea
kulifanyia kazi hilo suala na kesho jioni
tutakutana na kupata
muafaka.Nafahamu kwa upande mmoja
hatufanyi sawa lakini kwa upande
mwingine tuko sawa kufanya hivi kwa
manufaa ya nchi.Uwe na siku njema
Jeneral Lameck.Nakutakia mafaniko
katika utendaji wa majukumu yako
mapya”akasema Rais na kuagana na
Lameck kisha akarejea ofisini kwake
“Haya ni maamuzi magumu mno
ambayo nimeyachukua kwa manufaa ya
nchi.Sioni namna nyingine ya
 
SEHEMU YA 26


kuwatokomeza hawa Alberto’s zaidi ya
hii ninayotaka kuifanya.Tayari
wamesambaa sehemu nyingi na
kuwaondoa mmoja mmoja itachukua
muda mrefu .Njia pekee ni kuwamaliza
wote kwa mara moja kwa
kuwalipua.Wabunge nao pia hawana
msaada wowote kwangu kwa
sasa.Siwezi kupata uungwaji mkono
kama nitaendelea kuwa na wabunge
hawa .Ili mambo yangu yaende vizuri
baada ya kuwamaliza Alberto’s lazima
na wabunge hawa niwaondoe pia
wote.Wapo wabunge safi ndani ya
bunge ambao si wafuasi wa Alberto’s
lakini ni wachache ukilinganisha na
idadi kubwa ya wabunge wafuasi wa
Alberto’s.Awali sikuwa nimefikiria
kufanya jambo kama hili lakini baada ya
kugundua kuwa hakuna msafi miongoni
mwa walionizunguka nimeona ni bora
nianze upya nitafute watu wapya” Rais
Ernest akatolewa mwazoni baada ya
mlango kufunguliwa akaingia Mukasha
“ Karibu Mukasha “
“ Ahsante sana mheshimiwarais”
akajibu Mukasha na kuketi
“ Mheshimiwa rais nimekuletea
orodha ile ya watu ambao ulinitaka
niwapendekeze kwa ajili ya uteuzi
katika baraza letu jipya .Hawa ni watu
waaminifu na waadilifu sana.Nimepata
majina kumi na tano ,utachagua
mwenyewe wale utakaoona wanafaa
lakini kwa upande wangu nimejiridhsha
kuwa wote wanafaa na ni watu safi”
akasema Mukasha.
“ Ahsante sana Mukasha
nitayafanyia kazi” akasema
Rais.Mukasha akataka kuinuka halafu
akaketi
“ Mheshimiwa rais haitakuwa
vyema endapo tutayajadili kwa pamoja
majina haya na kuchagua wanaoweza
kutufaa?
“ Ahsante Mukasha lakini kama
nilivyokueleza nitayapitia yote na
nitachagua mimi mwenyewe wale
nitakaaoona wananifaa.” Akasema
Ernest na Mukasha akainuka
“ Sawa mheshimiwa rais,pale
utakapokuwa tayari utanijulisha”
akasema na kuanza kupiga hatua
kuelekea mlangoni mara akasimama na
kugeuka
“ Mheshimiwa rais,bunge linaanza
vikao vyake kesho kutwa.Nadhani ni
wakati sasa wa kunitangaza kuwa
mbunge mteule ili nianze kujenga
marafiki bungeni na jina langu
litakapopelekwa bungeni kwa ajili ya
kuidhinishwa nipate uungwaji mkono
wa kutosha.” Akasema Mukasha huku
akitabasamu.Bila kumtazazma Mukasha
usoni rais akasema
“ Mukasha suala hilo ni juu yangu
kuamua ni lini nikutangaze kuwa
mbunge.Kuanza kwa vikao vya bunge
kusikupe shida.” Akasema rais huku
akiendelea na kazi zake.Mukasha
akaondoka
“Ernest kabadilika ghafla.Toka
asubuhi ya leo tulipoonana
hajanichangamkia kama
nilivyozoea.Namfahamu Ernest lazima
kuna kitu hakijakaa sawa.Hata
nilipompa ile karatasi ya majina kwa
ajili ya uteuzi hakuonekana kuipokea
kwa furaha.yawezekana tukio la
kupigwa risasi Austin limemfanya awe
hivi.ngoja nimpe muda .Sitakiwi
kumshinikiza.sasa ngoja nikaonanae na
Janet”akawaza Mukasha
 
SEHEMU YA 27



********************
Mukasha aliwasili katika hoteli
maarufu inayomilikiwa na mwanamama
mwenye asili ya kiarabu maarufu kama
Sakina.Hii ni moja kati ya sehemu
zinazotajwa kuwa na chakula kizuri
sana kiasi cha kuwavutia watu wengi
hata viongozi kwenda kupata
chakula.Tayari Janet alikwisha fika
mahala hapo na alikuwa akimsubiri
Mukasha.Aliposhuka garini Mukasha
akanyoosha moja kwa moja upande wa
nyuma alikokuwa amekaa Janet
“ Sorry I’m late” akasema Mukasha
huku akivuta kiti na kuketi akatazama
Janet na kutabasamu
“ Umezidi kupendeza Janet.Wakati
wenzako tunazidi kuzeeka wewe
unazidi kuchanua .Nini siri ya mafanikio
yako? Unazidi kumchanganya Ernest”
Akatania Mukasha na wote wakacheka
“ Acha utani Mukasha.Vipi
maendeleo yako? Ni muda umepita
hatujaonana” akasema Janet
“ Ni kweli Janet ni muda umepita
hatujaonana.Mambo siwezi kusema
kuwa ni mazuri kumekuwa na
changamoto nyingi za hapa na pale
lakini tunakabiliana nazo.Nina imani
nyote mmesikia kinachoendelea hivi
sasa lakini mambo yatatulia tu muda si
mrefu.Leo ameapishwa mkuu wa
majeshi na hivi karibuni atatangazwa
waziri mkuu mpya kwa hiyo mambo
yanatulia taratibu” akasema
Mukasha.Muhudumu akafika wakaagiza
chakula
“ Wilson what’s real going on?
Mbona rais amefanya maamuzi haya
makubwa ghafla sana kuna nini? Ninyi
watu wa karibu yake lazima
mnafahamu kinachoendelea” akasema
Janet
“ Hilo hasa ndilo lililonifanya
nikakuita hapa.Kusema kweli hata sisi
ambao tuko karibu na rais hatujui
chochote .Hata mimi ambaye ni msiri
wake mkubwa sifahamu na
hajanishirikisha katika maamuzi
yake.kwa ufupi ni kwamba katika haya
yanayoendelea rais anafanya peke yake
bila ushauri wa mtu.Haya yote yalianza
siku ile ulipoomba kukutana naye.”
Mukasha akanyamza akamtazama Janet
alivyobadilika
“ Mara tu ulipoachana naye siku ile
rais aliniomba nimtafutie mtu ambaye
ni mahiri katika upelelezi.Nilimtafutia
kijana mmoja anaitwa Austin ambaye ni
mtanzania mwenye uraia wa Afrika ya
kusini aliyewahi kufanya kazi katika
idara ya ujasusi wa taifa hadi alipoacha
na kuanza kufanya shughuli zake
binafsi.Haikuwa rahisi kumshawishi
Austin aje Tanzania kufanya kazi ya rais
hadi alipoahidi kumsaidia kumtoa
gerezani mdogo wake aliyefungwa
nchini China.Austin aliwasili nchini
tayari kwa kazi hiyo ya rais lakini mara
tu alipoonana naye wakazungumza na
ndipo upepo ulipoanza kubadilika na
haya yote yakatokea.Amevunja baraza
la mawaziri ,akamvua madaraka mkuu
wa majeshi na mambo mengine
anayoendelea kuyafanya.Mambo haya
anayoyafanya Ernest yameufanya
usalama wake kuwa mdogo baada ya
kutengeneza maadui wengi.Jana usiku
Yule kijana aliyemleta toka afrika ya
kusini kumfanyia kazi zake,alipigwa
risasi na watu wasiojulikana na hivi
sasa yuko katika hati hati ya kupoteza
maisha.Sote tunajiuliza kuna nini
kinaendelea? Kazi gani ambayo Ernest
amempa Austin aifanye? Maswali kama
haya ndiyo yamenileta kwako nikiamini
nitapata majibu.Ninachokihitaji
kufahamu ni kitu gani ulioongea na rais
siku ulipokutana naye? Mimi ni rafiki
yako na rafiki wa Ernest pi,ni msiri
wenu nyote kwa hiyo Janet nisaidie
nifahamu mlichoongea siku ile”
akasema Mukasha .Janet akamtazama
Mukasha
“ Please Janet “ akasisitiza
Mukasha
“ Mukasha nilichoongea na Ernest
siku ile hakihusiani kabisa na haya
yanayoendelea kutokea.Tuliongea
masuala yetu binafsi yanayohusiana
nasi na hatukuongea chochote kuhusu
serikali” akasema Janet
 
SEHEMU YA 30



anet hicho mlichokiongea ndicho
hasa kilichombadilisha Ernest .Kuwa
muwazi kwangu tafadhali.Usiogope
kunieleza hata yale masuala ya ndani
kabisa.Hakuna cha kunificha”
akaendelea kusisitiza Mukasha.Janet
akamkazia macho na kusema
“ I’m sorry Mukasha siwezi
kukueleza chochote.Mambo tuliyoongea
mimi na Ernest ni mambo binafsi na
hayahusiani chochote na haya
yanayoendelea.Naomba uniamini
tafadhali. Mukasha wewe ni mtu wa
karibu na rais na ni mtu wangu wa
karibu pia lakini siwezi kukueleza
mambo binafsi ninayoongea na
rais.Fahamu neno binafsi linamaamisha
nini.Ni mambo yanayonihusu mimi na
yeye pekee.Kwa hiyo Mukasha naomba
niwe wazi kwako kwamba siwezi
kukuambia tulichoongea na rais”
akasema janet
“Ulipoongea naye ndipo alipoanza
kutafuta mtu wa kumfanyia kazi
yake.Lazima kazi hiyo ambayo amempa
Austin amfanyie unaifahamu kwani
imetokana na maongezi yenu siku
ile.Sikulazimishi unieleze mambo yenu
ya siri lakini lengo langu ni zuri kutaka
kumsaidia rais.Ninakuomba kwa mara
ya mwisho unieleze nini ulimwambia
Ernest?
Janet akaonekana kukerwa na
Mukasha ,akainuka
“Mukasha naona
hatuelewani.Nimekwambia kwamba
mambo tuliyoongea mimi na Ernest ni
binafsi.Kama unahitaji kufahamu nenda
kamuulize Ernest.Ahsante kwa
kunipotezea wakati wangu” akasema
Janet na kunyakua mkoba wake
akaondoka.Uso wake ulikuwa
umejikunja kwa hasira
“ janet !! janet !! ..akaita Mukasha
lakini janet hakugeuka Mukasha
akagonga meza kwa hasira
“Najua kuna kitu ananificha huyu
mwananme,hata hivyo sikati tamaa
nitaendelea kumchimba hadi niufahamu
ukweli” akawaza Mukasha akachukua
simu yake na kuzitafuta namba za Boaz
akapiga lakini simu
haikupokelewa.Akainuka na kuondoka
Janet alisimamisha gari kituo cha
mafuta akajaza mafuta halafu akasogeza
gari pembeni akachukua simu na
kuzitafuta namba za Ernest akampigia
“ Janet nimekwisha kupa
maelekezo kwamba usinipigie katika
namba hii labda kama una jambo kubwa
la kunieleza” akasema Ernest mara tu
alipopokea simu ya Janet
“ hallow Ernest.Umesahau hata
kusalimia?
“ Oh ! I’m sorry Janet . How’re you?
“I’m ok.Vipi wewe unaendeleaje?
“ Ninaendelea vizuri .How’s
Monica?
“ Monica anaendelea vizuri.”
“ Haya niambie kuna jambo gani
hadi ukaamua kunipigia ?
“ Ernest we need to talk”
“ Talk ?!
“ Yes.We need to talk”
“ tuongee kuhusu nini?
“ Siwezi kukueleza katika
simu.Naomba tuonane tafadhali”
“ Janet nina mambo mengi
makubwa ninayoshughulikia hivi sasa
kwa hiyo usiponieleza maongezi hayo
yanahusu nini itakuwa vigumu kwangu
kuonana nawe”
“It’s about Monica”
Ernest akastuka
“ Monica kafanya nini?
“ Nina wasi wasi na usalama wake”
Ernest akafikiri kidogo na kusema
“ Ninaelekea Kobwe hospital kuna
mtu naenda kumuona amelazwa
pale.Naomba tukutane hapo hospitali “
akasema Ernest na kukata simu
“ Lazima Monica atakuwa katika
hatari .Nitamlinda kwa nguvu zangu
zote” akawaza Ernest .
********
 
SEHEMU YA 31



nica aliendelea na kazi zake
lakini kila mara alikuwa anaitazama saa
yake ili asichelewe kwenda kumtazama
Austin mchana
“ Nimeguswa sana na hiki
kilichomtokea Austin.Kwa nini
binadamu wanakuwa wakatili kiasi
hiki? Siku hizi kutoa uhai wa mtu
imekuwa ni kitu cha kawaida
sana.Natamani kusikia watu waliofanya
shambulio hili wanakamatwa na
kufikishwa mbele ya sheria.Nina bahati
mbaya ,nimepata marafiki wawili na
wote ndani ya siku chache za
kufahamiana nao wamepigwa risasi na
watu wasiojuilikana.Lakini nashukuru
Mungu kwani wote wawili wako salama
kabi..” Mnoca akatolewa mawazoni
baada ya simu yake kuita.Alikuwa ni
David Zumo.Haraka haraka akabonyeza
kitufe cha kupokelea
“Hallow mpenzi.habari yako?
Akasema Monica huku uso wake ukiwa
na tabasamu kubwa
“ Hallow malaika wangu .Vipi hali
yako?
“ Mimi mzima kabisa.Nimekutafuta
sana asubuhi ya leo simuni lakini
hukuwa ukipatikana”
“ Utanisamehe sana malaika
wangu .Sikuweza kupatikana asubuhi ya
leo,hali ya Pauline ilibadilika ghafla
usiku wa kuamkia leo .Madaktari
wamehangaika usiku mzima hata hivyo
imebidi asafirishwe haraka sana
kwenda Ufaransa ili akafanyiwe
upasuaji wa kichwa.Mimi najiandaa
nielekee huko pia.Nimeamua nikupigia
nikujulishe kinachoendelea huku ila
naomba usihofu sana Mungu yuko nasi
na kama ikimpendeza anaweza
akamuongezea Pauline maisha maerefu
zaidi lakini kwa hali aliyokuwa nayo
wakati anasafirishwa tujiandae kwa
lolote linaloweza kutokea.Yote haya ni
mapenzi ya Mungu na lolote
litakalotokea inatubidi tulipokee na
kumshukuru yeye” akasema David na
kukawa kimya.Monica alikosa neno la
kusema ,macho yake yalijaa machozi
akashindwa kujizuia kulia kwa kwikwi.
“ Monica !! ..akaita David baada ya
kumsikia Monica akilia kwa kwikwi
“ David nimeshindwa kujizuia”
“ Pole Monica lakini hupaswi
kulia.Unapaswa kuwa
jasiri.Tumuombee Pauline.Nitakupigia
simu nikiwa ufaransa kwani naambiwa
ndege yangu iko tayari.Kabla sijaondoka
napenda kukufahamisha kwamba
ninatuma ujumbe wangu kuja kuonana
na wazazi wako ili kuanza mara moja
taratibu za uchumba.Ujumbe wangu
una watu ishirini na saba .wataondoka
leo saa tisa alasiri na kesho watakutana
na wazazi wako.kwa hiyo naomba
ufikishe taarifa hizi kwa wazazi ili
mfanye maandalizi ya kuupokea ugeni
huo”
“ David huwezi kuahirisha kwa
muda suala hili hadi hapo hali ya
Pauline itakapokuwa nzuri?Najihisi
vibaya sana kuendelea na mchakato huu
wakati Pauline yuko hoi”
“ Usihofu malaika wangu.Hali hii
ya Pauline haiwezi kuzuia masuala
mengine yasiendelee.Suala la mimi na
wewe kuoana ni suala ninalolipa
umuhimu mkubwa sana.Hakuna
kinachoweza kuuzuia mchakato huu
usiendelee.Lolote litakalotokea lazima
mchakato huu usonge mbele.Naomba
ufanye maandalizi ya kuwapokea hao
wajumbe niliowatuma.Naomba
nikuache malaika wangu nitakupigia
nikiwa ufaransa.Uwe na siku njema”
akasema David na kukata simu
“ Taarifa mbaya bado zinaendelea
kuniandama .Hii taarifa ya Pauline
imenitoa macozi.Ni mwanamke
mwenye upendo wa ajabu sana.Siwezi
kuusahau ucheshi na ukarimu
wake,alinipokea kwa upendo mkubwa
sana nilipokwenda Congo.Kwa moyo
mkunjufu kabisa akanishawishi nikubali
kuolewa na mume wake.Hakuna
mwanamke katika dunia hii ya sasa hata
kama anajua hana maisha marefu
atakubali kumuona mume wake akioa
mwanamke mwingine lakini kwa
Pauline imekuwa tofauti .Namuombea
apate nafuu ya haraka na maisha
marefu” akawaza Monica na kufuta
machozi
“ Sasa naamini kweli David
amedhamiria kunioa.Kuamua kuutuma
ujumbe uje Tanzania ni hatua
kubwa.Nitawajulisha wazazi ili tufanye
maandalizi ya kuupokea ugeni huo
mkubwa japokuwa imekuwa ni ghafla
sana.kwa sasa ngoja niende hospitali
kumtazama Austin halafu nikitoka huko
nitakwenda kuonana na wazazi
nyumbani kuwapa taarifa hizi njema.”
Akawaza na kuingia katika kijichumba
kidogo ndani ya ofisi yake akarekebisha
uso na kuondoka kuelekea hospitali
 
SEHEMU YA 32

ukasha alirejea ikulu na moja
kwa moja akaelekea katika chumba cha
mawasiliano na kumbu kumbu na
kunyooka moja kwa moja katika meza
ya Irene
“Irene tunaweza kuongea kwa
dakika mbili? Mukasha akamueleza
mwanadada mmoja aliyemkuta ndani
ya kile chumba .Irene akaacha kazi
aliyokuwa anaifanya akamfuata
Mukasha wakaenda pembeni kidogo
“ Irene juzi uliniomba nikusaidie
uonane na rais.Ulikuwa na tatizo gani?
“ Lilikuwa ni tatizo binafsi ambalo
nilitaka kumuomba rais anisaidie”
“ Ni tatizo gani? unaweza
kunieleza?
“ Ni suala binafsi mzee Mukasha”
akasema Irene
“ Usiogope kunieleza
Irene.Ninaweza kukusaidia”
Irene akatazama pande zote kama
kuna mtu maeneo yale halafu akasema
“ Baba yangu ni mgonjwa sana ana
tatizo la ini anatakiwa apelekwe nje ya
nchi akapandikizwe ini lakini mpaka leo
tumekuwa tunapigwa dana dana
wakitutaka tugharamie wenyewe
matibabu.Sisi hatuna uwezo huo na
ndiyo maana nilihitaji kuonana na rais
nimuombe msaada wake anisaidie baba
yangu aende nje ya nchi “ akasema
Irene
“ Hilo ni tatizo dogo sana Irene na
ninaweza kukusaidia leo hii hii kibali
cha kumpeleka mzee wako nje ya nchi
kikapatikana.Anazo pasi za kusafiria?
“Kila kitu kiko tayari .Ni kibali tu
ndicho tunachokisubiri”
“ Good.Nitakusaidia na utakipata
kibali leo hii”
“Ahsante sana mzee
Mukasha.Jambo hili limekuwa
linanikondesha .Sijui nikushukuruje
mzee Mukasha” akasema Irene kwa
furaha .Mikasha akatabasamu na
kusema
“Irene hesabu kuwa jambo hilo
limekwisha na leo utakipata kibali
lakini na mimi kuna kitu nataka
unisaidie”
“ Kitu gani mzee Mukasha?
Akauliza Irene kwa wasi wasi
Mukasha akatazama kama kuna
mtu maeneo yale ya karibu
anayewasikia na alipohakikisha wako
wenyewe akasema
“ Nataka unisaidie kudukua simu
ya rais.Nataka kujua ameongea na nani
leo na wameongea nini.Ukinitekelezea
hilo tu basi kibali unakipata haraka
sana”
Irene akamtazama Mukasha kwa
mshangao
“ Kudukua simu ya rais?? Akauliza
“ Sikiliza Irene,rais yuko kwenye
hatari hivi sasa na watu tulio karibu
naye tuna jukumu la kumlinda.Sitaki
kuongea mengi zaidi katika
hilo.Nifanyie kazi yangu uokoe uhai wa
baba yako”
Irene akahisi kuchanganyikiwa
akawaza kwa muda na kusema
“ Simu anayotumia rais haiwezi
kudukuliwa.Imewekewa mfumo
maalum wa kuzuia kudukuliwa kwa
hiyo suala hilo ni gumu na
haliwezekani”
“ C’mon Irene,wewe ni mtaalamu
mkubwa na wa pekee kabisa hapa ikulu
na ndiye tunayekutegemea na
kujivunia.Do something.Ninajua
unaweza kufanya hiyo kazi na hujawahi
shindwa na kitu chochote kile naamini
hata kwa hili huwezi
kushindwa.Nisaidie nami
nikusaidie”Akasema Mukasha
.Wakatazamana kwa muda Irene
akasema
“ Let me see what I can do.Lakini
naomba nikikufanyia kazi yako nikipate
kibali hicho mara moja.Jambo hili ni la
hatari na endapo nitagundulika
nninaweza kwenda gerezani
nikamuacha baba na familia yangu
wanateseka.”
“Usihofu Irene nitakulinda”
akasema Mukasha
“Sawa nitajaribu kuifanya kazi
yako.Tunatakwia kwenda katika
chumba chenye kompyuta kubwa za
kuhifadhi kumbu kumbu zote.Nisubiri
hapa nikachukue kompyuta yangu”
akasema Irene na kwenda kuchukua
kompyuta yake mpakato.Wakati
wakielekea katika chumba chenye
kompyuta kubwa za kuhifadhia kumbu
kumbu Mukasha akachukua simu na
kupiga kwa katibu mkuu wizara ya afya
na kumtaka aandae kibali cha
kumpeleka nje ya nchi baba yake Irene
kwa matibabu.Irene alifurahi sana
aliingia katika chumba kile
chenye kompyuta za kuhifadhia kumbu
kumbu .Irene akaanza kufanya kazi
yake huku Mukasha akitazama bila
kuelewa alichokuwa anakifanya.Baada
ya dakika zaidi ya kumi na tano Irene
akasema
“ Got it!!
“ Real ?? akauliza Mukasha
“ Yes”
“I knew you can do it” akasema
Mukasha kwa furaha
“ Nataka ufuatilie kuanzia leo
asubuhi ameongea na nani?
Irene akabonyeza haraka haraka
kompyuta yake na kusema
“ Leo asubuhi amepiga simu sita
nje ya nchi.Ni simu nne tu za ndani
alizopigiwa”
“ Ok nataka kuzifahamu simu hizo
amempigia nani?akauliza Mukasha
 
Lege acha utani bana shusha vitu miez yote hii unashusha sehem saba tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…