QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

SEHEMU YA 97



nataka kufahamu kuhusu Yule rafiki
yangu niliyekuomba unisaidie kama zoezi
lile lilifanikiwa.Nina wasiwasi mwingi
kuhusu maisha yake”
“Oh ! samahani sana Monica
nilisahau kabisa kumuuliza rais wa
Tanzania kama suala lile lilifanikiwa.Ngoja
nimpigie sasa hivi” akasema David na
kuchukua simu akatafuta namba za
Ernest Mkasa akampigia
“ Hallow David “ akasema Ernest
alipopokea simu
“ Habari za asubuhi Ernest “
“ habari nzuri David ,habari za
Kinshasa?
“ Huku kwema kabisa.Ernest
nimekupigia ili kufahamu kuhusu ule
msaada niliokuomba wa kumuondoa Yule
kijana hospitali,je lile zoezi lilifanikiwa?
“ Ndiyo David lile zoezi
lilifanikiwa.Samahani sana sikukutaarifu
mapema.Dr Marcelo ameondolewa pale
hospitali na kwa sasa amehifadhiwa
sehemu salama tukisuburi maelekezo
yako”
“ Ahsante sana Ernest.Ninaomba
uendelee kumuhifadhi sehemu salama
nitakupa maelekezo hivi karibuni.Naomba
unijulishe kama kuna gharama zozote
zinahitajika”
“ usijali David hakuna gharama
zozote kuwa na amani”
“ Ahsante sana Ernest” akajibu David
na kukata simu akamgeukia Monica
“ Monica usiwe na wasi wasi tena
malaika wangu lile zoezi limefanikiwa na
rafiki yako yuko sehemu salama kwa sasa”
Monica akamkumbatia David kwa furaha
na kumbusu
“ Ahsante sana David .Hiki
ulichokifanya ni kitu kikubwa mno
kwangu” akasema Monica
“ Monica kwa ajili yako niko tayari
kufanya jambo lolote .Hata hivyo rais
anasubuiri maelekezo ya nini kitafuata
baada ya kumuondoa Marcelo
hospitali.Umepanga kumsaidiaje rafiki
yako?
“ Kitu kikubwa nilichokihitaji
kwanza ni kumtoa hospitali na baada ya
hapo nitajua nini kitafuata pale
nitakaporejea Dar es salaam.”
“ Ukihitaji msaada wa aina yoyote ile
usisite kunitaarifu”
“ Nitakutaarifu David kila pale
nitakapohitaji msaada” akasema Monica
 
SEHEMU YA 98



DAR ES SALAAM – TANZANIA
Habari kubwa iliyoliamsha taifa
asubuhi hii ni hotuba ya rais aliyoitoa
usiku .Maamuzi aliyoyafanya yaliendelea
kuwa gumzo kila kona ya nchi.Wengi
walipiga simu katika vituo vya redio na
televisheni wakimpongeza rais Ernest
Mkasa kwa maamuzi yake ya busara
kuhusiana na muswada ule wa haki za
binadamu pamoja na kulivunja baraza la
mawaziri.Wakati mjadala wa maamuzi
yale ya rais ukiendelea ,kurugenzi ya
mawasiliano ikulu ikatoa taarifa kwa
vyombo vya habari ambayo ilizidi
kuwashangaza wengi.Taarifa hiyo ilieleza
kwamba rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania amemvua wadhifa mkuu wa
majeshi na Jenerali Bonifasi Kandima na
papo hapo amempandisha cheo Luteni
jenerali Lameck Msuba kuwa jenerali na
kumteua kuwa mkuu wa majeshi kushika
nafasi iliyoachwa wazi na jenerali
Bonifasi.Uteuzi huo unaanza mara
moja.Taarifa hii ilizidi kuukoleza moto wa
mjadala uliokuwa ukiendelea.
Austin akiwa sebuleni akifuatilia
habari zilizoliamsha taifa pamoja na
uchambuzi wa magazeti ,mara mtangazaji
aliyekuwa akichambua kurasa za magazeti
akasitisha na kutangaza habari
iliyowafikia pale muda huo kuhusiana na
rais kutengua uteuzi wa mkuu wa majeshi
na kumteua jenerali Lameck Msuba kuwa
mkuu mpya wa majeshi.Austin akaruka
kwa furaha
“ Good !! Very good.Sasa vita imeanza
rasmi” akaongea mwenyewe pale sebuleni
“ Vita gani Austin? Akauliza Dr
Marcelo baada ya kuingia pale sebuleni na
kumkuta Austin akizungumza mwenyewe
kuhusiana na vita.Austin akastuka na
kugeuka akajikuta akitazamana na
Marcelo
“ Marcelo,vipi maendeleo yako?
Akauliza

Ninaendelea
vizuri
Austin.Nimekusikia unaongea mwenyewe
kuhusu vita,ni vita ipi hiyo unaiongelea?
“ Forget about that.Nilikuwa
natazama taarifa ya habari rais ameteua
mkuu mpya wa majeshi”
“ Austin nini kinaendelea? Jana rais
kaufuta muswada wa haki za binadamu
pamoja na kulivunja baraza la
mawaziri,leo kamvua wadhifa mkuu wa
majeshi ,nini kinaendelea? Akauliza Dr
Marcelo.Kabla Austin hajajibu Marcelo
akauliza tena
“ Who are you Austin? Kuna kitu gani
kinaendelea kati yako na rais?
“ Dr Marcelo itakuwa vyema endapo
hutajihusisha na masuala yoyote
yanayohusiana na mimi wala rais.Kikubwa
unachopaswa kukitilia mkazo kwa sasa ni
kupona na kuhakikisha wale wote
wanaokuwinda wakuue wanapatikana.”
Akasema Austin.Dr Marcelo akamtazama
Austin kwa makini na kusema
“ Austin kuna jambo ambalo
limeninyima usingizi kabisa.Kama
nilivyowaeleza jana kwamba nimestuka
sana kusikia eti rais wa Congo ndiye
aliyemuomba rais wetu anisaidie kunitoa
pale hospitali.Sijapata usingizi usiku wa
leo nikitafakari namna David Zumo
 
SEHEMU YA 99



alivyoingia katika hili suala
langu.Sifahamiani naye na wala hatuna
mahusiano yoyote ya kindugu.Kwa kuwa
uko karibu na rais naomba unisaidie
kumuomba amuulize David Zumo
amezipata wapi taarifa zangu.Nahitaji
sana kufahamu.Au kama kuna uwezekano
niongee na David moja kwa moja kwa
simu.Yawezekana kuna jambo limejificha
hapa na silifahamu”
“ Sawa Marcelo nitaongea na rais na
kuufikisha ujumbe wako .Halafu kuna
jambo lingine ni kwamba leo nitatoka
kuna sehemu ninakwenda.Utabaki peke
yako hapa kwa hiyo usiogope.Hapa ni
sehemu salama na hatari yoyote ikitokea
nitajua na nitajua nini cha
kufanya.Usijaribu kutoka nje kama humu
humu ndani na usimfungulie mlango mtu
yeyote Yule zaidi yangu.” Akasema Austin
“ Nimekuelewa Austin.Nitakupa pia
orodha ya dawa ninazozihitaji
ukaninunulie ” akasema Marcelo na
kuelekea chumbani kwake akimuacha
Austin akiandaa stafstahi.
“ Suala la David Zumo kufahamu
kuwa ninataka kuuawa bado
linanishangaza mno.Mtu pekee ambaye
nilimuomba msaada ni Monica lakini toka
nilipomueleza jambo hili sijamuona tena
.Amepotelea wapi? Au yawezekana
aliogopa kujiingiza katika masuala haya ya
hatari .Naanza kuhisi kuwa tayari
nimekwisha mpoteza Monica.Kwanza
aligundua nina saratani ya damu na
halafu nikapigwa risasi na nikamuomba
anisaidie kunitorosha hospitali.Naweza
kukiri kwamba nilimtwisha mzigo
mkubwa tofauti na uwezo wake.Lakini
nilifanya hivyo kwa kuwa sikuona mtu
mwingine ninayeweza kumuamini katika
jambo nyeti kama hili.Ninamlaumu sana
baba kwani yeye ndiye chanzo cha haya
yote.Ninaamini matatizo yote haya
yamesababishwa na kile kitabu.Kitabu
kile kilikuwa na nini ndani yake? Naanza
kuhisi kuna jambo kubwa limejificha
ambalo nahitaji kulifahamu.Ni nani
aliingia chumbani kwangu akachukua
kitabu kile?Mtu ambaye nilipewa namba
nimpigie ni nani? Kuna mtu mmoja tu
ambaye anaweza kunisaidia kupata
majibu ya maswali haya ambaye ni
Austin.Nitaongea naye nimueleze ukweli
na nitamuomba anisaidie kuutafuta
ukweli.Anaonekana ni mtu jasiri katika
kazi yake na mwenye mbinu nyingi.Kwa
mbinu aliyoitumia ili kunitoa pale
hospitali inaonyesha ni jinsi gani alivyo
mahiri “ akawaza Marcelo na kujikuta
akizama zaidi mawazoni
“ Austin na rais Ernest wana jambo
gani la siri? Nilistuka sana kumuona rais
hapa tena akiwa katika muonekano wa
tofauti kabisa kiasi cha kumfanya iwe
vigumu kutambulika.Ni wazi rais hataki
kujulikana kama anakuja hapa
usiku.Kama ni hivyo lazima kuna jambo
linaloendelea kati yao.Austin ni nani?
Anaweza kuwa mlinzi wa siri wa rais ?
Akajiuliza
“ Ngoja niachane na mambo yao
nielekeze nguvu katika masuala yangu ila
jioni ya leo nitazungumza na Austin na
nitamueleza kwa kirefu suala langu na
kumuomba anisaidie kwani sielewi
hatima ya maisha yangu “ akaendelea
kuwaza Marcelo
Wakati Austin akifanya maandalizi
kwa ajili ya kuanza kazi ya pili ya kutafuta
ukaribu na Monica,katika ikulu ya Dar es
 
SEHEMU YA 100



salaam hali ilikuwa tofauti na siku
nyingine.Maamuzi
yaliyoendelea
kufanywa na rais yaliwastua wengi.Wengi
walijaribu kujiuliza sababu ya maamuzi
yale makubwa lakini wengi hawakujua
kwa nini rais alichukua maamuzi yale .
Ernest Mkasa aliingia ofisini kwake
mapema mno tofauti na kawaida
yake.Alikuwa na mambo mengi ya kufanya
siku hii
“ Siku mpya na mapambano
yanaendelea.Habari hii ya maamuzi
niliyoyafanya imesambaa dunia nzima
.Naamini hivi sasa maadui zangu
watakuwa wanajipanga ili kukabiliana
nami.Natakiwa kufanya mambo haraka
haraka kuwadhibiti.Nitauzingatia ushauri
wa Austin kubadilisha kikosi cha
kumlinda rais kwani picha niliyoiona jana
si nzuri kabisa. Alberto’s wanaweza
wakaniua wakati wowote .Hata hivyo
wapo walinzi wawili ambao wataendelea
kuwa walinzi wangu Evans na
Winnie.Siwezi kumuacha Winnie katika
orodha ya walinzi wangu kwani licha ya
kuwa ni mlinzi wangu lakini amekuwa ni
mfariji wangu kwa muda mrefu sasa.”
Akawaza Ernest na kutabasamu kwa mbali
“ Ninashukuru kwa ujio wa Austin.Ni
kijana jasiri asiyeogopa na mwenye akili
nyingi.kwa sababu yake nimepata ujasiri
wa kuja kufanya haya niliyoyafanya.kwa
muda mrefu nilikuwa nimefikiria
kuanzisha mapambano na Alberto lakini
sikuwa nimepata mtu sahihi wa
kushirikiana naye.Kwa sasa baada ya
kumpata Austin lazima niwafutilie mbali
mashetani hawa” akawaza Ernest
“ Kinachonila akili kwa sasa ni nani
nimteue awe waziri mkuu? Nahitaji
haraka sana kuunda serikali lakini bado
mpaka sasa sijampata mtu ambaye
anaweza kuwa waziri mkuu.Asilimia
kubwa ya wabunge ni wafuasi wa Alberto’s
na sitaki kurudia makosa. sitaki tena
kuwa na Alberto katika serikali
yangu.Nitaanza kwanza na waziri
mkuu.Nataka awe ni mtu ninayemuamini
.Kichwani kuna majina mawili tu ambayo
yanazunguka.Austin na Mukasha.Austin
angefaa sana kuwa waziri mkuu tena
kijana mzalendo na mchapakazi lakini
yeye ndiye ninayemtegemea asimame
mstari wa mbele kuongoza mapambano
haya.Nikimtoa Austin ninabaki na
Mukasha.Huyu amefanya kazi ikulu kwa
muda mrefu,ni mtu mzuri mwadilifu na
muaminifu.Anafaa sana kuwa waziri
mkuu.Nitaongea naye kuhusu jambo hili
na
kumuomba
anisaidie.Endapo
tutamaliza mapambano haya salama
Austin nitamtafutia nafasi nyingine
serikalini aidha uwaziri au nimteue awe
mkuu wa usalama wa taifa” akawaza
Ernest akamuita Evans mlinzi wake
anayemuamini sana
“ Evans wewe ni mmoja wa watu
ninaowaamini mno” akasema Ernest
“ Ahsante mheshimiwa rais” akajibu
Evans
“ I know at any second you are ready
to take a bullet for me.”
“ Yes Mr President “ akajibu Evans
kwa adabu.
“ Ahsante sana kwa hilo.Evans
nimekuita hapa kukueleza kwamba kwa
sasa ninapitia wakati mgumu sana katika
uongozi wangu.Hiki ni kipindi ambacho
nakuhitaji mno.Nahitaji ulinzi wa kutosha
na wa uhakika kwa ajili hiyo basi kuna
mabadiliko kidogo nitayafanya katika
kikosi cha kumlinda rais.Nitaunda kikosi
kidogo cha watu wachache ambacho
utakiongoza
wewe.Nitakufahamisha
baadae kwa kina zaidi kuhusu jambo hili
lakini kwa sasa kuna sehemu nataka
nikutume.Nataka uende pale katika ofisi
za Ernest group of campanies utakutana
na mtu mmoja anaitwa Susan yombo kuna
mzigo atakupatia nataka uupeleke kule
hotelini ukauhifadhi katika chumba
changu.”
“ sawa mheshimiwa rais nitafanya
hivyo ulivyoagiza” akasema Evans kwa
ukakamavu
“ Ahsante Evans .Nitakuwa na
maongezi nawe marefu jioni ya leo.”
Akasema Ernest na evans akatoka
kuelekea mahala alikotumwa
 
Asante lege.niliisuburia wee mwisho umetuwekea. Najua sometimes unavyotucheleweshea hufanyi makusudi.asante
 
kaeni mkao wa kula story nyingine toka kwa mtunzi yule yule aliyetunga peniela now kaja na kitu kiitwacho queen monica. kutana na kijana AUSTIN JANUARY mtanashati na jasusi hatari anafanya mambo makubwa sana.

ALBERTOS kundi hatari linalotaka kuitawala dunia limeingia pia tanzania
Kumbe yakutungwa na mtunzi
 
Back
Top Bottom