SEHEMU YA 2: SEASON 5
Evans aliwasili ikulu na moja
kwa moja akaenda kuonana na rais
“Evans hebu nieleze kilichotokea
hadi ukashindwa kuikamilisha kazi
niliyokutuma” akauliza rais
akionekana kujawa hasira
“Mheshimiwa rais utanisamehe
kwa kushindwa kuikamilisha ile kazi
uliyonituma.Mpango nilikuwa
nimeuandaa vizuri sana .Kuna watu
niliokuwa nimewaweka wakimfuatilia
Mukasha na uliponipa ruhusa ya
kumuondoa nilimfuata sehemu
alikokuwa amekwenda
usiku.Nilifanikiwa kuingia na
kujificha katika gari lake hadi
alipotoka hotelini na kuingia katika
gari na kuondoka.Lengo langu
lilikuwa ni kumpoteza kabisa yeye na
gari lake na tayari nilikwisha andaa
kivuko ili nikamzamishe majini yeye
na gari na hakuna ambaye angemuona
tena.Tatizo lilitokea pale nilipojitokeza
na kumuamuru atii kila
nitakachomuelekeza na akaanzisha
vurugu na kupambana nami ,hali
iliyosababisha gari liserereke na
kutaka kutumbukia
mtaroni.Nilifanikiwa kumdhibiti
lakini ghafla akatokea mtu na kuvunja
kioo cha gari nikapigwa ngumi nzito
nikatetereka kidogo na nilipogeuka
nikajikuta nikitazamana bastora na
yule mtu akaniamuru nishuke
niondoke zangu.Nikashuka na
kukimbia yeye akaondoka na
Mukasha.Kwa hiyo mheshimiwa rais
hivyo ndivyo ilivyotokea na
kusababisha nishidwe kummaliza
Mukasha” akasema Evans
“Oh my God !! akasema rais na
kumtazama Evans kwa hasira
“Ulibahatika kumuona huyo
jamaa aliyekuvamia na kuondoka na
Mukasha? Rais akauliza
“Ndiyo nilibahatika
kumuona..Ana nywele nyingi na
pembeni ya jicho lake la kulia kuna
kovu.”
“Jesu christ !! akasema rais kwa
mstuko
“Mukasha alikugundua?
Akauliza rais Evans akakaa kimya
“Nakuuliza Evans Mukasha
alikugundua?
“Ndiyo mzee alinifahamu.Yule
jamaa aliponidhibiti akamuamuru
Mukasha anivue kofia niliyoitumia
kufunika uso na nikatazamana na
Mukasha”
Sura ya rais ikabadilika na
kumtazama Evans kwa hasira
kali.Akachukua simu na kuzitafuta
namba fulani akapiga.Hakutaka
kuongea mbele ya Evans akaelekea
chumbani kwake
**********************
Kengele iliyoashiria kuna mtu
getini ilimuamsha Austin .Akatazama
saa ilionyesha ni saa kumi na mbili
kasoro dakika ishirini na tatu
“Tayari kumekucha.Usiku
umekuwa mfupi sana” akawaza
Austin akainuka na kuhisi maumivu
hasa ya kifua.Akajikaza na huku
akisaidiwa na fimbo akaenda getini na
kumkuta Amarachi ,wakasalimiana
akaingia ndani
“Samahani Austin sikuweza
kurejea jana usiku kama
nilivyokuahidi.Ilinilazimu kumfuata
daktari nyumbani kwake ili aanze
mara mohja kushughulikia zile
sampuli.Baada ya kutoka hospitali
nikapita nyumbani kuchukua baadhi
ya vitu vyangu vidogo vidogo vya
lazima .Vipi maendeleo yako?akauliza
Amarachi
“Pole sana Amarachi kwa
kukubebesha mzigo huu mzito”
akasema Austin
“Usijali Austin.Ninajisikia fahari
kuwepo katika timu hii yenye watu
walioyatoa maisha yao kwa ajili ya
nchi yao.Ninaipenda Tanzania kwani
imenihifadhi na kunifanya niyafurahie
maisha kwa hiyo yeyote yule mwenye
nia ovu na nchi hii ni adui yangu
mkubwa.” Akasema Amarachi na
wote wakatabasamu.
“Vipi maendeleo yako?
Amarachi akauliza
“Ninaendelea vizuri sana.Mwili
unapata nguvu kwa kasi ya
kushangaza.”
“Hizo ni habari nzuri sana .Vipi
Monica anaendeleaje?
“ Bado amelala.Anatakiwa
aamshwe aende nyumbani kwake
atupe nafasi ya kuendelea na mambo
mengine” akasema Austin na
Amarachi akaenda katika chumba
alimolala Monica akamuamsha
“Mhh !!kumepambazuka !!
akasema Monica kwa uchovu huku
akiinuka na kukaa kitandani akashika
kichwa.
“Mwili umechoka na macho
mazito mno.Natamani niendelee
kulala” akasema Monica
“Monica tayari ni asubuhi kwa
hiyo natakiwa kukurejesha nyumbani
kwako kuendelea na majukumu
mengine” akasema Amarachi
“You are right.How’s Austin?
“Austin anaendelea
vyema.Anazidi kuimarika” akasema
Amarachi
“Good” akasema Monica na
kuinuka akaenda kujitazama katika
kioo
“I look like a pig” akasema huku
akiziweka vizuri nywele zake
“Jana nilitokewa na kitu cha
ajabu sana na cha aibu.Kusinzia mbele
ya rais ni aibu kubwa” akasema
Monica
“ Mimi ndiye wa kulaumiwa
Monica kwa kukuletea mvinyo ule
bila ya kukuuliza kama ni mtumiaji
wa vilevi vikali.Mvinyo ule
anaoutumia rais ni mkali
mno.Samahani sana”
“Usijali Amarachi” akajibu
Monica
“Kabla sijaondoka nahitaji
kumuona Austin.Unaweza nipeleka
nikaonana naye? Akasema Monica
“Hakuna neno hata naye
atafurahi pia” akasema Amarachi
wakatoka na kuelekea katika chumba
alimolala Austin.Amarachi akagonga
mlango na sauti ya Austin ikaruhusu
waingie ndani.Sura ya Austin
ikaonyesha tabasamu baada ya
kuwaona Monica na Amarachi.
“Hallow Austin.Vipi maendeleo
yako? Monica akauliza
“Ninaendelea vizuri .Afya yangu
inaimarika kwa kasi ya ajabu.Vipi
wewe unaendeleaje?
“Uhhm ! Ninaendelea vyema
japokuwa mwili bado mzito sana na
ninahisi uchovu mwingi.Natamani
kutwa nzima ya leo nishinde
nimelala.Utanisamehe Austin kwa
kitendo cha aibu nilichokifanya jana
cha kujifanya mnywaji wa mvinyo
halafu nikajikuta nikiuchapa usingizi
mbele ya rais.It was so embarrasing.I
don’t know how it happened na sijui
rais atanichukuliaje lakini naomba
uniombee msamaha sana na mueleze
wazi kwamba mimi si mtumiaji wa
vileo vikali “ akasema Monica
“Usijali Monica.Rais ameelewa
kilichotokea jana.Hata yeye
mwenyewe alishangaa sana kusikia
kwamba tumekupatia mvinyo ule
anaokunywa yeye ambao ni mvinyo
mkali sana.Utatusamehe sana sisi kwa
kukupa mvinyo ule bila kukuuliza”
akasema Austin
“Usijali Austin yamekwisha pita”
“Thank you.Vipi maongezi yenu
yalikwenda vizuri? Austin akauliza
“ Ndiyo tuliongea na
tukaelewana lakini bado hatukuwa
tumemaliza maongezi ndipo
nilipopatwa na hali ile .Naomba
endapo utaonana na rais mkumbushe
kuhusu maongezi yetu na ataelewa
atakupa jibu kisha utanijulisha”
akasema Monica
“Nitafanya hivyo.Monica na
kushukuru sana kwa kututembelea na
ninaomba isiwe ni mara ya mwisho
kufika hapa.Nakukaribisha tena siku
nyingine kwa chakula na hata
maongezi na ninakuomba usiseme
hapana pale nitakapokualika”
akasema Austin na wote
wakatabasamu
“Usihofu Austin nitakaribia.Uwe
na siku njema na upone
haraka.Nitakupigia simu baadae kujua
maendeleo yako.Hakikisha
unaendelea kufuata maelekezo yote
uliyopewa na daktari” akasema
Monica wakaagana akaongozana na
Amarachi wakaondoka
“Nahisi mwili kama si wa
kwangu” akasema Monica wakiwa
garini akirejeshwa nyumbani
“Pole sana Monica”
“Usijali Amarachi.Mvinyo ule
lazima utakuwa ni mkali sana.Mimi
hutumia mvinyo lakini mwepesi sana
kuliko kile kigongo nilichokutana
nacho jana.Hapa nilipo mwili wote
unaniuma na ninahisi kama vile
nimechomwa sindano katika baadhi
ya sehemu.” Akasema Monica na kwa
mbali akasikia mlio wa simu yake
.Zilikuwa namba ngeni
kabisa.Akaipokea simu ile
“Hallow “ akasema
“Hallow Monica.Ni mimi David”
ikasema sauti ya upande wa pili
“Ouh David habari yako
mpenzi”
“Habari yako
Monica.Nimekupigia sana jana usiku
lakini hukupokea.Kuna tatizo lolote?
Akauliza David
“Hakuna tatizo lolote David.Jana
nilichoka sana nikaisahau simu
sebuleni katika chaji nikaenda
kulala.Nisamehe mpenzi wangu.Vipi
maendeleo ya huko?
“ Nilikupigia simu ili kukupa
taarifa za huku.Si taarifa nzuri.Pauline
ametutoka saa saba na dakika nane za
usiku akiwa katika chumba cha
upasuaji.Madaktari walijitahidi sana
kwa kadiri ya uwezo wao lakini
hayakuwa mapenzi ya Mungu apone”
Kikapita kimya na mara Monica
akasikika akilia kwa kwikwi
“Monica “ akaita David
“David taarifa hii imenistua
mno.Pole sana kwa tatizo hili
kubwa.Mungu akupe nguvu za
kuhimili kipindi hiki kigumu”
“Pole nawe Monica.Najua
umeumizwa pia na kifo hiki cha
Pauline”
“Nimeumizwa mno
.Nimemfahamu Pauline katika siku za
mwisho wa uhai wake.Alikuwa
mwanamke mwenye upendo wa ajabu
na sijui namna ya kumuelezea.Vipi
kuhusu shughuli za msiba?
“Bado hatujapanga chochote .Ila
nitakuwa na kikao na viongozi na
wana ukoo ili kupanga taratibu za
mazishi.Nitakutaarifu kila kitu
tutakachokiamua” akasema David
“David nimekosa neno la kusema
kwa namna nilivyoumizwa na taarifa
hizi.” Akasema Monica
“Monica pole sana.Kitu cha
muhimu kwa sasa ni kuendelea na ule
mchakato wetu .Ujumbe tayari
umekwisha fika Dar es salaam kama
nilivyokueleza jana na ninatumai
tayari mmekwisha fanya maandalizi
ya kuwapokea na kukutana nao
.Usiku wa leo baada ya kumaliza
kikao wataondoka kurejea
Kinshasa.Taratibu zitakapokamilika
za mazishi nitatuma ndege kuja
kuwachukua wewe na wazazi wako ili
mshiriki katika kumsindikiza Pauline
katika safari yake ya mwisho.”
Akasema David
“David Mungu akupe nguvu ya
kuhimili kipindi hiki kigumu.”
Akasema Monica wakaagana na
kukata simu.Monica akainama na
kulia kwa kwikwi
“Monica kuna tatizo? Nini
kimetokea? Nimesikia unazungumza
kuhusu msiba nani kafariki? Akauliza
Amarachi.Pauline akafuta machozi na
kusema
“Mke wa rais wa Kongo anaitwa
Pauline kafariki.Imeniumiza
sana.kweli vizuri havidumu”
“Pole Monica”
“Ahsante ” akajibu Monica
“Mambo yanazizi
kuniandama.Kila siku linaibuka jambo
jipya.Kwa kweli kifo hiki cha Pauline
kimenichoma sana .Hata hivyo hatuna
budi kumshukuru Mungu kwa kila
jambo yeye ndiye mwenye kutoa na
kutwaa.Nakumbuka nilivyokuwa
naonge na Pauline huku akionekana
ni mtu mwenye afya njema na hakuna
ambaye angehisi kuwa alikuwa katika
siku zake za mwisho.Mungu ampe
pumziko la milele” akawaza Monica
SEHEMU YA 3 : SEASON 5
Amarachi alirejea baada ya
kumfikisha Monica nyumbani kwake
“Monica amefika salama lakini
bado analalamika mwili mchovu sana
ila mpaka sasa bado hajagundua
chochote” Amarachi akamwambia
Austin
“ Good” akajibu Austin
“Kuna jambo lingine” akasema
Amarachi
“Jambo gani?
“ Tukiwa garini Monica alipewa
taarifa za msiba .Anasema mke wa
rais wa Kongo amefariki dunia”
“Mke wa rais wa Kongo? Monica
anahusiana nini na msiba huo?
“Hata mimi nilijiuliza lakini
inaonekana wana uhusiano kwani
nilisikia akilitaja jina la David na
inaonekana alikuwa anazungumza na
David Zumo.Halafu …” akasema
Amarachi na kusita
“Ah ! tuachane na mambo
hayo.Nini kinaendelea sasa? Akauliza
Amarachi
“Kwa sasa tunarejea kwa Job .Leo
tuna kazi nyingi za kufanya.Tunahitaji
kufahamu mambo mengi toka kwa
Maria na baba yake Boaz” akasema
Austin na kabla hawajatoka ikaingia
simu toka kwa rais Austin akaipokea
“Shikamoo mzee” akasema
“Marahaba Austin.Vipi
maendeleo yako? Akauliza Rais
“Ninaendelea vizuri sana mzee”
“Nafurahi kusikia hivyo.Vipi
Monica naye anaendeleaje?
Alifanikiwa kurejea kwake salama?
“Amerejea kwake asubuhi
hii.Alishindwa kurejea kwake jana
usiku alikuwa anahisi uchovu mwingi
hivyo akalala hapa na ameondoka
asubuhi hii.Hata hivyo anaendelea
vizuri.Kuhusu zile sampuli tayari
zimewasilishwa maabara na tayari
zimeanza kufanyiwa kazi na majibu
yatakapotoka tutakukabidhi.”
“Ahsante sana
Austin.Nawatakieni maendeleo
mazuri katika shughuli zenu
zote.Simu yangu iko wazi na endapo
kuna lolote unahitaji usisite
kunitaarifu mara moja”
“Nitafanya hivyo mzee” akajibu
Austin wakaagana rais akakata
simu.Austin na Amarachi
wakaondoka kurejea nyumbani kwa
Job
Iliwachukua zaidi ya saa moja
kufika nyumbani kwa Job kutokana na
uwingi wa magari barabarani asubuhi
hii.Hawakutaka kuwasumbua akina
Job hivyo Amarachi akashuka ili
kufungua geti lakini akastuka baada
ya kukuta geti halijafungwa
akalisukuma na kuingiza gari
ndani.Gari la Job halikuwepo mle
ndani.Mara akatokea Marcelo
“karibuni sana .Habari za toka
jana? Vipi maendeleo yako Austin?
Akauliza Marcelo huku akimsaidia
Austin kupanda ngazi kuelekea
sebuleni
“Naendelea vyema.Afya yangu
inaimarika kwa kasi kubwa.Habari za
hapa? Anaendeleaje Job na wageni
wetu?
“Habari za hapa nzuri ila Job
sijaonana naye toka nimeamka.Jana
usiku aliniambia anatoka kuna
sehemu anakwenda .Usiku nilisikia
milango ya gari ikibamizwa nikahisi
ni Job au ninyi mmemrejea
nikaendelea kulala.Nimeshangaa
asubuhi kukuta Job wala ninyi
hampo.” Akasema Marcelo.Austin na
Amarachi wakatazamana.Austin
akamtaka Amarachi aende
akawatazame akina Maria na Marcelo
akaanza kushughulikia majeraha ya
Austin
Wakati Marcelo akiendelea
kumuhudumia Austin,Amarachi
akashuka ngazi kwa kasi ya ajabu
akiwa ameshika kitu mkononi.
“Amarachi kuna tatizo lolote?
Akauliza Austin
“Kuna kitu kimetokea hapa
ndani jana usiku” akasema na
kukikunjua kitambaa alichokishika na
kuwaonyesha akina Austin sikio la
mtu.Wote wakabaki na mshangao
mkubwa
“Nini kimetokea hapa? Hili sikio
la nani? Maria na Boaz wote wazima?
Akauliza Austin
“Maria na Boaz wote wako
salama ila katika chumba cha Maria
kumetapakaa damu nyingi na humo
ndimo nimelitoa sikio hili.” Akajibu
amarachi
“Marcelo nini kimetokea hapa
ndani jana? Austin akamuuliza
Marcelo
“Austin sifahamu nini kimetokea
hapa jana kama nilivyokueleza
kwamba baada ya Job kuondoka na
mimi nikaenda kupumzika na sikujua
kilichoendelea” akajibu Marcelo
“Amarachi mpigie simu Job
tufahamu yuko wapi” akasema Austin
na bila kuchelewa Amarachi
akampigia simu Job.Simu ya Job ikaita
bila kupokelewa,akapiga tena na
safari hii ikakatika na haikupatikana
tena
“Somethinhg is wrong here”
akasema Austin na kumtazama
Amarachi
“Twendeni chumbani kwa
Maraia” akaamuru Austin na wote
wakaelekea katika chumba cha
Maria.Mara tu mlango ulipofunguliwa
Austin akakutana na harufu ya damu
“Nini kimetokea humu?
Akajiuliza na mara akakutanisha
macho na Maria wakatazamana.Maria
aliyekuwa amefungwa kitini
alionekana kudhoofu .Austin
akapandwa na hasira za ghafla
alipomuona Maria akajitahjidi
kujizuia.
“Marcelo nenda kaandae mlo wa
asubuhi niache mimi na Amarachi”
akasema Austin na Marcelo akatoka
mle chumbani.
“Amarachi mfungue Maria
ajisafishe kisha usafishe humu
chumbani hatuwezi kuhojiana kukiwa
katika hali hii” akasema Austin na
Amarachi akampa Austin bastora
yake kisha akamfungua Maria
akampeleka bafuni akamswafi na
kumrejesha chumbani .Akaenda
kuchukua baadhi ya nguo zake
akambadilisha Maria halafu akafanya
usafi ndani ya kile chumba kukawa
safi.
“Now we can talk” akasema
Austin lakini kabla hawajaanza
kuzungumza chochote Marcelo
akatokea akiwa na sinia lenye
chakula,Maria akafunguliwa mikono
akala mlo ule uliokuwa ni supu na
chapati tatu,alionekana kuwa na njaa
kwani alimaliza chakula chote ndani
ya muda mfupi.Amarachi akataka
kumfunga tena mikono Austin
akamzuia
“Let her relax” akasema Austin
na kuketi akamtazama Maria kisha
akasema
“Hello Maria”
Maria hakujibu kitu akainamisha
kichwa.Hakutaka kumtazama Austin
usoni
“Nafahamu unahitaji sana kujua
maendeleo yangu .Ninaendelea
vyema na hali yangu inazidi kuboreka
kila uchao.Mungu amenipigania na
kusudio lako la kutaka kunitoa uhai
limeshindikana.Nitaongea nawe
baadae kuhusu suala hilo lakini kwa
sasa nataka kufahamu kilichotokea
humu ndani jana usiku.”
Maria hakujibu kitu bado
aliendelea kuinamisha kichwa.
“Maria tafadhali naomba
unieleze ni kitu gani kimetokea humu
chumbani jana usiku? Austin akauliza
tena lakini bado Maria hakutaka
kujibu chochote
“Hutaki kujibu? Akauliza Austin
“Austin this girl is trying us”
akasema Amarachi
“Anataka kuongea kwa lazima”
Austin akamtazama Maria kisha
akamgeukia Amarachi
“Do it Amarachi.Make her talk”
akasema Austin na bila kupoteza hata
sekunde moja Amarachi akafungua
sanduku lenye vifaa mbalimbali
akachukua koleo ndogo mbili
akamfunga Maria mikono katika kile
kiti kisha akakibana kidole kimoja
kwa koleo na kuanza kubandua
kucha.Maria akapiga ukelele mkubwa
sana kwa maumivu makali
aliyoyapata.
“Can you talk now? Akauliza
Amarachi
“Yes !! Yes!!! Akasema Maria
.Amarachi akachukua kichupa fulani
chenye dawa akaimimina katika
kidole kile na kukifanya kiwe na ganzi
hivyo kupunguza maumivu
“Now tel us what happened in
here last night? Akauliza
Amarachi.Maria akavuta pumzi ndefu
na kusema
“Job alikuja humu usiku akiwa
na mzee mmoja akanitambulisha
kuwa ni msaidizi wa rais lakini
anajihusisha na mtandao wa dawa za
kulevya.Alimtaka mzee yule amtajie
majina ya watu anaoshirikiana nao
lakini yule mzee hakuwa tayari na
ndipo alipomkata sikio.Baada ya
kukatwa sikio Yule mzee alimueleza
mambo fulani ambayo sikuyasikia
kisha wakatoka humu na hawajareja
tena.”
“Mukasha!!! Akasema Austin
“Job alimchukua
Mukasha.Amempeleka wapi? Kwani
nini akafanya hivyo bila ya
kutushirikisha? Akauliza
Amarachi.Austin akafkiri kidogo na
kusema
“Maria nitarejea baadae bado
mimi na wewe tuna mengi ya
kuzungumza” akasema na kisha
wakatoka mle chumbani
“Kwa mara ya kwanza toka
nimefahamiana na Job
amenikasirisha.Kwa nini kafanya hivi
bila ya kutushirikisha?We’re working
together so why he did this to
us?akauliza Amarachi akionekana
kuwa na hasira
“Calm down Amarachi.Job
amekosea lakini tunatakiwa tuelekeze
nguvu kumtafuta mahala aliko”
akasema Austin
“I don’t like this.Tunakwenda
mbele na kurudi nyuma .Kwa sasa
itatulazmu kusimamisha baadhi ya
mipango mingine ili kumtafuta.This is
not good.Amef…………” Amarachi
akanyamz baadaya simu yake
kuita.Akastuka baada ya kuliona jina
la mpigaji alikuwa Job
“It’s him” akasema huku
akimuonyesha Austin kisha
akabonyeza kitufe cha kupokelea.
“Halow Job,where are you ??
akauliza Amarachi
“Hallow” ikasema sauti ya
upande wa pili na sura ya Amarachi
ikabadilika baada ya kugundua kuwa
sauti ile haikuwa ya Job.Akamtazama
Austin kisha akasema kwa sauti
ndogo.
“It’s not him”
“Hallow habari yako? Nani
mwenzangu? Akauliza Amarachi
“Naitwa Kinyogoli,nashughulika
na uvuvi.Mwenye namba hizi
unamfahamu?
“Ndiyo namfahamu.Uko naye
karibu nizungumze naye?
“Nisikilize vizuri shangazi.Huyu
jamaa tumemuokota alfajiri ya leo
hapa ufukweni baada ya kutoka
katika shughuli zetu za uvuvi
.Alikuwa na majeraha makubwa
.Tumejitahid kumpa huduma zetu za
kienyeji na tukamuhifadhi ili baadae
tumpeleke hospitali lakini tunaona
hali yake inazidi kubadilika.Bado
hajaamka mpaka sasa.Naomba uje
umchukue umkimbize hospitali.Hali
yake ni mbaya.” Akasema yule jamaa.
“Ahsante sana ndugu kwa taarifa
hiyo.Naomba unielekeze tafadhali
mahala ulipo ili nije hapo mara moja
kumchukua na kumkimbiza
hospitali.” Akasema Amarachi na yule
jamaa akamuelekeza mahala walipo
“Nenda huko mara
moja.Utaongozana na Marcelo.”
Akasema Austin.Amarachi akamfuata
Marcelo na kumtaka waondoke
haraka wamfuate Job.Kabla
hawajaondoka Austin akamtaka
Amarachi amlete Julieth pale sebuleni
anahitaji kuzungumza naye.
“Hallo Julieth.Vipi hali yako?
Akauliza Austin .Julieth akamtazama
na kusema
“Ninyi ni watu katili
sana.Mmeniweka katika chumba
kisicho na kitu chochote hata
godoro.Nimelala sakafuni tena bila
hata kupewa chakula.Kwa nini mna
roho mbaya kiasi hicho? Akauliza
Julieth kwa ukali
“Naitwa Austin” akasema Austin
“Sihitaji
kukufahamu.Ninachohitaji mimi ni
kutoka hapa”
“Not so fast Julieth.Uwezekano
wa kutoka hapa ni mdogo sana labda
kama utaonyesha ushirikiano kwetu
tunaweza kukuachia ukaenda zako
lakini kwa sasa sahau kabisa habari ya
kurejea nyumbani”
“Mnataka nini toka kwangu?
Jana mmeniuliza kuhusu Boaz
nikawaeleza kila kitu.Mnataka nini
kingine? Akauliza Julieth kwa
ukali.Austin akamtazama kwa
sekunde kadhaa na kusema
“Naitwa Austin January.Mimi ni
mtanzania ambaye kwa sasa ninaishi
nchini Afrika ya kusini .Kazi yangu ni
upelelezi.Nimekuja Tanzania hivi
karibuni kwa ajili ya kazi moja tu ya
kumuokoa mtu aliyekuwa katika
hatari ya kuuawa.Nilifanikiwa
kumuokoa mtu huyo ambaye ni kaka
yako Marcelo.Mimi ndiye nliyemtoa
hospitali na kumpeleka sehemu
salama.Marcelo is a good
person.Nilijiuliza sana sababu za yeye
kutakiwa kuuawa na nilipomuhoji
hata yeye hakuwa anafahamu kwa
nini anatafutwa auawe.Tukiwa katika
kutafuta sababu za yeye kutaka
kuuawa nikakutana na Boaz ambaye
ninaishi naye Afrika kusini na mimi
ndiye msimamizi wa miradi yake yote
na nina uhusiano wa kimapenzi na
mwanae anaitwa Maria kwahiyo Boaz
ninamuheshimu kama baba
yangu.Boaz alinitaka nimtafute
Marcelo hadi nimpate.Akanipa
maelezo kwamba kuna kitabu
ambacho Marcelo aliachiwa na baba
yake ambacho kina maelezo yote
kuhusiana na biashara za ubia kati
yake na baba yake Marcelo.Boaz alidai
kwamba Marcelo amekificha kitabu
hicho kwa lengo la kumiliki miradi
yote peke yake.Yote haya yalikuwa ni
uongo mtupu kumbe kitabu
alichokuwa anakitafuta ni kitabu
chenye orodha ya wafanya biashara
wa dawa za kulevya .Tayari tunacho
kitabu hicho na muda si m refu
wataanza kukamatwa mmoja baada
ya mwingine.Hakuna atakayebaki
salama katika hili na tayari tumeanza
na Boaz mwenyewe na hautamuona
tena katika maisha yako yaliyobaki”
akasema Austin na kumstua sana
Julieth
“Mmemuua” akauliza
“Hapana sisi si wauaji
hatujamuua bali hataonekana
tena.You and him its over” akasema
Austin na kumtazama Julieth kwa
muda na kusema
“Julieth wewe ni msichana
mrembo na nafsi yangu inaniambia
nisikuharibie maisha yako kama
tutakavyowafanya hawa wengine
akina Boaz.Nataka unieleze ni kitu
gani hasa kilichokufanya uungane na
Boaz na kumsaliti ndugu yako wa
damu? Boaz anakulipa kiasi gani hadi
utake kumuua ndugu yako? Ungepata
faida gani endapo Marcelo angeuawa?
Nijibu tafadhali na pengine unaweza
kunishawishi nikafikiria kukuachia”
akasema Austin .Macho ya Julieth
yakajaa machozi
“Kuwa huru Julieth.Nieleze
tafadhali.Nini hasa unakipata katika
mahusiano na yule mzee? Anakupa
pesa kiasi gani hadi ukafikia maamuzi
ya kutaka kumtoa roho ndugu yako?
Akauliza Austin Julieth akaendelea
kulia
“Julieth kulia hakutakusaidia
kitu.Tafadhali nijibu maswali yangu”
akasema Austin.Julieth akafuta
machozi akamtazama Austin na
kusema
“Machozi yamenitoka kutokana
na haya maswali uliyoniuliza.Nafsi
yangu imeumia sana hasa
nikikumbuka mambo maovu
niliyoyafanya” akanyamaza akafuta
machozi na kuendelea
“Boaz hakunitafuta bali mimi
ndiye niliyemtafuta” akafuta tena
,machozi na kuendelea
“Mimi na Marcelo baba yetu ni
mmoja lakini mama tofauti.Baada ya
mama yake Marcelo kufariki dunia
baba yake akamuoa mama
yangu.Baba alimpenda mno Marcelo
na alimpatia kila kitu,elimu bora nje
ya nchi lakini mimi sikubahatika hata
kupanda ndege lichaya utajiri
mkubwa wa baba.Upendo huu
mkubwa kwa Marcelo ulianza kujenga
chuki kati yetu na tulianza kumchukia
Marcelo.Siku moja mama alibahatika
kuusoma kwa siri wosia aliouandika
baba na katika wosia huo karibu mali
zote zilikuwa za Marcelo.Nilimuuliza
mama kwa nini baba afanye vile ndipo
akanieleza siri ambayo sikuwa
nikiifahamu hapo kabla.Aliniambia
kwamba yule hakuwa baba yangu bali
mimi ninaye baba yangu.Baada ya
kumzaa Marcelo Dr Richard hakuwa
tena na uwezo wa kuzaa hivyo
ikalamzimu mama kutoka nje ya ndoa
kutafuta mtoto na kitendo hicho
kilimchukiza mno baba na ndiyo
sababu ya kumpendelea zaidi Marcelo
kuliko mimi.Baada ya kuufahamu
ukweli huo ndipo na mimi nilipoamua
kuingia rasmi katika utafutaji wa pesa
ili niwe na maisha mazuri .Boaz
alikuwa ni rafiki yake baba na alikuwa
akija nyumbani mara kwa mara hivyo
nikaanza kujiweka karibu naye na
hapo ndipo uhusiano wetu
ulipoanza.Nilianza kujifundisha
biashara ya dawa za kulevya .Nilianza
kwa kubeba na kufikisha mzigo
mahala nilikoagizwa na kisha kulipwa
fedha nyingi.Nilivutiwa na biashara
hiyo kwani kwa muda mfupi nilianza
kuwa na mafanikio na nikaamua hiyo
iwe ndiyo kazi yangu ya
kudumu.Hivyo ndivyo nilivyokutana
na Boaz na tukawa na mahusiano hadi
hii leo.Nilikubaliana na mpango wa
Boaz wa kumuua Marcelo kwa lengo
la kurithi mali kwani Marcelo hadi leo
hii bado hajausoma wosia alioachiwa
na baba yake na bado hafahamu kama
mimi na yeye si ndugu wa
damu.Maswali yako yamenichoma
moyo sana na kuamia kukueleza
ukweli wote.Sijawahi kumweleza mtu
yeyote mambo haya niliyokueleza”
akasema Julieth na kufuta machozi
“Kwa nini ukafanya maamuzi
haya Julieth.Huoni kwamba
umeyaharibu maisha yako mwenyewe
kwa kujiingiza katika biashara ya
dawa za kulevya?Boaz
alikundanganya sana .He was just
using you.Amekutumia kujinufasha
yeye mwenyewe.Unadhani Marcelo
angefariki ungezipata mali
zake?Umejidanganya sana Julieth”
“I’m sorry Austin.Please help
me.Ni wivu tu na tamaa ya mali
vimeniponza” akasema
Julieth.Marcelo akamtazama kwa
zaidi ya dakika tatu na kusema
“Nilijawa na hasira nawe sana
baada ya kufahamu kuwa wewe ni
chanzo cha mahangaiko ya Marcelo
.Amenusurika kuuawa kwa risasi na
chanzo ni wewe.Ukweli huu
ulionieleza pamoja na kukiri kosa lako
ninatamani nikusaidie.Bado ni
msichana mdogo na mrembo pia na
unaweza ukabadilikana ukaachana na
biashara hizi haramu ukafanya
biashara za halali.Nikikutazama
naiona picha ya mdogo wangu
anaitwa Linda ambaye ni makamu
yako na yeye alikuwa amefungwa
nchini China kwa sababu ya biashara
hiyo ya dawa za kulevya.Nimefanya
juhudi na kufanikiwa kumtoa na sasa
ninamtengenezea maisha
mapya.Sitaki ajihusishe tena na
biashara hii haramu.Natamani sana na
wewe nikusaidie kama mdogo
wangu”
“Mdogo wako anaitwa Linda
nani? Akauliza Julieth
“Linda January”
“Linda January ni mdogo wako?
“Ndiyo.Unamfahamu?
“Linda aliwahi kuwa na
mahusiano na Boaz.Huyu mzee ndiye
sababu ya Linda kufungwa.Ana
kawaida ya kutafuta wasichana
wadogo akajenga mahusiano nao
akawadanganya kwa pesa na vitu
vizuri na mwishowe huwaingiza
katika bisahara ya dawa za
kulevya.Linda ni mmoja wa
waathirika wa mchezo huo.Wasichana
wengi wamepotea kwa sababu ya
huyu mzee” akasema Julieth na sura
ya Austin ikabadilika
“Haya unayonieleza ni ya kweli
Julieth?
“Kweli kabisa.Kukamatwa kwa
Linda ulikuwa ni mpango wa Boaz na
aliwahi kunieleza kwamba anataka
msichana yule aozee gerezani na
hivyo akasuka mpango ili Linda
akamatwe” maneno yake ya Julieth
yakazidi kumpandisha hasira Austin
“ Austin” akaita Julieth
“Toka jana nilipoletwa hapa
nimejiuliza maswali mengi ni vipi
iwapo ningekamatwa na polisi ?
Nimetafakari sana kuhusu biashara hii
niifanyayo na maisha yangu kwa
ujumla.Nimeamua kubadilika na
kuachana na maisha haya ninayoishi
.Niko tayari kuwaeleza kila kitu
kuhusu Boaz na hata kama mkitaka
naweza kuwapeleka sehemu ambako
Boaz na wenzake huwa wanajificha na
huko ndiko huwa wanaficha mizigo
yao ya dawa za
kulevya.Nitawaonyesha kila kitu
lakini kwa sharti moja tu mniachie
huru na mnihakikishie
ulinzi.Nakuomba sana Austin nisaidie
kama mdogo wako.Usiniache
nikapotea tafadhali.” Akaomba
Julieth.Bado sura ya Austin ilikuwa na
hasira
“Nitaangalia namna ya
kukusaidia lakini ni lazima umueleze
ukweli wote Marcelo na yeye ndiye
atakayeamua kukusamehe au
vipi.Hata hivyo naahidi kukusaidia
kwani umenisaidia sana kufahamu
kuhusu mdogo wangu Linda.Sikujua
kama mtu niliyemuheshimu kama
baba yangu ndiye aliyemtenda hivi
mdogo wangu.Boaz ameniumiza
sana” akasema Austin na kumpeleka
Julieth jikoni akachukua chakula na
kumrejesha katika chumba
alimofungwa.
“Alichokisema Julieth kimenistua
sana.Kumbe ni Boaz ndiye
aliyeyaharibu maisha ya Linda.Kwa
nini lakini? How could he do that to
me? Mambo haya yote niliyomfanyia
hii ndiyo shukrani yake? Ameniumiza
mno.Bahati yake ninaumwa lakini
ningekuwa mzima angenena lugha
kumi na mbili leo.Ningemtesa mno
leo.Hata hivyo nitamkabidhi
Amarachi kazi hiyo amfundishe
adabu.Huu ni mwisho wa enzi zake
za kuishi kama malaika na sasa
anaanza kuishi kama
shetani.Nitahakikisha anaujutia ubaya
wake wote alioutenda.Ameharibu
maisha ya wasichana wengi.Yeye na
mwanae lazima wajute kunifahamu”
akawaza Austine akiwa na hasira
zisizomithilika.
SEHEMU YA 4 :SEASON 5
Amarachi ambaye siku zote ni
mwanamke jasiri alishindwa kuzuia
machozi kumtoka kwa hali
aliyomkuta nayo Job.Alikuwa
amelazwa katika mtumbwi kuu kuu
na hakuwa na fahamu huku akiwa na
majeraha kichwani na mwilini.Hali
yake ilikuwa mbaya.
“Who did this to you Job?
Akasema Amarachi huku akilia.
“Nyamaza kulia Amarachi.We
have to help him !!! akasema Marcelo
na kumpima Job
“He’s still breathing !! akasema
Marcelo na kumchoma Job sindano
“Tunatakiwa kumpeleka
hospitali haraka” akasema Marcelo
.Wavuvi wakambeba Job hadi katika
gari la Amarachi kisha Amarachi
akawapa shilingi laki mbili
akawashukuru kwa msaada mkubwa
walioufanya
“Tunampeleka hospitali ipi?
Akauliza Amarachi
“Tumpeleke katika hospitali
yangu.Tukimpeleka katika hospitali
nyingine watahitaji taarifa ya polisi”
akasema Marcelo na kumuelekeza
Amarachi iliko hospitali yake
“Kwa nini Job aliamua kufanya
kazi peke yake bila kutushirikisha
hadi yakamkuta haya? Angeweza hata
kuuawa.Please Lord save this
man.He’s very important to me”
akasema Amarachi kwa sauti ndogo
Waliwasili katika hospitali ya
familia ya Marcelo ambayo ni maalum
kwa ajili ya kutibu wagonjwa wa
maradhi ya saratani.Kwa takribani
dakika tatu Dr Marcelo alizungukwa
na madaktari na wauguzi wa hospitali
ile wakimkumbatia na kumpa pole
huku wengine wakilia.Hawakuamini
kumuona tena Marcelo pale
hospitali.Marcelo akawafahamisha
kwamba amekuja na mgonjwa katika
gari ambaye ana hali mbaya.Haraka
haraka Job akashushwa garini na
kukimbizwa katika chumba cha
wagonjwa mahututi akaanza
kushughulikiwa
“Amarachi tafadhali usihofu.Job
atapata huduma nzuri kwani hapa
kuna madaktari wazuri sana.”Marcelo
akamwambia Amarachi aliyekuwa
amekaa nje ya chumba alimoingizwa
Job
“Marcelo siwezi kuacha kuwa na
hofu.Job ni mtu wangu wa muhimu
mno.Toka tumefahamiana hii ni mara
ya kwanza amenifanya niumie.Kwa
nini afanye hivi? Kwa nini afanye kazi
kimya kimya bila kutushirikisha
wenzake” akauliza kwa hasira
Amarachi
“Punguza hasira
“Relax Amarachi.Job will be
fine.Endelea kupumzika hapa mimi
nakwenda kuungana na madaktari
kumuhudumia Job” akasema Marcelo
na kuingia ndani ya chumba cha
wagonjwa mahututi
“Nafahamu Job ana hasira nyingi
dhidi ya wale waliomtenda ubaya na
kumsababisha aishi maisha magumu
kwa miaka kadhaa lakini hakutakiwa
kufanya jambo hili kwa haraka namna
hii.Watu hawa wanapaswa
kuwaendea kwa akili nyingi.They are
very smart and animals.Alinitaka
nijenge urafiki na dogo Bill ili niweze
kumchunguza lakini mpaka sasa
sijafanikiwa kugundua lolote kwani ni
watu waangalifu mno na wana mbinu
nyingi za kujificha.Amefanya kosa na
endapo akiamka nitamnasa vibao kwa
hili alilofanya” akawaza Amarachi na
kuchukua simu akampigia Austin
“Hallo Amarachi.Nipe taarifa za
huko? Mmefanikiwa kumuona
Job?akauliza Austin
“Tumefanikiwa kumpata .He’s in
bad shape.Ana majeraha makubwa
kichwani na mwilini.Mpaka sasa bado
hajapata fahamu na imetulazimu
kumleta katika hospitali ya Dr
Marcelo.Hivi sasa ameingizwa katika
chumba cha wagonjwa mahututi
madaktari wanajitahidi kuokoa
maisha yake.” Akasema Amarachi
“Thank God.Tumuombee kwa
Mungu aweze kupona kwani
tunamuhitaji sana.Kwa kuwa tayari
yuko katika uangalizi wa madaktari
muache Marcelo aendelee
kumshughulikia wewe rudi huku
kuna kazi za kufanya.” Akasema
Austin
“Vipi kuhusu Marcelo,are you
sure he’ll be safe here alone? Akauliza
Amarachi
“Marcelo is safe.Mtu aliyekuwa
anamtafuta ni Boaz ambaye tayari
tunamshughulikia kwa hiyo yuko
salama ingawa bado ataendelea kukaa
nasi hapa hadi hapo
tutakapohakikisha kwamba hakuna
tisho lolote la usalama kwake.”
Akasema Austin
“Sawa Austin ninakuja hapo
nyumbani muda si mrefu” akajibu
Amarachi na kukata simu.Sekunde
kadhaa baada ya kuongea na
Amarachi ikaingia simu toka kwa rais
“Shikamoo mzee” akasema
Austin
“Marhaba Austin .Unaendeleaje?
“Naendelea vizuri sana mzee.”
“Good to hear that.Wengine wote
wako salama? Akauliza rais
“Wako salama isipokuwa
Job.Amepatwa na tatizo na hali yake si
nzuri”
“Amepatwa na nini Job?
“Jana usiku tukiwa kule
nyumbani tulimuacha hapa na
akaondoka bila kututaarifu
amekwenda wapi na hajarejea hadi
asubuhi ya leo tulipopokea simu toka
kwa wavuvi waliotujulisha kwamba
Job ameokotwa ufukweni akiwa
hajitambui.Hivi sasa anatibiwa katika
hospitali ya Dr Marcelo.Tunasubri
apate nafuu ili atueleze kilichotokea”
“Pole sana .Pamoja na hayo yote
yanayoendelea kutokea nawasihi
msikate tamaa endeleeni kupambana
.Endapo kuna msaada wowote
mnaouhitaji toka kwangu msisite
kunijulisha mara moja.Vipi kuhusu
vipimo kuna taarifa zozote?
“Hapana mzee bado hakuna
taarifa zozote .Watakapokuwa tayari
tutajulishwa na tutakukabidhi wewe
majibu hayo.”
“Thank you Austin.Make sure
I’m the first one to see the results”
akasema rais wakaagana akakata
simu.
“Rais hajagusia chochote kuhusu
Mukasha ina maana hana taarifa
zozote za Mukasha kukatwa sikio? Au
mtu aliyemchukua Job hakuwa
Mukasha? Ngoja tusubiri Job
azinduke atueleze ukweli.” Akawaza
Austin
Alipomaliza kuzungumza na
Austin rais akazitafuta namba fulani
katika simu yake akapiga
“Hallo Mr Persident” ikasema
sauti ya upande wa pili
“You did a huge mistake last
night.You didn’t kill him.He’s alive”
“What ?! That’s not true Mr
president.Mimi mwenyewe
nilihakikisha amekata pumzi
nikawatuma vijana wakamtupe
.Nashangaa kusikia eti yuko hai
.That’s a miracle then”akasema mtu
yule aliyekuwa akiongea na rais
simuni
“He’s alive but in critical
condition.Nimetoka kuzungumza na
mwenzake muda si mrefu na
amenieleza kuwa Job yuko hai bado”
“ Kwa hiyo tufanye nini mzee?
“Kwa sasa msifanye chochote
,tusubiri kwanza maendeleo ya hali
yake halafu tutajua nini cha kufanya
lakini safari nyingine ukipewa kazi
jitahidi kuifanya kwa ukamilifu
wake.Watu kama hawa si wa kufanyia
mchezo hata kidogo.They have more
lives than a cat” akasema rais
“Sawa mzee ninasubiri taarifa
toka kwako” akasema yule jamaa
“One more thing” akasema rais
“Tunatakiwa kumundoa
Mukasha haraka sana.Huyu ni mtu
hatari mno kwetu kwa sasa”
Kimya kikapita na yule mtu
aliyekuwa anaongea na rais akasema
“Mr President,Mukasha he’s one
of ours.”
“I know that, lakini kwa sasa ni
mtu hatari mno kwetu .Bado
hafahamu kama mimi na wewe ni
washirika ingawa mimi nafahamu
mambo yake yote.Hawa vijana tayari
wameanza kumchunguza na
ninakuhakikishia vijana hawa ni
hatari mno na wakidhamiria jambo
lazima walifanikishe.Lengo lao ni
kumchimba Mukasha na kuufahamu
mtandao wake wote kwa hiyo lazima
tujihami mapema kwa kumuondoa
Mukasha.Tukimuondoa Mukasha na
tutamuondoa pia yule kijana kule
hospitali ndipo tutakapopumua kwani
yule ndiye aliyeelezwa mambo mengi
na Mukasha.We don’t have to wait for
the situation to get ugly,we have to
clear everythig now!! Akasema rais
“Nimekuelewa mzee.Toka jana
usiku Mukasha alipelekwa hospitali
kutibiwa jeraha na kwa taarifa
nilizonazo alikuwa amelazwa.Niachie
suala hili nilishughulikie haraka
iwezekanavyo”
“Thank you.Nitawasiliana nawe
baadae kukupa taarifa nitakazokuwa
nimezipata” akasema rais na kukata
simu
SEHEMU YA 5; SEASON 5
Amarachi ashuka garini akaingia
sebuleni akakutana na Austin.Sura
yake ikaonyesha wazi alikuwa
mawazo mengi.
“Habari za hapa? Akauliza
Amarachi
“Habari za hapa nzuri .Vipi huko
utokako? Kuna taarifa zozote za
maendeleo ya Job?
“Mpaka naondoka hakukuwa na
taarifa zozote bado madaktari
wanaendelea kumtibu.Why Job did
that? Akauliza Amarachi na machozi
yakamtoka,Austin akainuka na
kumfuata sofani akamshika bega
“Nitazame usoni Amarachi”
akasema Austin.Amarachi akafuta
machozi na kumtazama Austin
“Nafahamu umeumizwa kuhusu
Job hata mimi nimeumizwa pia lakini
hatufahamu bado kwa nini aliamua
kufanya vile alivyofanya bila
kutushirikisha? .Nafahamu lengo lake
kubwa ni kumpata mwanae Millen na
nimekwishamuadi kuwa lazima
tutampata mwanae sasa sijui nini
kilitokea akafanya vile
alivyofanya.Hata hivyo tunapaswa
kumuombea ili apone na kutueleza
nini hasa kilichotokea.Kuna mengi
anayotakiwa kutujibu.Usiwaze sana
he’s in good hands and he’ll wake
up.Kitu kikubwa unachopaswa
kukitambua ni kwamba tuko katika
mapambano na na kuumia kwa
mmoja wetu hakuwezi kuturudisha
nyuma.Lazima tuliobaki tuendeleze
mapambano kwa niaba
yake.Tulikuwa watatu na sasa
tumebaki wawili kwa hiyo lazima
tuifanye kazi ya watu
watatu.Amarachi I need you more that
ever.I need you to focus.Maumivu
yote tunayoyapata kwa kilichomtokea
Job tuyaelekeze katika kuikamilisha
kazi iliyoko mbele yetu.Umenielewa
Amarachi ? akauliza Austin .Amarachi
akafuta machozi na kusema
“Nimekuelewa Austin.Lets do
this for Job”
“Good” akasema Austin na
ukimya mfupi ukapita
“Sina hakika kama nimekwisha
kueleza historia yangu” akasema
Austin
“Job alinieleza kwa ufupi sana”
akajibu Amarachi.Austin akamueleza
Amarachi historia yake hadi
alipokombolewa na Boaz toka katika
mikono ya Alshabaab
“Kwa hiyo Boaz ni mtu ambaye
binafsi namuheshimu sana kama baba
yangu.Kama ilivyo katika filamu
ambapo kuna mambo tusiyoyajua
yanafanyika nyuma ya pazia,hata
mimi na Boaz kuna mambo
yaliyokuwa yanaendelea nyuma ya
pazia ambayo sikuyafahamu”
akanyamaza kwa muda halafu
akaendelea
“baada ya Boaz kunikomboa toka
kwa Alshabaab alinipeleka kuishi
Afrika kusini na nikawa msimamizi
mkuu wa miradi yake yote.Nikiwa
Afrika kusini Boaz alianzisha
mahusiano na mdogo wangu Linda
na baadae akamuingiza katika
biashara ya dawa za
kulevya.Kukamatwa kwa Linda
nchini China ulikuwa ni mpango wa
Boaz.Amekuwa na tabia ya
kuwatumia wasichana wadogo katika
biashara zake za dawa za kulevya na
mdogo wangu Linda ni mmoja wa
waathirika .Jambo hili limeniumiza
sana.Huyu Boaz ni mnyama mno”
akasema Austin
“Umemuhoji akakiri ? akauliza
Amarachi
“Hapana sijamuhoji.Julieth ndiye
aliyenieleza kila kitu”
“Julieth? Akauliza Amarachi
“Ndiyo .Amenieleza kila kitu
kuhusu chanzo cha mahusiano yake
na Boaz na kwa nini anataka kumuua
Marcelo”
“Do you believe her?
“Yes I do .”akajibu Austin
“Kumbe yule baba ni shetani
mkubwa.Muonekano wake na
matendo yake haviendani kabisa”
“Ni mtu anayejitahidi sana
kuficha maovu yake lakini arobaini
yake imewadia na safari hii hataweza
kuchomoka katika kabali yangu.”
Akasema Austin
“Kile kitabu tulichokipata jana
umekipitia? Amarachi akauliza
“Hapana bado
sijakipitia.Tutakipitia baadae lakini
kwa sasa ni wakati wa kuzungumza
na Boaz.” Akasema Austin na
kuongozana na Amarachi kuelekea
katika chumba alimofungwa
Boaz.Chumba kilikuwa giza ,taa
ikawashwa na Boaz aliyekuwa
amelala akaamka.Alistuka mno
alipojikuta akitazamana na Austin
“ Austin ??.. Boaz akasema kwa
mstuko.Hakuamini alichokiona mbele
yake
“I cant believe this.Is that you my
son? Akauliza
“Hallow Boaz.Hii si ndoto bali ni
kitu cha kweli kabisa
unakishuhudia.Its me Austin”
akasema Austin akavuta kiti na kuketi
akamuamuru Amarachi amfungue
Boaz mikono akainuka na kukaa
akamtazama Austin na kutikisa
kichwa
“Bado siamini macho yangu
kama ni wewe kweli Austin ndiye
uliyenifanya hivi.Nimekukosa nini
Austin hadi umenifanyia hivi?Shetani
gani amekuingia na kukudanganya
unifanyie hivi kijana wangu?
Nilikutoa katika mikono ya Alshabaab
lakini haya ndiyo malipo yake?
akauliza Boaz
“Maswali yako hayatakusaidia
kitu Boaz,tayari umeingia katika
himaya yangu na huu ni mwisho wa
enzi zako za kuishi kama malaika na
sasa utaanza kuishi kama
shetani.Unapoingia katika himaya
yangu haijalishi ni ndugu yangu au
nini umenifanyia,unapata nafasi ya
kunifahamu vyema mimi ni nani
hasa.Katika himaya yangu I’m a
monster.” Akasema Austin .Uso wa
Boaz ulionekana kuloa jasho
“Are you trying to scare me? Are
you starting a war with me son?
Please don’t do that.You don’t know
me at all.baada ya kugundua kwamba
wewe ndiye uliye nyuma ya ujinga
huu nakuomba unifungue niende
zangu.Nakuambia hivi angali
mapema na endapo utanifungua
nitakusemehe lakini endapo
utaendeleza ujinga wako huu Iswear
you’ll pay for this!!! Akafoka
Boaz.Austin akatabasamu kidogo na
kusema
“Mr Boaz,nilikwambia toka awali
kwamba tayari umeingia katika
himaya yangu na huna uwezo wa
kuniamuru chochote.I’m the boss
here.Wakati wako umefika and I’ll
destroy you completely” akasema
Austin
“ Unataka kunifanya
nini,kuniua? Kwa wema wote huu
niliokutendea unataka kuniua? What
kind of a man are you? I gave you
good life,I gave you my daughter and
this is how you repay me?? Akafoka
Boaz.Austin akavua fulana aliyokuwa
amevaa
“Just the day before I was shot
four times.Risasi moja ilipita karibu
sana na moyo wangu na lengo la
aliyenipiga risasi hizo ni kuniua na
kwa bahati mbaya kwake na nzuri
kwangu mkono wake ulicheza kidogo
hivyo lengo lake
halikutimia.Hayakuwa mapenzi ya
Mungu niondoke duniani hadi pale
nitakapokuwa nimekamilisha zoezi la
kuifanyia usafi nchi hii yenye watu
wachafu kama wewe !! akasema
Austin huku akimtazama Boaz kwa
hasira
“Unafahamu nani aliyetaka
kunitoa uhai? Its yor daughter
Maria.You are the family of monsters
!!
Boaz akaonyesha mshangao
mkubwa
“Maria ndiye aliyekupiga risasi”
akauliza
“Ndiyo .Binti yako mpendwa
ndiye aliyetaka kuniua”
“I cant believe you.Maria katu
hawezi kufanya kitu kama hicho.Si
Maria huyu ninayemfahamu mimi”
akasema Boaz
“Tuachane na hayo ya Maria
nataka unieleze kwa nini uliyaharibu
maisha ya Linda?
“Linda? I don’t know any Linda”
akasema Boaz
“Linda mdogo wangu.Wakati
ukifahamu kabisa kwamba sina
mpango wa kurejea Tanzania
ukamrubuhi ,ukamchezea utakavyo
na haikutosha hadi ukamuingiza
katika biashara ya dawa za kulevya na
mwisho ukasuka mpango
akakamatwa nchini China na dawa za
kulevya akafungwa gerezani.Kwa nini
ukamfanyia hivi yule binti ambaye ni
sawa na mwanao? Kwa nini umekuwa
na roho ya kikatili kiasi hicho?
Akauliza Austin
“Austin I don’t know any
Linda.Simfahamu msichana yeyote
anayeitwa Linda.Nakumbuka uliwahi
kuniambia kwamba unaye mdogo
wako simkumbuki jina na ukaniambia
nijapo Tanzania niwe napita
kumtazama na kumsaidia kama ana
tatizo.Sikuwahi kuonana naye
nashangaa leo hii unanituhumu kwa
kumuharibia maisha yake.Huu ni
ukosefu mkubwa wa adabu
Austin.Najuta kwa nini nilipoteza
fedha zangu nyingi kukukomboa mtu
kama wewe usiye na shukrani hata
chembe.Sikujua kama ninafuga nyoka
ambaye sasa umegeuka na kuniuma
mwenyewe” akasema Boaz
“Tayari nafahamu kila kitu Boaz
ila ninachotaka ni wewe ukiri kwa
mdomo wako kitu ulichokifanya
lakini kwa kuwa unaonekana mjeuri
unanilazimisha nikufumbue mdomo
kwa lazima” akasema Austin na
kumtaka Amarachi amfunge Boaz
mikono
“He’s all yours.Make him talk”
akasema Austin na kutoka mle
chumbani.Hakutaka kuona namna
Amarachi anavyoshughulikia Boaz
“Austin what’s the meaning of
this?? Akapiga ukelele Boaz lakini
Austin hakugeuka akaelekea
sebuleni.Muda mfupi tu baada ya
Austin kutoka mle chumbani
ukasikika ukelele mkubwa sana.Boaz
alikuwa analia kama mtoto mdogo.
SEHEMU YA 6; SEASON 5
Silvanus Herman Kiwembe
mkuu wa idara ya usalama wa taifa
aliwasili ikulu kwa mwito wa
rais.Sura yake ilionyesha wasi wasi
mwingi kwani hakujua ni kitu gani
alichoitiwa na rais.Alishuka garini na
kuelekea moja kwa moja ofisini kwa
rais
“Mr kiwembe ,karibu sana” Rais
akamkaribisha
“Nashukuru sana mheshimiwa
rais.habari za siku mbili tatu?
“Nashukuru naendelea
vizuri.Mikiki mikiki ya hapa na pale
lakini naendelea vyema.”
“Nashukuru kusikia hivyo
.Nimeitika wito wako mheshimiwa
rais” akasema Silvanus au Silva kama
alivyozoeleka.
“Ahsante kwa kufika kwa wakati
Silva.Kuna jambo mimi na wewe
nataka tulizungumze lakini si
hapa.Tutatoka kidogo kuna mahala
tutakwenda.Mwambie dereva wako
aondoke kwani tutakuwa na siku
ndefu kidogo” akasema rais na sura
ya Silva ikabadilika na kuonyesha
wasi wasi mwingi,akachukua simu
akampigia dereva wake na kumtaka
aondoke.
Silva akaongozana na rais
wakaelekea katika helkopta wakaingia
na helkopta ikaondoka bila ya Silva
kujua walikokuwa wanaelekea.Safari
ilikuwa ya kimya kimya .Waliruka juu
ya anga la Dar es salaam kuelekea nje
kabisa ya jiji na taratibu helkopta
ikatua katika eneo lenye majengo
mfano wa kiwanda
kilichotelekezwa.Helkopta ikagusa
ardhi na mlango
ukafunguliwa.Kulikuwa na watu
wanne waliovalia suti nyeusi
waliokuwa wamesimama karibu
kabisa na mahala helkopta
ilikotua,wakaisogelea helkopta , rais
akashuka akiwa ameongozana na
Silva pamoja na makomando wanne
wanaomlinda .
“This way Mr president”
akasema mmoja wa wale jamaa
“Is everything set? Akauliza rais
“Yes Mr president” akajibu yule
jamaa
Rais na wote aliokuwa
ameongozana nao wakaingia ndani ya
mojawapo ya jengo ambalo lilikuwa
tupu.Rais akawaambia wale walinzi
wake wamsubiri pale ila Silva
akamtaka aongozane naye pamoja na
wale jamaa wenye suti.Walitembea
kimya kimya wakashuka ngazi na
kufika katika mlango wa chumba
fulani mmoja wa wale jamaa
akaufungua na rais akaingia Silva
naye akafuata.Ndani kile chumba
kulikuwa na sofa nzuri na meza
ilionekana ni kama ofisi.Silva
akaelekezwa sehemu ya kukaa na
kisha akaamriwa avue
shati.Akamtazama rais kwa mshangao
“Mr President what’s the
meaning of this? Akauliza
“Just do it Silva” akajibu rais
Silva akavua shati na wale jamaa
wakamkagua endapo kuna kifaa
chochote amekivaa kinachoweza
kuwa kinarekodi maongezi,kisha
akaruhusiwa avae shati
“Thank you gentlemen I’ll take it
from here” Rais akawaeleza wale
jamaa wenye suti nyeusi wakatoka.
“What is this place Mr President?
Why am I here? Akauliza Silva.Rais
akamtazama kwa muda na kusema
“Silva nimekuleta hapa kwa ajili
ya maongezi nyeti na ya muhimu
sana.kabla sijakueleza nilichokuitia
hapa nataka nikufahamishe kwamba
wewe ni mmoja wa Alberto’s walio
katika nafasi za juu ambaye mpaka
sasa sijakuondoa katika nafasi
yako.Nimefanya hivi kwa sababu
maalum kwani naamini mimi na
wewe bado kuna mambo tunayoweza
kufanya kwa pamoja licha ya tofauti
zangu na Alberto’s”
“Nashukuru kusikia hivyo
mheshimiwa rais lakini ningependa
kufahamu kuna tatizo gani limetokea
hadi ukaamua kutofautiana na
Alberto’s” akauliza Silva
“Hayo ni mambo yangu binafsi
na siwezi kukueleza
chochote.Kikubwa nilichokuitia hapa
nataka kufahamu kuhusu mwanamke
mmoja anaitwa Yasmin Esfahani.”
Silva akastuka baada ya kusikia
jina lile likitajwa.
“Yasmin Esfahani? Akauliza
“Ndiyo.Nataka taarifa zake,ni
nani,yuko wapi na kwanini mpaka leo
hii sijapewa taarifa zake? Akauliza
rais.Silva akabaki kimya akimtazama
rais
“Nahitaji jibu Silva” akasema rais
“Mheshimiwa rais hilo ni jina
geni kabisa kwangu na nimelisikia
toka kwako leo hii .Sifahamu chochote
kuhusiana na huyo mwanamke.”
Uso wa rais Ernest ukaanza
kubadilika kwa jibu lile la Silva
“Sijabahatisha kuhusu jambo hili
Silva.Nafahamu mwanamama huyu
yuko hapa Tanzania amefungwa
mahala nataka kufahamu ni wapi na
kwa nini amefungwa na mwisho kwa
nini sijataarifiwa?
“Mheshimwa rais ,kama
nilivyokueleza kuwa ni mara yangu
ya kwanza kusikia jina hilo.Idara
yangu haina taarifa zozote za
kumuhusu huyo Yasmini.kama
tungekuwa na taarifa zake
tungekwisha zifikisha kwako .”
“Silva mimi na wewe ni marafiki
na ndiyo maana mpaka sasa
sijakugusa katika nafasi yako kwa
sababu naamini kuna mambo mengi
mimi na wewe tunaweza
kusaidiana.Naomba tafadhali unieleze
kuhusiana na huyu mama”
“Mheshimwa rais sina sababu ya
kukuficha jambo lolote.Sina taarifa
zozote kuhusiana na huyo
mtu.Yawezekana waliokupa taarifa
hizo hawakukupa taarifa sahihi”
“Are you sure you don’t know
anything about Yasmin Esfahani?
Akauliza rais
“Yes I am Mr president” akajibu
Silva.Rais akainuka akabonyeza kitufe
kidogo chini ya meza yake na mlango
ukafunguliwa wakaingia wale jamaa
wanne waliovaa suti nyeusi.
“Silva sisi ni watu wazima na
haipendezi kucheza michezo ya
kitoto.Nimekuuliza swali rahisi lakini
badala ya kunijibu unaleta dana
dana.Muda huo wa kuzungushana
sinao kwa hiyo nakukabidhi kwa
hawa jamaa ambao wataendelea
kukuuliza badala yangu.Hawataki
mchezo give them answers” akasema
rais na kuwageukia wale jamaa
“Gentlemen do your job”
akasema rais na wale jamaa
wakamkamata Silva wakamvua nguo
zote na kumfunga katika kiti.Rais
akakaa pembeni kabisa akishuhudia
kilichokuwa kinaendelea.Mashine
kadhaa zikaingizwa mle ndani kwa
ajili ya kumtesa Silva
“Mr President don’t do this to me
please” akapiga ukelele Silva
“Silva nakupa nafasi ya mwisho
kabla vijana hawajaanza kuifanya kazi
yao.Nieleze kuhusu Yasmin”akasema
rais
“Sifahamu chochote mheshimiwa
rais”akasema Silva na rais akawapa
ishara wale jamaa waendelee na kazi
yao
Silva akamwagiwa maji ya baridi
yaliyochanganyika na barafu halafu
akafungwa kitu fulani katika mkono
wake ambacho kiliunganishwa katika
mashine na mmoja wa wale jamaa
akaiwasha na kuweka kiwango cha
umeme kinachotakiwa na kuruhusu
umeme upite.Silva akauma meno kwa
nguvu huku akitetemeshwa kwa chaji
za umeme.Yule jamaa aliyekuwa
anaongoza mashine akapewa ishara
akazima
“ Uko tayari kuongea? Akauliza
jamaa aliyekuwa amesimama mbele
ya Silva.Bado alikuwa anatetemeka
“Uko tayari kuzungumza ?
akauliza yule jamaa kwa ukali.Bado
Silva hakujibu kitu alibaki
kimya,mashine ikawashwa tena.Baada
ya sekunde kadhaa ikazimwa na Silva
akaulizwa tena kama yuko tayari
kuongea lakini alionekana kutokuwa
tayari kuzungumza chochote.
Baada ya kurudia mara tatu na
kuonekana bado hataki kuzungumza
rais akaomba zoezi lile lisimamishwe.
“Silva kwa nini unakubali
uteseke kiasi hiki? Tell me about that
woman.Hautatoka humu hadi
unieleze kuhusiana na
Yasmin.Endapo hautakuwa tayari
nitakwenda moja kwa moja kwa
familia yako.Hivi tuongeavyo kuna
watu tayari wamewekwa katika kila
sehemu alipo mmoja wa wanafamilia
yako na wanachosubiri ni simu yangu
tu ili wote wachukuliwe na
kupelekwa katika sehemu ambayo
hautawaona tena katika maisha
yako.Kwa nini unataka kuiharibu
familia yako? Nipe ninachohitaji na
uiokoe familia yako” akasema rais na
huku akitetemeka mwili Silva
akapandwa na hasira
“Don…don’t..touch my family or
I’ll kill you!! Akasema Silva
“Kwa sasa hauna uwezo wa
kuniamuru chochote na kama
utaendelea na kiburi chako
nitaiangamiza familia yako.I’m a
father too na inaniuma sana kutaka
kuigusa familia yako lakini sina
namna nyingine ya kufanya
,ningekuwa wewe nisingekubali hata
kidogo familia yangu kuingizwa
katika hatari.” Akasema rais
“You touch my family I’ll kill you
I swear !!! akasema Silva .Rais
akawapa ishara wale jama waendelee
na zoezi lao.Safari hii akafungwa kitu
Fulani katika uume wake na mashine
ilipowashwa akapiga yowe
kubwa.Mashine ikazimwa rais
akamfuata
“Silva answer me !! akasema rais
kwa ukali.Silva hakujibu kitu alikuwa
analia kwa kwikwi.
“Gentlemen this is not
working.I’m taking down his family”
akasema rais kwa hasira na kuchukua
simu yake kabla hajapiga silva
akapiga ukelele
“Stop !!
Rais akamtazama
“Are you ready to talk now?
“Nitakueleza unachokitaka
.Swear to me you wont touch my
family”
“I swear I wont touch your
family” akasema rais na kuwataka
wale jamaa watoke mle chumbani
akabaki yeye na Silva
“Now tell me” akasema rais.Silva
akainamisha kichwa na kusema
“Ni kweli Yasmin Esfahani
anashikiliwa hapa Tanzania kwa zaidi
ya miaka kumi sasa.” Akanyamza
akavuta pumzi ndefu bado mwili
wake ulikuwa unamtetemeka.Rais
akainuka na kumfunika koti.Silva
akaendelea
“ Yasmin ni mwanamke mwenye
asili ya Afrika lakini ana uraia wa Iran
na kwa muda mrefu amekuwa akiishi
nchini Syria.Huyu ni mfuasi wa
kikundi cha kigaidi cha dola ya
kiislamu na inasemekana kwamba ni
mtu hatari.Kikundi hiki cha dola ya
kiislamu kilianza kujitanua katika
bara la Afrika hususan katika afrika
mashariki.Tulipata taarifa za
kiintelijensia toka shirika la ujasusi la
Iran kwamba Yasmin anaishi hapa
nchini na lengo lake ni kuanzisha
kikundi cha dola ya kiislamu
Tanzanian na Afrika mashariki kwa
ujumla.Tulizifanyia kazi taarifa hizo
na kumkamata Yasmin ambaye ni
kweli alikuwa anaishi hapa nchini na
alikuwa amezaa na raia mtanzania
mtoto mmoja na tulimkamata akiwa
katika harakati za kutoroka baada ya
kugundua kwamba
anatafutwa.Hatukufanikiwa kumpata
mtoto wake wala mwanaume
aliyekuwa akiishi naye.Baada ya
kumkamata Yasmin aliwekwa mahala
pa siri ambako hana mawasiliano na
mtu yeyote na hapo ndipo
tunapowahifadhi wale wote
wanaokuwa hatari kwa
taifa.Mheshimiwa rais kuna gereza la
siri hapa nchini ambalo tunalitumia
kuwaficha wale wote ambao
wanahatarisha usalama wa nchi.Ni
mahala pa siri mno na si rahisi kwa
mtu wa kawaida kupafahamu na hata
rais wa nchi huwa hataarifiwi kuhusu
gereza hili la siri.Wote wanaohudumu
katika gereza hili hula kiapo cha
kutunza siri hata ikiwalazimu kufa.”
Akasema Silva na kuinamisha kichwa
“Kwa nini hukunieleza mapema
kuhusu jambo hili hadi
ukanisababisha nikufanyie hivi? Mimi
ndiye mkuu wako na ulipaswa
kunifahamisha kuhusu jambo hili
mapema”akasema rais
“Mheshimiwa rais nisingeweza
kukueleza chochote juu ya jambo hili
kwani niko chini ya kiapo na leo hii
nimevunja kiapo changu kwa sababu
ya kuiokoa familia yangu.Naomba
tafadhali ukumbuke ahadi yako ya
kutoigusa familia yangu”akasema
Silva
“Nimekwisha kuahidi kwamba
sintaigusa famila yako.Nataka
kufahau mnapata wapi fedha za
kuwahudumia hawa mnaowahifadhi
katika hilo gereza? Jambo hili
halifahamiki serikalini na hakuna
fungu lolote katika bajeti kwa ajili ya
kuhudumia gereza hili.Mnamudu
vipi?
“Ni kweli mheshimiwa rais
hakuna fungu toka serikalini kwa ajili
ya kuendesha gereza hili la siri lakini
pesa zote za uendeshaji zinatoka kwa
mataifa makubwa ya nje ya
nchi.Wanaofungwa katika gereza hili
ni watu kutoka mataifa ya Marekani
na Uingereza na hao ndio wachangiaji
wakuu .Kuna watu ambao
wanawaletwa ili kuja kufichwa huku
kwa maisha yao yote au kuja kuuawa”
“Mpaka sasa mnawashikilia
watu wangapi katika hilo gereza?
“Hilo siwezi kukujibu
mheshimiwa rais .Ulitaka kufahamu
kuhusu Yasmin na tayari nimekujibu”
Rais akamtazama Silva kwa
sekunde kadhaa na kusema
“Kuna mambo mawili ambayo
nataka uyafanye.Moja kuna watu
ambao nataka waingie katika hilo
gereza na kupotelea humo kwa
maisha yao yote yaliyobaki.Jambo la
pili namuhitaji Yasmin Esfahani.”
“Mheshimiwa rais ,gereza hili
tunaliongoza sisi pamoja na watu
walioko Marekani kiasi kwamba
hatuwezi kumtoa au kuingiza mtu
yeyote bila ya wenzetu kufahamu na
lazima idhini ya kuingiza mtu itoke
kwao.Kwa umuhimu wa gereza hilo
wameelekeza satelaiti maalum ili
waweze kufuatilia kile kinachofanyika
hapo.Kwa hiyo mheshmiwa rais si
rahisi kumpata Yasmin”
“Namuhitaji Yasmin .Namuhitaji
mno.Ili mimi na wewe tuende sawa
utakwenda kumchukua Yasmin na
watu hao ninaokuambia utawaingiza
katika hilo gereza .Kwa sasa
utaendelea kukaa hapa na jioni ya leo
nitakuja kukuchukua ukanipatie
Yasmin” akasema rais na kutoka
akawaagiza wale jamaa wenye suti
nyeusi waendelee kumlinda Silva
kisha akaondoka.
SEHEMU YA 7: SEASON 5
Austin akiwa sebuleni katika
tafakari nzito,akainua kichwa baada
ya kusikia hatua za mtu akishuka
ngazi.Amarachi alikuwa anashuka
ngazi taratibu huku akiwa
amechafuka damu.Akasimama mbele
ya Austin wakatazamana kwa muda
“He’s ready to talk” akasema
Amarachi
“Thank you Amarachi.Good Job”
akasema Austin huku akinyanyuka
“Go wash yourself.We still have
job to do” akasema Austin huku
akipanda ngazi kuelekea chumbani
alimo Boaz.Akaingia ndani kumkuta
Boaz akigugumia maumivu.Hakuwa
anatazamika usoni alikuwa ameloa
damu
“Uko tayari kuzungumza sasa?
Akauliza Austin
“Siamini Austin kama leo
umenifanyia hivi.You are such a
monster”
“Boaz sina muda wa kupoteza
.Are you ready to talk or not” akauliza
Austin.Boaz hakujibu kitu
“You are not ready.Ngoja
nimuite Amarachi aendelee na zoezi
lake hadi pale utakapokuwa tayari
“No ! No ! No !!.” akasema Boaz
“Tafadhali usimlete tena yule
mwanamke shetani humu chumbani.
Sitaki kumuona tena” akasema Boaz
“Ukitaka nisimlete tena anza
kunieleza kwa nini uliamua
kuyaharibu maisha ya mdogo wangu?
“Nisamehe sana Austin.Ni
shetani alinipitia .Nilikuwa na nia
nzuri ya kumsaidia lakini niliingiwa
na tamaa nikaanza kumtumia
kimwili.Ni yeye mwenyewe
aliyependa kuingia katika biashara ya
dawa za kulevya ili kujiongezea
kipato na sikuona sababu ya
kumkatalia.Austin sina maneno mengi
ya kuongea.Najua nimekukosea sana
na ninachokihitaji toka kwako ni kitu
kimoja tu.Nahitaji msamaha
wako.Naomba unisamehe sana kwa
yote niliyokukosea .Sina neno zuri la
kukuomba msamaha lakini nakuahidi
nitafanya kila niwezalo kuhakikisha
ninayajenga upya maisha ya
Linda.Nakuahidi Austin nitatoa pesa
nyingi kwa ajili ya Linda.Naomba
uniamini” akasema Boaz
“It’s too late Boaz.Tayari
umechelewa mno.Ulipaswa kufanya
hayo kabla sijafahamu kuwa wewe
ndiye uliyeyaharibu maisha ya mdogo
wangu.Kwa nini Boaz ukanifanyia
hivi? Nilikuchukulia kama baba
yangu lakini kumbe ni shetani
mkubwa.Wewe na genge lako
mnaoshirikiana kuwaharibu mabinti
wadogo kwa kuwatumia katika
biashara zenu za dawa za kulevya
mwisho wenu umefika.Nitaonana
nawe tena baadae.Maongezi nawe
hayajamalizika” akasema Austin
akiinuka
“Austin!! Austin !!!! ..akaita Boaz
lakini Austin hakugeuka
“Amarachi amefanya kazi nzuri
sana.Kweli huyu ni jembe la kazi.Sasa
ni zamu ya Maria” akawaza Austin na
kushusha pumzi.Akashuka sebuleni
na kumkuta Amarachi tayari
amekwisha badili mavazi
“Umefanya kazi nzuri sana
Amarachi.Thank you” akasema
Austin
“Siku ya leo imenikumbusha
maisha yangu ya msituni chini ya
Boko haram.Walinifundisha mambo
mengi hata namna ya kumfanya
mateka hata awe mgumu kiasi gani
aongee.Kwa hiyo Austin kama kuna
mtu yeyote ambaye unahitaji aongee
nikabidhi mimi na ninakuahidi lazima
ataongea tu labda awe ni bubu”
akasema Amarachi .Ile sura yake
iliyojaa tabasamu ilikuwa imetoweka
na sasa alikuwa na sura ya kazi.
“Good.Ni zamu ya Maria sasa”
akasema Austin na kutazamana na
Amarachi
“Kwa nini usiniache
nikamalizane naye? Yule alikuwa
mpenzi wako na unaweza kuingiwa
na moyo wa huruma .Niache niende
peke yangu” akasema Amarachi
“ Ahsante Amarachi ila
tunakwenda pamoja.” Akasema
Austin
“Are you sure? Amarachi
akauliza
“ Yes” akajibu Austin
Amarachi akaufungua mlango
wa chumba alimofungwa Maria
wakaingia,Austin akavuta kiti akaketi
na bila kupoteza muda akasema
“ Sweetheart I’m back”
akanyamaza na kumtazama Maria
“Nilipokuja awali nilikuonya
kwamba nataka ushirikiano na
endapo utashindwa kunipa
ushirikiano wako utanisababisha
nichukue maamuzi ya kutumia nguvu
kitu ambacho sikitaki” akanyazama
tena akamtazama Maria na kusema
“ Nataka unipe namba za siri za
kufungulia hii kompyuta yako”
Maria akamtazama Austin na
kubetua midomo kwa dharau
“Umenisikia Maria? Nataka
namba za siri unazotumia kufungulia
hii kompyuta yako” akasema
Austin.Maria hakujibu kitu
akainamisha kichwa.Austin akainuka
na kumfuata akamshika kichwa
“Look at me Maria.I’m not the
same Austin you loved.Nitakufanyia
kitu kibaya sana endapo utaendelea
kuwa na kiburi” akasema Austin
“Unanitishia kuniua? You are so
fool .I’m not scared of death
Austin.Ninakuhakikishia hata unitese
vipi hutaweza kupata chochote toka
kwangu.Ni bora uniue kuliko
kuendelea kupoteza muda wako”
akasema Maria
“Austin huyu hatakueleza
chochote.Naomba unipe dakika kumi
tu na atasema” akasame Amarachi
.Austin akainuka na kutoka
akamuacha Amarachi na Maria
“Nimekuwa katika mahusiano na
Maria kwa muda wa miaka kadhaa
kwa nini nilishindwa kugundua kama
yuko hivi? Who is she? Akajiuliza
Ausytin huku akishuka ngazi
kuelekea sebuleni.Hakutaka kabisa
kuwepo eneo lile wakati Amarachi
anaifanya kazi yake.
“Nimeishi na nyoka ambaye
alikuwa anatafuta siku ili
animeze.Bahati mbaya kwake Mungu
amenionyesha mapema ni mwanamke
wa aina gani niliyekuwa naye.Hata
hivyo mwisho wao umefika yeye na
baba yake”
Baada ya dakika kumi kama
alivyoahidi Amarachi akarejea
sebuleni akiwa na kompyuta
iliyofunguliwa akaiweka mezani
“ Tayari ameifungua” akasema
Amarachi.Austin akamtazama na
kusema
“Thank you”
“She need a doctor.She’s
bleeding “ akasema Amarachi
“Dah! Ama kweli leo nimekutana
na kifaa.Sijui hawa watu anawafanya
nini hadi wanafunguka na
kuongea.Nashukuru Job
kunikutanisha na huyu mtu muhimu
sana ambaye naweza kumuta ni binti
wa chuma” akawaza Austin na
kumuomba Amarachi akamfungulie
mlango wa chumba alimo Maria
Chumba chote kilitapakaa
damu.Maria hakuwa anatazamika,uso
wake uliloa damu
“Kulikuwa na shughuli pevu
humu ndani.Huyu Amarachi ni
mwanamke wa hatari sana.Ukimpa
nafasi ya kumuhoji mtu unapaswa
uwe karibu vinginevyo anaweza
akaua.Huyu anafaa sana kuwa
mshirika wangu katika kazi” akawaza
Austin na kumwambia Amarachi
amfungue Maria .Akamtaka Maria
asimame lakini hakuweza.Miguu
ilikuwa imetobolewa na kifaa cha
kutobolea vitu vigumu.Amarachi
akamshika mabegani akamvuta hadi
bafuni akamuogesha kisha
akamrudisha chumbani akaenda
kuchukua nguo nyingine akamvisha
kisha kwa pamoja wakasadia kumtibu
majeraha yake na walipomaliza
Austin akasema
“Pumzika kwa sasa.Tutarudi
baada ya muda mfupi kuendelea na
maongezi.Endapo utakuwa kiburi
utapata mateso mara mbili ya haya
uliyoyapata” akasema Austin na
kutoka
“Austin utanisamehe kwa
nilichomfanyia mpenzi wako lakini
naomba ufahamu kwamba
nilichokiona kwa Maria ni kitu cha
kushangaza sana.Ni mwanamke
mwenye uwezo mkubwa wa
kuvumilia mateso
makali.Nilifundishwa namna ya
kutesa nikiwa msituni na Boko Haram
na ndiyo maana nimeweza
kumfungua mdomo lakini watu wa
aina hii ya Maria ni watu waliokula
kiapo cha kutokutoa siri hata
ikiwalazimu kufa.Utanisamehe kwa
hili nitakalolisema bali watu wa aina
hii ya Maria mara nyingi huwa
wanabeba siri kubwa na aidha ni watu
waliobeba siri za nchi au ni
magaidi.Nimeishi na Boko Haram
kwa miaka kadhaa na tukiwa masituni
tulifundishwa namna ya kuficha siri
hata kama itakulazimu kutoa uhai
wako na hiki ndicho nilichokiona kwa
Maria.Anacho kitu kikubwa endapo
tukimbana anaweza akatueleza.”
Akasema Amarachi
“Nakubaliana nawe
Amarachi.Maria ni mtu ambaye
hatujamfahamu bado kwa undani na
tunapaswa kumbinya hadi atueleze
yeye ni nani na tuifahamu siri
aliyonayo.Tuanze kwanza kuipekua
kompyuta yake.” Akasema Austin
Walianza kuipekua kompyuta ile
ya Maria lakini hawakuweza kupata
kitu chochote cha kuwasaidia kwani
mafaili mengi yalikuwa yanahusu
mambo ya kazi.Wakaiunganisha
kompyuta ile na mtandao wa intanet
ili waweze kutazama katika
mawasiliano yake ya barua pepe na
hapo walifanikiwa kugundua kitu
fulani
Katika kumbukumbu ya barua
pepe alizotuma Maria kulikuwa na
barua pepe aliyotuma kwa mtu mmoja
anaitwa Bin Omar iliyosomeka
“Sintaweza kuja huko kama
ulivyotaka , nakwenda Tanzania
.Nimeamua kwenda mwenyewe kumtafuta
mama kwani nimekuwa nikipewa ahadi
mara kwa mara kuhusiana na kumtoa
mama lakini mpaka leo hii hakuna
chochote kilichofanyika.Ninakwenda Dar
es salaam kuna mtu yuko kule atanisaidia
kumtafuta mama”
Baada ya ujumbe huo kukawa na
ujumbe mwingine wa majibu toka
kwa Bin Omar uliosomeka
“Shamim hicho unachotaka
kukifanya ni kitu cha hatari sana.Kuna
watu wetu wenye ujuzi wa kutosha
wanalifanyia kazi suala hilo”
Baada ya ujumbe huo Maria
akajibu
“Nina uhakika na mtu ninayetaka
kumtumia kwa ajili ya kazi ya kumtafuta
mama.Ni mtu mwenye uwezo mkubwa na
amewahi kufanya kazi katika idara ya
usalama wa taifa Tanzania
.Nimemuandaa mtu huyu kwa muda
mrefu na kwa gharama kubwa kwa ajili ya
kunisaidia katika kazi hii.Endapo
nitashindwa kufanikiwa nitakujulisha”
Hakukuwa tena na majibu toka
kwa Bin Omar .Austin na Amarachi
wakatazamana
“Hatimaye mwanga umeonekana
na tunaanza kumfahamu huyu Maria
ni nani” akasema Austin
“ Her name is not Maria.Ana jina
lingine anaitwa Shamim.Amefanya
mawasiliano na huyu mtu anaitwa Bin
Omar siku moja kabla hajaja Dar es
salaam.Huyu Bin Omar ni nani?
Akauliza Austin
“ Katika maelezo yake Maria au
Shamim anaeleza kwamba kuna mtu
wake ambaye atamtumia katika
mpango wa kumpata mama
yake.Hapa nina uhakika alikuwa
anamaanisha wewe.kwa muda huu
wote uliokuwa naye amekuweka
karibu kwa dhumuni la kukutumia
katika mpango wake.Mwanamke
mshenzi sana huyu!!! Akasema
Amarachi
“How could I be so stupid? Kwa
nini kwa muda huu wote niliokuwa
naye sijabahatika kugundua kama
Maria ni mtu hatari? Hakukuwa na
hata chembe ya mapenzi kati
yetu,kumbe ulikuwa ni uongo
mkubwa na alikuwa anataka
kunitumia kwa manufaa
yake.Imeniumiza sana kwa kuwa
mjinga kiasi hiki na kushindwa
kugundua hili” akasema Austin na
kuinamisha kichwa
“Huyu mama yake ni nani hasa?
Yuko wapi na kwa nini? Maria
hajawahi kukutamkia chochote
kuhusu mama yake? Amarachi
akamuuliza Austin aliyekuwa
ameinamisha kichwa akainua kichwa
na kumtazama Amarachi na kusema
“Wote wawili Boaz na mwanae
walinihakikishia kwamba mama yake
Maria alifariki angali Maria akiwa
bado mdogo .Kwa mujibu wa maelezo
yao ni kwamba Maria hakuwahi
kumuona mama yake.Kumbe huu
wote ulikuwa uongo mkubwa .Hii
familia imekuwa ikiishi kwa uongo
mkubwa lakini mwisho wao
umewadia.Twende kwa Maria
akatueleze ukweli” akasema Austin
wakaelekea chumbani kwa Maria”
akasema Austin wakaelekea chumbani
kwa Maria.Austin akavuta kiti na
kuketi karibu na Maria akamtazama
na kusema
“kwa mara ya kwanza katika
maisha yangu niliyafurahia maisha ya
mapenzi baada ya kukutana
nawe.Nilijua nini maana ya kupenda
na kupendwa.Nilikupenda kwa moyo
wangu wote na nilikuwa tayari
kuacha kila kitu kwa ajili ya kuwa na
wewe.Niliamini wewe ndiye
mwanamke yule ambaye umeumbwa
kwa ajili yangu na tayari nilikwisha
amua kuanza maisha mapya ya
familia nikiwa nawe.Nilikupenda
kweli toka moyoni lakini kumbe
nilikuwa namwaga maji ndani ya
pakacha.Wakati nikijitoa kukuonyesha
namna gani ninakupenda kumbe
mwenzangu ulikuwa unanifanyia
maziongaombwe.Ulikuwa na malengo
yako.Hili limeniumiza mno.How
could you do that to me Maria? How
could you be so cruel? Akauliza
Austin huku akimtazama Maria kwa
macho makali
“Sihitaji maelezo yoyote toka
kwako kwani ukweli wote tayari
ninaufahamu .Ninachohitaji toka
kwako kwa sasa ni majibu sahihi ya
maswali yangu.” Austin akamtazama
Maria kwa hasira kisha akauliza
“Tumekuta mawasiliano ya
barua pepe kati yako na mtu anaitwa
Bin Omar.Katika mawasiliano hayo
umemwambia Omar kwamba unakuja
Dar es salaam kumtafuta mama yako
ambaye wewe na baba yako
mliniambia kwamba alifariki angali
ukiwa mdogo. Omar anakukataza
kwamba usifanye hivyo kwani kuna
watu wenye ujuzi wanalishughulikia
jambo hilo lakini unamuhakikishia
kwamba kuna mtu yuko dar es salaam
ambaye unamuamini na
umemtayarisha kwa miaka kadhaa
kwa ajili ya kazi hii na una imani
atakusaidia kumpata mama yako na
mtu huyo nina uhakika ulikuwa
unamaanisha mimi na hii
inadhihirisha wazi kwamba hukuwa
na mapenzi yoyote nami bali lengo
lako ni kunitumia kwa ajili ya mambo
yako binafsi.Nataka kufahamu huyo
Bin Omar ni nani na yuko wapi?
Mama yako ni nani na yuko wapi?
Naomba tafadhali unipe majibu ya
maswali yangu ama ukishindwa
kufanya hivyo nitakuharibu Maria na
mipango yako yote ya kuonana tena
na mama yako itakuwa imefikia
ukingoni.” Akasema Austin
Baada ya sekunde kadhaa Maria
akainua kichwa akamtazama Austin
na kuuma meno kwa maumivu kasha
akasema
“It’s ok..Its over.Let’s put and
end to this” akanyamaza akafumba
macho akionekana kuwa katika
maumivu
“Austin you can’t get anything
from me unless we have a deal”
“A deal ? Austin akasema kwa
ukali
“ Yes .A deal “ akajibuMaria
“ Siwezi kufanya makubaliano
yoyote nawe na utanieleza kila kile
ninachokihitaji” akasema Austin
“ Kama umekataa kufanya
makubaliano nami basi hutaisikia tena
sauti yangu .I’d rather die than tell
you anything .The choice is yours”
akasema Maria
“ Naomba unielewe vizuri
Maria,sintofanya makubaliano yoyote
nawe.Kwa sasa kile tulichokuwa
nacho kimekwisha kwa hiyo sioni
tatizo kukuharibu.I’ll destroy you
Maria!! Akasema Austin.Maria
akainamisha kichwa.Amarachi
akamtaka Austin watoke nje ya kile
chumba wazungumze
“ Austin I’m sorry to say this but
she’s not going to tell us
anything.Kama nilivyokueleza awali
kuna siri kubwa anayo huyu Maria na
ili kuifahamu inatulazimu
kukubaliana na anachokitaka.Make a
deal with her.She’d rather die than tell
us what we want” akasema Amarachi
Austin akamtazama Amarachi na
kusema
“ She lied to me,She nearly killed
me.Are you sure you want me to make
a deal with her? Akauliza Austin kwa
ukali.Amarachi akamshika bega na
kusema
“ Nimeishi kwa miaka kadhaa na
watu hatari na magaidi wakubwa na
wamenifundisha mambo mengi na
hata kumtambua mtu ambaye yuko
tayari kufa kuliko kutoa siri na
nikimtazama Maria ni kweli yuko
tayari kufa kuliko kusema chochote”
akasema Amarachi.Austin
akainamisha kichwa akafikiri kwa
muda na kusema
“ Sawa Amarachi .Nakubaliana
na ushauri wako.Ngoja tusikie
anachokitaka Maria” akasema Austin
wakarejea tena ndani ya kile chumba
“ Ok tell me what do you want”
Austin akamuuliza Maria ambaye
aliinua kichwa akamtazama na
kusema
“ Are you sure you want this?
“ Yes tell me what do you want”
akasema Austin.Maria akavuta pumzi
ndefu na kusema
“ Nitakueleza kile unachotaka
kwa sharti moja tu.”
“ Acha kuzunguka sema
unachokihitaji”
“ It’s my mother.Her name is
Yasmin Esfahani.Anashikiliwa na
serikali ya Tanzania .Kuna sehamu ya
siri amefungwa kwa zaidi ya miaka
kumi sasa na mahala alikofungwa
hatatoka kwa maisha yake yote.I want
you to get her out of
there.Ukilifanikisha hilo I promise you
I’m going to tell you a very big secret
that I have” akasema Maria .Austin
akamtazama na kusema
“ Mama yako amefungwa wapi
hapa tanzani?
“Sifahamu ni sehemu gani but
you have many connectins so find out
where she is.Ukimpata utapata jambo
kubwa ila ukishindwa kufanikisha
hilo I’ll die with my secret.Big things
are about to happen so hurry up,give
me my mother and I’ll tell you
everything” akasema Maria .Austin na
Amarachi wakatazamana
“ Let me see what I can do”
akasema Austin halafu wakatoka mle
chumbani
“ Yasmin Esfahani..” akasema
Austin
“ Ni mara ya kwanza kulisikia
jina hili.Ni nani huyu mwanamke?
Kwa nini anashikiliwa mahala pa siri?
Is she dangerous? Akajiuliza Austin
“ Ni wazi lazima atakuwa ni mtu
hatari na ndiyo maana anashikiliwa
mahala pa siri kwa miaka hiyo yote.”
Akasema Amarachi
“ Kama mama yake ni mtu hatari
hata Maria naye ni mtu hatari na watu
wanaoshirikiana nao pia ni watu
hatari pia” akasema Austin
wakaelekea sebuleni
“ Kuna njia moja tu ya kuweza
kumpata huyo mwanamke” akasema
Austin na kuchukua simu yake
akazitafuta namba za simu za rais
akampigia
“ Hallow Austin.Vipi maendeleo
yako? Akauliza rais baada ya kupokea
simu
“ Naendelea vizuri mzee.”
“ Good.Kuna taarifa gani mpya?
Vipi Job anaendeleaje?
“ Bado tunasubiri taarifa toka
hospitali anakotibiwa na nitakujulisha
maendeleo yake.” Akasema Austin na
kunyamaza kidogo kisha akasema
“ Mzee samahani kwa usumbufu
mchana huu”
“ Hakuna usumbufu wowote
Austin.Simu yako muda wowote ni ya
muhimu mno kwangu na hata kama
niko kati kati ya jambo lolote kubwa
nitasimamisha na kuipokea.”
“ Nashukuru mheshimiwa
rais.Nimekupigia kuomba msaada
wako .Kuna mwanamke mmoja
anashikiliwa na serikali ya Tanzania
mahala pa siri anaitwa Yasmin
Esfahani.Ninamuhitaji huyu
mwanamke kwa haraka” akasema
Austin na kumstua sana rais
“ Umesema Yasmin Esfahani?
Akauliza rais
“ Ndiyo mzee. Namuhitaji sana
huyo mwanamke siku ya leo”
akasema Austin na zikapita sekunde
kadhaa kisha rais akajibu
“ Ni nani huyo mwanamke?
Mbona mimi sina taarifa zake?
“ Hauna taarifa zake? Austin
akashangaa
“ Ndiyo Austin sina taarifa zake
zozote.Una hakika mwanamke huyo
yuko Tanzania? Anashikiliwa na
chombo gani cha ulinzi hapa nchini?
Inanishangaza kidogo kwani mimi
ndiye amiri jeshi mkuu na vyombo
vyote vya ulinzi na usalama viko chini
yangu lakini sina taarifa za
kushikiliwa mtu kama huyo hapa
Tanzania.Una uhakika Austin
kwamba mwanamke huyo yuko hapa
nchini?
“ Mheshimiwa rais nina uhakika
mwanamke huyo yupo na
anashikiliwa hapa nchini.Tafadhali
nisaidie kufahamu mahala
alipo,namuhitaji ni muhimu sana
kwangu”
“Unamuhitaji kwa ajili ya
shughuli gani?
“Kuna jambo nalifuatilia na
nitakapolikamilisha nitakufahamisha
lakini ili likamilike lazima nimpate
Yasmin”
“ Jambo hilo unalolichunguza
liko katika ile mipango yetu dhidi ya
Alberto’s? akauliza rais
“ Hapana mheshimiwa rais.Hili
ni suala ambalo halina uhusiano wa
moja kwa moja na Alberto’s
“ Austin nitajaribu kuwauliza
wakuu wa idara za usalama wa nchi
kama kuna idara yoyote
inayomshikilia huyo mwanamama
lakini ningependa kukushauri
kwamba kwa sasa ungeelekeza nguvu
kubwa katika suala kubwa lililo mbele
yetu la kupambana na Alberto’s na
baada ya kulikamlisha hilo
utaendelea na huo uchunguzi wako
mwingine.Tukiweka mambo mengi
kwa mara moja tutapoteza uelekeo
.Umenisikia Austin? Akauliza rais
“Nimekuelewa mzee” akajibu
Austin
“Good.Nitakupigia simu endapo
nitafanikiwa kufahamu chochote
kuhusiana na huyo mwanamke
unayemtafuta” akasema rais na
kukata simu
“This is strange.Inashangaza eti
rais hana taarifa za huyo mwanamke
Yasmin Esfahani.Kama kweli Yasmin
anashikiliwa kwa siri hapa Tanzania
lazima rais afahamu.Au amefichwa
jambo hili?.Kama ni hivyo kwa nini
basi afichwe jambo hili kwa miaka hii
yote?akauliza Austin
“Maria hawezi kutudanganya,ni
kweli mama yake yuko hapa Dar es
salaam kwani amekuja kwa dhumuni
la kumtafuta kwa hiyo tufanye kila
namna ili tumpate.” Akasema
Amarachi
“ Tusubiri taarifa toka kwa rais
kama atafanikiwa kumpata au
vipi.Endapo hatafanikiwa kumpata
itatulazimu sisi wenyewe kuingia
kazini kumtafuta hadi tumpate.Kwa
sasa tuendelee kukipitia kile kitabu
chenye orodha ya wauza unga wote
wakubwa wa hapa nchini “ akasema
Austin
SEHEMU YA 8: SEASON 5
Ernest Mkasa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania alistuka sana
kwa Austin kulitaja jina la
Yasmin.Aliegemea kiti chake kwa
sekunde kadhaa akitafakari baada ya
kumaliza kuongea na Austin simuni
“ Hili sasa ni jambo jipya
limeibuka.Austin amefahamu vipi
kuhusu Yasmin?Anamtaka kwa ajili
ya jambo gani? Kuna nini
anakichunguza? Inawezekana akawa
amefahamu kuhusiana na mpango
wangu wa kumuachia huru Yasmin
na sasa anataka kuuvuruga? Lakini
mpango huu ni wa siri sana na nina
hakika bado hafahamu chochote na
nitahakikisha hafahamu chochote.Yule
kijana anaanza kuonekana kuwa
hatari kwangu.Nisipokuwa makini
anaweza akaikwamisha mipango
yangu mingi .Nadhani kuna jambo
natakiwa kulifanya.Mara tu
atakaponikabidhi majibu ya kipimo
kile cha vinasaba nitalazimika
kumuondoa haraka sana ili asije
kunivurugia huko mbeleni.Natakiwa
kumuwahi kabla
hajaniwahi.Wenz……” Rais
akaondolewa mawazoni na mlio wa
simu akatazama mpigaji na kuipokea
haraka haraka
“ Mheshimiwa rais samahani
kama nimekusumbua ila kuna jambo
nataka kukutaarifu” akasema mtu
aliyempiga simu ile
“ Go ahead” akasema rais
“ Kuna jambo
limetokea.Mukasha ametoweka”
“ What ???Rais akashangaa.
“Nimewatuma vijana wangu
wamfuate Mukasha katika ile hospitali
aliyokuwa amelazwa jana usiku na
kumkosa.Inasemekana aliondoka
usiku bila hata ya kuruhusiwa.Vijana
wakaenda hadi nyumbani kwake na
kumkosa pia yeye na familia yake na
inaonekana wameondoka haraka
haraka kwani nyumba imevurugwa
sana.I’m sorry mr President I failed
you again”
Ukimya mfupi ukapita rais
akasema
“ Sawa nitawatuma vijana wangu
wamsake kokote aliko na
atapatikana.Kwa sasa elekeza nguvu
kwa yule kijana aliyeko hospitali.Kuna
mambo mengi atakuwa ameyafahamu
toka kwa Mukasha kwa hiyo
tunatakiwa tuhakikishe kwa namna
yoyote ile hatoki pale hospitali
salama.Anatibiwa katika hospitali ya
saratani ya Dr Richard
Memorial.Peleka vijana pale.This time
no mistake!! Akasema rais
“Sawa mheshimiwa
rais.Nitafanya hivyo.” Akasema yule
jamaa na kukata siku .Rais akagonga
meza kwa hasira
“ Mambo yanaanza kwenda
ndivyo sivyo.Endapo nitamruhusu
Mukasha atoweke nitakuwa
nimefanya kosa kubwa sana kwani
yule ni mtu anayefahamu mambo
yangu mengi kwa hiyo ni mtu hatari
na anaweza kuwa adui yangu
mkubwa.Nitatumia uwezo wangu
wote kumtafuta Mukasha hadi
nihakikishe nimempata.Sitaki
operesheni yangu ya kusafisha nchi
iiingiliwe na tatizo lolote.”
SEHEMU YA 9; SEASON 5
Job alitolewa katika chumba cha
wagonjwa mahututi baada ya jitihada
za madaktari kufanikiwa ,akapelekwa
katika chumba cha uangalizi
maalum.Hii ilimpa fursa Marcelo
kusalimiana na wafanyakazi na
kupata taarifa fupi kuhusiana na
mambo yanavyokwenda pale hospitali
katika kipindi ambacho hakuwepo
halafu akaelekea ofisini kwake akaketi
kitini na kutabasamu
“ Ni kama muujiza kukalia tena
kiti hiki .Sikutegemea kabisa kuwa
huru tena .Shukrani za pekee
zimuendee Austin na wenzake ambao
wamefanya kazi kubwa usiku na
mchana kuhakikisha ninakuwa
salama.Lakini bado swali moja
linaendelea kuzunguka
kichwani,David Zumo alipataje taarifa
zangu na kuamua kunisaidia?
Akajiuliza na kumkumbuka Monica
“ Nadhani ni wakati sasa wa
kumtafuta Monica na kufahamu
kilichompata na kwa nini sikuwahi
kumuona tena kuja kunitazama?
Kama hakuwa na uwezo wa
kunisaidia kwa nini asingekuja na
kunieleza ukweli kuliko kutokomea
kabisa? Monica ni mtu niliyemuamini
mno hadi nikamshirikisha katika
jambo hili kubwa na nyeti ”
akaendelea kuwaza ,akalifungua
kabati na kutoa kitabu ambacho
hukitumia kuhifadhi namba za simu
za watu mbali mbali akaitafuta namba
ya simu ya Monica kisha akatumia
simu ya ofisi akampigia.
“Hallo” ikasema sauti laini ya
Monica.Marcelo akababaika na ulimi
ukawa mzito kutamka chochote
“ Hallow” Monica akaita tena
“ Hallow Monica “ akasema
Marcelo
“ Who is this? Monica akauliza
“ It’s…it’s me …Marcelo”
“Marcelo? Is that real you?
“ Yes it’s me.How’re you
Monica? Akauliza Marcelo .Monica
akasikika simuni akipiga makelele ya
furaha
“ Huu ni muujiza.Vipi
maendeleo yako? Uko wapi sasa hivi?
” akasema Monica
“Kwa sasa niko hapa hospitali
kwangu na kuhusu maendeleo yangu
ninaendelea vyema.Vipi wewe
unaendeleaje?
“Mimi ninaendelea vyema.Tayari
umetoka mafichoni? Are you sure you
are safe? Monica akauliza
“ Monica uko wapi sasa
hivi?Tunaweza kuonana? Kuna
mambo mengi ambayo nahitaji
kuzungumza nawe”
“ Hata mimi nina mengi ya
kuzungumza nawe lakini kwa muda
huu au kwa siku ya leo kuna jambo
kubwa limenibana na sintaweza
kabisa kupata nafasi ya kuonana nawe
ila kesho asubuhi kabla sijaenda kazini
nitakutafuta ili tuongee.” Akasema
Monica
“ Sawa Monica,tutaonana hiyo
kesho japokuwa nilihitaji sana
kuonana nawe leo”
“ Laiti kama ningekuwa na
uwezo hapa nilipo ningepaa na kuja
kuonana nawe lakini haitawezekana
Marcelo.kesho asubuhi na mapema
nitakutafuta kama
nilivyokuahidi.Kwa heri Marcelo”
akasema Monica na kukata simu
“Nimefurahi kuongea na Monica
na ningefurahi mno endapo
ningeonana naye ana kwa ana kwa
sababu kesho sina hakika kama
ninaweza kupata wasaa wa kuonana
naye tena kwani ninarejea kule kwa
akina Austin.Kwa sasa ngoja niende
nyumbani kwangu nikachukue baadhi
ya vitu vyangu vya muhimu”
akawaza Marcelo akatoka akachukua
mojawapo ya magari ya hospitali
akaelekea kwake.
Alifika nyumbani kwake na
kusalimiana kwa furaha na
mfanyakazi wake wa ndani ambaye
alimwaga machozi mengi baada ya
kumuona tena mwajiri wake .Marcelo
hakutaka kupoteza muda mwingi
hapo akachukua baadhi ya vitu vyake
vya muhimu na kutoka akaondoka
kurejea hospitali.Alipowasili hospitali
akapewa taarifa kwamba wakati
hayupo kuna watu wawili
wasiofahamika walionekana
wakizunguka zunguka katika chumba
alimolazwa Job na walipoulizwa
shida yao waliondoka haraka haraka.
“Job is in great danger.I must
take him ot of here now.Naamini
kabisa watu hao walitumwa kuja
kummaliza” akawaza Marcelo na
haraka haraka akaamuru Job apakiwe
katika gari la wagonjwa na baadhi ya
vifaa alivyovielekeza kisha akaagana
na wafanyakazi wa hospitali ile bila
kuwaeleza anaelekea wapi akaondoka
“ Nimeingia katika ulimwenu
mpya ambao sijauzoea wenye maisha
yaliyojaa hatari nyingi.Kila uchao
uhakika wa kuimaliza siku ni mdogo
kwani kila siku maadui
wanaongezeka.Hawa watu hawana
maisha ya kawaida,hawafurahii
maisha kama sisi.Muda wote wako
kazini kuhakikisha nchi inakuwa
salama.Watu hawa wanastahili
heshima ya pekee kabisa kwani
wanayatoa maisha yao kwa ajili ya
wengine.I’m proud to be just a part of
them” akawaza Dr Marcelo akikatisha
mitaa mbali mbali ya jiji la Dar akiwa
na gari lile la wagonjwa akieleka
nyumbani kwa Job waliko akina
Austin
SEHEMU YA 10: SEASON 5
Ulikuwa ni mshangao mkubwa
kwa Amarachi aliyetoka kutazama
mtu aliyekuwa getini pale alipokutana
na gari la kubebewa wagonjwa
.Haraka haraka akaupeleka mkono
wake ilipo bastora lakini kabla
hajafanya chochote akamuona
Marcelo ndani ya gari akatabasamu na
kufungua geti.Wakasaidiana
kumshusha Job na kumuingiza ndani
“ What happened Marcelo?
Akauliza Austin .Marcelo akamaliza
kumtundikia Job chupa ya maji kisha
akawaeleza kilichotokea hadi
akaamua kumuhamisha Job na
kumleta pale nyumbani.
“Thank you Marcelo for saving
his life.You did a great thing to bring
him here” akasema Austin
“ Vipi maendeleo yako Austin?
“ Naendelea vyema.Mwili
unaimarika kwa kasi kubwa.”
“ I’m glad to hear that .Hata
hivyo ni muda sasa wa kupata dawa
na nimekuja na vifaa mbali
mbali,ninaweza kufungua hospitali ya
muda humu ndani hadi pale
mapambano yatakapokwisha”
akasema Marcelo ,Austin na Amarachi
wakatabasamu.
“ Marcelo kuna mambo mawili
ambayo nataka yafanyike” Akasema
Austin
“ Kwanza utawahudumia wageni
wetu majeraha yao ambayo
wameyapata wakati wakifanyiwa
mahojiano.Mara nyingi huwa ni
vigumu kupata taarifa toka kwa watu
tunaowahoji kwa hiyo hulazimika
kutumia nguvu ndogo hadi kubwa
pale inapobidi ili kupata kile
tunachokihitaji kwa hiyo
usishangazwe na majeraha
utakayoyaona.Ni jambo la kawaida
kwetu.Baada ya hapo kuna jambo la
pili” akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Nilipata nafasi ya kukaa na
kuzungumza na Julieth.Kuna mambo
amenieleza ambayo nadhani
unapaswa kuyafahamu.Tafadhali
naomba umsikilize kwa makini na
baada ya hapo utafanya
maamuzi.Hatima ya Julieth naiweka
mikononi mwako wewe ndiye
utakayeamua nini kifuate.Yule ni
ndugu yako kwa hiyo endapo
ukiamua kumsamehe sisi hatuna
tatizo lolote .Ukiamua kumpoteza vile
vile hatuna tatizo na hilo kwa hiyo
msikilize kwa umakini na utafanya
maamuzi wewe mwenyewe.”
Akasema Austin.Marcelo akainamisha
kichwa kwa muda akawaza na
kusema
“ Austin wewe ni kiongozi
wangu hapa na chochote
utakachonielekeza
nitakitii.Nitazungumza naye na
nitatoa msimamo wangu baada ya
kusikia hicho anachotaka kunieleza.”
Akasema Marcelo kisha akaongozana
na Amarachi wakaelekea ghorofani
kwa ajili ya kuwahudumia akina Boaz
majeraha yao.
“ Ni nani hawa wanaotaka
kumuua Job? Wamefahamuje kama
job yuko pale hospitali? Mtu pekee
tuliyemtaarifu kama Job yuko
hospitalki ni rais sasa hawa jamaa
wamefahamu vipi kama Job yuko
pale? Hii inashangaza sana.Kama
waliweza kumfuata hadi hospitali
kuna uwezekano mkubwa
wakamfuata hadi hapa
nyumbani.Kuna ulazima wa
kuimarisha ulinzi eneo hili” akawaza
Austin akiwa amesimama pembeni ya
kitanda alicholazwa Job,akamtazama
kwa makini na kusema
“ Please Job wake up and tell us
what real happened out th….” Austin
akakatisha mawazo yake baada ya Job
kuchezesha kichwa halafu akafumbua
macho
“ Job !! Job !! akaita Austin kwa
furaha.Job akajitahidi kutaka
kunyanyuka Austin akamzuia.
“ Pumzika Job.Usinyanyuke
tafadhali”
Job akazungusha macho
kutazama huku na huku
“Where am I? akauliza
“ Uko hapa nyumbani kwako”
akasema Austin .Baada ya muda Job
akasema
“ Mukasha …Mukasha.”
“ Job endelea kwanza kupumzika
hadi hapo utakapopata nguvu kisha
utatueleza nini kilitokea” akasema
Austin
“ Austin find him!! Find
Mukasha..” akasema Job kwa sauti
dhaifu.Austin akamtazama na kusema
“ Kitu gani kilitokea Job.Can you
tell me? Akauliza Austin
Job akamtaka asogee karibu
akamnong’oneza kitu sikioni
“ Thank you Job.Kwa sasa
endelea kupumzika.Niachie suala hili
nilishughulikie” akasema Austin na
kuwafuata akina Marcelo ghorofani
akawakuta katika chumba cha Maria
“ Mambo yanakwendaje hapa?
Akauliza
“ Ninamalizia kumtibu
Maria.Baba yake tayari “ akasema
Marcelo na Maria akastuka sana
“ My father is here? Akauliza
kwa mshangao
“Yes,he’s here too.You family is
complete” akasema Amarachi huku
akitabasamu
“ You are so cruel you devils!!
Austin please don’t do anything to my
father!! Akapiga ukelele Maria.
“I’m done” akasema Marcelo
baada ya kumaliza kumfunga Maria
majeraha
“ Good.Job is awake” Austin
akawaambia
“ Real ?! akauliza Amarachi kwa
furaha.
“ Marcelo nenda kamtazame
Job,Amarachi I need to talk to you”
akasema Austin
“ What is it Austin? Akauliza
Amarachi walipotoka nje ya kile
chumba
“ Kuna jambo amenieleza Job”
“ Can he talk? Akauliza
Amarachi
“ Yes he can” akajibu Austin
“ Amenieleza kwamba jana
alifanikiwa kumpata Mukasha na
akamtaka amueleze alipo mkewe na
mwanae.Alimkata sikio moja na ndipo
alipomueleza kwamba mtu ambaye
alikuwa anaamini kuwa ndiye
aliyemtorosha mkewe na mtoto yaani
dogo Bill si yeye bali kuna mtu
mwingine mkubwa ambaye hata yeye
hamfahamu anayefahamika kwa jina
moja tu la Don.Ni dogo Bill pekee
anayemfahamu mtu huyo na huyo
ndiye anayefahamu mke wa Job na
mwanae waliko.Job anadai kwamba
walikwenda katika klabu moja kwa
ajili ya kuonana na Dogo Bill na huko
ndiko alikovamiwa na walinzi
anaoamini ni wa Bill wakampiga hadi
alipopoteza fahamu na kuzinduka
mchana huu” akasema Austin
“ Hata hivyo suala hili tutaliweka
kwanza pembeni na tutalishughulikia
pale tutakapokuwa tumekamilisha
masuala yetu makubwa ya
msingi.Kuna mambo kadhaa
yanatukabili kama kupambana na
Alberto’s,kumtafuta Yasmin na kwa
uchache wetu huu hatuwezi kujigawa
katika mambo hayo yote kwa hiyo
tutaliweka pembeni suala hili la Job
.Hata hivyo nitazungumza na rais na
kumfahamisha kuhusu maendeleo ya
Job na kumuomba atusaidie
kumdhibiti Mukasha hadi pale
tutakapomuhitaji” akasema Austin
akachukua simu na kumpigia rais
“ Hallo Austin.Unaendeleaje?
akasema rais baada ya kupokea simu
“ Naendelea vizuri mzee”
“ Good.Kuna taarifa yoyote
mpya? Akauliza rais
“ Ndiyo mzee.Nimekupigia
kukufahamisha kwamba Job
amezinduka mchana huu na
anaendelea vizuri.Tumemuondoa
hospitali baada ya kugundua kwamba
kuna watu walikuwa wanamfuatilia
ambao hatufahamu lengo lao lilikuwa
nini.Tuko naye hapa nyumbani .”
“ That’s good news” akasema
rais
“ Kuna mambo amenieleza
ambayo alielezwa na Mukasha.Katika
mtandao wa akina Mukasha kuna mtu
ambaye anajulikana kwa jina moja tu
la Don ambaye anayemfahamu ni mtu
mmoja tu dogo Bill.Inasemekana mtu
huyo ndiye anayefahamu waliko mke
na mtoto wa Job.Hata hivyo
tutalishughulikia suala hilo baada ya
kukamilisha operesheni zetu
tulizonazo.Lakini mara
tutakapokamilisha operesheni zetu za
kuisafisha nchi tutaanza kuuchimba
mtandao wa akina Mukasha na hadi
tutampata huyo Don .Tunachokiomba
mheshmiwa rais tusaidie kumdhibiti
dogo Bill weka vijana wamfuatilie ili
asije akatoroka na kwenda nje ya
nchi.Huyo ndiye njia ya kutufikisha
aliko Don” akasema Austin na ukimya
ukatanda
“Mheshimiwa rais” akaita Austin
“ Uhmm !! Austin nimekusikia
na kukuelewa.Nitayafanyia kazi hayo
uliyonieleza”
“ Ahsante mzee.Vipi kuhusu
Yasmin tayari umepata taarifa zake
zozote?
“ Mpaka sasa bado sijapata
chochote kuhusiana na huyo Yasmin
.Vyombo vyangu vinaendelea na
uchunguzi na pindi nikipata chochote
nitakujulisha mara moja.” Akasema
rais wakaagana akakata simu na
kuvuta pumzi ndefu
“ Sitakiwi kabisa kulipuuzia
suala hili.Mukasha amekwisha wapa
mwanga akina Austin na sasa tayari
wanafahamu kuhusu Don na
hawatalala usingizi hadi wahakikishe
wamemtia mikononi.I wont let them
find out who that Don is.Wakifahamu
kama huyo Don ni mimi utakuwa ni
mwisho wangu.Yule kijana Job
ambaye ameishi kama mwenda
wazimu kwa miaka kadhaa
atanitafuna nyama.Natakiwa
kuwadhibiti kuanzia sasa ili wasifike
huko wanakotaka kufika na njia pekee
ya kuwadhibiti ni kuwanyamazisha
wote na hata Bill naye natakiwa
kumuondoa kwani ni yeye pekee
anayenifahamu.Endapo wakimpata
Bill watamtesa sana kama
walivyomtesa Mukasha na atatoa
siri.Huyu Bill naweza kumjumuisha
katika hoteli ile wakatayokuwemo
Alberto’s kesho ili naye awe ni mmoja
wa watakaokufa.Nitampigia simu na
kumtaka tukutane pale .Hawa vijana
akina Austin nasubiri kwanza
wanikabidhi majibu ya kipimo kile
cha vinasaba baada ya hapo
nitawafutilia mbali.” Akawaza na
mara sura ya mwanamke mmoja
ikamjia kichwani akatabasamu
“ Nampenda sana Monalisa na
siwezi kumuacha.Bill alifanya kosa
kubwa kumuacha Job hai akidhani
kweli ni kichaa kumbe alikuwa
anaigiza na sasa ameibuka na kuwa
tishio kwetu na kama hatadhibitiwa
haraka anaweza kusababisha madhara
makubwa.” Akawaza na kuchukua
simu akazitafuta namba fulani
akapiga
“ Hallow my love” ikasema sauti
nzuri laini ya mwanamke upande wa
pili
“ Monalisa my angel,vipi hali
yako? Sijakujulia hali kwa siku kama
mbili hivi kutokana na mambo mazito
yanayonikabili kwa sasa.Natumai
umesikia kinachoendelea hivi sasa”
akasema rais Ernest
“Pole sana mpenzi.Nafahamu
mambo yanayoendelea hivi sasa na
ndiyo maana hata mimi nimekaa
kimya nisikusumbue hadi
utakapomaliza kuweka sawa mambo
hayo.Vipi maendeleo yako?
“ C’mon Mona hutakiwi kukaa
kimya malaika wangu.Nakuhitaji sana
hasa katika kipindi kama hiki.Wewe
ndiye mfariji wangu na kila kitu
changu” akasema rais
“ Nafurahi kusikia hivyo.Mambo
yanakwendaje lakini?
“ Mambo yanakwenda vizuri na
ninashukuru ninakabiliana vilivyo na
kila changamoyo ninayokutana
nayo.Mona nimekupigia kukutaarifu
jambo moja.Kwa kuwa Millen
anakaribia kufunga shule nataka
muende mapumzikoni ulaya.Mtakaa
huko kwa muda wa mwezi mzima na
mtakaporejea hapa mtakuta tayari
mambo yametulia na tutaendelea na
maisha yetu kama kawaida na safari
hii nitawahamishia Dar es salaam
kwani hakutakuwa na kikwazo tena”
akasema rais
“ Really my love? Akauliza
Monalisa kwa furaha
“ Kweli kabisa
Mona.Ningetamani sana kama
ningeungana nanyi katika mapumziko
hayo lakini kutokana na mambo
yanayoendelea hapa nchini kwa sasa
sintaweza kuungana nanyi.Nataka
mkazunguke katika nchi mbalimbali
duniani kwa mwezi mzima.”
“ Sijui nikushukuruje mpenzi
wangu kwa namna unavyotujali mimi
na mwanangu.Nimefurahi mno kwa
hili ulilonieleza .”
“ Mona ni wajibu wangu
kuhakikisha katika siku zote za
maisha yenu hapa duniani mnakuwa
na furaha.Ninawapenda sana zaidi ya
ninavyoweza kuwaeleza”
“ Ahsante sana mpenzi
wangu.Mungu akubariki sana”
“ Amina mpenzi wangu.Anza
kufanya maandalizi na siku chache
zijazo mtaondoka kwenda
ulaya.Nikipata nafasi usiku wa leo
nitakupigia tena simu” akasema rais
na kukata simu
“ Sauti ya Monaliza hupenya
ndani kabisa ya ubongo wangu na
hunifanya nijihisi kama vile niko
mbingu ya saba.Nitafanya kila lililo
ndani ya uwezo wangu kuhakikisha
kwamba hakuna atakaye vuruga
uhusiano wangu na Mona.Ni
mwanamke niliyempenda mara tu
nilipomtia machoni kwa mara ya
kwanza na nimetumia gharma kubwa
hadi kumpata kwa hiyo siko tayari
mtu yeyote amuondoe katika himaya
yangu” akawaza Ernest
SEHEMU YA 11: SEASON 5
Zaidi ya saa mbili ,Marcelo
alitumia kwa maongezi na dada yake
.Wakiwa sebuleni Austin na Amarachi
wakawashuhudia Marcelo na Julieth
wakishuka ngani wakiwa
wameshikana mikono
“ Amarachi na Austin ,napenda
kuwataarifu kwamba nimezungumza
na Julieth kwa takribani saa mbili na
amenieleza mambo mengi.Mambo
aliyonieleza yanasikitisha sana lakini
amekiri kosa alilofanyana na kulijutia
.Kuna mambo ya kifamilia
amenieleza ambayo sikuwa
nikiyafahamu .Baada ya kusikia hayo
yote,toka ndani kabisa mwa moyo
wangu nimeamua kumsamehe dada
yangu na tunakwenda kufungua
ukurasa mpya.Ameniahidi kuachana
na biashara zote haramu na badala
yake tutashirikiana kuendeleza mali
na miradi aliyoiacha baba.Kwa hiyo
ndugu zangu kama mimi
nilivyomsamehe dada yangu
nawaomba nanyi pia mumsamehe
kwa yale yote aliyokosa” akasema
Marcelo .Austin na Amarachi
wakatazamana
“ Marcelo” akasema Austin
“ Kama nilivyokueleza awali
kwamba hatima ya ndugu yako iko
juu yako na kwa vile umeamua wewe
mwenyewe kwa hiari yako
kumsamehe Julieth sisi hatuna neno
.Binafsi ninaamini sana katika nguvu
ya msamaha kwa hiyo naamini Julieth
atakuwa mtu mpya baada ya kutoka
hapa.Kwa sasa ataendelea kukaa hapa
ndani hadi pale tutakaporidhika kuwa
kweli ameamua kubadilika ndipo
tutakapomuachia.Tumeelewana
Julieth?
“ Nimekuelewa Austin na
ahsante saba kwa kunisaidia
nimeweza kuonana na ndugu yangu
na kwa pamoja tumeanza ukurasa
mpya.Sikuwa nimelitegemea kabisa
jambo hili.Nakuahidi kuwa sintarejea
tena katika njia zangu ovu” akasema
Julieth
“ Good.Marcelo show her the
kitchen.She’ll be cooking for us.Wewe
una majukumu makubwa ya kutunza
afya zetu hapa ndani” akasema
Austin
SEHEMU YA 12: SEASON 5
Tayari Job alikuwa na nguvu na
aliweza kuzungumza vizuri japokuwa
mdomo wake ulikuwa
umevimba.Ilikaribia saa kumi na mbili
za jioni na alikuwa tayari kuwaeleza
akina Austin kile kilichotokea usiku
uliopita
“ Usiku wa jana” akasema Job
“ Wakati nikiendelea kukipekua
kitabu kile chenye orodha ya wauza
dawa za kulevya ,simu ya Boaz ikaita
alikuwa ni Mukasha.Nilipandwa na
hasira nikamkumbuka mwanangu
ikanilazimu kuwasiliana
naye.Nikamtumia ujumbe kwa
kutumia simu ya Boaz nikamtaka
tuonane akanielekeza sehemu ya
kukutana nikaenda.Nilipofika mahala
hapo nikamtumia ujumbe mwingine
kwamba nimeahirisha hadi siku
nyingine.Aliamini kwamba alikuwa
anawasiliana na Boaz.Baada ya muda
nikamuona Mukasha akitoka hotelini
na kueleka katika gari lake akaingia na
kuondoka nikaanza
kumfuatilia.Alifuata barabara ya
Bahari drive ambayo kwa usiku huu
haikuwa na magari mengi”
akanyamaza kidogo na kuendelea
“ Ghafla gari la Mukasha
likaanza kuyumba ,likatoka nje ya
barabara na ilibaki kidogo litumbukie
katika mtaro.Nilishuka haraka katika
gari na kulifuata gari la Mukasha
nikachungulia ndani na kuona kuna
mtu anapambana na
Mukasha.Nikafanya haraka nikavunja
kioo na kumdhibiti yule jamaa halafu
nikamuamuru aondoke zake kwani
lengo langu mimi lilikuwa ni kumpata
Mukasha.Niliondoka na Mukasha na
kuja naye hapa nyumbani nikamuhoji
na kumtaka anieleze kuhusiana na
mtandao wake na alipo mwanangu
Millen.Mukasha hakuwa tayari
kunieleza na ndipo nilipomuondoa
sikio moja na akaamua kunieleza kila
kitu” akanyamaza tena kidogo kisha
akaendelea
“ Mukasha alinieleza kwamba
dogo Bill si mkubwa wa mtandao wao
kama nilivyokuwa nadhani bali kuna
mtu anaitwa Don ambaye ndiye
mkubwa.Anayemfahamu huyo Don ni
dogo Bill peke yake.Huyo Don ndiye
ambaye yuko na mke wngu na mtoto
kwa sasa.Dogo Bill alitumika kama
mshenga tu wa Don.Ili kumpata Don
natakiwa kumpata kwanza Bill na
Mukasha akasema yuko tayari
kunipeleka mahali aliko
Bil.Tukaelekea huko na mara
tulipofika katika klabu moja Mukasha
akashuka garini na kupiga ukelele na
ghafla nikajikuta nimezungukwa na
watu zaidi ya ishirini wenye
silaha.Nilijitahidi kadiri ya uweo
wangu kupambana na watu wale
lakini nikazidiwa nguvu nikapoteza
fahamu hadi nilipofumbua machgo na
kujikuta niko hapa ndani.Ahsanteni
sana kwa juhudi zenu mlizofanya
kuniokoa.Hivyo ndivyo ilivyotokea
jana usiku” akasema Job.Austin
akamtazama kwa makini na kusema
“ Job wewe ni mmoja wa watu
ninayekuamini sana na hata kama
nitakufa leo ninaamini wewe
utayaongoza mapambano haya lakini
kwa kitendo ulichokifanya jana usiku
naweza kusema kwamba ninaanza
kufikiria mara mbili uamuzi wangu
wa kukushrikisha katika operesheni
hii.How could you do such a stupid
thing? Ni vipi endapo wangekuua
hawa jamaa? Unafahamu kabisa kuwa
hawa watu ni hatari na wamejizatiti
vilivyo kwa nini ukaamua kwenda
kupambana nao peke yako? Why Job
?? akauliza Austin aliyeonekana
kukasirishwa na kitendo kile cha Job
“I’m sorry Austin.I wasn’t
thinking clearly” akasema Job
“ Sorry isn’t enough.Nawezaje
kukuamini tena endapo haufikiri sawa
sawa? Job you are a proffesional agent
but what you did,makes me think you
are not that Job I know” akasema
Austin
“Austin I’ve said I’m sorry.I did a
mistake .What do you want me to say?
Kichwa changu kinataka kupasuka
nikimuwaza mwanangu Millen.Hata
ugekuwa wewe mahala pangu
ungefanya kama nilivyofanya “
akasema Job
“Nisingefanya ujinga kama
ulioufanya.Nilikuahidi tutapambana
pamoja kuhakikisha tunampata
mwanao .Watu hawa si watu wa
kufanyia mchezo.Ni watu waliojizatiti
sana.Kwa hiki ulichokifanya tayari
umekwisha wastua na itakuwa vita
ngumu sana kati yetu na
wao.Mukasha atawapelekea taarifa
kuwa tunawatafuta na hivyo
watajizatiti zaidi au hata kutoweka
kabisa” akasema Austin
“ Austin I’m sorry.Najua
nimefanya kosa kubwa na
ninakuahidi sintorudia tena kosa la
namna hii.Ninachoomba baada ya
operesheni fagio kumalizika unisaidie
niweze kumpata tena mwanangu
Millen.Naomba sana Austin” akasema
Job
“Ni vyema umegundua kosa lako
na ninaomba usirudie tena na hii si
kwa Job peke yake bali kwenu
wote.Amarachi na Marcelo pia.Sitaki
tena litokee jambo kama alilolifanya
Job.Ni afadhali nikafanya kazi peke
yangu kuliko kuwa na timu ya watu
wasiofikiri sawasawa.You understand
me all? Akauliza Austin
“ Yes we do “ Amarachi na
Marcelo wakajibu
“ Good.Sasa inabidi kujipanga
upya namna ya kuwakabili hawa
jamaa lakini kwanza tuendelee na kazi
iliyoko mezani hivi sasa” akasema
Austin
“ Kabla ya kuendelea kuna jambo
moja ambalo ni vyema
nikawafahamisha” akasema Job
“ Niliwaeleza kwamba kuna mtu
aliyekuwa anapambana na Mukasha
ndani ya gari .Alikuwa amevaa kofia
ya kuficha sura yake.Nilipomdhibiti
nikamwambia Mukasha amvue kofia
na akamtambua kuwa anaitwa
Evans.Baadae akaniambia kwamba
yule ni mlinzi wa rais na anashangaa
kwa nini akamvamia na kutaka
kumdhuru”
“Evans? Austin akashangaa
“Evans ni mlinzi wa rais
anayemuamini sana.Nimeshangaa
kusikia kwamba ndiye aliyemvamia
Mukasha.Kwa nini alifanya hivyo?
Akauliza Austin
“ Hata Mukasha mwenyewe
alishangaa sana na hakuamini”
akasema Job
“Evans hawezi kuwa alitumwa
kumshambulia Mukasha? Amarachi
akauliza
“Hilo linawezekana na je kama
kweli ametumwa ni nani aliyemtuma
na kwa nini? Akauliza Austin ukimya
ukapita Austin akasema
“ Nakumbuka rais aliponitamkia
kwamba anataka kumteua Mukasha
kuwa waziri mkuu,Evans alikuwepo
pia na alionyesha kustuka sana .Nahisi
labda wawili hawa wana mambo yao
binafsi .Nadhani rais anapaswa
kulifahamu hili” akasema Austin na
kuchukua simu akampigia rais
“ Hallo Austin” akasema rais
“ Mzee,samahani kwa
usumbufu,jioni hii ila kuna jambo
nataka nikufahamishe.Kwanza
kuhusu Job anaendelea vyema na
tayari ametueleza kila kitu
kilichotokea jana” akasema Austin
“ Nafurahi k usikia hivyo Austin
lakini ndani ya dakika chache zijazo
nategemea kupokea simu ya muhimu
sana kwa hiyo naomba twende haraka
kidogo.” Akasema rais
“ Sawa mzee.Ni kwamba jana
tukiwa katika chakula Job aliamua
kumtafuta Mukasha akampata lakini
kabla hajampata lililotokea tukio
moja.Mukasha alivamiwa na mtu
aliyejificha ndani ya gari yake na Job
akafanikiwa kumdhibiti mtu
huyo.Baada ya kumvua kofia
aliyokuwa ameitumia kujificha uso
Mukasha akamtambua mtu huyo
kuwa ni Evans mlinzi wako”
“ Evans? Rais akashangaa
“ Ndiyo mzee.Unafahamu
chochote kuhusu hilo? Mukasha
amekueleza chochote?
“ Hapana sifahamu chochote
hadi sasa.Nipe muda nilifuatilie suala
hili kisha nitakupa jibu.Nitawasiliana
nawe baadae Austin” akasema rais na
kukata simu.
“ This is strange.Rais anadai
hafahamu chochote hadi sasa
kuhusiana na Evans kumvamia
Mukasha.Ina maana hadi sasa
hafahamu kilichomtokea Mukasha?
Inawezekanaje Mukasha
asimfahamishe kuhusu kuvamiwa na
Evans?Kingine kinachoshangaza rais
hajataka maelezo mengi kuhusu
jambo hili kwa nini? Akauliza Austin
“ Tuachane na hilo
tutalishughulikia baadae kilichopo
mezani kwa sasa ni kumpata Yasmin
Esfahani.Rais hajatoa jibu lolote kama
amefanikiwa kumpata au bado”
akasema Austin
“ Yasmin Esfahani? Akauliza Job
“ Ndiyo .Leo tumemuhoji Maria
,kwanza akafungua kompyuta yake
ambamo tumekuta mawasiliano ya
barua pepe kati yake na mtu mmoja
anaitwa Bin Omar .Baada ya kumuhoji
amekataa kusema chochote na
ikatulazimu kufanya makubaliano
naye na ametutaka tumtafute mama
yake anaitwa Yasmin Esfahani
aliyefungwa hapa Tanzania mahala pa
siri kwa zaidi ya miaka kumi
sasa.Nimezungumza na rais kama
anataarifa zozote kuhusiana na
Yasmin lakini rais amesema kwamba
hafahamu chochote.Alinitaka nimpe
muda alifanyie kazi suala hili na
atanipa jibu.Mpaka sasa hajasema
chochote.Kuna jambo Maria analo na
hawezi kutueleza hadi tutakapompata
mama yake.Hiyo ndiyo kazi iliyoko
mezani kwa sasa wakati tukisubiri
majibu ya kipimo cha vinasaba.”
Akasema Austin
“ Wakati ninafanya kazi katika
idara ya ujasusi ya taifa niliwahi
kulisikia jina hilo likitajwa.Huyo
mwanamke ni gaidi hatari kabisa
ambaye yuko katika mtandao wa
kigaidi wa IS.Niliwahi kusikia
kwamba ameonekana Tanzania na
tetesi za chini chini zilizozipata ni
kwamba alitakiwa kukamatwa ingawa
jambo hili lilikuwa la siri kubwa
sana.” Akasema Job
“ Kama idara ya ujasusi ilikuwa
na taarifa za Yasmin na kukawa na
mipango ya kumkamata ,basi lazima
yuko hapa hapa nchini amefungwa
mahala kama alivyosema
Maria.Nimestuka sana kusikia
kwamba Yasmin ni gaidi toka IS.Kama
ni hivyo nalazimika kuamini kwamba
hata Maria au Shamin kama
anavyoitwa atakuwa mfuasi wa IS pia
.Ninaamini hivyo kutokana na wepesi
wake wa kutumia silaha na nilijiuliza
maswali mengi amejifunzia wapi
mambo haya ya silaha? Sasa nimepata
jibu.Ni wazi Maria ni mfuasi wa IS.Ili
kulithibitisha hilo tunapaswa
kuyachimba maisha yake toka akiwa
mdogo,sehemu alizotembelea ,mahala
alikosoma na hata safari zake nyingi
huwa anaelekea wapi?” akasema
Austin na kushika kichwa
“ Kwa nini nilikuwa mjinga kiasi
hiki na kushindwa kutambua Maria ni
mtu hatari namna hii? Austin
akasikitika.
“ Austin hata mimi nakubaliana
nawe kwamba huyu Maria anaweza
kuwa mfuasi wa siri wa IS na kama ni
hivyo basi kuna vita kubwa itaibuka
kati yetu na wao.Tunachopaswa
kukifanya ni kuliendea suala hili
taratibu.Tuhakikshe kwanza
tunampata huyo Yasmin na kisha
Maria atueleze hicho anachotaka
kutueleza” akashauri Job
“ Rais ameahidi kunipigia simu
baadae.Nitaongea naye kwa kirefu
zaidi suala hili hata hivyo naomba
niwe wazi kwenu kwamba
tunakoelekea mambo yanazidi kuwa
magumu zaidi kwa hiyo nahitaji nyote
mjiandae kimwili na kiakili kwa
mapambano makali yanayokuja mbele
yetu.Siwaogopeshi bali hiyo ndiyo
hali halisi lazima tujiandae.It’s going
to be tough than we think” akasema
Austin