LEGE
JF-Expert Member
- Oct 14, 2011
- 5,122
- 9,209
- Thread starter
-
- #1,421
SEHEMU YA 119
Kuna kundi kubwa la vijana
limeathirika na dawa za kulevya.Kwa
tathmini iliyofanywa ,katika kila vijana
kumi wanne ni waathirika wa dawa hizo
.Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana hivi
sasa na nguvu kazi kubwa ya vijana
inapotea.Hii yote ni mipango ya Alberto’s
ya kuharibu nguvu kazi ya taifa ili hapo
baadae iwe rahis kwao kuingia na
kutawala Afrika.Mpango huu ni wa siri na
wa muda mrefu na tayari athari zake
zimekwisha anza kuonekana na kama hali
ikiendelea hivi ndani ya miaka kumi ijayo
basi hatutakuwa na nguvu kazi kabisa ,
vijana wengi tayari watakuwa
wamejitumbukiza katika matumizi ya
dawa za kulevya.Albertos’a wana mtandao
mkubwa sana wa kusafirisha na
kusambaza dawa za kulevya duniani na
hiki ni chanzo chao kikubwa cha
mapato.Kwa mwaka wanakusanya trilioni
nyingi ambazo ndizo zinazowasaidia
katika kuendesha mambo yao.Rais wa
nchi unapokubali kushirikiana na
Alberto’s kuna masharti unapewa na
mojawapo ya masharti hayo ni
kuhakikisha kwamba unafungua njia kwa
biashara ya dawa za kulevya kuingia
nchini kwako na kuwalinda wale wote
wafanyabiashara wakubwa wa dawa
hizo.Toka nilipoingia madarakani vita
dhidi ya dawa za kulevya imelega lega
sana na Tanzania imekuwa ni kama ghala
na njia kuu ya kupitisha dawa za kulevya
kwa ukanda huu wa Afrika
mashariki.Bandari ,viwanja vya ndege
,vinatumika katika kuingiza na
kusafirishia
dawa
za
kulevya.Austin.Ninajiona kama nimekalia
kiti cha damu kwani mimi ndiye chanzo
cha haya yote” akasema Ernest na kukawa
kimya .Ernest akachukua sigara katika
mkebe akaiwasha na kuvuta
“ Austin nimekueleza haya ili
ufahamu kwamba tunapoingia katika vita
dhidi ya Alberto’s tunaingia vile vile katika
vita dhidi ya mtandao wao mkubwa wa
wauzaji wa dawa za kulevya.Watu hawa ni
hatari na wanaroho za kikatili mno.Wengi
wao ni matajiri na walipa kodi
wakubwa.wanamiliki biashara kubwa
kubwa na wametengeneza ajira nyingi.Ni
watu ambao huwezi kuwagusa kwani
wameushika uchumi wa nchi.Ukiwagusa
watu hao lazima uchumi wa nchi
utetereke.I have to be honest with you
Austin,these people are very very
dangerous but we must stop them !!
akasema Ernest.Austin akavuta pumzi
ndefu na kusema
“ This war is bigger than I though”
“ Yes ! It’s a big war.Austin najua
nimeiharibu nchi hii ila ninataka
kuitengeneza
tena.Katika
hilo
nakutegemea sana wewe.Please help me
to rebuild the country and make it great
again” akasema Ernest na ukimya
ukatanda.Baada ya kimya cha dakika mbili
Austin akasema
“ Mheshimiwa rais,naomba
nikuhakikishie kwamba nimejitoa mhanga
kwa hiari yangu mwenyewe kupambana
na watu hawa na ninakuahidi kupambana
hadi tone la mwisho la damu .Japokuwa ni
watu hatari lakini siwaogoi.Mheshimiwa
rais nina swali moja tu kwako ,do you
know them? Do you have a list?
“ Ninawafahamu wachache ambao
nilipewa maelekezo ya kuwalinda na
kuwasaidia kila pale wanapokwama lakini
kuna sehemu ninaweza kupata orodha
yao.Nitakupa orodha hiyo pindi nikiipata”
“Sawa mheshimiwa rais” akasema
Austin wakaendelea na maongezi mengine
na baadae wakaagana rais akaondoka
“ Kama isingekuwa ni kwa ajili ya
mdogo wangu ,katu nisingekubali kuingia
katika vita hii ambayo ni mbaya na ngumu
kuliko nilivyotegemea.Hata hivyo sina
namna nyingine ya kufanya lazima
nipambane na Alberto’s.Ili nifanikiwe
lazima nitafute msaada” akawaza Austin
baada ya rais kuondoka
Kuna kundi kubwa la vijana
limeathirika na dawa za kulevya.Kwa
tathmini iliyofanywa ,katika kila vijana
kumi wanne ni waathirika wa dawa hizo
.Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana hivi
sasa na nguvu kazi kubwa ya vijana
inapotea.Hii yote ni mipango ya Alberto’s
ya kuharibu nguvu kazi ya taifa ili hapo
baadae iwe rahis kwao kuingia na
kutawala Afrika.Mpango huu ni wa siri na
wa muda mrefu na tayari athari zake
zimekwisha anza kuonekana na kama hali
ikiendelea hivi ndani ya miaka kumi ijayo
basi hatutakuwa na nguvu kazi kabisa ,
vijana wengi tayari watakuwa
wamejitumbukiza katika matumizi ya
dawa za kulevya.Albertos’a wana mtandao
mkubwa sana wa kusafirisha na
kusambaza dawa za kulevya duniani na
hiki ni chanzo chao kikubwa cha
mapato.Kwa mwaka wanakusanya trilioni
nyingi ambazo ndizo zinazowasaidia
katika kuendesha mambo yao.Rais wa
nchi unapokubali kushirikiana na
Alberto’s kuna masharti unapewa na
mojawapo ya masharti hayo ni
kuhakikisha kwamba unafungua njia kwa
biashara ya dawa za kulevya kuingia
nchini kwako na kuwalinda wale wote
wafanyabiashara wakubwa wa dawa
hizo.Toka nilipoingia madarakani vita
dhidi ya dawa za kulevya imelega lega
sana na Tanzania imekuwa ni kama ghala
na njia kuu ya kupitisha dawa za kulevya
kwa ukanda huu wa Afrika
mashariki.Bandari ,viwanja vya ndege
,vinatumika katika kuingiza na
kusafirishia
dawa
za
kulevya.Austin.Ninajiona kama nimekalia
kiti cha damu kwani mimi ndiye chanzo
cha haya yote” akasema Ernest na kukawa
kimya .Ernest akachukua sigara katika
mkebe akaiwasha na kuvuta
“ Austin nimekueleza haya ili
ufahamu kwamba tunapoingia katika vita
dhidi ya Alberto’s tunaingia vile vile katika
vita dhidi ya mtandao wao mkubwa wa
wauzaji wa dawa za kulevya.Watu hawa ni
hatari na wanaroho za kikatili mno.Wengi
wao ni matajiri na walipa kodi
wakubwa.wanamiliki biashara kubwa
kubwa na wametengeneza ajira nyingi.Ni
watu ambao huwezi kuwagusa kwani
wameushika uchumi wa nchi.Ukiwagusa
watu hao lazima uchumi wa nchi
utetereke.I have to be honest with you
Austin,these people are very very
dangerous but we must stop them !!
akasema Ernest.Austin akavuta pumzi
ndefu na kusema
“ This war is bigger than I though”
“ Yes ! It’s a big war.Austin najua
nimeiharibu nchi hii ila ninataka
kuitengeneza
tena.Katika
hilo
nakutegemea sana wewe.Please help me
to rebuild the country and make it great
again” akasema Ernest na ukimya
ukatanda.Baada ya kimya cha dakika mbili
Austin akasema
“ Mheshimiwa rais,naomba
nikuhakikishie kwamba nimejitoa mhanga
kwa hiari yangu mwenyewe kupambana
na watu hawa na ninakuahidi kupambana
hadi tone la mwisho la damu .Japokuwa ni
watu hatari lakini siwaogoi.Mheshimiwa
rais nina swali moja tu kwako ,do you
know them? Do you have a list?
“ Ninawafahamu wachache ambao
nilipewa maelekezo ya kuwalinda na
kuwasaidia kila pale wanapokwama lakini
kuna sehemu ninaweza kupata orodha
yao.Nitakupa orodha hiyo pindi nikiipata”
“Sawa mheshimiwa rais” akasema
Austin wakaendelea na maongezi mengine
na baadae wakaagana rais akaondoka
“ Kama isingekuwa ni kwa ajili ya
mdogo wangu ,katu nisingekubali kuingia
katika vita hii ambayo ni mbaya na ngumu
kuliko nilivyotegemea.Hata hivyo sina
namna nyingine ya kufanya lazima
nipambane na Alberto’s.Ili nifanikiwe
lazima nitafute msaada” akawaza Austin
baada ya rais kuondoka