QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 119



Kuna kundi kubwa la vijana
limeathirika na dawa za kulevya.Kwa
tathmini iliyofanywa ,katika kila vijana
kumi wanne ni waathirika wa dawa hizo
.Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana hivi
sasa na nguvu kazi kubwa ya vijana
inapotea.Hii yote ni mipango ya Alberto’s
ya kuharibu nguvu kazi ya taifa ili hapo
baadae iwe rahis kwao kuingia na
kutawala Afrika.Mpango huu ni wa siri na
wa muda mrefu na tayari athari zake
zimekwisha anza kuonekana na kama hali
ikiendelea hivi ndani ya miaka kumi ijayo
basi hatutakuwa na nguvu kazi kabisa ,
vijana wengi tayari watakuwa
wamejitumbukiza katika matumizi ya
dawa za kulevya.Albertos’a wana mtandao
mkubwa sana wa kusafirisha na
kusambaza dawa za kulevya duniani na
hiki ni chanzo chao kikubwa cha
mapato.Kwa mwaka wanakusanya trilioni
nyingi ambazo ndizo zinazowasaidia
katika kuendesha mambo yao.Rais wa
nchi unapokubali kushirikiana na
Alberto’s kuna masharti unapewa na
mojawapo ya masharti hayo ni
kuhakikisha kwamba unafungua njia kwa
biashara ya dawa za kulevya kuingia
nchini kwako na kuwalinda wale wote
wafanyabiashara wakubwa wa dawa
hizo.Toka nilipoingia madarakani vita
dhidi ya dawa za kulevya imelega lega
sana na Tanzania imekuwa ni kama ghala
na njia kuu ya kupitisha dawa za kulevya
kwa ukanda huu wa Afrika
mashariki.Bandari ,viwanja vya ndege
,vinatumika katika kuingiza na
kusafirishia
dawa
za
kulevya.Austin.Ninajiona kama nimekalia
kiti cha damu kwani mimi ndiye chanzo
cha haya yote” akasema Ernest na kukawa
kimya .Ernest akachukua sigara katika
mkebe akaiwasha na kuvuta
“ Austin nimekueleza haya ili
ufahamu kwamba tunapoingia katika vita
dhidi ya Alberto’s tunaingia vile vile katika
vita dhidi ya mtandao wao mkubwa wa
wauzaji wa dawa za kulevya.Watu hawa ni
hatari na wanaroho za kikatili mno.Wengi
wao ni matajiri na walipa kodi
wakubwa.wanamiliki biashara kubwa
kubwa na wametengeneza ajira nyingi.Ni
watu ambao huwezi kuwagusa kwani
wameushika uchumi wa nchi.Ukiwagusa
watu hao lazima uchumi wa nchi
utetereke.I have to be honest with you
Austin,these people are very very
dangerous but we must stop them !!
akasema Ernest.Austin akavuta pumzi
ndefu na kusema
“ This war is bigger than I though”
“ Yes ! It’s a big war.Austin najua
nimeiharibu nchi hii ila ninataka
kuitengeneza
tena.Katika
hilo
nakutegemea sana wewe.Please help me
to rebuild the country and make it great
again” akasema Ernest na ukimya
ukatanda.Baada ya kimya cha dakika mbili
Austin akasema
“ Mheshimiwa rais,naomba
nikuhakikishie kwamba nimejitoa mhanga
kwa hiari yangu mwenyewe kupambana
na watu hawa na ninakuahidi kupambana
hadi tone la mwisho la damu .Japokuwa ni
watu hatari lakini siwaogoi.Mheshimiwa
rais nina swali moja tu kwako ,do you
know them? Do you have a list?
“ Ninawafahamu wachache ambao
nilipewa maelekezo ya kuwalinda na
kuwasaidia kila pale wanapokwama lakini
kuna sehemu ninaweza kupata orodha
yao.Nitakupa orodha hiyo pindi nikiipata”
“Sawa mheshimiwa rais” akasema
Austin wakaendelea na maongezi mengine
na baadae wakaagana rais akaondoka
“ Kama isingekuwa ni kwa ajili ya
mdogo wangu ,katu nisingekubali kuingia
katika vita hii ambayo ni mbaya na ngumu
kuliko nilivyotegemea.Hata hivyo sina
namna nyingine ya kufanya lazima
nipambane na Alberto’s.Ili nifanikiwe
lazima nitafute msaada” akawaza Austin
baada ya rais kuondoka
 
SEHEMU YA 200




Austin aliwahi sana kuamka
akafanya mazoezi na alipomaliza
akachukua kisinia chenye dawa akaenda
kugonga katika mlango wa chumba cha Dr
Marcelo
“ Austin habari za asubuhi?
“ Habari nzuri ,unaendeleaje?
“ Nashukuru naendelea vizuri
.Maendeleo
yangu
mazuri.Dawa
ulizoniletea jana zimenisaidia sana
nikalala usingizi mnono.Nilisikia sauti za
watu jana ,alikuwa ni rais?
“ Ndiyo alikuwa ni rais” akajibu
Austin
“ Alisemaje kuhusu ombi langu?
Alifanikiwa kuwasiliana na David Zumo?
“ Hapana hakufanikiwa kuongea
naye jana ila amesema atajaribu leo kama
ataweza kufanikiwa kuzungumza naye”
akasema Austin
Kauli
ile
ikaonekana
kumnyong’onyeza sana Marcelo.Austin
hakumjali akamsogelea na kumsafisha
vidonda
“ Austin umesomea pia mambo haya
ya utabibu? Unaonekana unayafahamu
vyema” akasema Austin
“ Ndiyo nimesomea.Kazi zetu hizi
zinakulazimu ufahamu mambo mengi
ikiwamo mambo kama haya” akasema
Austin
“ Unanifurahisha sana namna
unavyofanya mambo yako.By the way
kuna mambo Fulani ambayo nataka
kuzungumza nawe na pengine unaweza
ukanisaidia kupata ufumbuzi.”
“ Ni mambo gani hayo “ akauliza
Austin
“Ni kuhusu hili suala langu.Kuna
mambo ambayo bado watu hawayafahamu
na sijayaweka wazi bado kwa mtu yeyote
.Naamini nikikueleza unaweza ukanisaidia
kupata ufumbuzi wa hili suala langu.”
Akasema Marcelo.Austin hakujibu kitu
akabaki anamtazama Marcelo
“ Marcelo anaonekana ana jambo
kubwa .Nataka nimsikilize na nione kama
ninaweza kumsaidia”
“ Austin saa ngapi utakuwa na muda
wa kutosha tuzungumze ? akauliza Dr
Marcelo
“ Nitatoka asubuhi kuna mahala
ninakwenda na nitakaporejea tunaweza
kuongea”
“ Ahsante Austin” akasema
Marcelo,Austin akatoka akaelekea jikoni
kuandaa kifungua kinywa.Ilipotimu saa
nne za asubuhi tayari alikwishamaliza
kujiandaa akaondoka tayari kwa
kukutana na Monica.Siku hii alipendeza
mno kupita hata siku iliyotangulia
*******************
Saa tatu na dakika ishirini Maria
akiwa tayari ameamka akijiandaa kupata
stafstahi alipigiwa simu na mtu wa
mapokezi akamtaarifu kwamba alikuwa
na mgeni wake na akaomba apelekwe
chumbani moja kwa moja
“ Huyu lazima atakuwa ni baba
ambaye niliwasiliana aye jana usiku
nikamuelekeza hoteli niliyofikia.Hakuna
mtu mwingine anayefahamu kama niko
hapa” akawaza Maria baada ya dakika nne
mlango ukagongwa akaufungua na
kukutana na baba yake wakasalimiana
“ Oh ! dady I missed you so much”
akasema Maria na kumkaribisha baba
yake
“ Umekuja saa ngapi baba?
“ Nimetua na ndege muda si mrefu na
toka uwanja wa ndege nimekuja moja kwa
moja hapa kukuona.How’s everything ?
Are you comfortable here?
“ I’m ok dady.This place is
good.Sikutaka kwenda katika nyumba
yetu kwa sababu sitaki mtu yeyote
afahamu kama niko hapa.Dady please help
me find Austin” akasema Maria
“ Nitakusaidia Maria kwani hata
mimi nimekuja kwa sababu yake.Kuna
masuala ya kibiashara nataka nizungumze
naye .Tutakwenda sote kuonana naye”
“ Una fahamu mahala anakoishi?
Akauliza Maria
“ Sifahamu amefikia wapi hapa Dar
es salaam lakini kuna mtu anayefahamu
atanielekeza” akasema Boaz na kulifungua
sanduku lake dogo akatoa simu na
kuweka laini ya simu ambayo huitumia
akiwa Tanzania akazitafuta namba za
simu za rais Ernest Mkasa kabla ya kupiga
akamtazama Maria aliyekuwa akimtazma
kwa makini
“Excuse me ,I need to make a phone
call” akasema Boaz na kutoka akampigia
rais.
“ Hallow” akasema rais baada ya
kupokea simu ya Boaz
“ Mr president it’s me Boaz”
“ Boaz? Ernest akashangaa kidogo
“ Ndiyo mheshimiwa rais
“ Nilijua uko nje ya nchi.Umekuja lini
Tanzania?
“ Nimekuja leo asubuhi mheshimiwa
rais”
 
SEHEMU YA 201






karibu sana Boaz.Nitafurahi sana
kabla haujaondoa tukipata nafasi ya
kuonana”
“ Ahsante kwa heshima hiyo
mheshimiwa rais,nitajitahidi kabla
sijaondoka tuonane.” Akasema Boaz na
kimya cha sekunde kadhaa kikapita kisha
Boaz akasema
“ Mheshimiwa rais samahani kwa
kukusumbua mapema hivi nina shida
ndogo naomba unisaidie”
“ Shida gani Mr Boaz?
“ Nahitaji kuonana na Austin.Kuna
masuala Fulani ya kibiashra nahitaji
kuzungumza naye lakini sijui namna ya
kumpata .Nielekeze tafadhali mahala
ninakoweza kumpata au kama una
mawasiliano yake unipe ili niwasiliane
naye” akasema Boaz na Ernest akafikiri
kidogo kisha akasema
“ Nielekeze mahala ulipo na saa
ngapi unataka kumuona Austin ili
nimtume kijana aje akuchukue akupeleke
mahala aliko Austin” akasema Ernest na
Boaz akampa maelekezo mahala
anakopatikana wakaagana Boaz akarejea
chumbani
“ Jioni ya leo tunakwenda kuonana
na Austin kwa hiyo itanilazimu nichukue
chumba hapa hapa katika hoteli hii ”
akasema Boaz na kufanya taratibu za
kupata chumba katika hoteli ile kwani
hakutaka kwenda katika jumba lake la
kifahari lililoko ufukweni mwa bahari
*******************
Monica alidamka asubuhi na
mapema akafanya mazoezi kama ilivyo
kawaida yake halafu akajiandaa tayari
kwa shughuli za siku.Baada ya kutoka
nyumbani kwake alielekea moja kwa moja
nyumbani kwa wazazi wake.Siku hii alivaa
suti nyeupe iliyomkaa vyema na kila
aliyemuona alikiri kwamba kweli huyu
anastahili kuwa malkia wa urembo
Afrika.Magari yalikuwa mengi asubuhi hii
hivyo akajikuta akilazimika kukaa katika
foleni
“ Nitaachana na adha hii ya kukaa
katika foleni muda si mrefu sana toka
sasa.Nimeanza kuyakumbuka maisha yale
niliyoishi Congo.Sikuwahi kukaa katika
foleni.Kila nilikokwenda niliongozwa na
gari lenye king’ora na magari yote
barabarani yakakaa pembeni kupisha
nipite.Nimeyapenda maisha yale” akawaza
Monica na mara akanyong’onyea baada ya
kumkumbuka Pauline mke wa David
Zumo
“Masikini Pauline ,amenisikitisha
sana.Kila
nimkumbukapo
na
kuyakumbuka maneno aliyonieleza nahisi
uchungu mwingi.Moyo unaniuma
sana.Why her? Akawaza na kwa mbali
macho yake yakalengwa na machozi
“ She’s so pretty.Ukimtazama ni
kama vile hana matatizo but she’s dying”
akashindwa kuyazuia machozi kumtoka
.Tayari magari yalianza kwenda
“ Anyway there is nothing I can do to
help her.Kitu pekee ninachoweza kufanya
ni kulitimiza ombi lake aliloniomba yaani
kuolewa na mume wake David
Zumo.Pamoja na kulikubali ombi lake
lakini lazima niendelee kumuombea ili
kama ikimpendeza Mungu afanye miujiza
yake na Pauline apone.Ana roho nzuri
sana” akawaza Monica na mara
akakumbuka kitu
 
SEHEMU YA 202




Dr Marcelo ni bingwa wa saratani
ya damu,hawezi kufanya kitu chochote
kuhusu Pauline? Nina uhakika anaweza
akawa na mchango fulani hata kama ni
mdogo.Tatizo ni kujua mahala
alipo.Nitazungumza na David baadae ili
anielekeze mahala aliko Marcelo”
akaendelea kuwaza Monica
Aliwasili nyumbani kwa wazazi wake
wakasalimiana kwa furaha na kujumuika
wote mezani kupata kifungua kinywa na
baadae wakaelekea bustanini kwa ajili ya
maongezi
“ Pole na safari Monica.Ni siku mbili
tu lakini umebadilika ,umezidi
kupendeza” akasema mzee Ben ambaye
alionekana kuwa na furaha iliyopitiliza
“ C’mon dady,niko vile vile
sijabadilika chochote” akasema Monica
“ Haya tueleze safari yako ilikuaje?
Mambo yamekwendaje huko Congo?
Anasemaje David Zumo? Akauliza mzee
Ben .Monica akatabasamu na kusema
“ Kwa ujuml safari yangu ilikuwa
nzuri mno zaidi ya nilivyotegemea
.Nilipokewa vizuri na mke wa rais
nikapelekwa katika jumba kubwa la
kifahari nikalala hapo.Asubuhi nikaja
kuchukuliwa na mke wa rais aitwaye
Pauline,tukapanda helkopta hadi katika
hoteli moja kubwa nje ya jiji tukawa na
maongezi marefu.Jioni ya siku hiyo
nikapelekwa katika jumba la mapumziko
la David Zumo.Ni jumba ambalo sipati
namna ya kulielezea lilivyo.” Akasema
Monica na kutabasamu
“ Usiku huo nikawa na maongezi
marefu na David Zumo .Kikubwa ambacho
kilitawala mazungumzo yote kuanzia
mchana nilipokutana na Pauline ni
kuhusiana na ombi la David la kutaka
kunioa.Wote walijaribu kunishawishi
nikubali kuolewa na David.” Monica
akanyamaza na kuwatazama wazazi wake
waliooneka kuwa na shauku kubwa ya
kutaka kufahamu kilichojiri huko Congo
“ Ulifikia maamuzi gani? Akauliza
Janet ambaye muda mwingi alikuwa
kimya .Huku akiona aibu kwa mbali
Monica akasema
“ Nimekubali kuolewa na
Dav.................” Kabla hajamaliza mzee Ben
akaruka kwa furaha na kwenda
kumkumbatia
“Thank you Monica.Thank you so
much.Umefanya jambo kubwa sana .I’m
proud of you my queen” akasema
Ben.Alikuwa na furaha isiyoelezeka
“ Hongera Monica kwa maamuzi
hayo lakini nahitaji kufahamu jambo moja
,maamuzi hayo yametoka moyoni?
Umekubali kwa moyo mmoja bila ya
shinikizo? Akauliza Janet na Ben
akamtazama kwa macho makali ,akataka
kusema kitu lakini Monica akamuwahi
“ Kusema kweli wazazi wangu,David
simfahamu vyema ni mwanaume wa
namna gani kwani tumefahamiana kwa
muda mfupi .Kwa tamaduni zetu zilivyo ili
ukubali kuolewa na mtu Fulani basi lazima
mtu huyo muwe mnafahamiana vyema na
mmekaa katika uchumba kwa muda wa
kutosha.Kwa mimi na David imekuwa
tofauti, hatujapitia hatua hizo lakini
nimekubali kuolewa naye baada ya
kumuona ni mtu mwenye mapenzi ya
kweli nami.I don’t know how much he
loves me but the little he loves me I’m sure
its true and I value that”
“ Are yu sure Monica? Akauliza Janet
“ David speaks from heart.When he
says he loves me, he mean it.He’s a good
person ,loving and caring.Hata mke wake
Pauline amenihakikishia hilo kuwa David
ni mtu mzuri.Mama sikutaka kuipoteza
nafasi
hiyo
kama
nawe
ulivyonishauri.Nisingeweza
kukataa
kuolewa na mtu kama David ambaye ana
karibu sifa nyingi za mwanaume wa ndoto
zangu.Hata kama bado moyo wangu
haujafunguka kwa sasa but I know
someday I’ll fall in love with him” akasema
Monica
“ Monica binafsi nakupongeza mno
kwa kukubali kolewa na David Zumo .Ni
uamuzi wa busara na wenye manufaa
makubwa kwako,kwetu na kwa nchi zetu
pia.David Zumo ni mtu mkubwa,yuko
kwenye orodha ya matajiri wa
dunia.Kukubali kwako kuolewa naye
kutakuingiza katika orodha ya watu
maarufu duniani.Hongera sana Monica”
akasema Ben
“ Mtazame huyu mjinga anachowaza
yeye ni mali tu hajui kuwa tunampeleka
mtoto
kwenye
matatizo
makubwa.Nililipinga jambo hili hadi
 
SEHEMU YA 203




kufikia hatua ya kutoa siri kubwa
niliyokuwa nayo lakini bado haijasaidia na
sasa Monica amekubali kuolewa na
David.Inaniuma mno ila sina cha kufanya”
akawaza bi janet huku akijlazimisha
kutabasamu
“ Monica” akaita Janet
“ Tell me abut this wife of David.Is
she happy?
“ Kuna jambo moja nataka
kuwafahamisha ambalo hata mimi
nimelifahamu jana wakati nikijiandaa
kuondoka”
akanyamaza
kidogo
akawatazama wazazi wake na kusema
“ Pauline is sick”
“ Sick ?? Ben na Janet wakauliza kwa
pamoja
“ yes ! She’s sick.Ana saratani ya
ubongo na kwa mujibu wa madaktari
wanaomtibu wanadai hakuna uwezekano
wa kupona.She’s going to die” akashindwa
kuyazuia machozi kumtoka.
“ Pole sana Monica.Jipe moyo”
akasema Janet.Monica akafuta machozi na
kusema
“ Pauline alifahamu kwamba
hataweza kupona ndiyo maana akamtaka
David Zumo atafute mwanamke mwingine
afunge naye ndoa ndipo David
aliponichaga mimi.Suala hili linaumiza
sana,Pauline ana roho nzuri.She’s so nice
and young to die” akasema na kufuta
machozi yaliyondelea kumtiririka
“ Sikuwa nikilifahamu jambo hili
hadi jana aliponieleza wakati nikijiandaa
kuondoka Congo.Amenisisitiza sana
nisibadili uamuzi wangu wa kuolewa na
David.Nimemkubalia na kumuhakikishia
kuwa sintobadili uamuzi wangu” akasema
Monica na wote wakabaki kimya.
“ Hivyo ndivyo ilivyokuwa huko
nilikokwenda.David atatuma ujumbe
wake muda wowote kuanzia sasa kwa ajili
ya kuanza taratibu za awali za ndoa
yetu.Hataki suala hili lichukue muda
mrefu”
“ Ahsante Mungu.Safari ya kuelekea
katika orodha ya matajiri 100 wa dunia
imewadia.Hii ilikuwa ni ahadi ya David
Zumo endapo Monica angekubali kuolewa
naye.Nitakapoingia katika orodha hiyo
nitakuwa na nguvu na sauti na huo
utakuwa ni wakati wangu mzuri wa kulipa
kisasi kwa Ernest Mkasa.Jambo
alilonifanyia siwezi kuliacha likaisha hivi
hivi.I must destroy him.Kama ikiwezekana
nitawashughulikia wote wawili Ernest na
mke wangu Janet ili siri ya kuwa Monica si
mwanangu isivuje na Monica ataendelea
kuwa mwanangu daima” akawaza Ben
Maongezi yalionekana kukolea na
ndipo Monica alipoamua kuwaaga wazazi
wake ili aelekee kazini kwa ahadi ya
kurejea tena jioni kwa maongezi zaidi.
“ Wameonekana kulifurahia jambo
hili hasa baba lakini mama mhhh !!!..
akawaza Monica akiwa garini akielekea
ofisini kwake baada ya kutoka nyumbani
kwa wazazi wake
“ Yawezekana labda hakuamka
vizuri siku ya leo ndiyo maana alionekana
kutokuwa na furaha na hata maswali yeye
ndiye alikuwa muulizaji mkubwa.Anyway
apende asipende tayari nimekwisha fanya
maamuzi ya kuolewa na David na hivyo
ndivyo
walivyotaka.Kikubwa
ninachopaswa kuwaza kwa sasa ni
mabadiliko ya ghafla katika maisha
yangu.Kutoka Monica Yule wa kawaida
hadi Queen Monica.Ama kweli maisha
yana maajabu sana.Sikutegemea kama
ningepata bahati ya kuolewa na tajiri
namba
moja
Afrika.Ninapaswa
kumshukuru Mungu sana kwa jambo hili.”
Monica aliwasili ofisini kwake
akasalimiana
wafanyakazi
wake
waliofurahi mno kumuona tena .Baada ya
salamu akaelekea ofisini kwake Linah
akamfuata
“ Austin amenipigia simu muda
mfupi uliopita nikamjulisha kuwa
umekwisha rejea na hivi tunavyoongea
yuko njiani anakuja “ akasema LInah na
Monica akatabasamu.
“Huyo
kijana
anaonekana
kumchanganya sana Linah.Sijawahi
kumuona Linah akimsifia mwanaume
kiasi hiki.Safari hii ameshikwa barabara.”
Akawaza Monica na kuendelea na kazi
zake.
“David amenipigia simu asubuhi
lakini hakuongea chochote kuhusu Dr
Marcelo.Nahitaji kujua maendeleo ya
Marcelo.Nahitaji sana kuonana naye.Jioni
ya leo nitamuomba tena anielekeze
mahala aliko Dr Marcelo nikamtaz...”
Monica akatolewa mawazoni na Linah
aliyeingia kwa kasi mle ofisini
onica “ akaita
“He’s
here.Austin
tayari
amekuja.Ngoja nikamchukue yupo
mapokezi “ akasema Linah na kutoka
.Baada ya dakika tano akarejea akiwa
ameongozana na kijana mmoja mtanashati
sana mwenye sura iliyojaa tabasamu
“Wow! What a handsome guy”
akawaza Monica baada ya kumuona
Austin.Alikuwa ni kama mtu aliyepigwa na
butwa kwa kitu alichokuwa anakitazama
mbele yake.
“Monica “ akaita Linah na kumstua
Monica
“Huyu anaitwa Austin January.Ndiye
mgeni Yule niliyekueleza alikuwa
anakutafuta”
“Austin huyu ndiye Monica Benedict
mwamsole,mkuu wa kampuni hii” LInah
akafanya utambulisho.Monica akasimama
na kumpa Austin mkono.
“karibu sana Austin.Nimefurahi
kukutana nawe”
“Hata mimi nimefurahi sana
kuonana nawe Monica” akasema Austin na
kuketi katika sofa.Linah akatoka na
kuwaacha Monica na Austin pale ofisini.









PENZI MSOMAJI MAMBO YANAZIDI
KUKOLEA......USIKOSE SEASON 3 YA
SIMULIZI HII....
 
LEGE we noma sana yani ndiyo kwanza story inaaza .....sijui utatupia mda ngani na lini tena nawaza tu kimoyomoyo maana duu ni shidaaaaaaaaaaaa
LEGE. LEGEEEEEEE
 
gud bway..tenks soo mich..!!
monnie nae kafa kwa austin...atazinguana na linah....
 
Back
Top Bottom