QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

QUEEN MONICA: Story yenye mambo ya kijasusi ndani yake

Sisi wa nje ya nchi tutapataje au ndio tutume buku 3 kwa western union?
 
QUEEN MONICA
SEASON 7
ILIPOISHIA SEHEMU
ILIYOPITA
“Mheshimiwa rais,mimi kama
mkuu wa majeshi nina haya ya
kusema.Tumeshambuliwa.Adui
aliyetushambulia anafahamika na
tayari amejitokeza hadharani
akakiri kuhusika na unyama huu
mkubwa uliotokea na kama
haitoshi bado anaendelea kutoa
vitisho vya mashambulio zaidi
iwapo hatutakuwa tayari
kutekeleza matakwa yake.Mimi
kama mkuu wa majeshi
napendekeza kwamba
tusikubaliane na matakwa yake
kwani huo ni ushindi kwake.Sisi ni
nchi yenye nguvu,sisi tunajeshi
kubwa lenye nguvu na
linaloogopeka afrika kwa nini
tusumbuliwe na kikundi kidogo
kama Alshabaab? Hatuwezi
kukulbali hilo.Kwa kuwa
Alshabaab wametangaza vita kazi
yetu ni kuwaonyesha sisi ni
nani.Dunia inapaswa kutambua
kwamba Tanzania ni nchi ya amani
lakini ikichokozwa kipigo chake
hakina mfano.Tuwaonyeshe kazi
hawa Alshabaab” akasema Jenerali
Lameck Msuba.Watu wote mle
ndani ya chumba wakabaki kimya
wakisubiri maamuzi ya rais.
“ Ndugu wajumbe
,nimeyasikia mawazo yenu
kuhusiana na jambo hili na kama
alivyosema Jenerali Lameck
kwamba hiki kilichofanywa na
Alshabaab ni tangazo la vita.Sisi
kama taifa hatutaweza
kukubaliana na uchokozi huu na
ninakubaliana na mkuu wa
majeshi kwamba hakuna muda wa
kupoteza kufanya uchunguzi
wakati tayari adui tunamfahamu
na anatamba.Mimi kama rais natoa
ruhusa ya kuwaonyesha kazi hawa
mashetani.Nataka mpaka
kutakapopambazuka tayari niwe
nimesikia jeshi letu limeanza
kuwafundisha adabu maharamia
hawa.Hatuwezi kuishi kwa
wasiwasi na kikundi kidogo kama
hiki.Mkuu wa majeshi kaa na
makamanda wako na mpange
namna ya kuanza kuwafunza
adabu hawa jamaa lakini kabla ya
kufanya shambulio lolote naomba
kwanza nijulishwe.” Akasema rais
kisha akainuka akatoka mle ndani
ya chumba akatoa simu na
kuzitafuta namba za Habib
akampigia
“ Mheshimiwa rais,kuna
taarifa nzuri unataka kunipa?
Akauliza Habib baada ya kupokea
simu
“ Habib kuna jambo nataka
kukutaarifu.Kwanza kuna taarifa
za kutia moyo kuhusiana na
mahala aliko Yasmin.Kuna kila
dalili kwamba anaweza
akapatikana hadi kufikia
asubuhi.Jambo la pili nataka
kukujulisha kwamba kwa saa
kadhaa sasa nimekuwa na kikao
na wakuu wa vyombo vya usalama
na kufuatia lile tamko lako kuwa
Alshabaab ndio wanaohusika
katika mashambulio yale
mawili,kikao kimeamua kwamba
yafanyike mashambulio katika
kambi za Alshabaab .Nimeona
nikujulishe hilo ili uwataarifu watu
wako wote watoke katika kambi
hizo zitakazoshambuliwa”
akasema rais
“Mnataka kutushambulia?
Mnataka kuharibu kambi zetu na
kuua watu wetu? Akauliza Habib
kwa mshangao
“ Habib lengo la kufanya hivyo
ni kuzuia kutokufanyika kwa
uchunguzi wowote kuhusiana na
mashambulio yaliyotokea na ndiyo
maana nimeamua kukupigia ili
kushauriana nawe kuhusu jambo
hili.Nakuahidi kwamba
nitagharamia mimi mwenyewe
ujenzi wa kambi hizo baada ya
kuharibiwa.Nitatoa fedha nyingi
katika suala hili.Naomba
tukubaliane katika hilo Habib”
akasema rais na wakajadiliana na
Habib kwa muda wa zaidi ya
dakika kumi kisha wakaagana
kisha akampigia simu Jenerali
Lameck na kumtaka waonane.
“Nimezungumza na Habib
muda mfupi uliopita.Nimemtaarifu
kwamba tunataka kufanya
mashambulio mawili katika kambi
zake.Haikuwa rahisi lakini
tumekubaliana na amenipa namba
za simu za mmoja wa makamanda
wake ambaye mtawasiliana na
atakupa maelekezo yote.” Akasema
rais.Wakati akijadiliana na Lameck
simu yake ikaita,zilikuwa ni
namba ngeni katika simu
yake.Akasogea pembeni na
kuipokea
“Hallow”akasema
“Hallow Mr president”
ikasema sauti ya mwanamke
upande wa pili na Ernest akastuka
sana.Akatazama kama kuna mtu
yeyote pale karibu yake kisha
akauliza
“Nazungumza na nani?
Mwanamke Yule akatoa
kicheko kidogo kisha akasema
“Ni kweli umeisahau sauti hii
au umechanganyikiwa baada ya
kuisikia? Akauliza Yule
mwanamke
“ tell me who are you or I’ll
hang up !! akafoka rais
“ Fine .Yuu want to know who I
am? Its me Agatha your wife”
Ernest akashusha
pumzi.Alikosa neno la kuongea
akabaki ameishikilia simu sikioni
“ I’m not dead mr
President.I’m still alive.” Akasema
Agatha.Bado rais aliendelea kukaa
kimya.Hakuamini kile
alichokisikia.
“Mr president samahani kwa
kukusumbua usiku huu najua una
mambo mengi kuhusiana na
shambulio lililofanywa na
Alshabaab.Nitakupigia tena siku
nyingine kwa sasa nakuacha
umalize kwanza shughuli za msiba
huu mkubwa wa taifa.”
Rais akavuta pumzi ndefu na
kusema
“ Where are you?
“ Just wait for my call mr
president anytime soon” akasema
Agatha na kukata simu.Ernest
akachanganyikiwa.
ENDELEA……………………
 
SEASON 7: SEHEMU YA 1

Austin na wenzake wakawasili
katika makazi ya yao.Job akashuka
akafungua geti na mara katika
mlango wa kuingilia sebuleni
akatokea Marcelo akiwa
amesimama na bastora
mkononi.Alipowaona ni akina
Austin akashusha pumzi
akawafuata.Austin akatabasamu
baada ya kuuona uso wa Marcelo
umeloa jasho.
“Nitakufundisha namna ya
kutoka ndani kama unahisi kuna
hatari nje.Kwa namna ulivyotoka
sebuleni kama tungekuwa ni
maadui ilikuwa ni rahisi sana
kukumaliza.Vipi hali ya hapa?
Kuna tatizo lote? Akauliza Austin
“Hakuna tatizo lolote.Kila kitu
kiko shwari.Nashukuru mmerejea
salama.Hakuna yeyote aliyepata
tatizo? Akauliza Marcelo
“ Hapana .Sote tuko salama”
akajibu Job kisha wote wakaelekea
sebuleni.Yasmin akawatazama
akina Austin na kusema
“ Austin na wenzako
nawashukuru sana.Sikuwahi
kuhisi kama Tanzania kuna vijana
wenye uwezo mkubwa kama
ninyi.Nawashukuru kwa
kuniondoa salama Zanzibar kwani
nilikuwa katika hatari kubwa
kama mlivyoshuhudia.Hata hivyo
kabla ya mimi na ninyi kuongea
chochote nataka kwanza kumuona
Shamim.” Akasema Yasmin
“ Shamim yupo na utaonana
naye lakini si mapema namna hii.”
Akasema Austin
“ Hakuna chochote
kitakachoendelea kama
sintamuona Shamim.Nataka
nihakikishe kama kweli yuko hapa
.Miaka mingi nimempoteza
mwanangu na nina hamu sana ya
kumuona.Nipeni nafasi hiyo ya
kumuona walau
nimkumbatie.Dakika tano tu
ninaomba” akasema Yasmin.Austin
akamtazama halafu akasema
“ Sawa .Dakika tano ”
Wakapandisha ghorofani
katika chumba alimofungwa
Maria.Wakiwa nje ya chumba kile
Maria aliweza kuonekana kupitia
kioo kikubwa akiwa ndani
amefungwa kitini.Yasmin
akasisimka
“Shamim !! akasema kwa sauti
ndogo.Job akaufungua mlango wa
kile chumba na Austin akaingia
akiwa ameongozana na Yasmin.
“Nakupa dakika tano za
kusalimiana na mwanao” akasema
Austin na kutoka mle chumbani
akaenda kusimama nje ya chumba
na wote wakawatazama Maria na
mama yake waliobaki peke yao
mle chumbani.Yasmin na Maria
wakatazamana kwa muda kisha
Yasmin akamfuata Maria
akamkumbatia pale katika kiti
“ Shamim” akasema Yamsin na
macho yake yalijaa machozi
“ Mama !! akasema
Maria.Hakuamini kama
amefanikiwa kumuona tena mama
yake baada ya maka mingi kupita
“ Mama siamini kama
nimekuona tena.”
“Usijali Shamim.Nimetoka na
tutakuwa pamoja tena kwa maisha
yetu yote.Sintakuacha tena
Shamim.Nimeishi kwa taabu
gerezani lakini nilikuwa na
uhakika simu moja nitatoka na
tutaungana tena pamoja.” Akasema
Yasmin huku machozi yakimtoka.
“ Vipi maendeleo yako?
Akauliza Yasmin
“ Maendeleo yangu ni kama
hivi unavyoniona.Kwa siku kadhaa
sasa toka nimeshikwa na hawa
jamaa maisha yangu yamekuwa ni
hapa kwenye kiti hiki.Nashukuru
umekuja mama unikomboe
ninateseka mno.Hawa jama
wananitesa mno.Tafadhali mama
waombe wanifungue walau niwe
huru.” Akaomba Maria
“Usijali Shamim.Utakuwa huru
muda si mrefu.Nimekuja mama
yako na hautapata shida yoyote
tena.” Akasema Yasmin.
“Shamim hawa jamaa
wamenipa dakika tano tu za
kuonana nawe .Mimi na wao
tutakuwa na maongezi na endapo
watakubaliana na matakwa yangu
basi tutaachana na maisha haya ya
shida na tutaishi maisha mazuri”
“ Mama unawaamini hawa
jamaa? Nakuomba usiwaamini
tafadhali ni watu wabaya na
wakatili sana.” Akasema Maria na
Shamim akatabasamu
“ Usiogope Shamim .Hakuna
tatizo lolote litakalotokea.Naomba
uendelee kuvumilia kwa muda
mfupi nitarejea tena na utakuwa
huru” akasema Yasmin na
kumbusu Maria shavuni .Amarachi
akaufungua mlango akatoka mle
chumbani.Aliwatazama akina
Austin waliokuwa wamesimama
nje ya kile chumba halafu
akamtazama Maria kupitia kioo
kikubwa na kusema
“ Tafadhali naomba
mwanangu afunguliwe awe
huru.Sitaki kumuona mwanangu
akiwa katika hali ile.Sintakaa na
ninyi kuzungumza chochote
endapo mwanangu hatafunguliwa
.Kama ikiwezekana mtoeni katika
kile kiti na mnifunge mimi pale.”
Akasema Yasmin
“ Sikiliza Yasmin.Kwa sasa
wewe hauna uwezo wa kutoa amri
yoyote ndani ya hii
nyumba.Utafuata maelekezo yote
utakayopewa.Tumeweka maisha
yetu rehani kwa ajili yako kwa
hiyo endapo hautaheshimu
makubaliano yetu utatulazimisha
tutumie nguvu kitu ambacho
sikipendi.Maria ataendelea kukaa
hapa ndani hadi hapo sisi na wewe
tutakapokuwa tumekaa na
kuzungumza .” akasema
Austin.Yasmin akamtazama na bila
kusema kitu wakaondoka
kuelekea sebuleni.
“ Karibu sana Yasmin.Kabla
hatujaendelea na chochote
naomba nikutambulishe washirika
wangu.Huyu anaitwa Job na yule
pale anaitwa Amarachi.Tunafanya
kazi kwa pamoja.Mimi tayari
unanifahamu naitwa Austin”
Akasema Austin
“ Baada ya utambulisho huo
nataka nikufahamishe kitu kingine
kwamba mwanaume uliyekuwa
naye katika mahusiano kabla
haujakamatwa na ukazaa naye
mtoto ambaye ni Maria ,tunaye pia
hapa” akasema Austin na sura ya
Yasmin ikabadilika
“ Boaz?!! Akauliza
“ Ndiyo Boaz.”akajibu
Austin.Yasmin akashusha pumzi
“Naye amefanya nini?
Ninaweza kuonana naye?
“ Utaonana naye lakini ni hadi
hapo tutakapokuwa tumemaliza
mazungumzo yetu” akasema
Austin
“ Tayari ni usiku mkubwa na
hatuna muda wa kuendelea
kupoteza.Tuelekee moja kwa moja
katika maongezi yetu” akasema
Austin.
“Samahani Austin lakini kabla
hatujaendela naomba niweke wazi
jambo ninalotaka.Ninataka
kuzungumza na wewe peke
yako.Sitaki awepo mtu mwingine
yeyote .Najua hawa ni wenzako
uko nao pamoja na unawaamini
lakini nahitaji kuzungumza nawe
pekee kwani nakuamini wewe
peke yako.” Akasema Yasmin
“ Hilo haliwezekani.Hawa ni
wenzangu na wanafahamu kila
kitu kuhusiana na wewe kwa hiyo
tutazungumza na wao wakiwepo”
akasema Austin
“ Hapana nataka watoke”
akasema Yasmin
“ Austin ngoja tutoke kama
anavyotaka” akasema
Amarachi.Yeye na Job wakainuka
na kutoka.Austin akamtazama
Yasmin kwa macho makali
“ Usikasirike Austin.Ni
kawaida yangu mimi huwa siamini
sana watu.Sasa tunaweza
kuendelea” akasema Yasmin.
“ Yasmin naona bado
hujanifahamu vyema mimi ni nani
kwa hiyo naomba nikueleze kwa
ufupi upate japo picha ya mtu
unayezungumza naye” akasema
Austin
“ Naitwa Austin January kama
nilivyokufahamisha awali.Niliwahi
kufanya kazi katika idara ya
ujasusi Tanzania hadi pale
nilipotakiwa kuuawa na watu
ndani ya serikali baada ya
kuugundua mpango wao muovu
dhidi ya rais na tukiwa katika
mapambano na wanamgambo wa
Alshabaab waliowateka
watanzania nilipigwa risasi
nikadhaniwa nimekufa nikaachwa
hapo.Niliingia katika mikono ya
Alshabaab ambao walihitaji kiasi
kikubwa sana cha fedha ili
waniachie huru.Boaz baba yake
Maria ndiye aliyelipa kiasi hicho
kikubwa cha fedha na kunikomboa
toka mikononi mwa Alshabab.Kwa
wakati huo mimi na Maria
tulikuwa katika mahusiano ya
kimapenzi .”
“ Ulikuwa na mahusino na
Shamim?!! Akauliza Yasmin kwa
mshangao
“ Ndiyo nilikuwa katika
mapenzi mazito na mwanao hadi
hivi juzi mapenzi yetu yalipofika
ukomo” akasema Austin.Ukapita
ukimya mfupi akaendelea
“ Baada ya kukombolewa
kutoka kwa Alshabaab nikaenda
kuanza maisha mapya nchini
Afrika ya kusini .Nimeishi na
familia ya Boaz toka wakati huo
hadi sasa. Tumeshi kwa mapenzi
makubwa na walinichukulia kama
sehemu ya familia yao” akasema
Austin na kunyamaza kwa muda
akamtazama Yasmin
“ Kama wao ndio
waliokukomboa kutoka kwa
Alshabaab wakakupa hifadhi
,wakayabadili maisha yako,kama
haitoshi umekuwa na mahusiano
na mwanangu na wamekuchukulia
kama familia kwa nini unawatenda
hivi? Kwa nini Maria umemfunga
namna ile?akauliza Yasmin.Austin
akaendelea
“ Niliitwa na rais kuja
Tanzania kufanya kazi fulani
muhimu.Wakati nikija Tanzania
Maria alikuwa Dubai.Nilimtaarifu
kwamba ninakuja Tanzania na
nilimkataza asije huku kwa
kuhofia usalama wake lakini
alinipuuza na akaja.Mmambo
yalibadilika nilipoonana naye
baada ya kufahamu kwamba Maria
amekuwa na majina matatu tofauti
na hakuwahi kunieleza kitu kama
hicho.Niliingiwa na wasiwasi sana
na kumtaka anipe maelezo
kuhusiana na suala
hilo.Kilichotokea ni kwamba
alijaribu kuniua.Alinipiga risasi
nne na hata hivi tuongeavyo bado
niko katika maumivu makali lakini
kutokana na uzito wa jambo
lililoko mbele yetu imenilazimu
kuingia kazini.Nilipaswa kuwa
hospitali muda huu.Kwa kitendo
kile ilitulazimu kumshikilia Maria
ili kumfahamu ni nani na imekuaje
akawa na uwezo mkubwa namna
ile wa kutumia silaha.Toka hapo
hatujathubutu kumuachia huru
baada ya kufahamu ni mtu hatari
na anayeweza kusababisha
madhara makubwa.Kwa maelezo
hayo mafupi niliyokupa nadhani
tayari umepata picha Fulani
kwamba mimi ni mtu wa karibu na
Maria lakini kwa kitendo chake
cha kutaka kuniua imenilazimu
niwe mkatili kwake na ataendelea
kuteseka hadi pale utakapoamua
kumtoa katika mateso .Niwewe
utakayeamua hatima ya mwanao
kwa kunieleza kile ninachohitaji
kukifahamu toka
kwako.Nikiridhika na maelezo yao
basi tunaweza kufanya
makubalinao lakini endapo
sintaridhika na maelezo yako
Maria ataendelea kupata mateso
makali sana na mwisho wake
atapotea na hautamuona tena”
akasema Austin
“ Austin maelezo yako
yamenipa picha kwamba japokuwa
Shamim amekufanyia kitendo
kibaya cha kutaka kukuua lakini
ndani ya moyo wako bado una kitu
kuhusu yeye.Naamini pamoja na
yote aliyoyafanya bado nafsi yako
inakuuma kwa hivi unavyomfanyia
Shamim.Naamini kwamba tutafikia
makubaliano na tutaweka sawa
mambo haya na Shamim atakuwa
huru.Si yeye peke yake hata baba
yake pia.Mimi na yeye tuliwahi
kuwa na maisha mazuri kabla
hatujaachana .Tuachane a hayo
mimi niko tayari kama
nilivyokueleza kufanya chochote
kile kwa ajili ya kumpata Shamim
pamoja na baba yake.Nitakupatia
kile nilichokuahidi endapo nawe
utakuwa tayari kunipatia kile
ninachokihitaji.” Akasema Yasmin
“ Kama utakachonieleza
kitakuwa na msaada mkubwa
kwangu nakuahid nitahakikisha
ninakusaidia na kukupatia yale
yote utakayohitaji” akasema
Austin
“ Nini hasa unahitaji
kufahamu? Akauliza Yasmin
“ Kitu cha kwanza nahitaji
kufahamu mahusiano yako na rais
na namna alivyoweza kukutoka
mahala ulikokuwa umefungwa ”
akasema Austin.
“ Austin una kinywaji
chochote humu kikali? Akauliza
Yasmin
“ Hapana.Hatutumii kileo
chochote tukiwa kazini” akajibu
Austin.Yasmin akainamiasha
kichwa akavuta kumbukumbu kwa
muda halafu akamtazama Austin
na kusema.
“ Mvua kubwa ilikuwa
inanyesha jijini Dar es salaam siku
niliyokamatwa.Nilikuwa najiandaa
kwenda uwanja wa ndege ili
kuondoka Tanzania baada ya
kugundua kwamba kulikuwa na
mpango wa
kunikamata.Nilifungwa kitambaa
usoni na sikujua nimepelekwa
wapi.Na siku hiyo ulikuwa mwisho
wangu wa kuliona jua.Niliwekwa
katika chumba ambacho nilielezwa
baadae kwamba kiko chini ya
bahari. Nimeishi humo kwa miaka
zaidi ya kumi hadi juzi usiku
alipokuja rais akajitambulisha
kwangu kwamba amekuja
kuniachia huru.Nilishangaa sana
kwani nilitegemea maisha yangu
yote yangeishia mle katika kile
chumba.Nilimuuliza rais sababu za
kutaka kuniachia huru akanieleza
kwamba amefanya makubaliano
na mtu mmoja anaitwa Habib
Alzaraq.Sikuwa nikimfahamu
Habib nikamtaka anieleze huyo
Habib ni nani ama sivyo
nisingetoka mle gerezani ndipo
aliponieleza kwamba Habib ni
kiongozi mkuu wa Alshabaab.”
Akanyamza akameza mate na
kuendelea
“ Rais alinitoa katika lile
gereza usiku ule akanipeleka
katika nyumba fulani aliyoiandaa
kwa ajili yetu usiku ule.Tukiwa
katika ile nyumba nilizungumza na
Habib halafu akaniunganisha na
viongozi wangu wa IS
nikazungumza nao wakanipa
maelekezo.”
“ Subiri kidogo.Rais ndiye
aliyewasiliana na watu wa IS?
Akauliza Austin
“ Rais alimpigia simu Habib na
huyo ndiye aliyeniunganisha na
viongozi wangu wa IS ambao
walinieleza kwamba kuna mambo
wameongea na Habib na moja kati
ya mambo waliyoongea ni mimi
kuachiwa huru.Baadae usiku huo
akaja mtu mwingine ambaye naye
alikuwa amefungwa gerezani
anaitwa Tariq.Huyu alikuwa
mratibu mkuu wa mashambulio
mengi ya Alshabaab.Huyu naye
aliachiwa kufuatia makubaliano
kati ya rais na
Alshabaab.Nilipowasiliana na
viongozi wangu wa IS walinieleza
kwamba mwanangu Shamim
amekuja Dar es salaam kwa ajili ya
kunitafuta.Nilimweleza rais
kwamba nahitaji kumpata
mwanangu na tukakubaliana
jambo fulani endapo angefanikiwa
kunisadia kumpata
mwanangu.Rais alikuwa
anafahamu mahala alipo Shamim
akachukua simu akapiga na
ninadhani alikupigia wewe na
nikafanikiwa kuzungumza kwa
mara ya kwanza baada ya miaka
mingi na mwanagu Shamim.Leo
tuliandaliwa ndege tukaondoka
kuelekea Mogadishu .Kabla
hatujaondoka niimuomba rais
anipatie bastora mbili na kiasi
fulani cha pesa na tukiwa ndani ya
ndege nilifanikiwa kuwatisha
marubani wakabadili uelekeo wa
ndege tukaenda kutua
Zanzibar.Tulifanikiwa kuvuka
salama pale uwanja wa ndege na
tukaenda Lepatido hotel.” Yasmin
akanyamaza kwa muda
akamtazama Austin kwa makini
halafu akaendelea
“ Nikiwa gerezani nilitafakari
mno kuhusiana na maisha yangu
na niliweka nadhiri kwamba
ikitokea siku moja nikatoka
gerezani sitaki tena kuendelea
kujihusisha na kundi hili la
IS.Nimekuwa mfuasi wa kundi hili
kwa muda mrefu na hakuna
chochote nilichokipata mpaka
sasa.Fursa hii niliyoipata
nimeamua kuitumia vyema kwa
kuachana na IS na kwenda
kuyaanza maisha yangu mapya na
mwanangu Shamim.Nilimueleza
Tariq nia yangu ya kutorejea tena
IS na nilimtaka naye pia afikirie
kuhusu kurejea tena
Alshabaab.tariq hakuwa tayari
kuachana na Alshabaab na
nilipokwenda kuoga akachukua
simu yangu na kuwapigia watu
wake wa Alshabaab.Nilikasirika
sana nikamuua.” Akanyamaza tena
kwa muda ,akaendelea
“ Austin nimefanya haya yote
ili niweze kuitimiza ndoto yangu
ya kuachana na IS na kuanza
maisha yangu mapya mahala
ambako hawataweza
kunipata.Narudia tena niko tayari
kufanya jambo lolote kwa ajili ya
kumpata mwanangu na kwenda
naye kuanza maisha mapya na
ndiyo maana nimerudi hapa Dar es
salaam bila kujali hatari
iliyopo.Shamim ni muhimu sana
kwangu kuliko kitu chochote”
akasema Yasmin
“ Nataka kufahamu
makubaliano kati ya rais na
Alshabaab hadi akaamua
kukuachiahuru.Wamempa kitu
gani hawa jamaa hadi akaamua
kukuachia wewe na Tariq?
Akauliza Austin
“ Sifahamu wamekubaliana
nini ila ninachoamini kuna jambo
kubwa walikubaliana hadi
nikaachiwa huru”akajibu Yasmin
“ Nataka kufahamu pia IS
wameingiaje katika makubaliano
ya rais na Alshabaab na kumuagiza
Habib uachiwe huru? Austin
akauliza
“Alshabaab lengo lao kubwa ni
kuiangusha serikali ya Somalia na
kushika uongozi wa taifa
hilo.Jambo hilo linawawia ugumu
kwa sasa kutokana na serikali
iliyoko madarakani kujizatiti kwa
kuunda jeshi imara kwa hiyo
Alshabaab wanalazimika kutafuta
msaada toka makundi mengine ya
kigaidi ili kuweza kuiangusha
serikali ya Somalia.IS
wamewaahidi kuwasaidia
kupambana ili kuhakikisha
wanaiongoza Somalia kwa hiyo
nao inawalazimu kufanya yale
ambayo IS wanayataka kwa mfano
mimi kuachiwa huru na mambo
mengine” akasema Yasmin
“ Yametokea mashambulio
makubwa mawili hapa nchini leo
ambayo yameua watu
wengi.Alshabaab wamejitokeza na
kukiri kufanya mashambulio yale
mawili kwa kisingizio cha
kuishinikiza Tanzania itoe
wanajeshi wake wanaolifundisha
jeshi la Somalia.Kama Alshabaab
wana mawasiliano ya moja kwa
moja na rais na wanaweza hadi
kufanya makubaliano kama
yaliyofanyika na mkaachiwa huru
kwa nini wasingemweleza rais
moja kowa moja kwamba hawataki
kuyaona majeshi ya Tanzania
nchini Somalia hadi wamwage
damu? Kwa nini wasingefanya
makubaliano pia katika suala hili
kama walivyokubaliana hadi ninyi
mkaachiwa huru ?.Umekuwa
katika kikundi cha IS kwa muda
mrefu unaliongeleaje shambulio
hili la leo? Akauliza Austin
“ Binafsi nimeumia sana kwa
hiki kilichotokea leo na mambo
kama haya ndiyo yaliyonipelekea
kuamua kubadilika na kuachana
na maisha haya ya kutoa roho za
watu wasio na hatia. Kwa mtazamo
wangu shambulio la leo linanipa
mashaka sana kuamini kama kweli
Alshabaab wanahusika kwani
hakuna sababu ya msingi ya
kufanya mauaji haya
makubwa.Kama tatizo lilikuwa ni
wanajeshi wa Tanzania nchini
Somalia naamini wangeweza
kuzungumza na rais na
wakalimaliza suala hilo..” Akasema
Yasmin
“ Kama si Alshabaab nani basi
aliyetekeleza shambulio hilo?
Akauliza Austin
“ Sikiliza Austin.Kwa
kukusaidia tu ni kwamba
shambulio hilo la leo litakuwa
limetekelezwa na watu wa kutoka
ndani.”
“ Kutoka ndani? Una maanisha
nini unaposema kwamba linaweza
kuwa limetekelezwa na watu wa
ndani?
“ Austin umekuwa katika kazi
hii kwa muda mrefu na nina imani
tayari unafahamu namna mambo
yanavyoendeshwa.Kuna
mashambulio mengine hutokea na
mitandao ya kigaidi kuhusishwa
au kujitangaza kuhusika na
shambulio hilo lakini ukweli
unabaki kuwa washambuliaji
wanakuwa wengine na wale
magaidi wanatumika kujitangaza
kuwa wamehusika kwa kulipwa
pesa nyingi.Usishangae hata haya
mashambulio ya Dar es salaam na
Dodoma yakawa yametekelezwana
watu wa ndani na Alshabaab
wakaubebaba mzigo wote.”
Akasema Yasmin
“ Yasmin maneno yameanza
kunipa mwanga fulani.Kuna kitu
ninakiona hapa.Ninaweza
kukubaliana nawe kwamba kuna
uwezekano mkubwa shambulio
hili limefanywa na watu wa ndani
na si Alshabaab.Swali ninalojiuliza
ni kwamba ni nani ambao
wamefanya mashambulio haya na
kwa nini? Akauliza Austin
“Austin” akaita Yasmin
“ Nadhani tayari nimekupa
mwanga wa kutosha kuhusiana na
yale mambo yaliyokuwa
yanakuumiza kichwa.Kuna lingine
unalotaka kulifahamu kutoka
kwangu?
“ Hicho ndicho kikubwa
nilichokuwa nakihitaji
kukifahamu.lakini kuna kitu
kingine” Akasema Austin na
kunyamaza kidogo halafu
akamtazama Yasmin.
“ Ulisema kwamba una kitu
cha thamani kubwa ambacho
utanipa ili kumuachia huru
mwanao Shamim.Ni kitu gani
hicho? Akauliza Austin
“ Ndiyo ninacho kitu kikubwa
kingine ambacho ni cha muhimu
zaidi kuliko hata haya
mashambulio yaliyotokea
leo.Lakini ili ukipate lazima
tufanye makubaliano maalum
kwanza ”
“ Nini unahitaji? Austin
akauliza
“ Nimeamua kuanza maisha
mapya kama
nilivyokueleza.Maamuzi haya ni
usaliti kwa IS ambao naamini
watanisaka hadi wahakikishe
wananipata na wakifanikiwa
kunipata adhabu yake ni kifo.
Nataka kwenda kuishi mbali
kabisa mahala ambako
hawataweza kunipata.Nataka
nihakikishe unatuwezesha mimi
na mwanangu Shamim na
ikiwezekana na baba yake tuende
mahala salama.Nataka tupate hati
mpya za kusafiria zenye majina
mapya.Nataka tuwe watu wapya na
tuachane na kila kitu cha
zamani.Huko tuendako nataka
tupate nyumba nzuri ya
kuishi,magari kwa ujumla tuwe na
kitu cha kutuwezesha kuendesha
maisha yetu kama vile biashara ”
Akasema Yasmin .
“ Yasmin hilo jambo
unalolitaka ni kubwa na gumu mno
kufanyika.Wewe ni mtu
unayefahamika kama mfuasi wa IS
na taarifa zako ziko katika mataifa
mengi kwa hiyo itakuwa vigumu
sana kukuwezesha kwenda kuanza
masha mapya mbali ambako IS
hawataweza kukupata” Akasema
Austin
“ Austin ninafahamu kwamba
unao uwezo wa kufanya hicho
ninachokitaka.Kama wewe hauna
uwezo huo tafuta namna yoyote ya
kufanya hilo
liwezekane.Nimekuachia suala hilo
utajua namna
utakavyofanya.Ukishindwa
kulitekeleza hilo na ukaacha
nikamatwe na IS au nikamatwe
tena na serikali ya Tanzania basi
utakosa kitu kimoja kikubwa sana
na cha muhimu mno” akasema
Yasmin
“ Yasmin ni kitu gani hicho
ulicho nacho unachodhani kina
thamani kubwa ya kunishawishi
nikubali kukusaidia ? akauliza
Austin
“ Austin ninacho kitu kikubwa
“ akajibu Yasmin
“ Ni kitu gani? Niambie
tafadhali ili nipime uzito wake
kama ninaweza kukusaidia”
“Austin kuna mambo
makubwa yanayoendelea hapa
nchini kwenu ambayo bado
huyafahamu.Nitakukupa kitu
ambacho hutaamini macho yako”
akasema Yasmin
“Yasmin naomba nikuweke
wazi kwamba pamoja na yote
aliyoyafanya mwanao Shamim kwa
kutaka kuniua lakini bado historia
ya maisha yangu itaendelea
kumkumbuka kwani kwa kupitia
yeye niliweza kutoka katika
mikono ya
Alshabaab.Alimshawishi baba yake
akakubali kulipa kiasi kikubwa
cha fedha kunikomboa.Katika siku
zote za maisha yangu
nitaliheshimu hilo jambo na kwa
sababu hiyo sina haja ya
kumuharibia maisha yake bali
nitafanya kila lililo ndani ya uwezo
wangu kuhakikisha kwamba
mnaanza maisha yenu mapya
kama unavyodai.Kwa hiyo Yasmin
naomba usijaribu kunifanya
nikabadili mawazo yangu ya
kuwasidia wewe na mwanao
kuyaanza maisha mapya.Nieleze
hicho kitu cha thamani unachodai
unacho.” Akasema Austin
Ilimchukua Yasmin zaidi ya
dakika mbili akifikiri kisha
akasema
“ Ninayo hati ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar.”
Austin akamtazama na
kuangua kicheko
“ Mbona unacheka Austin”
Yasmin akauliza
“ Imenilazimu kucheka kwa
hiki ulichokitamka” akasema
Austin
“ Austin hiki si kichekesho.Ni
kitu cha kweli kabisa.Ninayo hati
ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.Tena si nakala bali ni hati
halisi iliyosainiwa na viongozi
waasisi walioziunganisha nchi
mbili hizi” akasema Yasmin
“Yasmin narudia
tena,unachokiongea ni kitu
ambacho hakiwezi kutokea.Hati ya
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ni nyaraka kubwa na ya
juu mno ya serikali ambayo
ilizalisha nchi inaitwa
Tanzania.Hiki si kitu ambacho
unaweza ukaingia na kukichukua
kama tunavyofanya kwa nyaraka
nyingine.Kutamka kwamba unayo
hati ya muungano ni kituko cha
karne kwani nyaraka hii
huhifadhiwa sehemu ya siri sana
na hakuna anayeweza kuifikia
akaichukua.Hati hii imewahi
kuonyeshwa hadharani mara moja
lilipotokea kundi la watu ambao
walianza kuwahadaisha wananchi
kwamba muungano huu si halali
kwa kuwa hakuna nyaraka
inayothibitisha kwamba nchi mbili
za Tanganyika na Zanzibar
ziliungana.Watu walianza kuamini
kauli hizi ndipo ilipomlazimu rais
aliyekuwapo madarakani wakati
huo aitoe hati hiyo hadharani
akawaonyesha wananchi kwamba
muungano huu ni halali na hati
iliyosainiwa na wakuu wa nchi
mbili wakati huo ipo na hapo
vuguvugu hilo likakosa
nguvu.Nimekueleza haya ili
kukupa picha ya ukubwa wa hiyo
nyaraka unayosema unayo.Hii si
nyaraka ya mchezo mchezo.Tafuta
namna nyingine ya kunishawishi
nikubali kukusaidia lakini si kwa
kunidanganya eti unayo hati ya
muungano” akasema Austin
“Austin nafahamu ni vigumu
kuamini kuhusu jambo hili lakini
nakuhakikishia kwamba ninayo
hiyo hati na nitakupatia wewe
iwapo utakuwa tayari kunisaidia
mambo niliyokueleza.”akasema
Yasmin
Aistin akafikiri kidogo na
kuuliza
“ Iko wapi hiyo karatasi
unayodai ni hati ya muungano?
Swali lile la Austin
likaonekana kumkasirisha Yasmin
sura yake ikabadilika
“ Austin naomba tuweke
mzaha pembeni.Tuko katika
kipindi kigumu hivi sasa na
sipendi tuwe na mzaha katika
mambo makubwa.Mimi ni mtu
mzima na ninayefahamu nini
ninaongea.Jiulize kwa nini
nisingeweza kutaja kwamba nina
nyaraka nyingine yoyote hadi
nikasema ninayo hati ya
muungano? Nimekwambia hivyo
kwa sababu ninayo kweli na wala
si utani kama unavyodhani”
akasema Yasmin
“ Iko wapi hiyo hati niione
kama kweli ni yenyewe? Akauliza
Austin
“ najua hauniamini labda hadi
nikueleze ukweli wote.Alshabaab
kabla ya kukubaliana na rais wenu
walishauriana kwanza na IS na
wakaelekzwa watake vitu viwili
toka kwa rais wa Tanzania.Moja ni
mimi kuachiwa huru na pili ni hati
ya muungano wa Tanganyika na
Zanzibar ambayo walielekeza
nikabidhiwe mimi .Rais
alikubaliana na masharti hayo na
akayatekeleza.Alinikabidhi hati
halisi ya muungano ili niondoke
nayo.Kwa hiyo niamini
ninapokwambia kwamba ninayo
hati ya muungano .Ni kweli ni
nyaraka kubwa kama ulivyosema
lakini iko chini ya mikono ya mkuu
wa nchi na yeye anaweza akafanya
chochote akitakacho “ akasema
Yasmin na ukimya ukatanda hapo
sebuleni
“ Austin muda
unakwenda.Fanya maamuzi
unakubaliana na ombi langu ili
nikupatie hiyo hati au bado
huamini ?
“ Yasmin unanipa wakati
mgumu wa kukuamini.Hiki si kitu
kidogo kama unavyodhani na rais
wa nchi hawezi kuitoa hati hii
kirahisi rahisi tena kwa mtandao
wa magaidi !! Hiki kitu ambacho
hakiingii akilini na hakiwezekani”
akasema Austin
“ Uwepo wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania ni kwa
sababu ya hati hiyo .Hawezi raisi
aliyeapa kuulinda muungano kwa
gharama zozote akacheza na
nyaraka kubwa kama hii ya
muungano wetu.Haiwezekani !!
akasema Austin kwa ukali
“Austin sipati maneno mazuri
ya kukueleza ili unielewe kuhusu
jambo hili.Ngoja nikueleze kitu
kingine labda kinaweza kukufanya
ukaniamini kile ninachokwambia.”
Akasema Yasmin akanyamaza
kidogo akamtazama Austin halafu
akaendelea.
“ Rais alitaka nifanye kila
niwezalo nimrejeshee hati hiyo na
anipe mwanangu Shamim .Hakuna
jambo lolote uliloambiwa na rais
kuhusu Shamim? Akauliza Yasmin
“ Nilielekezwa na rais kwamba
nimpeleke Maria ikulu
anamuhitaji” akajibu Austin
“ Umeona namna mambo
yanavyokwenda Austin? Rais
lengo lake lilikuwa ni mimi
kumrejeshea hati aliyonipa na
yeye anipe mwanangu.Simuamini
sana rais na ndiyo maana sikutaka
kufanya kama alivyoniagiza bali
nikaamua kufanya makubaliano
moja kwa moja na wewe.”akasema
Yasmin akanyamaza na
kumtazama Austin
“ Umeanza kupata picha
Fulani ya kile ninachokwambia?
Akauliza
“ Kwa mbali kuna kitu picha
ndogo ninaipata kwa hicho
unachokisema.Kuna mambo Fulani
Fulani ambayo hata mimi
yalinishangaza kidogo kuhusu
rais.” Akasema Austin
“ Baada ya kunusurika
kuuawa na Maria,tuliikagua
kompyuta yake tukagundua
alikuwa anawasiliana na mtu
mmoja anaitwa Bin Omar na katika
mawasiliano yao Maria alimtaarifu
Omar kwamba anakuja Tanzania
kwa lengo la kumtafuta mama
yake.Omar alimuonya kwamba
asifanye hivyo kwani kuna watu
wataalamu wanaoifanya hiyo kazi
lakini Maria akamuhakikishi Omar
kwamba asiwe na shaka hata yeye
ana mtu wake ambaye ana uhakika
atamsaidia sana kumpata mama
yake.Mtu huyo ni mimi.Nilimuhoji
Maria kuhusiana na mama yake na
nilitaka pia kufahamu mtu yule bin
Omar ni nani?Maria alikataa
kunieleza chochote hadi pale
nitakapomsaidia kumpata mama
yake anaitwa Yasmin Esfahani
ambaye amefungwa mahala pa siri
hapa Tanzania.Aliniambia kwamba
kuna jambo kubwa atanieleza
endapo nitafanikisha kumpata
mama yake.Ilinilazimu
kukubaliana naye na nikamuuliza
rais kuhusiana na Yasmin Esfahani
akakana kumfahamu.Baadae usiku
alinipigia simu akataka kuongea
na Maria akiwa peke yake.Maria
alianza kuzungumza nawe kwa
lugha ya kiarabu ambacho
ninakifahamu vyema na nilisikia
maongezi yenu yote.Nilishangaa
sana kwa nini rais akanificha kama
anakufahamu.? Kama hiyo haitoshi
bado akataka kumchukua na Maria
ili amkabidhi kwako” akasema
Austin halafu akanyamaza kimya
kwa muda
“ Yasmin ninataka
kukubaliana nawe lakini kuna
swali ambalo nahitaji unijibu.Kwa
nini IS wakaitaka hati ya
muungano?
“IS wana mpango wa
kujitanua zaidi na sasa
wanaelekeza nguvu zao barani
Afrika na mimi walinituma kuja
afrika mashariki kupeleleza
namna tutakavyoweza kuanzisha
kundi letu huku.Nimeishi Tanzania
kwa miaka kadhaa nikifanya
uchunguzi na katika uchunguzi
wangu niligundua kwamba IS
itafanyakazi zake kwa ufanisi zaidi
katika ukanda huu wa Afrika
mashariki endapo tutakitwaa
kisiwa cha pemba.Jambo hili
lilionekana kuwa gumu kwa
sababu kisiwa kile kiko ndani ya
jamhuri ya muungano wa Tanzania
na ili kukipata lazima kwanza
muungano kati ya Tanganyika na
Zanzibar uvunjike na kisha Pemba
ijitenge kutoka Zanzibar na kuwa
kisiwa huru.Kujibu swali lako ni
kwamba IS wanaitaka hati ya
muungano ili kuuvunja muungano
na kukitwaa kisiwa cha Pemba.”
Akasema Yasmin.Austin
akatafakari na kusema
“ Sasa ninaanza kukuamini
kile unachokisema.Kama rais
alikubali kutoa hati ya muungano
ni wazi yuko radhi muungano huu
kuvunjika.Kuivunja nchi ni jambo
kubwa mno.Kwa nini akafanya
hivi? Alshabaab wamempa nini
hadi akaitoa hati ya muungano?
Akauliza Austin
“ Sifahamu wamempa nini
lakini ni wazi kitu walichompa ni
kikubwa na chenye thamani
kushinda hata muungano
wenyewe” akasema Yasmin
“ Kuna jambo lingine ambalo
mimi na wenzangu tumekuwa
tunajiuliza.Rais amefanya
makubaliano na Alshabaab lakini
shambulio la pale hotelini Dar
lilitokea wakati rais akiwa mita
chache sana kufika hotelini hapo.Je
shambulio hilo lililenga kumuua
rais ? Iweje watake kumuua
mshirika wao? Akauliza Austin
“ Austin kama nilivyokueleza
awali kwamba shambulio hili
halijafanywa na Alshabaab au
kikundi kingine cha magaidi.Mimi
nimekuwa na IS muda mrefu
ninafahamu namna magaidi
wanavyopanga mashambulio
yao.Kwa namna mashambulio haya
mawili yalivyotokea inaniwia
ugumu kukubali kwamba
yamefanywa na Alshabaab ingawa
wenyewe Alshaabab wamejitokeza
na kukiri kuhusika.Kwa mtazamo
wangu inawezekana kabisa
kwamba shambulio lile lilitokea
wakati rais akiwa karibu na hoteli
ili kuwahadaa watu kwamba
mlengwa katika shambulio lile
alikuwa ni rais.” Akasema Yasmin
“ Kauli yako inaashiria
kwamba rais anaweza kuwa
anahusika katika jambo hili?
Akauliza Austin
“ Hakuna ushahidi wa moja
kwa moja wa kumuhusisha rais na
suala hili lakini kwa namna
mtiririko wa matukio ulivyo kuna
chembe chembe ndogo za
kushawishi kwamba rais kuna kitu
anakifahamu kuhusiana na
shambulio hili.Hizo ni hisia zangu ”
akasema Yasmin.
“ kwa maelezo uliyonipa hata
mimi ninahisi hivyo kwamba rais
kuna kitu anakifahamu kuhusiana
na matukio haya mawili.Mimi na
wenzagu hatutalala usingizi hadi
tuhakikishe kwamba kama rais
amehusika katika mashambulio
haya mawili lazima afikishwe
katika sheria.Haya ni mauaji
makubwa sana kuwahi kutokea
nchini kwetu.” Akasema Austin na
kunyamza kidogo kisha akauliza
“ Hati hiyo iko wapi?
Yasmin akatabasamu na
kusema
“ Iko mahala salama
nimeificha.Endapo utanisaidia
hayo niliyokuomba nitakuonyesha
mahala ilipo.Ni sehemu salama.”
akasema yasmin
“Yasmin unanipa wakati
mgumu kukuamini na
kukusaidia.Kazi hii uliyonipa ni
ngumu na siwezi kuifanya peke
yangu.Kukutoa hapa nchini kwa
wakati huu ambao unatafutwa
sana si jambo rahisi hata
kidogo.Mimi ninaweza kukuamini
lakini wenzangu ninaoshirikiana
nao haitakuwa rahisi kwao na
watakuwa tayari kuifanya kazi hii
endapo tu watakuwa na
uthibitisho wa hicho
unachokisema kama kweli
kipo.Nionyeshe au nipeleke
mahala ulipoiweka hati hiyo na
tuichukue tuihakiki kama kweli ni
yenyewe na tukiridhika kama ni
yenyewe nakuahidi nitakuondoa
hapa nchini na utaenda kuyaanza
maisha mapya mahala
unakotaka.”akasema Austin
“ Austin wewe ni kiongozi wa
hawa wenzako kwa hiyo
ukiniamini wewe lazima na hawa
wenzako pia waniamini.Hiki si kitu
cha kutunga.Naomba uniamini
tafadhali.Ile ni nyaraka kubwa
kama ulivyosema na siwezi
kutembea nayo kama chapati
isitioshe ndicho kitu pekee
kikubwa kitakachonifanya nifikie
malengo yangu ya kuishi maisha
ninayoyataka.Tekelezeni hayo
mambo niliyokueleza na mtaipata
hiyo hati.” Akasema Yasmin
Austin akazama mawazoni
kwa dakika mbili halafu akasema
“ Nahitaji kwanza
kuzungumza na wenzangu kuhusu
jambo hili .Kwa sasa tutakuweka
katika chumba kimojawapo humu
ndani.” Akasema Austin
“Austin nakuomba tafadhali
nikae na mwanangu na
ninakuomba usiendelee kumfunga
Shamin namna ile.Ameteseka vya
kutosha .Mmemuumiza mno.Kwa
kuwa niko hapa nawaomba
mumfungue awe huru.Moyo wangu
unaniuma sana kama mama
kumuona mwanangu akiwa katika
hali ile” akasema Yasmin.Austin
akamtazama na kuuliza
“ Unadhani ni machozi gani
angelia mama yangu angelikuwa
hai endapo ningeuawa na mwanao
Shamim? Akauliza Austin huku
akiinuka.
“ Mwanao ataendelea kukaa
vile vile .Wewe una nyaraka na
mimi nina mwanao.” Akasema
Austin na kumtaka Yasmin
asimame wakaongozana kuelekea
ghorofani akamtaka Job
akamfungie Yasmin katika
mojawapo ya vyumba
“ Austin naomba tafadhali
nionane walau na Boaz
nimsalimie”akaomba Yasmin
“ Utaonana naye wakati
mwingine kwa sasa nenda
kapumzike siku imekuwa ndefu
sana” akasema Austin .Job
akamchukua Yasmin na
kumpeleka katika chumba
kimojawapo chenye kujitosheleza
kila kitu ndani halafu wakaelekea
sebuleni.
“ Ndugu zangu nimezungumza
na Yasmin na kutokana na maelezo
yake tuna mlima mrefu wa
kupanda.Kwanza kabla sijasema
chochote nataka niwakumbushe
kwamba tuna mtu hatari humu
ndani ya nyumba.Yasmin ni gaidi
na hashindwi kufanya chochote
muda wowote anaotaka kwa hiyo
umakini mkubwa unatakiwa .Kwa
muda atakaokuwa hapa lazima
tuwe macho saa ishirini na nne
kumchunga.”
“ Usihofu kuhusuh ilo
Austin.Nyumba hii ilitengenezwa
kwa namna ya kipekee
kabisa.Kuna kamera za siri katika
kila chumba kwa hiyo tutaweza
kumfuatilia Yasmin kirahisi kiola
anachokifanya.”
“ Good” akasema Austin
“ Nimezungumza na Yasmin na
kuna mambo
Kwanza nilitaka
kufahamu mahusiano yakena rais
na namna alivyotoka gerezani pia
kuhusu makubaliano aliyoyasema
kati ya rais na
Alshabaab.Amenieleza kwamba
rais ndiye aliyemfuata mahala
alikokuwa amefungwa
akamwambia kwamba
amelekezwa na Habib kiongozi wa
Alshabaab amuachie huru.Rais
alikuwa na makubaliano maalum
na Alshaabab hadi akakubali
kumuachia huru Yasmin na mtu
mwingine ambaye alikuwa
amefungwa katika gereza moja
hapa nchini anaitwa Tariq .Sharti
la kuachiwa kwa Yasmin lilitoka
kwa IS.”
“ IS? .” akauliza Amarachi
“ Jambo hili limekaa
hivi.Alshabaab wanatafuta
kuongeza nguvu ili kuiangusha
serikali ya Somalia na IS
wamewaahidi kuwasadia ili
kuhakikisha wanaing’oa
madarakani serikali na Alshabaab
kuitawalaSomalia. Alshabaab
,walifanya mashauriano na IS
ambao walitoa masharti mawili
.kwanza walitaka Yasmin ambaye
ni mtu wao aachiwe huru na pili
walitaka hati ya muungano wa
Tanganyika na Zanzibar” akasema
Austin .Job na Amarachi
wakatazamana.Austin akaendelea.
“ Rais alimtoa Yasmin
gerezani kama moja ya sharti
alilopewa katika makubaliano
yake na Alshabaab.Kama haitoshi
alitekeleza pia na sharti la pili la
kuitoa hati ya muungano wa
Tanganyikana Zanzibar kwa IS.”
“ That’s a lie.!! Akasema Job
“ That’s not possible.Austin
this woman is lying to us!!
Akasema Job kwa ukali
“ Relax Job.”akasema Austin
“ Austin kitu alichokwambia
Yule mwanamke si cha kweli.Hicho
ni kitu kisichowezekana hata
kidogo” akasema Job
“ Job naomba tafadhali uwe na
subira hadi nimalize kuwaeleza
kile nilichozungumza na Yasmin”
akasema Austin.
“ Hata mimi nilipata mstuko
kama wako Yasmin aliponieleza
kuhusiana na suala hili.Kwa ufupi
ni kweli rais ana makubaliano na
Alshabaab ingawa hatujui ni
makubalino gani.Tumejadili
kuhusiana na mashambulio
yaliyotokea hapa nchini Yasmin
kwa uzoefu wake akanihakikishia
kwamba ana uhakika kwamba
mashambulio yale
hayajatekelezwa na Alshabaab bali
yamefanywa na watu toka ndani ya
nchi”
“Mbona Alshabaab tayari
wamekiri kuhusika katika
mashambulio hayo? Akauliza Job
“ Ndiyo wamekiri kuhusika
lakini hakuna ushahidi wa moja
kwa moja wa kuwahusisha na
mashambulio hayo.Ukilichambua
suala hili kwa mapana zaidi utaona
kwamba kuna uwezekano mkubwa
Alshabaab wakatumika kuuhadaa
ulimwengu kuhusu kuhusika kwao
katika mashambulio yale.Yasmin
anafahamu namna magaidi
wanavyotekeleza mashambulio
yao na ndiyo maana hata yeye ana
wasi wasi kama kweli ni Alshabaab
ndio walifanya unyama huu.Swali
tunalopaswa kujiuliza kama si
Alshabaab ni nani ? akanyamaza
na kuwatazama wenzake kisha
akaendelea
“ Shambulio la Dar es slaam
limetokea wakati rais akiwa mita
kadhaa kabla ya kuifikia hoteli
iliyoshambuliwa.Kwa picha ya
haraka haraka utaona kuwa
mlengwa wa shambulio lile
alikuwa rais lakini tunapaswa
kujiuliza rais na Alshabaab wana
makubaliano yao ni watu wenye
mawasiliano iweje walenge
kumuua mtu ambaye ana
makubaliano nao? Haiingii akilini
kabisa . Tukiunganisha mtiririko
wa mambo kuanzia rais kuwa na
mawasiliano na
Alshabaab,kuwaachia akina
Yasmin na Tariq,shambulio
kutokea mita chake kabla
hajaifikia hotel kuna chembe
chembe ndogo za kutuwezesha
kuhisi aidha anahusika au kuna
kitu anakifahamu kuhusiana na
mashambulio haya.Hiyo ni kazi
yetu kuchunguza na kuupata
ukweli” akanyamaza tena akameza
mate kulainisha koo kisha
akendelea
“ Yasmin na Tariq
waliandaliwa ndege maalum
iwapeleke Mogadishu lakini
wakiwa angani Yasmin
akawalazimisha marubani kutua
kwa dharura kisiwani Zanzibar
kwa kisingizio cha hitilafu katika
injini.Yasmin na Tariq
wakapelekwa hospitali kwa madai
ya kupata mstuko wakati ndege
ilipopata hitilafu angani na safari
yao ikaishia hapo.Walipotoka
hospitali wakaenda hotelini na
huko Yasmin akamuua Tariq
baada ya kumfuma akiwasiliana na
Alshabaab kuhusu kile alichokuwa
amekifanya Yasmin.Baada ya hapo
ndipo aliponipigia simu na kutaka
msaada wetu na Mungu
ametusaidia tumefanikiwa
kumpata.Kwa hiyo majibu
tumepata kwamba rais ana
mawasiliano na Alshabaab na
wana makubaliano ambayo
hatuyafahamu bado.” Akanyamaza
kidogo na kuendelea
“ Kama mtakumbuka kwamba
nilipozungumza na Yasmin jana
asubuhi alinieleza kwamba anacho
kitu kikubwa na cha thamani
ambacho ili kukipata lazima
kwanza nitimize masharti yake
anayotaka. Kitu hicho alichokuwa
anakisema anacho na cha thamani
ni hati ya muungano” akasema
Austin Job akasimama
“ Austin bado naendelea
kupingana na yule
mwanamke.Hiki kitu
alichokwambia kuhusu hati ya
muungano si cha kweli.Huu ni
uongo mkubwa .lazima kuna kitu
anakitafuta.Tunatakiwa kuwa
makini sana naye.She’s a
professional liar!! akasema Job
“ Job relax brother.Una haki ya
kuwa na wasiwasi na Yasmin.Hata
mimi wakati ananieleza suala hili
ilinichukua muda kidogo
kumuelewa.” Austin akanyamaza
akawatazama Amarachi na Job
“ Kama ni kweli,kwa nini
Alshabaab wameitaka hati ya
muungano? Katika vitu vyote
ambavyo wangeweza kuvihitaji
kwa nini watake hati hiyo?
Akauliza Job
“Swali hilo nilimuuliza pia
Yasmin.Ninavyowafahamu
Alshabaab wangeweza kutaka
fedha kwa ajili ya kujiendesha au
silaha lakini wameacha vitu hivyo
vyote na wakataka kupewa hati ya
muungano.Maelezo aliyonipa
Yasmin yamenipa mwanga kidogo
kuhusiana na swali hili
tunalojiuliza.Anasema kwamba IS
wana mpango wa kujitanua zaidi
katika ukanda huu wa afrika
mashariki na yeye Yasmin
alitumwa kuja Afrika miaka zaidi
ya kumi iliyopita kufanya
uchunguzi ni namna gani
wanaweza kulitanua kundi lao
huku .Katika uchunguzi wake
Yasmin aligundua kwamba
wanaweza wakaanzisha kundi lao
huku Afrika mashariki lakini
wangeweza kufanya shughuli zao
kwa ufanisi mkubwa iwapo
wangefanikiwa kukiweka kisiwa
cha Pemba katika himaya yao.Toka
wakati huo ,kukipata kisiwa cha
Pemba umekuwa ni mpango
mkubwa kwa IS .Kama
tunavyoelewa kwamba kisiwa cha
Pemba kiko ndani ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania kwa hiyo
ili kuweza kukipata kisiwa hicho ni
lazima kwanza muungano kati ya
Tanganyika na Zanzibar uvunjike
na halafu visiwa vya Unguja na
Pemba kila kimoja kiwe huru na
hapo ingekuwa rahisi kwao
kuweza kuingia kisiwani Pemba
na kujiimarisha huko.” Austin
akanyamza kidogo halafu
akaendelea
“ IS wametumia mbinu mbali
mbali kujaribu kuuvunja
muungano kwa kupandikiza watu
hata ndani ya serikali ambao
wamekuwa wakifanya jitihada
mbali mbali ili muungano huu
uvunjike lakini mpaka sasa bado
hawajafanikiwa.Walipoipata fursa
hii wameamua kuitumia vyema
kwa kuitaka hati inayohalalisha
muungano wa Tanganyika na
Zanzibar.Endapo Alshabaab
watafankisha IS kuipata hati hiyo
watalipwa pesa nyingi sana na vile
vile watasaidiwa katika vita yao ya
kuiangusha serikali ya Somalia
kitu ambacho wamekuwa
wakikipigania kwa miaka
mingi.Kwa hiyo siyo Alshabaab
wanaoitafuta hati ya muungano
bali IS na lengo lako kubwa ni
kuuvunja muungano huu na
kukitwaa kisiwa cha Pemba ili
waweze kuimarisha kikundi chao
huko” akasema Austin.Job
akainamisha kichwa akatafakari
kwa muda halafu akainua kichwa
na kumtazama Austin.
“Austin I want to hear one
thing from you” akasema na
kumkazia macho Austin
“ Tell me you believe her and
I’ll believe her too” akasema
Job.Austin akameza mate na
kusema
“ I believe her”
“ Good.Wewe ni kiongozi wetu
na kama umechagua kumuamini
Yasmin hata sisi hatuna budi
kuamini hicho anachokisema japo
kichwa changu bado kina maswali
mengi sana kwa nini rais ambayue
aliapa kuulinda muungano huu
afanye kitu kama hiki? Kwa nini
ahatarishe muungano huu
uliodumu kwa zaidi ya miaka
hamsini? Akauliza Job
“ Bado ni mapema sana
kupata majibu ya maswali yako
Job.Kilichopo mbele yetu ni
kufanya uchunguzi mkubwa wa
suala hili na kuupata ukweli.Kwa
hiyo ndugu zangu tunaweka
pembeni mambo mengine yote
kwa wakati huu ili tulishughulikie
suala moja tu lililoko mbele yetu
nalo ni kuhakikisha tunaipata hati
ya muungano na kuinusuru nchi
yetu kuvunjika vipande
viwili.Usalama wa Tanzania uko
katika mikono yetu kwa hiyo
lazima tupambane kufa au kupona
kuhakikisha kwamba jambo hili
halifanikiwi.Na kama ni kweli rais
amefanya kitu kama hiki
hatutakuwa na namna nyingine
zaidi ya kumuondoa madarakani
na kumfikisha mbele ya
sheria.Guys this is not an easy
thing” akasema Austin na
kushusha pumzi .Wote wakawa
kimya
“Hati hiyo iko wapi? Yasmin
amekuonyesha ili tuwe na uhakika
kama ni yenyewe? Akauliza
Amarachi
“ Hati hiyo hanayo kwa
sasa,anadai ameificha sehemu
salama na endapo akitimiziwa kile
anachokitaka basi atatuonyesha
mahala alikoificha hiyo hati.”
Akajibu Austin.
“ Anahitaji nini? Akauliza Job
“ Ameamua kuachana na IS
kwa hiyo anataka tumuwezeshe
kuondoka hapa nchini na kwenda
kuishi mbali ambako IS
hawataweza kumpata.Anahitaji
maisha mapya”akasema Austin
“ Umempa jibu
gani?Umemkubalia matakwa
yake? Job akauliza
“ Imenilazimu
kumkubalia.Tunahitaji hati
yetu.Nimechagua kumuamini na
tutafanya kila analolitaka ili aweze
kutuonyesha mahala ilipo hati ”
akasema Austin
“ Austin japokuwa
umetuhakikishia kwamba
unamuamini huyu mwanamke
lakini kwangu bado kuna mambo
yananipa shaka sana.Hati hiyo
ameificha wapi? Kwa nini
ameificha badala ya kuipeleka kwa
wenzake waliomuagiza aipeleke?
Job akauliza
“ Sifahamu hati hiyo kaificha
wapi lakini anadai kwamba
alificha hati hiyo kwa ajili ya
kufanya mabadilishano na
mwanae.Mtakumbuka nilipongea
naye alisema kwamba ana kitu cha
thamani sana atatupatia endapo
tutampatia mwanae kwa hiyo
hakuwa na sababu ya kuipeleka
hati hiyo kwa IS wakati tayari
amekwisha fanya maamuzi ya
kuachana nao na kuanza maisha
mapya.Job nafahamu wasiwasi
wako lakini kwa sasa hatuna
namna ya kufanya lazima tukubali
kumuamini Yasmin kwani
tukiipoteza fursa hii tunaweza
tusiipate hiyo nyaraka muhimu
sana kwa taifa letu.Lazima
tukubali kumtimizia kila
anachokitaka” akasema Austin
“ Austin kwa nini tusitumie
mbinu zetu,tumtese huyu mama
hadi atakapotueleza ukweli wote
mahala alikoificha hiyo hati?
Akauliza Job
“ Nipeni mimi jukumu hilo
nimuhoji na ninawahakikishia
nitarejea na majibu.Isitoshe huyu
mwanamke ni mtu hatari
japokuwa anadai kwamba
ameamua kubadilika na kuachana
na IS lakini tutafanya kosa kubwa
tukimuacha aende.Kubalini
ushauri wangu ndugu zangu
tumuhoji na atueleze mahala
alipoiweka hiyo hati .” akasema
Job
“ Hapana Job.Hatuwezi
kufanya hivyo.That wont work”
akasema Austin
“ Austin yuko sahihi.Magaidi
wote hula kiapo cha kutokutoa siri
yoyote .Kwao ni afadhali kupoteza
uhai kuliko kutoa siri.Nimeishi na
magaidi kwa miaka kadhaa
ninawafahamu vyema.Tukimtesa
hatutapata chochote.Tufanye kama
anavyosema Austin tumkubalie
kile anachokitaka” akasema
Amarachi.
“ Tutawezaje kumtoa humu
nchini ? Tutampeleka wapi
akaanze maisha mapya yeye na
mwanae? Tutawezaje kupata pasi
mpya za kusafiria kwa wakati huu?
Akauliza Job
“ Guys kama nilivyowaeleza
awali kwamba hili si suala rahisi.Ni
jambo gumu sana na tukilichukulia
kimchezo mchezo tutakosa kila
kitu.Tunapaswa kutumia akili
nyingi.Kwa hivi sasa itakuwa
vigumu sana kwetukuweza kumtoa
Yasmin hapa nchini na kumpeleka
nje ya nchi.Ingekuwa rahisi sana
kama rais angekuwa upande wetu
lakini nyote mnaona yule si
mwenzetu tena.Tunatakiwa
kutafuta namna nyingine ya
kuweza kufanikisha suala hili la
Yasmin.” Akasema Austin na
kunyamaza kidogo akawatazama
wenzake kwa zamu halafu
akasema
“ Kuna njia moja tu ya
kutusaidia katika jambo hili.Ni
kwa kumtumia Monica” akasema
Austin
“ Monica again? Amarachi
akauliza
“ Austin yule binti hataweza
tena kukubali kushirikiana na sisi
hasa kwa kile kilichotokea usiku
huu.Maneno aliyoyatamka ni wazi
hataki tena ukaribu wowote na
wewe na hataweza kutusaidia”
akasema Job
“ We don’t have a choice .She’s
the only one who can help us .I
promise you she will help us”
akasema Austin
“ Are you sure Austin?
Akauliza Amarachi
“ Yes I’m sure.I’ll do anything
for her to help us” akasema Austin
na kuchukua simu yake akapiga
namba za Monica lakini simu yake
haikuwa ikipatikana.
“ Amezima simu.Hata hivyo
kesho asubuhi na mapema
nitampigia siku na kama bado
atakuwa hajawasha simu yake
nitamfuata nyumbani
kwake.Lazima atusaidie” Akasema
Austin
 
Back
Top Bottom