SEHEM YA KWANZA
Kumepambazuka tena na habari
kubwa iliyotawala mitandao ya kijamii na
katika vyombo mbali mbali vya habari
Tanzania asubuhi hii ni habari
iliyochapishwa katika jarida la The Face
ambalo ni maarufu kwa habari za mitindo
na urembo duniani ,inayohusiana na
matokeo ya utafiti uliofanyika barani
afrika kuhusu masuala ya urembo.
Ukurasa wa mbele wa jarida hili
maarufu ulipambwa na picha kubwa ya
mwanamke wa kiafrika mwenye uzuri
uliotukuka akiwa ndani ya tabasamu
kubwa na huku kukiwa na maandishi
makubwa yaliyosomeka QUEEN OF
AFRICA.
Ukurasa wa nne wa jarida hili
kuliandikwa habari ndefu inayohusiana
na picha ile ya yule mwanamke
aliyeupamba ukurasa wa mbele.Habari
hiyo ilielezea kwa kina kuhusiana na
matokeo ya utafiti uliofanywa na jarida
hilo barani afrika matokeo yaliyoonyesha
kuwa msichana Monica Benedict
Mwamsole anayetokea Tanzania ambaye
picha yake iliwekwa katika ukurasa wa
mbele wa jarida lile ndiye mwanamke
mrembo zaidi barani afrika.
Habari hii ilisababisha kuwepo kwa
mijadala mingi katika mitandao ya kijamii
na katika vyombo mbali mbali vya habari
duniani.Watu walimjadili Monica na wengi
ambao hawakuwa wakimfahamu walitaka
kumfahamu ni nani huyu msichana hadi
atajwe kuwa ndiye mrembo zaidi kuliko
wote barani Afrika.
Monica Benedict Mwamsole ana
umri wa miaka 25 .Ni mtoto wa pili na wa
mwisho kwa mzee Benedict na bi Janet
Mwamsole.Monica anatokea katika familia
iliyobarikiwa utajiri mkubwa.Baba yake
mzee Benedict Mwamsole ni mmoja wa
mabilionea wakubwa wanaotambulika na
kuheshimika ndani na nje ya nchi .Kwa
uchache tu mzee Benard anamiliki
kampuni kubwa ya usafirishaji ,kiwanda
kikubwa cha kutengeneza mvinyo wenye
soko kubwa katika nchi za ulaya,anamiliki
pia biashara nyingine kubwa kubwa ndani
na nje ya nchi.
Monica mwenye urefu wa futi 5.9 ni
msichana mwenye ngozi nyororo na
weupe wa kung’aa.Ana nywele ndefu
ambazo huzitengeneza katika mtindo wa
kipekee ambao humfanya awe na uzuri
usioelezeka.Monica amebarikiwa mwili
mzuri mwembamba wastani ambao
huwafanya wengi waamini ameufanyia
upasuaji na kuufanya uonekane vile.
Kielimu Monica ni msomi mwenye
shahada katika mahusiano ya kimataifa
.Ukiacha sifa na uzuri wa nje Monica ana
sifa za kipekee za ndani.Ni msichana
mpenda watu asiye na makuu licha ya
kuogelea katika bahari ya utajiri mkubwa
wa familia yao.Pamoja na uzuri wake
uliopelekea apewe jina la Black Angel au
malaika mweusi,Monica hakuwa na
majivuno aliongea na kila mtu
,hakuchagua mtu wala tabaka Fulani la
watu kuwa nao karibu.Aliwasikiliza wote
waliomuendea na shida mbalimbali na
kuwasaidia kadiri alivyoweza.Alikuwa na
taasisi yake aliyoianzisha kwa ajili ya
kusaidia watu wenye matatizo mbali mbali
lakini akilenga zaidi watoto na wazee
wasiojiweza.Kwa ujumla Monica alikuwa
ni mwanamke mwenye sifa lukuki na
kipenzi cha watu.Alipendwa na wakubwa
na wadogo.
Alipohitimu elimu yake ya
juu,Monica alichagua kufanya kile
ambacho alikuwa anakipenda kwa dhati
toka akiwa mtoto mdogo yaani
mitindo.Alipenda sana mambo ya mavazi
na urembo hivyo alianzisha kampuni yake
inayojishughulisha na masuala ya mitindo
kampuni ambayo imeliteka soko la afrika
mashariki kutokana na aina ya mitindo ya
mavazi wanayoibuni iliyotokea kupendwa
sana na watu wengi.
Kwa ufupi huyu ndiye Monica
Mwamsole ambaye jina lake maarufu
nchini Tanzania ni malaika mweusi jina
ambalo alipewa kutokana na uzuri wake
na matendo yake.Taarifa za yeye
kutangazwa na jarida la The Face kuwa
ndiye msichana mrembo zaidi barani
Afrika
hazikuwashangaza
wengi
waliomfahamu bali walikubaliana na
matokeo ya utafiti huo na kuwapongeza
watafiti ,Monica alistahili heshima hiyo ya
kuwa mrembo wa afrika.