SEASON 7: SEHEMU YA 2
Kwa zaidi ya dakika tatu sasa,
rais Ernest Mkasa alikuwa
ameegemea ukuta akionekana
kuchanganyikiwa kwa ile simu
aliyopigiwa na mke wake
Agatha.Alihisi shati likiloana kwa
kijasho kilichokuwa kinamtoka
“ Bado siamini hiki
nilichokisikia.” Akawaza
“ Imewezekanaje? Akajiuliza
“ Sauti ni ile ile ya
Agatha.Kama kweli ni yeye
imetokeaje hadi asiwepo ndani ya
ule ukumbi kama tulivyokuwa
tumekubaliana? Kama alikuwemo
ukumbini ameokoka vipi? Na kama
hakuwepo ukumbini ni kwa nini
hakuwepo? Je kuna kitu chochote
alikwisha kihisi? Akajiuliza na
kukuna kichwa.
“ Naona kichwa changu
kinazidi kulemewa kwa mzigo
mzito wa mawazo.Imewezekanaje
Agatha asiwepo ukumbini wakati
yeye ndiye aliyekuwa mstari wa
mbele kukusanya wenzake wafike
pale ukumbini? Isitoshe yeye ni
mmoja wa viongozi wa Alberto’s
hapa nchini alitakiwa kuwepo mle
ndani.Kuna kitu chochote
alikigundua kuhusiana na mpango
wangu?
“ I’m not dead mr President.I’m
still alive.”
Maneno haya ya Agatha
yakaendelea kuzunguka kichwani
kwake
“ kwa maneno haya mni wazi
ananiambia kwamba
nilichokikusudia kwake
hakijatimia na bado mzima.Kama
kweli ni yeye this is going to be a
big war.Lazima atakuwa
anafahamu kuhusu mpango
wangu.Kama tayari anafahamu
nani kamueleza? Mtu pekee
aliyekuwa anafahamu kuhusiana
na mpango wangu ni Jenerali
Lameck na wengine ni wale
makamanda na marubani
waliopewa amri ya kuyalipua
majengo yale mawili ambao nina
imani walikula kiapo cha
kutokusema chochote.Agatha
amefahamu vipi mpango huu?
Akajiuliza rais
“ Just wait for my call mr
president anytime soon”
Maneno haya ya mwisho
aliyoyaongea Agatha kabla ya
kukata simu yalizidi
kumchanganya zaidi Ernest
“ Alimaanisha nini aliposema
kwamba nitegemee simu yake
muda si mrefu? Anataka
kuniambia jambo gani?
Akaendelea kujiuliza
“ Tayari nilianza kushangilia
mpango wangu wa kuwaondoa
Alberto’s kufanikiwa lakini simu
hii ya Agatha imetibua kila
kitu.Amewezaje kukwepa janga
hili? Huyu mwanamke ni kikwazo
kikubwa sana kwangu kwa
sasa.Idadi ya watu ninaotakiwa
kuwashughulikia kwa haraka
inazidi kuongezeka.Kwanza
walikuwa ni Austin na wenzake na
sasa ameongezeka
Agatha.Ameichanganya akili yangu
na sijui nifanye nini” akawaza na
mara akakumbuka kuwa alikuwa
na Jeneral Lameck akamtaka
waelekee katika chumba cha
maongezi ya faragha.Rais akavua
koti na shati lake lililoa jasho
“Pole mheshimiwa
rais.Mambo yanazidi kuwa
magumu lakini usihofu
tutayamaliza moja baada ya
lingine.” Akasema Lameck
“ Ahsante Lameck.” Akasema
rais na kumtazama Lameck
“ Lameck kwa silimia tisini na
saba naweza kusema kwamba
mpango wetu umefanikiwa na kile
tulichokuwa tumekilenga
tumekipata .Idadi kubwa ya
Alberto’s kama si wote wamefariki
dunia,na hata wabunge wafuasi
wao karibu wote wamefariki
dunia.Tumechafuka kwa damu zao
lakini ni ushindi kwetu na kwa
nchi pia.Pamoja na ushindi huo
kumejitokeza baadhi ya matatizo
.Kwanza ni Yasmin ambaye tayari
tuna uhakika kwamba yuko ndani
ya jiji la Dar es salaam.Huyu ana
nyaraka ya muhimu sana ambayo
lazima tuipate kwa haraka.Yasmin
yuko na akina Austin na lazima
atawaeleza kila kitu na anaweza
akawapatia hati hiyo ili wampatie
mwanae.Kama hilo likitokea
tutakuwa katika matatizo
makubwa.Wale vijana wanaweza
wakaharibu mafanikio haya yote
tuliyoyapata.Ni vijana hatari sana
kwetu ambao kwa kila namna
itakayowezekana lazima kabla ya
jua kuzama siku ya kesho
tuwapate.” Akanyamaza na kuuma
meno kwa hasira.
“ Sikutegemea kabisa kama
nitaingia katika vita na hawa
vijana.Niliwaamini nikawapa kazi
wanifanyie na sasa wamegeuka
adui zangu.” akasema rais
“ Ukiachana na hao vijana
kuna jambo lingine limetokea
muda mfupi uliopita na ambalo
limenifanya mwili wote uloe jasho.
Lameck tuna tatizo kubwa”
akasema rais na kuvuta pumzi
ndefu
“ Tatizo gani limejitokeza
mzee? Akauliza Lameck.
“ Agatha is still alive” akasema
na kumshangaza Lameck
“ Agatha yupi mzee? Akauliza
Lameck
“ Agatha mke wangu”
“ What ? Lameck akapatwa na
mshangao mkubwa
“ Imewezekanaje?
Amenusurika vipi? Hakuwepo
katika ile hoteli? Akauliza Lameck
“ Hata mimi bado najiuliza
maswali kama hayo na sifahamu
nini kimetokea hadi akanusurika”
akasema rais
“ Mzee umeajuaje kama kweli
yuko hai?
“ Amenipigia simu muda si
mrefu nilipomaliza kuzungumza
na Habib.Tumeongea kwa muda
mfupi sana na alichokisema ni
kwamba amenipigia kunijulisha
kuwa yuko hai na mwisho akasema
kwamba nisubiri simu yake hivi
karibuni.Lameck
nimechanganyikiwa.Agatha ni mtu
ambaye nilihitaji sana awepo
katika orodha ya watakaofariki
lakini imeshindikana.Maneno yake
yanaonyesha wazi kwamba
anafahamu kuhusu ule mpango
wetu Kama ni kweli ameufahamu
mpango wetu sijui nini
kitatokea.Sifahamu atataka nini
akipiga hiyo simu aliyoahidi
kupiga”akasema rais
“Mzee una uhakika kuwa
uliyeongea naye ni Agatha?
Haiwezekani mtu mwingine
akajitokeza akaiga sauti akajifanya
kuwa yeye ni Agatha? Akauliza
Lameck
“ Lameck ninamfahamu mke
wangu vizuri.Nimeishi naye kwa
miaka mingi kwa hiyo naifahamu
vyema sauti yake hata nikiisikia
nikiwa usingizi.Niliyeongea naye ni
Agatha” akasema rais
“ Umejaribu tena kumpigia
kwa kutumia namba hizo za simu
alizokupigia?akauliza Lameck
“ Hapana sijajaribu” akasema
rais na kupiga zile namba za simu
alizotumia mke wake lakini
akapewa angalizo kwamba namba
zile hazikuwa sahihi .Akazidi
kuchanganyikiwa.
“ Lameck namfahamu huyu
mwanamke ni mjanja sana na
hawezi kutumia namba ya simu
ambayo itatuwezesha kumpata
kirahisi .Nina hakika lazima kuna
kitu anakiandaa kuja nacho.”
“ Mheshimiwa rais suala hili
linanichanganya sana.Unadai
lazima atakuwa anafahamu
kuhusu mipango yetu ,kama ni
kweli anafahamu,nani kampa
habari hizi? Mpango huu
umepangwa na watu wawili tu
mimi na wewe,umevuja vipi?
Akauliza Lameck
“ Hilo ni swali ambalo hata
mimi nimejiuliza sana.Nahisi
inawezekana mmoja wa wale
marubani au makamanda
uliowashirikisha amevujisha siri
hii” akasema rais
“ Hapana mzee.Nina wamini
sana vijana wangu na wamekula
kiapo cha kutokusema chochote
kuhusiana na jambo hili.Kama
Agatha amefahamu mpango wetu
lazima kuna tatizo kubwa mzee.”
Akasema lameck na ukimya mfupi
ukapita.
‘”Kwa hiyo tunafanya nini
mzee? Mambo yameanza
kutubadilikia na tunapaswa
kuanza kuyatafutia ufumbuzi wa
haraka kuanzia sasa na kabla jua
halijatoka tayari tuwe na
mwangaza wa tunakoelekea ili
mambo yasiharibike” akasema
Lameck
“ Nataka Silvanus arejee dar es
salaam haraka sana ili
alishughulikie hili.Nguvu kubwa
kwa usiku huu inatakiwa
kuelekezwa kuwatafuta Agatha na
akina Austin ambao najua kwa
msaada wa Monica tunaweza
kuwapata kirahisi.Tatizo liko kwa
Agatha namna ya kumpata .Silva
nataka atumie rasilimali zote
zilizopo katika idara yake kumpata
Agatha.” Akasema rais.Lameck
akawaza kitu halafu akasema
“ Mzee nina wazo moja”
“ Sema Lameck nakusikia
“ Mambo mapya yanazidi
kuibuka moja baada ya
lingine.Alikuwa ni
Yasmin,wakaongezeka akina
Austin na sasa ameongezeka
Agatha na mpaka sasa hatuna
fununu zozote watu hawa wako
wapi ingawa wako hapa hapa Dar
es salaam .Nina wasi wasi
tunaweza tusifanikiwe kuwapata
kwa muda tunaotaka na kadiri
tutakavyozidi kuchelewa tunaweza
kujikuta kila kitu tulichokifanya
kikaharibika na tukashindwa
kufikia malengo yetu.Wazo langu
kwa nini usitafute muafaka na
akina Austin?
“Muafaka?! Rais akastuka
“ Ndiyo mzee.Kwa nini
usiwaite wale jaama ukazungumza
nao ukawaeleza ukweli wote ?
Waeleze kila kitu kilichotokea na
kwa nini tumefanya vile.Mwisho
waombe mshirikiane katika
kuitafuta tena hati ile ya
muungano.Wewe na Austin
mliyaanzisha mapambano dhidi ya
Alberto’s nina uhakika nyote lengo
lenu lilikuwa moja kuwaondoa
kabisa Alberto’s hapa nchini na
nina uhakika lazima Austin
atakubaliana na hiki
tulichokifanya.Nakushauri mzee
ufanye hivi angali bado mapema
na lengo kubwa la kukushauri
ufanye hivi ni kupunguza idadi ya
maadui tunaotakiwa
kuwapata.Nina uhakika mkubwa
kama tukiwashirikisha hawa akina
Austin basi uwezekano wa kuipata
hati ya muungano ni mkubwa
sana.Tukimalizana na hawa jamaa
tutabakiwa na mtu mmoja tu
ambaye ni Agatha.Huyu tutatumia
nguvu kubwa kumtafuta na
tutampata kirahisi.” Akasema
Lameck.Rais akainamisha kichwa
akazama katika mawazo halafu
akamtazama Lameck na kusema
“Lameck wazo lako ni zuri
lakini halitaweza kufaa kwa
sasa.Tumechelewa tayari.Kama ni
kuwashirikisha tulitakiwa
kuwashirikisha kuanzia
mwanzo.Mimi na wao tulikuwa na
mipango ya kuwafagia Alberto’s
hapa nchini lakini niliwageuka na
kuja na mpango huu wa kulipua
hoteli na bunge mpango ambao
umefanikiwa kuwaondoa Alberto’s
wengi kwa mara moja.Tayari uadui
umeingia kati yetu.Wamekwisha
gundua kwamba siko upande wao
kwa hiyo haitawezekana
kushirikiana nao katika jambo
lolote.Kitu pekee cha kufanya hapa
ni kuwatafuta kokote waliko na
ninatoa amri ya kuwapiga risasi
wote baada ya kuwa tumeipata
hati ya muungano watakayokuwa
wamepewa na Yasmin,kwani lengo
la kwenda kumchukua Zanzibar ni
ili k uipata hati hiyo” Akasema rais
na kumpigia simu Silvanus
Kiwembe akamtaka arejee Dar es
salama haraka iwezekanavyo kuna
jambo la dharura limejitokeza
“ Lameck nenda kashughulikie
ule mpango wa kufanya
mashambulio katika kambi za
Alshabaab.Jukumu hili la
kuwatafuta Agatha na akina Austin
nitampa Silva ambaye atawasili
muda si mrefu kutoka
Zanzibar.Kwa sasa ngoja
nikapumzishe kichwa changu
nahisi kinaweza kupasuka kwa
mawazo mengi
niliyonayo.Utanijulisha kila kitu
kitakavyokwenda” akasema rais
na kuelekea chumbani kwake.
“ Mambo yamekwenda vizuri
sana ila hapa mwishoni kuna
mdudu ameingia na anataka
kuharibu kila kitu.Hata hivyo
nashukuru kwamba kwa asilimia
kubwa nililolitaka
limetokea.Alberto’s karibu wote
hapa nchini nimewafyeka.Natumai
kesho asubuhi nitapata orodha ya
watu wote walioteketea ili
nitathmini mafanikio .Ninaamini
tayari nimeuzika mtandao wa
Alberto’s hapa nchini.Kwa sasa
nguvu natakiwa kuielekeza katika
kukabiliana na yale yaliyojitokeza
na yanayoendelea kujitokeza
baada ya mashambulio haya na
kikubwa ni kuwapata kwanza
akina Austin ambao nina uhakika
Yasmin atakuwa amewaeleza kila
kitu kilichotokea.Austin ni kijana
mwenye akili sana kwani alitaka
kwanza nifahamu kama Monica ni
mwanangu na alipofanikiwa katika
hilo akamfuata Monica akamtaka
awasiliane nami akijua wazi
kwamba siwezi kumkatalia Monica
jambo lolote.How could I be such a
fool?Kwa nini nimekubali
kuchezewa akili na kijana mdogo
kama yule? Akajiuliza huku akivua
shati na kujilaza kitandani
“ Anyway yamekwisha tokea
na kilichobaki kwa sasa ni
kuhakikisha kwa gharama zozote
zile ninaipata hati ya muungano na
kuirejesha mahala pake na hii
itapatikana endapo nitampata
Yasmin na akina Austin.Wale ni
vijana wadogo siwezi kushindwa
kuwpata wakati majeshi yote yako
chini yangu.Nitatumia kila nguvu
niliyonayo ili kuwapata akina
Austin kabla ya jua kuzama hiyo
kesho.Jiji la Dar kesho lazima
lifungwe hakuna kuingia wala
kutoka mtu hadi Austin na kundi
lake wapatikane.Najuta kwa nini
nilimtumiahuyu kijana.Nilimuona
wa thamani kubwa kwangu lakini
sasa amegeuka mzigo na adui
mkubwa.Lazima nimmalize haraka
kwani nikichelewa
atanimaliza.Kuhusu Alshabaab
nitamalizana nao .Nitazungumza
nao ili niwapatie kitu kingine
badala ya ile hati” akawaza rais na
mara akainuka na kukaa
“ Ni vipi endapo sintafanikiwa
kuipata tena hati ya muungano?
Akawaza na kukumbuka kitu
“ Mzee Pantaleo amekutwa
amejinyonga.Vijana wamefanya
kazi nzuri.Huyu angekuwa
kikwazo kikubwa kwangu kwani ni
yeye pekee aliyefahamu kuwa hati
ile iko kwangu.Endapo
sintafanikiwakuipata hati ile tayari
ninacho kitu cha kusema kwamba
Pantaleo ameshirikiana na watu
wakaiba hati ile ikulu na kuipeleka
mahala kusikojulikana na baada ya
kuona kwamba atagundulika
akaamua kujinyonga.Ninaamini
wananchi wataelewa.Isitoshe bado
tutaendelea kuwa taifa kwani kuna
hati nyingine kama ile iko umoja
wa mataifa kwa hiyo bado
tutaendelea kutambulika kama
taifa la Tanzania.Pamoja na hayo
lazima nihakikishe kwamba hati
inapatikana kwa gharama zozote.”
Akawaza na kuinamisha kichwa
“ Agatha!! Akasema kwa sauti
ndogo
“ Huyu naye ameibuka na
kufanya mambo kuwa magumu
zaidi.Nashindwa kupata jibu
ameokoka vipi? Kwa nini
hakuwemo katika kikao kile? Je
tayari alifahamu kuhusu mpango
niliokuwa nimeupanga dhidi
yao?Huyu mwananke kuendelea
kuwa hai ni hatari kubwa kwangu.
Najuta kwa nini sikummaliza
wakati ninayo nafasi.Ukiacha huyu
kuna mwingine ambaye ni hatari
zaidi pia Mukasha.Huyu naye
anatakiwa atafutwe kwa udi na
uvumba hadi
apatikane.Nikifanikiwa
kuwamaliza hawa nitakuwa
nimefunga kazi na nchi itabaki
salama.Nina hakika ndani ya wiki
hii lazima niwe nimefanikiwa
kuwapata wote. Mukasha ,Agatha
na akina Austin.Kwa sasa ngoja
nipumzike walau kwa saa moja
.Imekuwa ni siku ndefu sana yenye
mambo mengi.Sijapata wasaa wa
kupumzika toka jana na siku ya leo
itakuwa ndefu na ngumu sana
kuzidi jana.” Akawaza rais na
kujilaza kitandani