SEHEMU YA 91
wengine sita wakaelekea meza kuu.Kabla
ya kikao kuanza yakafanyika maombi
halafu wimbo wa maalum wa kumtukuza
Alberto mkuu ukaimbwa huku ubani
ukifukizwa na baada ya hapo kikao
kikaanza.
“ Ndugu wajumbe ,tumekutana hapa
kwa dharura ili tujadili kile ambacho
kimetokea leo.Kilichotokea leo ni anguko
kubwa ambalo halijawahi kutokea tangu
Alberto mkuu wa kwanza .Mtu ambaye
tulimuamini
kwamba
angeweza
kutuvusha hapa Tanzania ,ametugeuka na
kufanya jambo ambalo hakuna
aliyetarajia.Nafikiri nyote mnafahamu
ugumu tulioupata kuingia hapa
Tanzania.Toka historia ya kuanzishwa
jumuia hii ya Alberto’s hakujawahi kuwa
na nchi ngumu kuingia kama Tanzania.Hii
inatokana na waasisi wa taifa hili kujenga
misingi imara na thabiti na hivyo
kulifanya taifa hili kutopenyeka
kirahisi.Ilitulazimu kutumia nguvu nyingi
na muda mrefu kupenya na kuotesha
mizizi hapa Tanzania.Mizizi imeota na
mmea umechipua na mti umemea na
kutoa maua yenye harufu nzuri lakini
wakati unakaribia kuanza kutoa matunda
ametokea
mwenzetu
mmoja
akaukata.Tulimuamini sana Ernest Mkasa
tukamuweka katika nafasi ya juu kabisa
lakini baada ya kufanikisha yale
aliyokuwa anayahitaji amechagua
kutusaliti.Ndugu zangu kufutwa kwa
muswada huu na kuvunjwa kwa baraza la
mawaziri ni pigo kubwa kwetu.Muswada
huu ulikuwa ni mwanzo wa kuipeleka
Tanzania kule tunakotaka na kufutwa
kwake kumetufanya turudi nyuma hatua
ishirini zaidi.Hili ni anguko kubwa ndugu
zangu na si suala la kupuuzia.Ofisi ya rais
ndiyo mzizi wetu mkuu kwa hiyo kama
tukiikosa ofisi ile hata sisi hatutakuwa na
nguvu tena na mambo yetu
yatakwama.Kwingineko kote duniani
ambako Jumuiya ya Alberto imeweka
mizizi yake marais wa nchi ndio wenyeviti
wa kamati kuu za Alberto za kila nchi
lakini hapa Tanzania ilikuwa tofauti
kidogo ,tulimpa urais mtu ambaye si
Alberto’s japokuwa ni kwa makubaliano
maalum lakini nataka nikiri kuwa
tulifanya kosa kubwa.tulitakiwa kuchagua
rais kutoka miongoni mwetu.Kosa
tulilolifaya sasa linatugharimu.Kwa hiyo
ndugu zangu tumekutana hapa kwa ajili ya
kulijadili suala hili.Nakaribisha sasa
maoni yenu lakini kabla ya yote napenda
kwanza nimpe nafasi ya kwanza
mwenzetu waziri mkuu mstaafu”akasema
Obi.Waziri mkuu aliyevuliwa madaraka
akasimama
“ Ndugu zangu sidhani kama kuna
haja ya kuendelea kulijadili suala hili
wakati kinachotakiwa kifanyike kiko
wazi.Ernest mkasa ametusaliti na kwa
mujibu wa sheria zetu yeyote
anayetusaliti au kushindwa kutimiza
wajibu wake na kuhatarisha maslahi ya
jumuia adhabu yake ni kifo.Rais
Ferdinand alikufa kwa kukataa
kushirikiana nasi na hivyo ndivyo
tunatakiwa kufanya kwa Ernest Mkasa.He
must die.Kama alivyosema mwenyekiti
kwamba ofisi ya rais ndiyo mzizi wetu
mkuu na hatutakiwi kuikosa basi
tumuondoe Ernest haraka ,tunaye Mr
Muhsini ambaye ni makamu wa rais
atashika usukani kwa muda na mambo
yetu yataendelea kama kawaida.Baadae
utafanyika uchaguzi na mtu wetu