QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 20


kuniita hivyo na leo imetimia” akasema
David.Uso wa Monica ukachanua kwa
tabasamu
“Kwa nini nisikuite hivyo David
wakati tayari nimekwisha ufungua moyo
wangu kwako? Tayari nimeukubali ukweli
kwamba mimi na wewe tumeumbwa ili
tuwe pamoja.Vipi hali yako? Anaendeleaje
Pauline?
“Sisi huku tunaendelea vizuri,hofu ni
kwako wewe.Sijui kwa nini kila wakati
ninakuwa na hofu sana juu yako huko
uliko.Natamani ungekuwa karibu ili
nikuone kila wakati na nihakikishe uko
salama.Monica una hakika uko salama?
Monica akatabasamu na kusema
“Usihofu David niko salama.”
“Nafurahi kusikia hivyo.Vipi wazazi
hawajambo? Umewaeleza kuhusu sisi?
Wamesemaje? Akauliza David
“Wazazi hawajambo na tayari
nimewaeleza kila kitu na hawana
tatizo.Wanajiandaa kuupokea ugeni
utakaoutuma kama ulivyoahidi”
“Ahsante .Nimefurahi kupita
maelezo.Vipi maendeleo yako kwa
ujumla?Kazi zako zinakwendaje?
“Kwa ujumla kila kitu kinakwenda
vizuri.Leo hii nilikuwa na vikao kadhaa
kufanya maandalizi ya ujenzi wa ile
shule.Bado naendelea kukushukuru sana
kwa msaada wako ule mkubwa kwa ile
shule”
“Usijali Monica.Nitakuunga mkono
katika miradi yako yote unayofanya kwa
jamii.U mwanamke wa pekee kabisa”
akasema David na ukimya mfupi ukapita
“David !! Monica akaita
“Naam malaika wangu”
“Samahani ,sikupokea simu yako
uliponipigia nilikuwa barabarani”
“Usijali mpenzi.Hata mimi nilihisi
hivyo.Hivi bado unaendesha gari
mwenyewe? Hauna dereva wa
kukuendesha ? Unaendesha gari la namna
gani?
“Ndiyo
ninaendesha
mwenyewe.Madereva wapo lakini
napenda kuendesha mwenyewe.Gari
ninayoendesha ni Marcedece benz.”
“ Ouh Monica,unatarajia kuwa malkia
wa Congo kwa hiyo unapaswa kuanzia
sasa kuendesha gari la hadhi ya
kimalkia.Najua hili hulipendi lakini
naomba unipe nafasi ya kukuhudumia
Monica.Mtu kama wewe unatakiwa
uendeshwe katika gari lenye hadhi kubwa
kama Limousine au uwe na helkopta
yako.”
“Ahsante David kwa kunijali .Si
kwamba ninakataa usinihudumie lakini
kwa muda huu mfupi kabla ya kufunga
ndoa niruhusu niendelee na maisha yangu
ya kawaida.Tutakapokuwa tayari katika
ndoa utakuwa ni mfalme wangu na kila
utakalolisema litakuwa ni amri kwangu.”
“Sawa
Monica”
akasema
David.Ukimya mfupi ukapita tena
“David” akaita Monica kwa sauti laini
“Unasemaje Monica?
“Nahitaji
kuonana
na
Marcelo.Umewasiliana na rais wa
Tanzania
akakuelekeza
mahala
alikohifadhiwa?
“Samahani kwa kutokufahamisha
mapema juu ya jambo hili lakini leo
sikuweza kuzungumza na rais
Ernest.Nimemtafuta sana kutwa nzima ya
leo bila mafanikio.Nadhani ni kutokana na
mambo yanayoendelea Tanzania kwa sasa
ndiyo maana imekuwa vigumu
kumpata.Nitamuwahi kesho asubuhi na
mapema halafu nitakujulisha.Usihofu
mpenzi utaonana na rafiki yako kwani
yuko salama .Je utamsaidiaje dhidi ya watu
wanaotaka kumuua?
“Bado sina mpango wowote hadi
hapo nitakapoonana naye ndipo tutapanga
kwa pamoja.Kwa sasa nahitaji sana
kuonana naye”
“Sawa Monica ila kumbuka endapo
utahitaji msaada wowote katika suala hili
mimi niko tayari kukusaidia”
“Ahsante sana David” akasema
Monica wakaendelea na maongezi
mengine ya kuhusu maisha yao,kila
mmoja akamueleza mwenzake historia ya
maisha yake lengo kubwa likiwa ni
kufahamiana
vizuri
zaidi.Baadae
wakaagana
“Oh my gosh ! David is so sweet.Ana
sauti
nzuri
anaongea
toka
moyoni.Utatamani uendelee kumsikiliza
usiku mzima.Anajua kubembeleza .Hapa
nilipo mwili wote unanichemka baada ya
kuongea naye.Huku sirini nahisi kama vile
..mhh !!
Monica akaupeleka mkono sirini
“ oh no ! I’m so wet !!.
Haraka haraka akainuka na kuingia
baduni kuoga
“Baada ya kuongea na David nahisi
kama ninahitaji kufanya mapenzi.”
Akawaza huku akiendelea kuoga
“This is very serious. I real need a
man.What am I going to do ? Hizi ndizo
athari za kuyajua mapenzi ukubwani.”
Akawaza
“Nitaiondoaje hali hii na mwanaume
wangu yuko mbali? Laiti kama David
angekuwa karibu ningemfuata usiku huu
huu.Natakiwa kutafuta namna ya
 
SEHEMU YA 21




kuidhibiti hali hii endapo itanitokea kwa
wakati huu ambao niko mbali na David
vinginevyo nitateseka mno kila mara
itakaponitokea kama hivi nitesekavyo
sasa.Sikuwahi kutokewa na hali hii kabla
sijayaanza mapenzi lakini kwa sasa baada
ya kuingia rasmi katika ulingo wa mapenzi
ni wazi kwamba hali hii itaendelea
kunitokea tena na tena.” Akawaza
akiendelea kuoga.
“Niliwahi kusikia kwamba kuna vifaa
ambavyo unaweza ukatumiwa mwenyewe
kujiridhisha pale ambapo unashikwa na
hamu ya kufanya mapenzi na mpenzi wako
yuko mbali nawe lakini vile vile nasikia
athari zake ni kubwa na endapo utazoea
mchezo huo ni hatari kubwa.Nitafanya nini
basi? Nitafute mwanaume wa kuwa naye
kwa siri kwa wakati huu ninaosubiri
kuolewa na David? Hili linaweza lisiwe
wazo zuri lakini inaweza ikawa ni njia
nzuri ya kunisaidia kuondokana na hali
hii.I don’t want to fali in love .I want a man
only for sex and nothing
else.Nitakapoolewa na David nitaachana
naye” akawaza na kuondoa sabuni mwilini
na kuzama tena mawazoni
“Mawazo gani haya yanaanza kunijia
kichwani? Jambo kama hili ni ktendo cha
usaliti kwa David.Ni vipi endapo
atagundua kwamba ninaye mwanaume
mwingine? Nitajuaje kama hajaweka watu
wa kunifuatilia na kuchunguza maisha
yangu? Natakiwa kuwa makini sana ama
sivyo nitajikuta ninaharibu kila kitu.Lakini
je nisipofanya hivyo nini litakuwa
suluhisho la hali hii? Kwa vyovyote vile
itakavyokuwa lazima nipate suluhisho la
jambo hili kwani bila kufanya hivyo
nitateseka mno.Suluhu peke hapa
ninayoiona ni kutafuta mwanaume wa siri
kwa ajili ya kazi moja tu ya kuniridhisha
kila pale ninapokuwa na hamu ya kufanya
mapenzi ila kama nikifanya hivyo
inatakiwa nilifanye jambo hilo kuwa siri
yangu kubwa.”
Monica akatoka ndani ya jakuzi na
kujifunga taulo akarejea chumbani
“Daniel ananipenda lakini siwezi
kumpa mwili wangu mtu kama Yule
mwenye wanawake karibu kila kona ya
jiji.Marcelo ambaye tayari nilianza
kuvutiwa naye lakini matatizo yake ni
kama haya kwanza ni mgonjwa halafu
yuko mafichoni.Who else? Hao wawili ndio
ambao kidogo akili yangu iliwahi
kuwafikiria” Mara akakumbuka kitu na
kutabasamu
“There is this new handsome guy
from south Africa,Austin.Ni kijana
mzuri.Japokuwa simfahamu tabia zake
laini ni kijana mzuri mtanashati na
,mstaarabu .Yule jamaa nahisi anaweza
akanifaa kwa sababu kwanza yeye si
mkaazi wa hapa,makazi yake ni afrika
kusini kwa hiyo hata kama nikifanya naye
mapenzi hataweza kufanya matangazo na
nikimtazama anaonekana ni kijana
mwelewa.Isitoshe ana hadhi yangu.Tatizo
ni namna ya kuweza kumpata kwani
siwezi kukurupuka tu na kumfuata
kumtaka tufanye mapenzi.Lazima nitafute
njia itakayomfanya ashawishike kutaka
kufanya
nami
mapenzi.Lazima
nimsisimue.Tena nimekumbuka aliniomba
kama tunaweza kutoka kwa chakula cha
usiku nikamwamia kwamba nitampa
jibu.Nadhani hapo ndipo sehemu nzuri ya
kuanzia .Nitakubali kutoka naye kesho
nitamchunguza nimfahamu ni mtu wa aina
gani ” akatabasamu
“Nadhani sasa nimepata muafaka na
suluhisho la tatizo hili.Austin anaweza
kunifaa.Najua sintakuwa namfanyia vizuri
David lakini sina namna nyingine ya
kufanya vinginevyo nitaikuta nimezidiwa
na kufanya mambo mengine yasiyofaa.”
Akachukua simu yake na kumuandikia
Austin ujumbe mfupi wa kukubali ombi
lake la kupata chakula usiku pamoja.
Taratibu Monica akajilaza kitandani
na kuanza kuutafuta usingizi alikuwa
amechoka sana
****************
Austin alikaribia sana kufika Rozana
night club ukaingia ujumbe katika simu
yake akapunguza mwendo wa gari na
kuufungua
akausoma
kisha
akatabasamu.Ujumbe ule ulitoka kwa
Monica ambao ulisomeka
“Dinner tomorrow. 8 Oclock”
“Thank you Monica.Good night”
Austin akaandika uumbe na kuutuma kwa
Monica
“Mambo yanazidi kukaa sawa.Monica
amekubali ombi langu la kukutana naye
kwa chakula cha usiku.Hii ni hatua kubwa
na nzuri katika kuikamilisha kazi ya
rais.Wakati mambo yangu yanakwenda
vizuri Boaz na Maria wameibuka na
wanataka kuharibu kila kitu.Hapana siko
tayari kuifanya kazi ya Boaz.Eti nimteke
Monica na kumtesa.Sintokubali kumgusa
malaika Yule.Lazima nitafute namna ya
kumlinda kwani hivi sasa tayari
amekwisha anza kuwindwa na Boaz.Naona
kuna mgogoro mkubwa unanukia kati
yangu na Boaz.Nikiingia katika mgogoro
na Boaz moja kwa moja nitakuwa
nimeingia katika mgogoro na Maria.Dah !
sikutaka jambo kama hilo litokee lakini
endapo itabidi iwe hivyo sintakuwa na
namna nyingine zaidi ya kuingia katika
mgogoro.Vyovyote itakavyokuwa lazima
nimlinde Monica” akawaza Austin huku
akipunguza mwendo akakata kushoto na
kushika ujia ulioeleka Rozana night
club.Kulikuwa na idadi kubwa ya watu na
magari kutokana na klabu hii kutoa
huduma ya burudani kwa saa ishirini na
nne.Alielekea sehemu ya maegesho
akaegesha gari na kushuka akaangaza
huku na huku kuhakiki usalama
akaridhika kila mtu alikuwa na hamsini
zake
“Pamechangamka sana mahali
hapa.Burudani zipo za kutosha” akawaza
Austin akaingia klabuni na kupanda ngazi
kuelekea ghorofani kama alivyokuwa
amekubaliana na Job.Watu walikuwa ni
wengi ndani ya klabu na viti vyote vya
kaunta vilijaa.Austin akapiga jicho pande
zote na kuwaona watu wawili wakiinuka
katika mojawapo ya meza iliyokuwa
karibu
na
kaunta
akaenda
kuketi.Muhudumu aliyevalia nadhifu
akafika haraka haraka na kumudumia
 
SEHEMU YA 22


kinywaji akaendelea kunywa taratibu
huku akivuta muda akimsubiri Job.Mara
akashikwa bega na mtu akageuka haraka
haraka na kuiona sura iliyomstua
“Jo......!!” akataka kusema neno lakini
Yule mtu akaweka kidole mdomoni ishara
ya kumtaka anyamaze halafu akamfanyia
ishara kwa kichwa amfuate.Austin
akainuka na kuangaza pande zote kisha
akamfuata Yule mtu
“Haya ni kama maajabu.Kweli Job ni
jasusi wa hali ya juu.Mchana ni kichaa
lakini usiku ni mtanashati namna hii kiasi
kwamba
ni
vigumu
hata
kumtambua.Mchana anavaa matambara na
usiku anavaa suti kali .Dah !
amenifurahisha sana kwa hii staili yake
.Huyu haswa ndiye mtu ninayemuhitaji
katika operesheni hii” akawaza Austin na
kuendelea kumfuata Job aliyeelekea katika
maegesho ya magari ,akaingia katika gari
moja jeusi,Austin naye akaingia katika gari
lake na kuondoka akilifuata gari alilopanda
Job
Walivuka daraja la Nyerere na
kuingia Kigamboni halafu wakaelekea
eneo la mto Kazi.Kwa kutumia kifaa cha
kufungulia toka mbali Job akalifungua geti
na kuingia ndani,Austin naye akafuata
kisha geti likajifunga
“Hapa ni wapi? Nani anaishi katika
jumba hili kubwa? Austin akajiuliza
maswali mara baada ya kushuka garini
“Karibu Austin” Job akasema na
kumfanyia ishara Austin amfuate
wakaelekea hadi katika sebule kubwa
ambayo karibu samani zake zilikuwa
zimefunikwa na ilionyesha wazi kwamba
hakukuwa na mtu aliyekuwa akiishi
pale.Job akafunua kitambaa kilichofunika
sofa na kupukuta vumbi
“Karibu uketi Austin”
“Job,first of all ,tell me what is this
place? Nani anaishi hapa? Why are we
here? Akauliza Austin
“Relax Austin,utafahamu kila kitu
lakini kabla ya yote kuna jambo nataka
kufanya” akasema Job akatoka pale
sebuleni na baada ya kama dakika tano
akarejea akiwa na kompyuta ndogo
akaiweka mezani akaiwasha na kuanza
kubonyeza halafu akamgeukia Austin
“Austin karibu sana .Utanisamehe
kwani humu ndani hakuna kinywaji
chochote.No body lives here”
“Job you are amazing.How can ....”
Kabla Austin hajamaliza alichotaka
kukisema Job akadakia
“I know what you want to say.I’m not
crazy Austin.I repeat I’m not crazy”
akasema Job huku akitabasamu
“Hii ni nyumba yangu ya siri.Hakuna
anayeishi humu ila huwa ninakuja mara
kwa mara hasa nyakati kama hizi au
wakati nina kazi za kufanya”
“Umewezaje
kufanya
hili
likawezekana na watu wasikutilie shaka?
Akauliza Austin
“Hahahaa!!!.Austin
umenisahau
kwamba mimi ndiye Job.Kwa kifupi tu ni
kwamba imenilazimu kuishi katika maisha
haya kwa miaka mitatu sasa na nmekuw
anikija hapa mara kwa mara nyakati za
usiku.Kila ni japo hapa huwa nachukua
tahadhari kubwa.Ninazo kamera saba za
siri ambazo nimezitega kwenye miti katika
njia ya kujia hapa ambazo si rahisi
kuonekana .Niingiapo hapa ndani huwa
ninafuatilia kamera zote za njiani kuhakiki
kama hakuna anayenifuatilia.Kwa hapa
nyumbani pekee ninazo kamera kumi na
tatu na hata niwapo kule kwa kaka huwa
ninaweza kujua kila kinachoendelea hapa
kupitia kifaa kidogo mithili ya simu
ninachotembea nacho kila sehemu.”
Akasema Job na kumuonyesha Austin
mfumo mzima wa kamera ulivyo
“That’s good.Kumbe umejizatiti
haswa.” Akasema Austin
“Nilinunua shamba hili toka kwa
mama mmoja wa kiarabu ambaye kwa
sasa anaishi Oman.Sikuwahi kumueleza
mke wangu juu ya shamba hili .Ni eneo
kubwa la ekari ishirini na saba.Kuna
nyumba saba za waliokuwa watumishi wa
huyo mama na niliponunua sikuwaondoa
watu hao bali niliboresha zaidi makazi yao
na kuwapatia kila mmoja sehemu ya
kulima na kufuga kwa hiyo hawa pia ni
walinzi wengine wazuri wa nyumba
hii.Kwa hiyo Austin hayo ndiyo maelezo
mafupi ya nyumba hii.Vipi unaendeleaje na
maisha yako? Unaishi wapi kwa sasa?
Akauliza Job halafu akamtazama Austin na
kutikisa kichwa huku akitabsaamu
“Nikikutazama siamini kama kweli ni
wewe Austin.Nilipokuona leo nilipatwa na
mstuko mkubwa nikadhani labda ni
mzimu wako umenijia kwani sikutegemea
kabisa kukuona tena katika maisha haya
kutokana na taarifa ya mwisho niliyoipata
kuwa ulipotea wakati wa operesheni ya
kuwakomboa wale watanzania waliotekwa
na Alshabaab nchini Somalia.Welcome
back to life brother..” akasema Job huku
akicheka.Austin naye akacheka kidogo na
kusema
“I’m back to life.They wanted me
dead but now I’m back to haunt them.I’ll
haunt each soul that signed for my death !!
akasema Austin kwa hasira
“What real happened brother? Please
tell me how you survived” akasema
 
SEHEMU YA 23


Job.Austin akameza mate kulainisha koo
halafu akasema
“ Ni hadithi ndefu kidogo .Tukiwa
katika ile operesheni ya kuwakomboa wale
watanzani waliotekwa na alshabaab mimi
nikiwa mstari wa mbele,nilipigwa risasi
kutokea nyuma na watu wetu ila mpaka
leo sifahamu ni nani aliyenipiga risasi ile
ila ninachofahamu ni kwamba risasi ile
haikuwa bahati mbaya bali lengo kubwa la
aliyefanya
vile
lilikuwa
ni
kuniua.Nilipoteza fahamu nilipopigwa
risasi ile na nilipofumbua macho
nikajikuta nikiwa hospitali na watu zaidi
ya ishirini wakinizunguka wakiwa na
silaha nzito.Nilifahamu moja kwa moja
kuwa nilikuwa katika himaya ya
Alshabaab.Kiongozi wao alinieleza
kwamba nilipigwa risasi ambayo ilipita
pembeni kidogo ya moyo .Nilifanyiwa
upasuaji katika hospitali yao kubwa na
nilipopata nafuu walihitaji kiasi kikubwa
cha fedha ili waniachie huru.Mimi kutaka
kuuawa ulikuwa ni mpango wa watu ndani
ya serikali kwa hiyo sikutaka Alshabaab
wadai malipo ya kutoka serikalini badala
yake nikawasiliana na mpenzi wangu
Maria ambaye ni mtoto wa bilionea
nikamuomba afanye kila awezalo
kumshawishi baba yake aweze
kunikomboa kwa kulipa kiasi kile kikubwa
cha fedha walichokihitaji Alshabaab.Baba
yake Maria alikubali kulipa na nikawa
huru.Mchakato huo ulifanyika kimya
kimya na hata ndugu zangu hawajui
mpaka leo hii kama bado niko hai.Baada ya
kuachiwa na Alshabaab sikurejea tena
Tanzania ,nikaelekea afrika ya kusini
nikabadili uraia na kuanza maisha
mapya.Sikuwahi kurudi Tanzania hadi
nilivyorejea hivi juzi.Leo baada ya
mizunguko yangu nikaona ni vyema
endapo nitakuja kukujulia hali,ndipo
nilipopata habari za matatizo
yaliyokupata.Nilistuka sana nikasema
lazima nikutafute nikuone.Hiyo ndiyo hali
halisi iliyonipata Job” akasema Austin
“Pole sana .Austin wewe ni mtu
ambaye ulijitoa mno kwa ajili ya nchi hii
na hukupaswa kabisa kufanyiwa haya
uliyofanyiwa .Lakini unadhani nini hasa
sababu iliyopelekea wewe utake kuuawa?
Unadhani ni bahati mbaya?
“ Ipo sabbau ambayo ndiyo naamini
ilipelekea mimi kutaka kuawa.Niligundua
mpango wa siri uliofanywa na watu ndani
ya serikali wa kutaka kumuua rais
Ferdinand .Walipojua kuwa tayari
nimefahamu ilitafutwa namna ya
kunimaliza na ndipo walipotumia
operesheni ile kwani hata kama ningekufa
ingejulikana kuwa nimekufa katika
mapambanao na Alshabaab.Mungu
mkubwa hawakufanikiwa kuniua bali
walifanikiwa kumuua rais Ferdinand
kwani kama nilivyokueleza kuwa baada ya
kuachiwa na Alshabaab sikurejea tena
Tanzania na hivyo wao wakatekeleza
mpango wao wakamuua rais”
“Oh my God !! Ina maana ajali ile
iliyosababisha kifo cha rais Ferdinand
haikuwa ajali ya kawaida?
“Ndiyo haikuwa ajali ya
kawaida.Ilikuwa ni ajali ya kupangwa japo
taarifa za uchunguzi zinaonyesha kuwa
ilikuwa ni ajali ya kawaida”
Ukimya mfupi ukapita Austin
akauliza
“What about you Job? What
happened to you? Kitu gani kimesababisha
ukaishi maisha haya ya sura mbili? Are you
undercover or something?
Job akavuta pumzi ndefu akainama
akawaza halafu akasema
“Nilipata tetesi nikiwa katika kozi
fupi nchini Korea kusini kuwa mke wangu
Monalisa ana mahusiano na mwanaume
mwingine.Sikuzipuuza tetesi hizo na
nilipanga kufanya uchunguzi wangu pindi
nitakaporejea nyumbani.Baada ya
kumaliza mafunzo na kurudi nyumbani
nilimkuta Monalisa akiwa na gari lenye
thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia
mbili.Nilistuka na kuuliza alikopata gari
lile akanieleza kuwa amechukua mkopo
benki na ameanza biashara ya madini
inayomuingizia fedha nyingi na faida
anayoipata ndiyo iliyomuwezesha
kununua gari lile la kifahari.Ni kweli
alikuwa na ofisi yake ya kununua na kuuza
madini ya vito.Sikutaka kuonyesha wasi
wasi wowote bali nilianza uchunguzi
wangu kimya kimya ili kubaini
ukweli.Nilipochunguza
nikagundua
kwamba ni kweli Mona alikuwa na
mahusiano na mtu mmoja anaitwa Dogo
Bill.Huyu ni mfanya biashara bilionea na
jina hilo alipewa kutokana na kupata
utajiri mkubwa akiwa bado kijana
mdogo.Jina Dogo Bill lina maamisha Dogo
Bilionea.Jina lake halisi ni Eliah
Mkobweka.Niliendelea kufanya uchunguzi
na kugundua kuwa huyu Dogo Bill ndiye
aliyemnunulia gari lile na ndiye aliyempa
mtaji wa biashara ya madini.Niliumia sana
hasa nikikumbuka nilikotoka na
Monalisa.Nilikwenda mbali zaidi na
kugundua kuwa Dogo Bill ni mmoja kati ya
wafanyabiashara wakubwa wa dawa za
kulevya Afrika mashariki na kwa kiasi
kikubwa utajiri wake unatokana na
biashara hiyo.Niligundua kuwa huyu
jamaa anaifanya biashara hiyo kwa siri
kubwa kiasi cha kuwa vigumu kumfaham
 
SEHEMU YA 24


kuwa anahusika na biashara
hiyo.Nilikwenda mbali zaidi nikagundua
kuwa kuna mtandao ambao unafanya kazi
ya kuteka watu toka mikoa mbalimbali
kuwaua na kisha hutengeneza nyaraka
Bandia za kuonyesha kuwa ni watu kutoka
mataifa ya nje na husafirisha maiti hiyo
kwenda nje ya nchi.Maiti hiyo hutolewa
kila kitu ndani na kujazwa dawa za
kulevya kisha husafirishwa.Kila mwezi
maiti zaidi ya kumi zimekuwa
zikisafirishwa kwenda nje ya nchi zikiwa
zimejaa dawa za kulevya.Mtandao huu ni
mpana na umesambaa katika sehemu zote
muhimu na ndiyo maana hadi leo hii
hakuna yeyote aliyewahi kuripotiwa
kukamatwa kwa jambo hili.Kilichonistua
zaidi ni kwamba kuna watu watatu
wakubwa kabisa waliokuwa karibu na rais
ambao nao wanajihusisha na biashara
hii.Primusi Buke aliwahi kuwa waziri
alifariki kwa maradhi ya kansa ya
ini,Philipo Muro alifariki kwa ajali ya gari
na ambaye yuko hai mpaka sasa ni
msaidizi wa rais anaitwa Wilson
Mukasha.Sina hakika kama rais
anamfahamu huyu msaidizi wake ni mtu
wa namna gani kwani kama angemfahamu
naamini asingekubali kumuweka karibu
yake.”
Austin akasimama kwa mstuko
alioupata
“Vipi Austin mbona umestuka?
“Umesema Wilson mukasha?
Akauliza
“Ndiyo,unamfahamu? Akauliza Job
lakini Austin hakujibu kitu
“ Austin !! akaita Job
“ Umestuka baada ya kumtaja Wilson
Mukasha ,unamfahamu?
“yes I know him” akajibu Austin
“Wakati nikiendelea na uchunguzi
wangu ili kubaini mambo mengi
yanayohusiana na mtandao huo,kuna kosa
moja nililifanya ambalo lilisababisha
niingie katika hali hii” akanyamaza
akashusha pumzi na baada ya muda
akasema
“Niligundua kwamba ndani ya
mtandao ule kulikuwa na watu wengine
wakubwa zaidi ya akina Mukasha.Usiku
moja niliondoka kuwahi jambo Fulani
linalohusiana na uchunguzi niliokuwa
naendelea kuufanya kumbe nilifanya kosa
moja kubwa.Nilisahau kuuficha ushahidi
wote nilioupata kuhusiana na mahusiano
ya Monalisa na Dogo Bill.Huku nyuma
Mona aliweza kugundua kuwa
ninamchunguza baada ya kuuona ule
ushahidi.Sikurejea nyumbani usiku ule na
niliporejea oh my gosh !!..” Job
akanyamaza
“What happened Job? Akauliza
Austin
“My wife and my daughter were
already gone.Aliondoka na kila ushahidi
niliokuwa nimeupata kuhusu yeye na dogo
Bill.I was left alone.Kwa kuwa simu yake
tayari nilikuwa nimeiwekea program
maalum ya kurekodi mawasiliano yake
yote anayoyafanya niliweza kusikia
mazungumzo ya mwisho kati yake na dogo
Bill,Mona akimfahamisha Bill kwamba
tayari nimegundua kuhusu mahusiano yao
na Bill akamwambia kwamba wakati
umefika kwa yeye kuondoka kwani kama
angeendelea kukaa kwangu mambo yao
yote yangeharibika.Mwisho alimuuliza
Mona kama yuko tayari kuachana nami na
bila kigugumizi Mona akajibu kuwa yuko
tayari.Bill akamwambia kwamba aanze
kujiandaa anatuma watu kwenda
kumchukua.Mwisho kabisa alimhakikishia
Mona kwamba asihofu nitashughulikiwa
na sintakuwa kikwazo tena kwao.Hayo
ndiyo yalikuwa maongezi ya mwisho ya
mke wangu na simu yake
ikazimwa.Haikuwahi kupatikana tena hadi
leo hii na sielewi yeye na mwanangu wako
wapi.Kwa mujibu wa mipango yao
kilichokuwa kinafuata ilikuwa ni
kunimaliza na kwa mtandao wao namna
ulivyo mkubwa lazima wangenimaliza
haraka sana hivyo ikanilazimu kujifanya
nimerukwa na akili.Wengi walistushwa
mno kwa hali ile ya ghafla lakini hakuna
anayeufahamu ukweli .Wote wanajua
kwamba nilipatwa na uchizi baada ya
kuachwa na mke wangu.Ndugu zangu
walinichukua wakanipeleka kwa mganga
wa kienyeji kutibiwa wakiamini kuwa
nimerogwa.Waliuza nyumba na vitu
vyangu vyote yakiwamo magari mawili
kwa kigezo cha kupata hela ya kunitibu
lakini fedha yote waligawana wakijua
kuwa mimi ni kichaa.Baada ya kuona kuwa
sipati nafuu wakanihamishia kule kwa
kaka ninakoishi na hakuna hata mmoja
anayenijali tena.Wote wanajua kuwa tayari
mimi ni kichaa na sintopona tena.Pamoja
na hali yangu hiyo lakini nimekuwa
nikiendelea na uchunguzi wangu kimya
kimya” akanyamaza na kumeza mate
“Unaendelea na uchunguzi upi?
Akauliza Austin
“Ukiacha wewe ,kuna mtu mwingine
mmoja ambaye anafahamu kuwa mimi si
kichaa.Anafahamu kuwa nini niko hivi
nilivyo na ndiye ambaye ananisaidia katika
uchunguzi.Naendelea kumchunguza Dogo
Bill na mtandao wake ili nipate taarifa za
kutosha kabla ya kuamua kufanya kitu.Mtu
huyo ambaye ninashirikiana naye anaitwa
Amarachi Inyike.Ni raia wa Nigeria lakini
kwa sasa anao uraia wa Tanzania na
 
SEHEMU YA 25


anajulikana kama Winifrida Osward ama
Winnie kama alivyozoeleka.Ninaye rafiki
yangu mmoja anaishi nchini Nigeria
aliniomba nimsaidie dada yake ambaye
aliwahi kutekwa na kundi la Boko Haram
akakaa msituni kwa miaka sita hadi yeye
na wenzake sitini walipookolewa na
majeshi
ya
serikali.Akiwa
msituni,Amarachi aliozwa kwa mmoja wa
kiongozi wa wanamgambo hao na
akazalishwa mtoto mmoja.Kwa miaka sita
wakiwa msituni walikuwa wanapewa
mafunzo mbali mbali ya kijeshi
wakiwaandaa kuja kuwa wanamgambo wa
kikundi hicho.Walifundishwa namna ya
kutengeneza na kutega mabomu,kutumia
silaha nzito za kivita,mbinu mbali mbali za
medani,kwa ujumla waliandaliwa kuwa
magaidi na walikuwa wameiva
barabara.Baada ya kukombolewa na
kurudishwa uraiani,maisha ya Amarachi
hayakuwa mazuri na yenye furaha.Jamii
iliwatenga na hakuna aliyetaka
kuchangamana nao.Mtoto wa Amarachi
aliuawa na watu wasiojulikana kwa madai
kwamba ni damu ya magaidi na siku moja
naye angekuwa gaidi.Zaidi ya mara tatu
Amarachi alinusurika kuuawa lakini
alijinusuru kutokana na kuwa na uwezo
mkubwa wa kujihami” Job akanyamaza
kidogo halafu aakendelea
“Nilipoombwa na kaka yake
nimsaidie sikusita kufanya hivyo
ikanilazimu nimuandalie nyaraka za
kuweza kumuingiza na kumuwezesha
kuishi nchini Tanzania.Kaka yake ni mtu
mwenye uwezo mkubwa kifedha hivyo
akamjengea hoteli kubwa hapa Dar
inaitwa Silver peak hotel .Amarachi au
Winnie ndiye pekee ambaye amekuwa
akinipa msaada kila ple
ninapohitaji.Ninapohitaji kuja hapa ni yeye
ambaye huja kunichukua katika sehemu
tuliyoipanga kukutana na hunileta huku
nikafanya kazi zangu kisha hunirudisha
.Amejitahidi kwa kadiri alivyoweza na
amefanikiwa kujenga urafiki na dogo Bill
na hivyo amekuwa akimchunguza lakini
mpaka sasa hajawahi kumuona Bill akiwa
na mke wangu Mona au hata kumtaja
jina.Bado haijulikani kama Mona yuko
hapa nchini au ameama nchi.Sijui kama
yuko hai au amekufa lakini sitaki kuumiza
kichwa kujua hali yake bali akili yangu ni
kwa mwanangu Millen.Kwa kumtumia
Amarachi nimeweza kupata taarifa nyingi
za kuhusiana na mtandao wa akina
Bill.Kwa ufupi hayo ndiyo yaliyonisibu na
kunifanya niishi maisha kama haya lakini
kilichomo moyoni mwangu ni kisasi kibaya
sana.Nataka niumalize mtandao huu
nikianzia na dogo Bill lakini nimechelewa
kufanya hivyo nikitaka kwanza kufahamu
alipo mwanangu Millen.Nitakapopata
taarifa za uhakika za mahala alipo
mwanangu wingu jeusi litatanda Dar es
salaam kwani nitalisimamisha jiji wakati
nikiwashugulikia
watu
hawa
waliosababisha
nikaishi
maisha
haya.Ninachofikiria kukifanya ni Mungu
pekee anayefahamu.”
“Pole sana Job.Haya ndiyo madhira
tunayokutana nayo katika kazi zetu
hizi.Tunajitoa mno kwa ajili ya kupigania
usalama wa nchi yetu lakini kinachotupata
ni majuto matupu.Mara nyingi huwa
ninawaza na kujuta kwa nini niliingia
katika kazi hii.Sikuwahi kufikiria eti siku
moja nitaukana uraia wangu na kwenda
kuishi nchi za ugenini.Naamini hata wewe
haukuwahi kufikiri kuwa iko siku ambayo
utaishi kwa kujifanya kichaa.Lakini haya
yote yanasababishwa na watu wachache
waliomo katika madaraka.Ukigusa maslahi
yao they make your life a living hell”
akasema Austin .Ukapita ukimya
“Tell me why are you here Austin?
What are you doing here? Aren’t you
scared of them anymore? Akauliza
Job.Austin akainuka na kwenda kufunua
pazia akachungulia nje baada ya muda
akageuka na kumtazama Job
“Niko hapa kwa kazi maalum”
akanyamaza kidogo halafu akasema
“Kwa sasa mimi ni meneja wa
kampuni ya A.A Safaris ltd nayomilikiwa
na baba mkwe wangu.Ninaishi maisha
mazuri nchini afrika kusini.Sikuwa
nimepanga kurejea Tanzania tena au
kufaya tena kazi hizi lakini nilipigiwa simu
na rais Ernest Mkasa akaniomba nirejee
Tanzania kuna kazi anataka kunipa.Sikuwa
tayari kwa hilo lakini akanieleza jambo
moja kuwa mdogo wangu Linda
amefungwa nchini China kwa kosa la
kujaribu kuingiza dawa za kulevya nchini
China.Ernest aliahidi kunisaidia kumtoa
mdogo wangu gerezani endapo
ningekubali kumfanyia kazi yake.Kwa ajili
ya mdogo wangu nilikubali kurejea
Tanzania kuifanya kazi ya rais.Kama
alivyoahidi alifanya kila aliloweza na
mdogo wangu akatolewa gerezani kwa
hiyo ni zamu yangu kufanya kazi yake”
akanyamaza kidogo baada ya sekunde
kadhaa akaendelea
“Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania anataka nimsaidie
kupata sampuli toka kwa mwanamke
mmoja ambaye ameelezwa kuwa ni
mwanae,kwa ajili ya kufanay kipimo cha
vinasaba kubaini kama kweli ni
mwanae.Tayari nimeianza kazi hiyo
ambayo si ngumu na nina uhakika wa
kuikamilisha ndani ya kupindi kifupi
 
SEHEMU YA 26


kijacho lakini ndani ya kazi hiyo
kumejitokea tena kazi nyingine ambayo ni
kubwa zaidi na ambayo imenibadili
msimamo wangu na kunirudisha tena
kazini” akatulia kidogo halafu akaendelea
“Nilikueleza awali kuwa sababu
kubwa ya mimi kutaka kuawa ni baada ya
kugundua mpango wa kumuua rais
Ferdinand.Kuna kikundi kijulikanacho
kama Alberto’s ambacho kimesambaa
katika sehemu mbalimbali za
dunia.Historia ya kikundi hiki kuna
kiongozi mmoja wa kanisa aliyeitwa
Alberto aliwahi kufukuzwa katika kanisa
lake baada ya kuchochea uasi ndani ya
kanisa kwa kutaka yafanyike mabadiliko
ambayo hayapo katika imani ya kanisa
hilo. Mambo ambayo Alberto alitaka
yakubaliwe na kanisa ni kuwaruhusu
makasisi na watawa kuoa na
kuolewa,kukubaliana na kuhalalisha
mapenzi ya jinsia moja.Utoaji
Mimba,matumizi
ya
mihadarati
n.k.Aliyekuwa kiogozi wa kanisa kwa
wakati huo hakufurahishwa na jambo hilo
hivyo akamvua daraja Alberto na
kumtimua katika kanisa.Baada ya
kufukuzwa alianzisha kikundi chake
ambacho yeye anakiita jumuiya ya Alberto
au the Alberto’s.Aliendeleza yale
yaliyomfanya
akafukuzwa
na
kanisa.Alianza kwanza kwa kuhakikisha
wakuu wa mataifa makubwa yenye nguvu
wanakuwa wafuasi wake.Alberto anatumia
nguvu za giza kwa hiyo alifanikiwa
kuwapata wakuu hao na mataifa mengi
makubwa ya amerika na ulaya
yakakubaliana na mambo yake ,wakayapa
nafasi .Wamehalalisha mapenzi na ndoa za
jinsia moja,utoaji mimba,matumizi ya
mihadarati n.k.Baada ya kusambaa katika
sehemu kubwa ya dunia Alberto’s
walielekeza nguvu zao bara la Afrika
ambako walianza ushawishi kwa viongozi
wa mataifa ya Afrika wakiyatumia mataifa
makubwa .Rais aliyekuwa madarakani
wakati huo Ferdinand alikataa kata kata
kushawishiwa na ndiyo sababu ya kifo
chake ili nafasi ya rais ishikwe na mtu
wanayemtaka wao” Austin akanyamaza na
kumtazama Job
“Sikufahamu chochote kuhusu suala
hili” akasema Job
“Si rahisi kufahamu kwani ni mambo
yanayokwenda kwa siri kubwa na kwa
kiapo kikali hivyo yeyote anayethubutu
kwenda kinyume adhabu yake ni kifo”
“Dah !” akasema Job kwa mshangao
“Kabla ya kuianza kazi ya rais
nilitaka kufahamu kama naye ni mmoja wa
Alberto’s.Awali aligoma kunijibu lakini
baadae akakiri kuwafahamu Alberto’s ila
yeye si mmoja wao.Alinieleza kwamba
Alberto’s walitumia nguvu yao
wakamuweka madarakani ili waweze
kumtumia katika kazi zao mbali mbali.Kwa
ufupi ni kwamba rais Ernest yuko pale
kama picha tu hana maamuzi
yoyote.Anapangiwa kila kitu na
Alberto’s.Makamu wa rais,waziri
mkuu,mawaziri na wakuu wa vyombo vya
usalama wote ni watu wa Alberto’s.Karibu
sehemu zote za muhimu Alberto’s
wamezishika .Alberto’s pia tayari
wamewaweka katika himaya yao asilimia
kubwa ya wabunge na hii inawafanya
wawe na nguvu kwani miswaada yote
yenye manufaa kwao itapita kirahisi bila
matatizo yoyote.Wanatumia pesa nyingi
kila mwezi kuwalipa wabunge hawa”
akasema Austin kisha akanyamaza akavuta
pumzi na kusema
“Baada ya kujihakikishia kwamba
nchi iko mikononi mwao waliandaa
muswaada wa sheria ya haki za binadamu
muswada ambao ndani yake una
kipengele cha kutambua haki za wapenzi
wa jinsia moja,haki za utoaji mimba ,haki
za watumia mihadarati n.k.Muswada huo
ulitarahjia kuwasilishwa bungeni hivi
karibuni na kwa sababu tayari Alberto’s
wana idadi kubwa ya wabnge basi
muswada huo ungepita kirahisi na kuwa
sheria.Nilimsoma Ernest hakuwa
amependezwa na kitendo cha yeye kuwa
kama rais picha asiye na maamuzi kuhusu
masuala ya nchi.Niliona namna
alivyokuwa na hamu ya kuondokana na
jambo hilo.Niliamua kutumia fursa hiyo
vizuri kwa kumpa darasa kuhusu athari za
Alberto’s na nini kitatokea kwa kizazi
kijacho endapo ataacha Alberto’s
waendelee kuiongoza nchi hii.Aliona
msingi wa kile nilichomueleza na
akakubali kuungana nami kupambana na
Alberto’s.Haikuwa
kazi
rahisi
kumshawishi lakini nashukuru Mungu
alikubali na kitu cha kwanza nilichomtaka
akifanye ni kuufuta muswada ule
usipelekwe bungeni na badala yake
uandaliwe muswada mwingine unaotaja
kuwa ni kosa la jinai kujihusisha na
mapenzi au ndoa ya jinsia moja,matumizi
ya mihadarati na utoaji mimba.Jambo la
pili nililomtaka alifanye ni kumvua
wadhifa waziri mkuu na kulivunja baraza
lote la mawaziri ili ateue wapya ambao si
wafuasi wa Alberto’s.Tatu nilimtaka
amuondoe mkuu wa majeshi na
nikamshauri mtu wa kumpa nafasi hiyo
ambaye ninamuamini ni mzalendo wa
kweli.Ernest alikubaliana na mawazo
yangu yote na tayari amekwisha yafanyia
kazi.Muswada umefutwa,waziri mkuu
 
SEHEMU YA 27


ameondolewa,baraza la mawaziri
limevunjwa,mkuu
wa
majeshi
ameondolewa na kwa haya aliyoyafanya
tayari ametoa tamko la vita kati yake na
Alberto’s” Austin akamtazama Job
aliyekuwa ametulia akimsikiliza.Job
akavua koti
“Ninahisi joto.Mambo haya si mambo
madogo.Ni mambo mazito mno” akasema
Job
“Ni kweli haya si mambo madogo.Hii
ni vita kubwa lakini tumeamua kuipigana
kwa ajili ya nchi yetu,kwa ajili ya vizazi vya
sasa na vijavyo.Ni vita ngumu lakini lazima
tuipigane huku Mungu tukimtanguliza
mbele.Alberto’s ni mtandao mkubwa na
wenye nguvu ,wana uwezo wa kufanya
jambo lolote kwa wakati wowote
wanaotaka kwa hiyo mimi na mheshimiwa
rais tayari tumeyatoa maisha yetu
kupambana na mashetani hawa na lolote
litakalotokea tuko tayari.Tumeanza
mapambano kwa kuukata mzizi mkuu wa
Alberto’s hapa nchini ambao ni ofisi ya
rais.Hii ni sehemu waliyokuwa
wakitegemea mno .Tumekata mzizi
mwingine ambao ni waziri mkuu na
baraza la mawaziri.Tumekana mzizi
mwingine ambao ni mkuu wa
majeshi.Haya yote yamefanyika katika
kipindi kifupi na kuwastua sana
Alberto’s.Pamoja na mizizi hiyo mikubwa
kukatwa bado kuna kazi kubwa inatakiwa
kufanywa.Makamu wa rais ni mfuasi wa
Alberto’s na kibaya zaidi hata mke wa rais
naye ni mfuasi wa mtandao huu.”
“Even first lady??!! Job akashangaa
“Ndiyo.Tena yeye ndiye aliyetumiwa
kumshawishi Ernest akubali kuwa rais”
“Kama ni hivyo basi mheshimiwa
rais yuko katika hatari kubwa!! Akasema
Job
“Ni kweli rais yuko katika hatari
kubwa sana na muda wowote kitu
chochote kinaweza kufanyika.Kabla ya
kutoa hotuba yake ile aliyotangaza
kulivunja baraza la mawaziri,watu wawili
asiowafahamu waliingia chumbani kwake
wakiwa na bastora na kumtisha asihutubie
lakini kwa kuwa tayari amekwisha jitoa
mhanga akaamua kuhutubia.He’s in great
danger.Na hilo ndilo hasa lililonifanya
nikakutafuta .Tayari nimeongea na rais
nikamfahamisha hatari inayomkabili na
yeye mwenyewe ameiona hatari hiyo kwa
hiyo tumeshauriana kufanya jambo
moja.Nitaunda kikosi kidogo cha watu
wenye weledi mkubwa katika masuala ya
usalama kwa ajili ya kumlinda
rais.Alberto’s wamesambaa kila kona kwa
hiyo hata walinzi wake wa sasa wanaweza
wakatumika kumuua kwa hiyo kwa
kutumia mamlaka yake atawaondoa
walinzi wake wa sasa na tutaweka walinzi
wapya tutakaowateua .I need you in that
team.” Akasema Austin.Job akacheka
kidogo na kusema
“Austin you’re my brother.Mimi na
wewe tumetoka mbali .Umenifundisha
mambo mengi .I respect you so much but I
cant be part of that team”
“C’mon Job.This is serious. I need
you” akasisitiza Austin
“No Austin” akajibu Job
“Kwa nini Austin? Wewe ni mmoja
wa watu wachache ninaotaka kushirikiana
nao katika hii vita.Hii vita si ya kwangu na
rais pekee bali tunapigana kwa ajili ya nchi
yetu kwa hiyo ungana nami
tafadhali.Nakuhitaji sana uwepo katika
kikosi cha kumlinda rais.Huyu ndiye
mwangaza wetu katika mapambano haya
hivyo anatakiwa alindwe.Ikitokea rais
akauawa kabla hatujaimaliza vita hii then
we’re done.The war will be over.Ili tusifike
hapo tunatakiwa kumlinda rais kwa nguvu
zetu zote.” Akasema Austin
“Austin ninaelewa unachokisema na
niko tayari kusaidiana nawe katika
mapambano haya lakini naomba nisiwe
sehemu ya timu ya kumlinda
rais.Nitakusaidia katika upande mwingine”
“Sikia Job.Vita hii si vita
nyepesi.Inahitaji watu wenye ujuzi na
uzoefu wa hali ya juu katika mapambano
kama haya na mmoja wa watu hao ni
wewe” akasema Austin na kuinamisha
kichwa kisha kwa sekunde kadhaa halafu
akamtazama Job
“Kuna jambo ambalo sikuwa
nimekueleza bado ambalo labda linaweza
kukushawishi ukakubaliana nami”
“Jambo gani hilo? Akauliza Job
“Hata mimi sikuwa nalifahamu ni
rais ndiye aliyekuja kunieleza.Ni kwamba
katika kila nchi ambayo rais wake ni
mfuasi wa Alberto anapaswa kuhakikisha
anawalinda na kuwawezesha wafanya
biashara wakubwa wa dawa za kulevya
wafanye biashara yao kwa uhuru bila
kubughudhiwa na chombo chochote cha
usalama.Hiki ni chanzo kikubwa cha
mapato kwa Alberto’s kwani wafanya
biashara hao walio chini yao hutoa kiasi
kikubwa cha fedha kama mchango wao
kwa ajili ya kuendesha jumuiya.Ernest
mkasa naye akiwa chini ya Alberto’s
alipewa sharti hilo na amelitekeleza na
ndiyo maana utaona katika kipindi cha
uongozi wake biashara ya dawa za kulevya
imeshamiri sana hapa nchini.Hii ni kwa
sababu wafanya biashara hawadhibitiwi
na wako huru kufanya biashara
zao.Nilimtaka anipe orodha ya wafanya
 
SEHEMU YA 28


biashara hao ili tuweze kupambana nao na
ameahidi kunipatia orodha hiyo .Baada ya
kuisikia historia yako ninahisi kuna
uwezekano mkubwa hata huyo dogo Bill
aliyepelekea ukaishi katika maisha haya
naye yumo katika hiyo orodha .It’s tme to
fight back.Ni wakati wetu wa kuwa
huru.Hatuwezi kuwa huru endapo
hatutawaondoa wale wote waliotufanya
tuishi maisha ya namna hii ,wale ambao
wameibinafsisha nchi hii na kuifanya
yao,hatutakuwa
huru
endapo
hatutafanikiwa kuwaondoa Alberto’s hapa
nchini.Mpaka lini nitaikimbia nchi yangu?
Makaburi ya wazazi wangu yako hapa
Tanzania kwa hiyo hata kama nitabadili
uraia lakini sintaweza kuibadili damu ya
Tanzania.Lazima mambo haya yafike
mwisho na yatafika mwisho endapo
tutaweza kuwaondoa Alberto’s na mizizi
yake hapa nchini.Nani wa kuwaondoa
Alberto’s hapa nchini? Ni mimi ,wewe na
wazalendo wengine wachache walio tayari
kuifia nchi yao.Tunaweza tusifanikiwe au
tusifike mbali katika vita hii lakini
tukianzisha tutaungwa mkono na watu
wenye nia njema na nchi hii.Naomba
usiogope Job,hii ni nafasi ya pekee
imejitokeza ambayo itakusaidia kulipiza
kisasi kwa wale wote waliofanya maisha
yako kuwa hivi pia kupata ukweli kuhusu
mke na mtoto wako walipo.This is our
chance brother” akasema Austin .Michirizi
ya machozi ikaonekana machoni mwa Job
“Austin umenichoma mno moyo
wangu na kuyaamsha tena machungu
niliyonayo dhidhi ya Dogo Bill na kundi
lake.Wamenifanyia unyama mkubwa
kuniachanisha na mke wangu.I loved Mona
so much lakini kwa tamaa ya pesa
akachagua kunikimbia.You are right.Its
pay back time.Austin nitaungana nawe
katika haya mapambano lakini si kwa
kuingia katika timu ya kumlinda
rais.Nataka niwe pembeni yako
tupambane kwa pamoja.Nitakusaidia
kutafuta watu watakaounda hicho kikosi
cha ulinzi wa rais.Nataka niwepo katika
uwanja wa mapambano na nihakikishe
ninamkamata dogo Bill kwa mikono yangu
mwenyewe.Nikubalie kwa hilo Austin”
akasema Job .Austin akamtazama kwa
muda halafu akatabasamu na kumpa Job
mkono
“Karibu
katika
operesheni
fagio.Tunakwenda kufagia nchi hii na
kuuondoa uchafu wote na kuifanya safi
tena kama ilivyokuwa awali enzi za
waasisi wetu” akasema Austin
“Mungu atusaidie “ akasema Job
“Austin baada ya kuwa tumekuwa
kitu kimoja naomba sasa unipe mikakati
yako namna ulivyopanga kuiendesha
operesheni hii.Lakini kabla hujanieleza
chochote nina ombi moja kwako”
“Omba chochote Job” akasema Austin
“Ahsante sana.Naomba ukubali
kumuingiza Amarachi katika operesheni
hii.She’s a great asset to us”
Austin akakuna kichwa akafikiri
kidogo halafu akamtazama Job
“ Job I have to be honest with you.Hii
ni opereseni tofauti sana na nyingi ambazo
tumewahi kuzifanya kwa hiyo napata
ugumu kidogo kulikubali ombi
lako.Tunakwenda kupambana na adui
mwenye nguvu na mbinu nyingi kwa hiyo
tunahitaji kuwa na watu wenye uwezo
mkubwa kama wewe.Zaidi ya yote I cant
work with people I don’t trust” akasema
Austin
“Nafahamu msimamo wako Austin
lakini
naomba
uniamini
ninachokwambia.This
woman
is
wonderfull.Ana uwezo mkubwa kiasi cha
kunishangaza hata mimi .Nakuhakikishia
anaweza kuwa na msaada mkubwa
kwetu.She’s well trained .Please let her in”
Austin akafikri tena kidogo na
kusema
“Sawa Job ,nimekuelewa lakini kabla
sijaamua chochote kama nimjumuishe ama
vipi I’ll have to talk to her in person. I want
her to understand how important this
mission is for me,you and for our nation”
akasema Austin
“Thank you”akajibu Job
“Ningetaka sasa nifahamu mikakati
yako kuhusiana na suala hili” akasema Job
“Kitu cha kwanza tunachotakiwa
kukifanya ni kutafuta namna ya kumlinda
rais.Nguvu aliyonayo ni msaada mkubwa
sana kwetu kwa hiyo lazima tumlinde kwa
nguvu zetu zote.Tunatakiwa haraka sana
tupate kikosi kipya cha kumlinda.Kwa sasa
tunaendelea kujipanga ,nitakapomaliza
kazi aliyonipa rais tutakaa pamoja na
kujadili nini cha kufanya na wapi kwa
kuanzia.” Akasema Austin
“Austin we have to make things
faster.Tukizidi kuchukua muda mrefu
tutawapa nafasi ya kujipanga na
wakatuzidi maarifa.Naamni hivi sasa
watakuwa katika mstuko mkubwa kwa hili
lililotokea so we have to take them by
surprise.Tusiwape nafasi” akasema Job
“Uko sahihi Job,lakini watu hawa
wamejiimarisha sana na mizizi yao tayari
imesambaa katika sehemu kubwa kwa
hiyo basi inabidi tukae chini tujipange
namna ya kuwakabili.Kwa pamoja
tutaamua namna bora ya kuwandoa”
Austin akanyamaza kidogo na kusema
 
SEHEMU YA 29


“Job kuna jambo lingine ambalo
nadhani itakuwa vyema endapo
ukilifahamu.Ukiacha kazi aliyonipa rais ya
kutafuta sampuli kutoka kwa
Monica,alinipa pia kazi nyingine.Alinitaka
nikamtoe hospitali daktari mmoja
aliyekuwa katika hatari ya kuuawa
anaitwa Dr Marcelo.Mtu huyu alipigwa
risasi lakini kwa juhudi za madaktari
waliyaokoa maisha yake.Watu waliotaka
kumuua bado waliendelea kumfuata hadi
hospitali na kutaka kummaliza ndipo rais
aliponitaka nikamtoe kwa siri.Nilifanikiwa
kwa hilo na Dr Marcelo niko naye mahala
ninapoishi.Leo hii nikiwa sina hili wala
lile,amekuja ghafla mpenzi wangu Maria
akiwa ameongozana na baba yake Mr Boaz
.Huyu Boaz ndiye aliyenikomboa toka
mikono ya Alshabaab kwa hiyo ni mtu
ninayemuheshimu na kumthamini
mno.Ujio wake kwangu jioni ya leo
ulikuwa ni kuniomba nimfanyie kazi
yake.Amenipa kazi ya kumtafuta Dr
Marcelo na kukipata kitabu ambacho
anakihitaji toka kwake. Alinipa maelezo
marefu kidogo kuhusiana na kitabu hicho
na umuhimu wake.Boaz anafahamu kuwa
Marcelo anashirikiana na watu Fulani na
ndio waliomtorosha hospitali lakini
hafahamu ni akina nani kwa hiyo amenipa
jukumu la kuwafahamu pia watu hao
.Alienda mbali zaidi na kunitaka
niwatafute na kuwapata watu wawili wa
karibu na Marcelo ambao ni Danel Swai
rafiki wa karibu wa Marcelo na Monica
Benedict ambao anahisi wanafahamu
mahala aliko Marcelo.Anataka nikiwapata
niwatese na waeleze wanachofahamu
kuhusu Marcelo na kisha niwaue.Huyu
Monica ndiye ambaye rais anataka
athibitishe kama ni mwanae kwa kutumia
sampuli aliyonipa kazi ya kuitafuta.”
“Oh my God !!! akasema Job
“Nimewekwa kati kati na sasa ni
jukumu langu kuamua niende upande
upi.Nikichagua upande wa Boaz ina maana
nitakuwa nimemsaliti rais na mapambano
dhidi ya Alberto’s hayataweza
kufanikiwa.Nikichagua upande wa rais
nitaingia katika mgogoro na mtu
aliyeyaokao maisha yangu na kunifikisha
hapa nilipoona endapo nitaingia katika
mgogoro na Boaz moja kwa moja nitakuwa
nimeingia katika mgogoro na Maria
ambaye ni mwanamke ninayempenda
kuliko wote.Hata hivyo nimechagua
kusimama upande wa rais.Niko tayari
kumkosa mpenzi wangu Maria kwa
manufaa ya nchi.Haya ni maamuzi
magumu sana nimeyafanya kwani mimi na
yeye tutapita lakini Tanzania itabaki daima
kwa hiyo nitapigana kwa ajili ya
Tanzania.Kwa hiyo Job tuna kazi kubwa ya
kufanya kumlinda Monica kwani endapo
nitashindwa kutekeleza matakwa ya Boaz
lazima atatafuta watu wengine wa
kuifanya kazi yake .Sababu nyingine ya
kumlinda Monica ni kwamba Alberto’s
wanaweza wakafahamu kuwa Monica ni
mtoto wa Ernest kwa hiyo wanaweza
wakamtumia kama silaha katika
kumlazimisha Ernest afanye yale
wanayoyataka.” Austin akanyamaza
kidogo kisha akaendelea.
“Jambo la pili nikwamba baada ya
kulivunja baraza la mawaziri,rais anahitaji
kuunda upya baraza lingine.Kabla ya
kuunda baraza jipya anahitaji kwanza
kumpata waziri mkuu.Rais amekuwa na
wakati mgumu wa kumpata mtu wa
kumpa nafasi ya waziri mkuu ambaye
atakuwa ni mzalendo na ambaye si mfuasi
wa Alberto’s.Jana alikuja kwangu na
kunipa taarifa kuwa tayari amefanya
maamuzi nani awe waziri mkuu mpya wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania na mtu
anayefikiria kumpa nafasi hiyo ni Wilson
Mukasha”
Job akapatwa na mstuko mkubwa
akainuka na kumsogelea Austin
“No ! That can’t happen!! Akasema
kwa sauti ya juu
“Hivyo ndivyo ilivyo Job.Mukasha
ndiye ambaye rais amemuona anafaa kwa
ajili ya kuwa waziri mkuu mpya wa
Tanzania ndiyo maana uliponitajia jina
hilo kuwa ni mmoja wa watu
wanaojihusisha na biashara ya dawa za
kulevya nilistuka sana.” Akasema Austin
“Austin rais atafanya kosa kubwa
sana endapo atamteua Mukasha kuwa
waziri mkuu.Hamfahamu vizuri Mukasha
ni mtu wa aina gani.Austin you have to
stop that.Do whatever you can to stop that
from happening” akasema Job na
kuinamisha kichwa
“Nini kinatokea kwa hili taifa?
Akasema kwa sauti ndogo halafu
akamtazama Austin.
“Austin we have to stop
that.Tukiruhusu rais akafanya kitu kama
hicho vita hii ambayo tumejitolea
kuipigana itakuwa kazi bure.All our
sacrifices will be for nothing !!
“Nimekuelewa Job lakini kuna tatizo
moja .Rais anamuamini mno Mukasha.Ni
mmoja kati ya watu wachache ambao rais
anawaamini mno.Ili tumzuie asifanye
hicho alichokusudia kukifanya yaani
kumteua Mukasha kuwa waziri mkuu
yatupasa tuwe na ushahidi wa kutosha
kumuhakikishia rais kuwa Mukasha hafai
na anashiriki katika biashara ya madawa
ya kulevya.Kumueleza kwa maneno
 
SEHEMU YA 30


matupu hataweza kutuelewa” akasema
Austin
“Austin una uhakika hata wewe
ukimueleza hatakuelewa? Akauliza Job
“Kwa muda mfupi niliomfahamu rais
Ernest Mkasa nimeshuhudia namna
anavyomuamini Mukasha.Hata akielezwa
na nani itakuwa vigumu kumuamini bila
kuwa na ushahidi wa kujitosheleza.Hivyo
basi tunatakiwa kufanya juu chini kutafuta
kila aina ya ushahidi utakaoweza
kumfanya rais abadili maamuzi yake”
“Hiyo nayo ni kazi nyingine akasema
Job
“Ni kazi mpya ambayo lazima
tuifanye.Lazima tuzuie jambo hili
lisifanikiwe.Tunapaswa kuanzia sasa
kuanza kumchuguza Mukasha kwa siri.”
Akasema Austin
“Kwa nini tusiutumie ukaribu wako
na rais kama sehemu ya kuanzia? Rais
anakuamini kwa hiyo tafuta namna
unavyoweza kuitumia nafasi hiyo
kumchunguza Muk...”
“Wait .! Austin akamkatisha Job
“Kuna kitu nimekikumbuka .Wakati
rais ananitambulisha kwa Mukasha
alinieleza kwamba Yule ni rafiki yake
,msiri wake na ndiye aliyempa taarifa
zangu.Hii ina maana kwamba Mukasha
ananifahamu vizuri na anafahamu kuwa
niko kwa Boaz na ndiye aliyewasiliana na
Boaz.Nakumbuka suala la kunikomboa
toka mikononi mwa Alshabaab lilikuwa la
siri kubwa kwa hiyo endapo Mukasha
anafahamu basi lazima atakuwa
ameelezwa na Boaz.Lazima yeye na Boaz
watakuwa na ukaribu.” Akasema Austin na
kutabasamu
“Boaz ni sehemu nzuri ya sisi kuanzia
kumchunguza Mukasha.Hawa wawili kuna
mambo wanashirikiana na endapo
tutachimba kwa undani zaidi kuna mambo
mengi tutayagundua” akasema Austin
“Boaz is your father in law,right?
Akauliza Job
“ Yes he is” akajibu Austin
“ Umekuwa naye karibu kwa kipindi
kirefu,unaweza ukamuelezeaje?
“Ninamfahamu Boaz ni mfanya
biashara ambaye ni mbunifu na aliye
tayari kufanya lolote linalowezekana ili
mradi biashara zake zikue.Ni mtu mwenye
ushawishi na malengo.Ni mtu
mpambanaji.Toka nimefahamiana naye
sijawahi kugundua jambo lolote baya na
hata biashara zake nyingi ni halali,hana
rekodi mbaya katika biashara zake ila
ninafahamu kuna biashara chafu
anazifanya ambazo hajawahi kuniweka
wazi ila sikutaka kufuatilia kwa sababu
sikutaka kuanzisha mgogoro na familia
ile.kazi aliyoniomba nimfanyie leo imenipa
mwanga kuwa Boaz ni mtu katili na
hatari.Huu ni wakati muafaka wa
kumfahamu ni nani hasa” akasema Austin
Job akamtazama Austin kwa makini
na kuuliza
“Your girlfriend Maria,how much do
you love her?
“More that I can explain.Why do you
ask?
“Going after his father will
complicate things between you two so I
want you to be sure of what you want to
do”
Austin akainamisha kichwa
akatafakari kidogo halafu akasema
“Sijawahi kuzama mapenzini kama
nilivyozama kwa Maria lakini kwa maslahi
ya nchi ni tayari kwa lolote”
“Good” akasema Job
“Ninacho chumba cha mahojiano
humu ndani ambacho tutakitumia
kumuhoji Boaz.Kina zana maalum kwa ajili
ya kumfanya mtu aseme kwa hiyo
nakuhakikishia Boaz akiingizwa humo
lazima atasema”
“Nategemea muda wowote kuanzia
kesho kuipata sampuli ninayoitaka toka
kwa Monica ambayo itatuwezesha kufanya
kipimo cha vinasaba na kuupata
ukweli.Baada ya hapo tutaifungua rasmi
operesheni fagio”
“So tell me about this woman Monica
Benedict.Is she pretty?
“C’mon Job huu si muda wa kuwaza
mambo kama hayo” akasema Austin
 
LEGE una vitabu au unajua wapi nitapata vitabu viwe vya Kiswahili?
unahitaji vitabu gani?? mkuu mm ninavyo vingi sana hasa vya kijasusi vya musiba karibia vyote na vingine mbali mbali lkn siuzi.ila ukitaka vya kununua nitakuelekeza
 
Huyu lege kwa mtazamo wangu
Uwa anachukuaga mahali hii hadithi
Nahisi wamemkatalia safari hii
Kwasababu wata wanakuwa wanaisoma huku so hawanunui vitabu
See me true
Hakuna ubize wa hivi
mkuu wewe utaongeya yote lkn ukweli kamwe hutoweza kuufahamu harafu why ulete ligi ya kutoa majibu ya kufikirilka mkuu fanya ujiongeze basi unajua kumbe hii ni story ya kulipia fanya basi na wewe ulipie buku 3 tuu inakushindaa maana maneno mengi sana..harafu ukisha lipia huko muulize atakaye kuuzia mzigo unasiku ngapi sokono
 
Ya kitoto mno mkuu
Hakuna serious man eti yupo bize anayeweza fanya hivi watu hamjang'amua tu
Mi mwenyewe nipo bize kishenzi
Bit not this way kama jamaa anavyojielezeaga
mkuu unataka kunifundisha nifuate ratiba kama zako eee?? kumbuka mm na wewe si sawa wewe wakishua mm mtoto wa uswahilini usawa wa kulenga kwa manati unauweza wewe??
 
Dahhhh LEGE wewe ni kiboko ndio maana tunaweweseka kila siku humu ndani ya thread yako.uwepo humu au ukipotea thread inaendelea kuonyesha kuwa wewe ni mtu muhimu sana.Mkuu wkend ndio hii tuonjeshe tena mkuu na hivyo ni siku nyingi tumekumisss .. ...
 
Back
Top Bottom