Queen Sendiga azindua rasmi mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku mkoa wa Manyara

PendoLyimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2014
Posts
1,062
Reaction score
1,138
📌Mhe. Queen Sendiga azindua rasmi mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku mkoa wa Manyara .

📌Mitungi 16,275 kusambazwa mkoa mzima.

📌Kila wilaya kupata mitungi 3,255.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo Julai 11,2025 wilayani Hanang amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku mkoa wa Manyara. uzinduzi huo umeongozwa na mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wa mkoa, wilaya, kata pamoja na vijiji na vitongoji vyake.

Mhe. Sendiga amesema lengo la uzinduzi mradi ni kuutambulisha rasmi mradi kwa wananchi wa mkoa wa Manyara ambao ndio walengwa na wanufaika wa mradi.

Mhe. Sendiga, amepongeza juhudi za Serikali na REA katika kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo litasaidia kutunza na kuhifadhi mazingira.

“Serikali, imeweka ruzuku ya asilimia 50, kwa hiyo wakina Baba na kina Mama wa mkoa wa Manyara, wajiandae kutumia gesi, tuwapunguzie wakina Mama kushika masizi, kutumia kuni na mikaa, kwetu sisi Mradi huu ni neema”. Alisema, Mhe. Sendiga.

Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi amesema kwa nchi nzima Mradi huo wa kusambaza mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa Wananchi utagharimu shilingi bilioni 8 ambapo kwa mkoa wa Manyara zaidi ya shilingi milioni 284 zitatumika kugharamia mitungi 16,275 kwa mkoa mzima na kila wilaya mitungi 3,255 itasambazwa

“Kampuni ya MANJIS imeshinda, tenda ya kusambaza mitungi hiyo, ilitangaza ofa ya kusambaza mtungi mmoja kwa shilingi 35,000 kwa kutambua hilo, Serikali italipia asilimia 50 ya bei hiyo, ambayo itakuwa shilingi 17,500.” Alifafanua, Mkomi.

Mkomi, amesema ili kupata mtungi huo wenye ruzuku ya Serikali kila Mwananchi anapaswa kuwa na kitambulisho cha NIDA.

Aidha Mhe. Sendiga amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wakutosha kwa mtoa huduma (MANJIS LOGISTICS LTD) ili kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuwasihi wananchi kutumia fursa ya upatikanaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku kuweza kuachana na matumizi ya nishati zisizo salama za kupikia ili kuweza kutunza na kuboresha afya zao ,mazingira pamoja na kuimarisha usawa wa kijinsia.

Mkoa wa Manyara una jumla ya wilaya 5 ambazo Wananchi wake watanufaika na mitungi ya gesi ni pamoja na wilaya ya Babati, Hanang, Simanjiro, Mbulu na Kiteto.

IMG-20250711-WA0104.jpg
IMG-20250711-WA0106.jpg
IMG-20250711-WA0105.jpg
IMG-20250711-WA0088.jpg
IMG-20250711-WA0102.jpg
 
Attachments

  • IMG-20250711-WA0103.jpg
    IMG-20250711-WA0103.jpg
    201.9 KB · Views: 38
  • IMG-20250711-WA0089.jpg
    IMG-20250711-WA0089.jpg
    117.4 KB · Views: 28
Wakianzisha kunywa bia kwa ruzuku mnishtue
 
Utapeli mtupu,wilaya Ina zaidi ya wakazi laki mbili,,,,mitungi aftatu ndo kumaanisha nini
Kwani Upendo huyu ni yule aliyekoswa na manati ya mzungu?P msaada kwa tuta?
 
Target siyo kumpa kila mkazi, labda ungesema ina kaya zaidi ya laki 3. Hata mjukuu wako ni mkazi lakin hana sifa ya kupewa mtungi.
 
RC SENDIGA AZINDUA UGAWAJI MITUNGI YA GESI YA RUZUKU​

HANANG, Manyara — Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amezindua kampeni ya ugawaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku kama sehemu ya juhudi za kitaifa za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa.

Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi ya zamani mjini Katesh, wilayani Hanang, ambapo mitungi 3,000 iliyokamilika na vifaa vyake imetolewa kwa wananchi kwa bei ya shilingi 17,500 kila mmoja. Kwa mkoa mzima wa Manyara, jumla ya mitungi 16,275 inatarajiwa kusambazwa kwa bei hiyo ya ruzuku.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Sendiga alisema mpango huo unalenga kuwawezesha wananchi, hasa wa kipato cha chini, kupata nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira kwa gharama nafuu.

“Natoa rai kwa wakuu wa wilaya wote kuhakikisha utaratibu unazingatiwa, na mitungi hii inawafikia walengwa kwa bei ya shilingi 17,500 kama ilivyopangwa. Hatutavumilia wafanyabiashara watakaojaribu kulangua na kuuza kwa bei ya juu ili kujipatia faida isiyo halali,” alisema Sendiga.

Alisisitiza kuwa kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kupambana na uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa, na kulinda afya ya wananchi dhidi ya madhara ya moshi unaotokana na nishati chafu.

Mpango huo wa ruzuku pia unalenga kupunguza gharama ya awali ya kuanza kutumia majiko ya gesi, hivyo kuongeza mwamko wa matumizi ya nishati safi kwa kaya nyingi nchini.
 
Attachments

  • Screenshot 2025-07-13 at 17-21-44 Instagram.png
    Screenshot 2025-07-13 at 17-21-44 Instagram.png
    851.7 KB · Views: 38
  • Screenshot 2025-07-13 at 17-21-27 Instagram.png
    Screenshot 2025-07-13 at 17-21-27 Instagram.png
    868.8 KB · Views: 35
📌Mhe. Queen Sendiga azindua rasmi mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku mkoa wa Manyara .

📌Mitungi 16,275 kusambazwa mkoa mzima.

📌Kila wilaya kupata mitungi 3,255.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga leo Julai 11,2025 wilayani Hanang amezindua rasmi mradi wa usambazaji wa mitungi ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku mkoa wa Manyara. uzinduzi huo umeongozwa na mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wa mkoa, wilaya, kata pamoja na vijiji na vitongoji vyake.

Mhe. Sendiga amesema lengo la uzinduzi mradi ni kuutambulisha rasmi mradi kwa wananchi wa mkoa wa Manyara ambao ndio walengwa na wanufaika wa mradi.

Mhe. Sendiga, amepongeza juhudi za Serikali na REA katika kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuongeza kuwa lengo la Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuwa ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia, jambo ambalo litasaidia kutunza na kuhifadhi mazingira.

“Serikali, imeweka ruzuku ya asilimia 50, kwa hiyo wakina Baba na kina Mama wa mkoa wa Manyara, wajiandae kutumia gesi, tuwapunguzie wakina Mama kushika masizi, kutumia kuni na mikaa, kwetu sisi Mradi huu ni neema”. Alisema, Mhe. Sendiga.

Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi kutoka REA, ndugu Abdulrazack Mkomi amesema kwa nchi nzima Mradi huo wa kusambaza mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa Wananchi utagharimu shilingi bilioni 8 ambapo kwa mkoa wa Manyara zaidi ya shilingi milioni 284 zitatumika kugharamia mitungi 16,275 kwa mkoa mzima na kila wilaya mitungi 3,255 itasambazwa

“Kampuni ya MANJIS imeshinda, tenda ya kusambaza mitungi hiyo, ilitangaza ofa ya kusambaza mtungi mmoja kwa shilingi 35,000 kwa kutambua hilo, Serikali italipia asilimia 50 ya bei hiyo, ambayo itakuwa shilingi 17,500.” Alifafanua, Mkomi.

Mkomi, amesema ili kupata mtungi huo wenye ruzuku ya Serikali kila Mwananchi anapaswa kuwa na kitambulisho cha NIDA.

Aidha Mhe. Sendiga amewaomba wananchi kutoa ushirikiano wakutosha kwa mtoa huduma (MANJIS LOGISTICS LTD) ili kufanikisha utekelezaji wa mradi na kuwasihi wananchi kutumia fursa ya upatikanaji wa mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku kuweza kuachana na matumizi ya nishati zisizo salama za kupikia ili kuweza kutunza na kuboresha afya zao ,mazingira pamoja na kuimarisha usawa wa kijinsia.

Mkoa wa Manyara una jumla ya wilaya 5 ambazo Wananchi wake watanufaika na mitungi ya gesi ni pamoja na wilaya ya Babati, Hanang, Simanjiro, Mbulu na Kiteto.

View attachment 3402294View attachment 3402295View attachment 3402297View attachment 3402298View attachment 3402302
Hapo huyo Sendiga na Convoy yake wanaweza kuwa wametumia zaidi ya milioni 300 kama gharama ya kwenda kuzindua mradi wenye thamani ya milioni 150.

Huenda pia hiyo mitungi wanapewa bure kwa kuchangisha matajiri wakubwa.

Nchi imekuwa ya ajabu sana kiasi kwamba watawala hawaogopi kutumia mabilioni kwenye zinduzi za miradi ambayo ina thamani ya mamilioni (sherehe za kuzindua miradi ni ghali zaidi kuliko thamani ya miradi yenyewe)
 
Back
Top Bottom