SEHEMU YA 1 SEASON 5
Jenerali Lameck msuba aliwasili
ikulu kuitika wito wa rais aliyemtaka
afike ikulu mara moja usiku
ule.Wakaelekea moja kwa moja
chumba cha maongezi ya faragha.
“Lameck samahani sana kwa
usumbufu huu mkubwa mida hii”
akasema rais
“Bila samahani mheshimiwa rais
.Sisi ni walinzi wa nchi na tuko kazini
muda wote kwa hiyo kuniita hapa si
kunipotezea muda wala usumbufu
bali ni sehemu yangu ya kazi.”
Akasema Lameck
“ Ahsante Lameck.Nimelazimika
kukuita hapa usiku huu
kukufahamisha kuhusu jambo moja la
dharura.Kama utakumbuka asubuhi
nilikueleza kwamba nitazungumza na
kiongozi mkuu wa kikundi cha
Alshabaab kuhusiana na ule mpango
wetu ili mara tutakapoutekeleza basi
wao wajitokeze na kuitangazia dunia
kwamba wao ndio waliohusika na
tukio hilo.Nimefanikiwa kupata
mawasiliano ya mkuu wa Alshabaab
anaitwa Habib, tumezungumza na
amelikubali ombi langu”
“ That’s good Mr President”
akasema Lameck huku akitabasamu
“Hata hivyo kuna mambo mawili
wanayoyataka ambayo ndiyo
yamenifanya nikuite hapa usiku huu”
“ Alshabaab wanahitaji nini
mzee? Akauliza Lameck.Rais akasita
kidogo halafu kusema
“Kwanza kabisa wanamuhitaji
mwanamke mmoja anaitwa Yasmin
Esfahani.Wanadai mwanamke huyo
amefungwa mahala pa siri hapa
Tanzania kwa zaidi ya miaka kumi
sasa.Simfahamu mwanamke huyo na
wala sina taarifa zake zozote lakini
nina hakika nitazipata taarifa zake na
nitamuachia huru kama
wanavyotaka.Hilo si jambo gumu
sana kwangu” akanyamaza kidogo na
kuendelea
“Jambo la pili walilolitaka
ambalo limenipa mstuko mkubwa ni
kwamba jamaa hawa wanahitaji hati
ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.”
Jenerali Lameck Msuba
akanyanyuka na kumtazama rais kwa
macho makali
“ Wanataka hati ya muungano?
akauliza
“Ndiyo wanataka hati ya
muungano “ akajibu rais na kumfanya
Lameck atoe kicheko kidogo
“Usicheke Lameck haya ni
mambo mazito sana na ndiyo maana
nimekuita hapa ili tusaidiane
mawazo”
“Mheshimiwa rais hiki kitu
walichokitaka hawa Alshabaab ni
kichekesho kikubwa na ndiyo maana
nimecheka kwani siku zote hawa
jamaa wanachokitafuta ni fedha za
kujiendesha na kununulia silaha
.Inashangaza kusikia leo hii wanataka
kitu kama hati ya
muungano.Wameacha kutaka
wapewe pesa ,au silaha au kitu
kingine chochote kwa nini wakaitaka
hati hiyo? Akasema Lameck
“Swali hilo hata mimi nimejiuliza
mara nyingi sana bila kupata
jibu.Naona akili yangu imefika
mwisho wake wa kufikiri hivyo
nimekuita hapa ili tusaidiane
mawazo.” Akasema rais
“Mheshimiwa rais ,hata mimi hili
jambo limenichanganya mno na
sielewi kwa nini Alshabaab wanaitaka
hati ya muungano.Ulijaribu
kuwaomba wachague kitu kingine
badala ya hiyo hati? Akauliza Lameck
“Ndiyo niliwaambia hicho
wanachokitaka hakiwezekani na
wakasema hawataweza kufanya kazi
yangu hila kuwapa
wanachokihitaji.Watanipigia simu
kesho jioni kupata jibu.Nyaraka
wanayoitaka ni muhimu na
inayolindwa zaidi ya mboni ya
jicho.Zipo nyaraka tatu ambazo ni
kiini cha uwepo wetu kama taifa
,jamhuri na muungano huru.Hizi ni
hati ya uhuru wa Tanganyika ya
mwaka 1961,hati ya Tanganyika kuwa
jamhuri ya mwaka 1962 na hati ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ya mwaka 1964.Kila rais
aingiaye madarakani hukabidhiwa
hati hizi azilinde na ndiyo maana
huhifadhiwa maeneo maalum ambayo
ni salama ili zisipotee wala kuharibika
na huwa hazitolewi.Hati ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ikitoweka hii inamaanisha
kwamba hakuna tena kitu kinachotwa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania.”akasema rais
“Mheshimiwa rais jambo hili
haliwezekani kabisa.Hicho kitu
wanachokitaka hawawezi
kukipata.Kwa kuwa suala hili
haliwezekanai hii ina maana hata ule
mpango wetu wa kulipua yale
majengo mawili kesho hautawezekana
tena”akasema Lameck
“Hapana Lameck ule mpango
wetu uko pale pale.Bila kufanya hivyo
Alberto’s hawatamalizika hapa nchini
na wataharibu nchi hii kabisa.Vizazi
vijavyo vitaisoma Tanzania ya maziwa
na asali vitabuni.Sitaki hilo
litokee.Nataka wafurahie kuzaliwa na
kuishi Tanzania.Sitaki kuwapa
Alberto’s nafasi kwa hiyo ulipuaji uko
pale pale.Alberto’s lazima niwafagie
wote!!! Akasema Ernest kwa ukali
“Mheshimiwa rais tukio kama
hilo ambalo makamu wa rais na
viongozi wengine watauawa pamoja
na idadi kubwa ya wabunge
halitaweza kupita hivi hivi bila
kufanyika uchunguzi wa
kina.Vyombo vya ndani na nje
vitalichunguza suala hili na inaweza
kubainika kwamba tunahusika na
jambo hili na adhabu yetu
tukigundulika ni kifo.Hakuna
atakayesimama upande wetu hata
kama tumeyafanya haya kwa nia
njema ya kuisafisha nchi yetu.”
Akasema Lameck.Rais akamtazama
kwa muda na kusema
“Kwa hiyo unanishauri nini
Lameck?
“Mpango wa kuwashirikisha
Alshabaab ulikuwa mzuri sana kwani
endapo wangejitokeza baada ya tukio
na kutangaza kuhusika na tukio hilo
na tungeweza kuzungumza nao ili
tufanye mashambulio mawili katika
kambi zao ili kuwadhihirishia
watanzania na ulimwengu kwamba
tumekasirishwa na tumeanza
kuchukua hatua hiyo ingepunguza
hasira kwa raia.Hiyo ingepunguza
shinikizo la kufanyika uchunguzi
kwani tayari muhusika atakuwa
anajulikana.Bila ushiriki wa
Alshabaab mpango huu utakuwa
mgumu mno kutekelezeka na endapo
ukifanyika lazima watanzania na
dunia watataka uchunguzi ufanyike
na lazima tutagundulika kuwa ni sisi
ndio tuliohusika na shambulio
lile.Kwa hiyo mheshimiwa rais kama
Alshabaab hawapo basi nakushauri
tuachane na ule mpango na tutafute
namna nyingine ya kuwaondoa
Alberto’s kuliko hii ya kuwaua wote
kwa kuwalipua” akasema Lameck
.Rais Ernest akainamisha
kichwa.Alionekana kuzidiwa na
mawazo.Kikapita kimya cha dakika
kama nne kila mmoja akitafakari kisha
rais akasema
“Lameck nakubaliana na
mawazo yako lakini pamoja na hayo
hakuna njia nyingine za kuwaondoa
Alberto’s zaidi ya hii ninayotaka
kuichukua.Ninawafahamu vizuri
hawa jamaa na ndiyo maana nataka
kuwafagia wote.Nazifahamu athari
zao kwa nchi na kwa vizazi
vyetu.Kwa vyovyote vile siwezi
kuwaacha .Lazima niwafyeke.Kwa
hiyo Lameck ,pamoja na ufafanuzi
mzuri ulionipa siwezi kubadili
msimamo wangu kuhusu
Alberto’s.Uamuzi wangu wa
kuwalipua utaendelea kusimama pale
pale.Kama lipo jambo lolote
litakalotokea na litokee lakini siwezi
kuwaacha Alberto’s wakaendelea
kuipeleka nchi katika shimo.Athari
zao ni kubwa zaidi ya unavyofikiri”
akasema rais
“Mheshimiwa rais,siwezi katu
kuyapinga maamuzi yako ila
nilichokifanya mimi ni kukupa
ushauri kuhusu jambo hili.Kama
unataka tuendelee hakuna wasi wasi
mimi niko pamoja nawe lakini lazima
ufahamu kuwa kutatokea msuko suko
mkubwa na endapo tutabainika kuwa
ni sisi tuliotekeleza shambulio hilo
tutaozea gerezani” akasema lameck
“ Kwa wakati huo hakutakuwa
na Alberto’s tena hapa
nchini.Usiogope Lameck hili jambo
lazima lifanyike na nitatumia kila
nguvu niliyonayo kulikamilisha.Hata
hivyo lazima nihakikishe
ninakubaliana na Alshabaab” akasema
rais na Lameck akastuka
“Bado unataka kuendelea na
Alshabaab?Unadhani wanaweza
kukubaliana nawe bila kuwapatia
wanachokihitaji yaani hati ya
muungano? Akauliza Lameck.Rais
akatafakari kidogo na kusema
“Kipi bora Lameck,kuuvunja
muungano au kuwaacha Alberto’s
waiharibu nchi na kuharibu kizazi
chetu?Muungano ni bora zaidi kuliko
kuwaokoa watoto wetu wasishiriki
mambo machafu yasiyompendeza
Mungu na mwisho wa maisha yao
wakaenda kupotea? Lameck sote ni
waumini na tunaamini katika Mungu
kwa hiyo tunaamini kuwa kuna
hukumu ya mwisho na wote wenye
kutenda maovu
wataangamia.Dhumuni kuu la hawa
wanaojiita Alberto’s ni kuwafanya
watu wamuasi Mungu kwa kutenda
matendo yale ambayo hayaendani na
matakwa ya Mungu .Mambo kama
utoaji mimba ni dhambi kubwa na
Mungu katika amri zake anakataza
kwamba tusiue lakini hawa Alberto’s
wanahalalisha kuua kwa kupigania
utoaji mimba.Mambo kama mapenzi
ya jinsia moja hakuna andiko hata
moja lenye kuruhusu mambo kama
haya ambayo ni machukizo makubwa
mbele za Mungu.Kwa hiyo Lameck
,tukiwaacha hawa jamaa waendelee
na mipango yao kizazi chetu
kinakwenda kuangamia.Narudia tena
ni afadhali tukaangamia sisi kuliko
watoto wetu.Mimi nadhani hati ya
muungano haiwezi kuwa bora kuliko
kuwafagia mashetani hawa.Ukipima
katika mzani utaona ni heri nchi
ikagawanyika vipande viwili kuliko
kuendelea kuwapa nafasi hawa
Alberto’s” akasema rais
“Mheshimiwa rais tafadhali
usifanye hivyo.Kama umeamua
kuendelea na mpango wa kuwafagia
Alberto’s ni afadhali tukaendelea na
mpango huo sisi wenyewe bila
kuwashirikisha Alberto’s.Niko tayari
kusimama kama mkuu wa majeshi
pale itakapothibitika kuwa
nimehusika na nitaitangazia dunia
mimi ndiye muhusika mkuu na
sintokuhusisha wewe lakini naomba
usithubutu kutoa hati ya muungano
kwa Alshabaab.Muungano huu
umelindwa kwa gharama kubwa sana
na wazee wetu hadi tumefika hapa na
umekuwa ni muungano wa mfano
duniani.Hata wewe wakati
unaapishwa uliapa kuulinda na
kuutetea muungano iweje leo ufikirie
kuuvunja?Nakuomba mheshimiwa
rais usifanye hivyo” akasema Jenerali
Lameck.Ukimya ukatawala mle
chumbani.Rais Ernest akafungua
mkebe akatoa sigara kubwa akawasha
na kuvuta mikupuo kadhaa.Baada ya
muda akasema
“Lameck nilikuita hapa ili
tushauriane kwa pamoja tufanye
nini.Ushauri wako nimeusikia lakini
sitaki kukuingiza wewe na
makamanda wote watakaoshiriki
katika mpango huu katika matatizo
makubwa.We must protect
them.Wanafanya jambo kubwa kwa
ajili ya nchi kwa hiyo lazima
tuwalinde wasipate matatizo baada ya
kuifanya kazi tuliyowatuma na ndiyo
maana nataka Alshabaab waubebe
mzigo huu kwa niaba yetu.Wataubeba
mzigo huu pale nitakapowapatia hati
ya muungano.Uamuzi wangu mimi ni
kuwapata kitu
wanachokihitaji.Kitakachotokea baada
ya hapo nitakabiliana nacho .Hati
kama hii ipo pia umoja wa mataifa
kwa hiyo hata kama tukiwapa hii
bado hakutakuwa na tatizo kwani
umoja wa mataifa bado utaendelea
kuitambua jamhuri ya muungano wa
Tanzania .Kwa hiyo Jenerali Lameck
naomba tukubaliane katika hilo ili
nchi yetu iweze kusonga mbele na
tufanikiwe kuwaondoa hawa
mashetani katika ardhi ya Tanzania “
akasema Ernest.Ukimya ukatawala
tena chumba kile huku Ernest
akiendelea kuvuta mikupuo ya sigara
“Mheshimiwa rais” akauvunja
ukimya Lameck
“Narudia kauli yangu
niliyokwambia leo asubuhi kwamba
wewe ni amiri jeshi mkuu na sisi sote
tuko chini yako.Hakuna wa kuipinga
kauli yako kwa hiyo basi kama
umeamua kulikubali takwa la
Alshabaab hakuna
atakayepinga.Tunachopaswa kufanya
sisi ni kuanza kujiandaa kukabiliana
na matokeo yatakayosababishwa na
maamuzi yetu .Kutatokea misuko
suko mingi mikubwa na nchi
itayumba lakini wajibu wangu mimi
kama mkuu wa majeshi ni
kuhakikisha nchi inakuwa
salama.Hata hivyo bado ninao ushauri
mdogo kama utakuwa tayari”akasema
Lameck
“Nakusikia Lameck”
“Ushauri wangu ni vipi endapo
tutaiwekea kitu Fulani hati hiyo kabla
hujawakabidhi Alshabaab ili baada ya
wao kujitangaza kuwa ndio
waliotekeleza shambulio tuanze
kuifuatilia mahala ilipo na kuirudisha
ikulu?Nadhani hapo tutakuwa
tumeua ndege wawili kwa jiwe moja
na nchi yetu itabaki salama.Unaonaje
mpango huo mheshimiwa rais?
Akauliza lameck
“Mpango huo ni mzuri lakini
unaweza ukatuletea matatizo
makubwa nchini kwetu kwani
tutakuwa tumetangaza vita na
Alshabaab na unafahamu ukiiingia
katika vita na hawa jamaa basi vita
hiyo haimaliziki na wanafanya
mashambulio ya kustukiza.Nadhani
unaona yanayoendelea katika nchi
majirani zetu.Kama ni nchi kuvunjika
acha ivunjike lakini si kusababisha
umwagaji mkubwa wa damu hapo
baadae.” Akasema Ernest
“Kwa hiyo Lameck” akaendelea
rais
“Suluhisho pekee hapa ni
kuwapatia Alshabaab kitu
wanachokihitaji ambacho ni hati ya
muungano.Baada ya hapo tujiandae
kukabiliana na kile kitakachotokea.”
Akasema rais na kukawa kimya
“Lameck nadhani tumekubaliana
katika hilo suala .Kama bado una
dukuduku niambie tafadhali.Mimi na
wewe tunapaswa kuwa katika
ukurasa mmoja na tukitoka hapa
tutoke na azimio moja nini
tunakwenda kufanya.” Akasema rais
“Mheshimiwa rais,mimi ni
mtekelezaji wa maagizo yako kwa
hiyo sina lolote la kupinga au
kuongeza kwa yale ambayo tayari
umekwisha yafanyia
maamuzi.Tunakwenda sawa
mheshimiwa rais” akasema Lameck
“Good” akasema rais kisha
wakaendelea na maongezi mengine
wakipeana mikakati kadhaa namna ya
kuutekeleza mpango wao.Baada ya
majadiliano marefu Lameck
akaondoka
“Siamini kama jambo hili la
kuwamaliza Alberto’s limenifikisha
mahala hapa pa kuhatarisha uhai wa
nchi.Lakini swali linalonila ubongo
wangu kwa sasa ni kwa nini
Alshabaab wametaka hati ya
muungano ?Lengo lao ni kuuvunja
muungano au nini hasa wanataka
kuifanyia hati hiyo?” akawaza na
kuinamisha kichwa
“Siwezi kupata jibu la swali hili,
kitu cha msingi kwa vile tayari
nimefanya maamuzi ya kuwapatia
hati hiyo natakiwa kujiandaa
kukabiliana na kile kitakachotokea
baadae.”Rais akatolewa mwazoni na
simu yake iliyoita.Mpigaji alikuwa
Evans
“Evans.Kazi umeimaliza?
Akauliza rais baada ya kuipokea simu
ya Evans
“Hapana mzee,kuna tatizo
limetokea.Nakuja huko kwako sasa
hivi kukueleza ana kwa ana
kilichotokea” akasema Evans na rais
akakata simu kwa hasira.
“Evans ameshindwaje
kummaliza Mukasha? Akajiuliza rais
huku akionekana kuchanganyikiwa
“Hili ni suala lingine limeibuka
.Nashindwa kuelewa imetokeaje hadi
Evans akashindwa kummaliza
Mukasha?Ninamuamini sana na ndiyo
maana nikamtuma aifanye hii
kazi.Ameniangusha sana huyu
kijana.” Akaendelea kuwaza rais
halafu akachukua simu na kumpigia
tena Evans.
“Hallo mzee” akasema Evans
“Uko wapi wewe mida hii?
“Niko njiani ninakuja huko
kwako mzee” akajibu Evans
“Hebu nieleze what real
happened?akauliza rais
“Siwezi kukueleza katika simu
mzee.Nitakueleza kila kitu nikifika
hapo muda si mrefu.Nimekaribia
sana” akasema Evans na rais akakata
simu
“Mukasha ni mtu amabye
hatakiwi kabis kauendela kuishi.Ni
mtu hatari sana kwangu kwa
sasa.Kwa namna yoyote ile lazima
Mukasha nimuondoe” akawaza rais